Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Hizi tuhuma ni nyepesi mno,sidhani kama tunahitaji kuzijadili hapa,huyo anayejiita mwana chadema mwenye uchungu na chama,tunamuomba hizi tuhuma azipeleke huko chamani wakajadiliane,siye hapa tupo busy kupambana na mafisadi sugu,mambo ya mabuzi na vimwana hayatuhusu,wala hayana maslahi kwa taifa.Taarifa kama hizo za ngono,mpelekeeni mrs Mbowe,au hana mke?Mbona Kingwendu ni tishio kwa totoz,au mmesahau hata enzi za mzee Ruksa?Mbona hayo ni mambo ya kawaida,acheni watu wazaliane bwana,shida haipo,bado tuna mapori
kibao tu.Huu udaku tu,au unasemaje Mnyika?
 
Kweli watu hawana la hoja hilo ni lake yeye Mbowe na wanawake zake sisi tunataka lile linalogusa maslahi ya taifa. Hili la Mbowe bila shaka hata aliyeandika hilo alikuwa na mke wa mtu pembeni. Hatuna ubishi nalo karibu kila "kioo" kina taswira yake pembeni, nani hana hawara katika hao viongozi wetu? Naomba wana JF kama kuna kionghozi clean kwa hili tumupe hongera zake huku JF nani huyo Sexial-Clean???????
 
Wakati tuhuma ya kwanza mpaka ya Tatu katika taarifa ya huyo mwandishi kwangu naona hazina uzito wowote ule kimantiki na "timing" ya habari yenyewe haimpi favour muandishi

lakini tuhuma ya nne ni nzito sana .kwa kutuhumiwa tu namna hii mtu makini hawezi kukaa kimya bila kuitolea kauli.

Kuvunja ndoa ya mtu/watu, kiongozi kurusha makonde na kudhuru, where is the dignity?.

Then watu wanataka kwenda ikulu, Ikulu yetu ikageuzwe kijiwe .

Well people change, no doubt about this, but we as a society to turn a blind eye on this kind of behaviour, will never serve our course.
 
Kweli watu hawana la hoja hilo ni lake yeye Mbowe na wanawake zake sisi tunataka lile linalogusa maslahi ya taifa. Hili la Mbowe bila shaka hata aliyeandika hilo alikuwa na mke wa mtu pembeni. Hatuna ubishi nalo karibu kila "kioo" kina taswira yake pembeni, nani hana hawara katika hao viongozi wetu? Naomba wana JF kama kuna kionghozi clean kwa hili tumupe hongera zake huku JF nani huyo Sexial-Clean???????

Bubu kwani isue ya Mengi ilikuwa inahusu nini? mengi ni bepari tuu na makampuni yake hapa alijadiliwa sana. Mbowe ni kiongozi na anaweza hata kuwa raisi wetu sioni sababu asijadiliwe kama kweli watu kama wakina Mengi wanaweza kujadiliwa karibu week nzima hapa. Naona muiache tuu kama watu wataona haina maana mada itakufa yenyewe. Si vyama kuchaguwa wa kujadili ni wengine wasijadiliwe.

Please refer hii thread kama nayo ilistahili kujadiliwa au lah.
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=6700

Kama kunautetezi utatokea kama ni kuiginore itakuwa ignored.
 
Tumewashtukia!

Hatutoki kwenye mstari wa kujadili kupinga ufisadi na kutetea rasilimali za taifa.

Mlianza na Zitto, mkatumia staili hii hii ya ujumbe kutoka kwa wanachadema- mkachemsha!. Mkahamia kwa Slaa, mkatumia staili hii hii ya ujumbe toka ndani ya CHADEMA(mbowe na Zitto) kuhusu Vita kali, Mkachemsha!. Sasa mmehamia kwa Mbowe, mtachemsha! Hapa sasa kinachotazamwa na ufisadi wa taifa na hatima ya rasilimali za nchi yetu. Mbowe kama kiongozi anastahili kujadiliwa, lakini hii haitotui mstari wa kujadili masuala ya ufisadi ndani ya Taifa na serikali ya Chama Cha Mafisadi.

