Hoja 2: Elimu
(a)Si wote wana elimu ya kidato cha sita. Hapa siongelei mambo ya kufaulu au kushindwa. Kuendana na record kutoka source nilizotaja hapo mwanzo ni kwamba Freeman Mbowe ana Stashahada ya Elimu. Mpaka sasa hivi sijafanikiwa kupata majibu kamili kutoka NECTA kama Mbowe alisomea hiyo stashahada baada ya Form Four au Form six, kwani wale wa miaka ya nyuma mtakumbuka kwenda kusomea ualimu uliweza kufanya baada ya kidato cha nne au cha sita. Pia kwa sasa siwezi kutaja shule na chuo alichosomea kwani sijathibitisha kutoka kwa mamla husika au shule.
Nadhani Mbowe mwenyewe ndiye anaweza kuondoa utata huu wakati tunasubiri NECTA watumwagie vitu.
b) Huwezi kulinganisha uelewa wa Mbowe na Chifupa, hata mtu mwenye akili makini hawezi kumlinganisha mtu aliyewahi kuajiriwa na Bank na mtu ambaye hakuweza kuajiri na vyombo vya Uandishi wa habari pamoja na Diploma yake uandishi wa habari (sijui kutoka chuo gani). Ijapokuwa ni fani tofauti lakini ukijaribu kulinganisha sidhani kuna mlinganyo.
c) Kuhusu mbowe kusomea shahada mbili kutoka vyuo tofauti hilo siyo swala geni hata kidogo. Usilinganishe Tanzania ambako mtu huwezi kufanya shada mbili kutoka vyuo tofauti, mfano Open University na Mlimani. Binafsi nikiwa nafanya shahada yangu nje, nilikuwa nafanya vyuo viwili tofauti katika miji tofauti, kuna kitu kinaitwa "interdisciplinary studies". hapa vyuo vina makubaliano na vyuo vingine ili kusimamia program ambazo hazipo chuoni kwao, lakini ni sehemu ya degree ya mwanafunzi. mfano mimi nilipata degree kutoka UK na Canada wakati muda wote nilikuwa kwenye chuo kimoja isipokuwa mara chache kama kwenye defense ya thesis.
d) Pia kumbuka Mbowe hasomi program za kawaida ambazo mimi na wewe tunaweza kusoma, tumeambiwa program zimetengenzwa mahsusi kwa ajili yake. Kwa hiyo course load inaweza kuwa tofauti kabisa na course work ya wanafunzi wa kawaida.
d)Kuhusu kutajwa Hull tu nadhani, kwenye gazeti habari ilisema rpogram moja imetengenezwa kwa kushirikisha vyuo vya Uingereza, japani na Marekani, haikusema kuwa atasomea kwenye vyuo vitatu. Naomba mwenye hile habari kwenye archieve zake aiweke tena hapa.
>>Nadhani Mbowe pia anaweza kujitokeza kuclarify mambo zaidi
e)Ndugu yangu nani alikuambia elimu inategema umri. Nyerere (rip) aliwahi kusema elimu haina mwisho wakati anaanzisha Elimu ya Watu wazima. Kama watu wangefuata umri kwenda shule basi tusingekuwa na maprofesa kwani hamna mtu anayepata huo uprofesa kwa sababu ana umri mdogo bali wanazotea bila kujali alianza akiwa na mwaka mmoja au hamsini.
Pia mtu mwenye majukumu ya kisiasa kama mbowe au kiongozi mwingine hawezi kufuata syllabus ya kawaida, pita dunia nzima na utaona huu ukweli.
Yaani wewe badala ya kumshauri Chifupa hata angalau ajiunge na open University tena wamtengenezee program maalum kwa ajili yake (kuenddana na habari za kimtandao hana sifa za kujiunga na University kama kweli alipata Division 0 kidato cha sita).