Bahati mbaya tu mambo yenyewe mliyoandika kuhusu Mbowe yamejaa uzushi wa kidaku ambao mtu yoyote anayetafakari anagundua kirahisi tu kuwa ujumbe utaishia wenyewe kwenye udaku.

Mnasema Mbowe aliomba rushwa ya Milioni 6 kwa Dewji ili asimpigie kampeni mgombea Ubunge wa CHADEMA jimboni kwake! Mzaha, inafurahisha kweli. Mbowe aliyechangia zaidi ya milioni 100 kwenye kampeni anaweza kuomba rushwa ya milioni 6 kuhujumu kampeni alizochangia? Hii ni kama kusema mtu anaweza kujitafuna kiungo chake mwenyewe eeeh!

Eti Mbowe anatakiwa kukamatwa ili serikali inaogopa kwa sababu za kisiasa! Mzaha mwingine, Mbona Cheyo, Mrema, Hamad Rashid wote mahakama imeshawahi kutoa order hadharani? Nao si wapinzani?

Kwamba Mbowe analala na mwanamke Ndesamburo akishuhudia kwa macho yake? Mzaha zaidi, hebu jaribu kutafakari kidogo tu, anashuhidia kwa macho yake, wakiwa wapi? Eti Rekodi zipo chamani, wapi ambao mimi kama kiongozi zijaziona?

Kwamba Mbowe alipigana na kiongozi wa chama kwenye sherehe za kikundi cha sanaa cha vijana wa Chama kinachoitwa Mwalongo. Duh, Mzaha mkubwa zaidi, sherehe hii ilifanyika wapi na lini? Sherehe ya kikundi cha sanaa cha chama aalikwe Mwenyekiti wa Taifa? Sherehe hii ilikuwa na upekee gani? CHADEMA haina kikundi cha sanaa kinachoitwa Mwalongo Sanaa troupe. Huu ni uzushi!

Hizo ndoa zilivunjwaje? Mashtaka yakapelekwa wapi kwenye chama mpaka nyinyi mnaojiita wanamabadiliko CHADEMA mkapewa? Labda wengine sisi sio wanachama wa CHADEMA ndio maana hatuyajui mambo hayo! Hii ni mizaha ya mwaka!

Maadili ni kitu cha muhimu, lakini tunapojadili tutoe mifano ya kweli, na tufautishe mijadala ya maadili binafsi ya kiongozi na maadili yanayoathiri umma na rasilimali za taifa kwa ujumla.

Mtanamsifia Mnyika na Kabwe ili kuendeleza ule ule mkakati wenu wa wagawe uwatawale eeeh(divide and rule). Hatuingii mtego huo. Leo mnamsema Mbowe, mkimaliza mtahamia kwa Mnyika, nawasubiria!

Mafisadi mnajua kujificha nyuma ya vivuli. Kama ni wanachama wenye nia njema si mjitokeze kama Bujiku alivyofanya kwa CCM?

Huu ujumbe ni wazi una harufu ya kutoka kwenye Chama Cha Mafisadi!

Endeleeni tu, sisi tunaendelea kujadili Ufisadi wa Taifa na hatma ya rasilimali za nchi yetu.

Slaa juzi alijibu, alisema kichaa akikuchukulia nguo ukimkimbiza wewe ndio unaonekana kichaa. Lakini mimi nimechukua hiyo nafasi ya kuonekana kichaa. Kwa sababu uongo ukiachwa ukasambaa sana waweza kuonakena ukweli.

Hatma ya yote, mnaweza kuwadanganya watu wachache kwa muda mchache lakini si watu wote wakati wote. Ukweli hudumu milele, nia ya mwongo ni fupi.

JJ
 
Mnyika,
Mambo mengine wala yasikutishe.Watu wengi humu wana akili zilizokomaa na wanajua kuchambua na kuelewa udaku na habari za kweli hata kama ushahidi haupo.Watu wakishaona hoja zenye upuuzi kama huu "eti kashfa nzito za Mh Mbowe"huzipita kama hawazioni.
 
Huu ujumbe mimi najua umeandikwa na wabaya wa Mbowe, inaweza kuwa CCM au hata CHADEMA wenyewe.

Nilivyoanza kuusoma, nilishajua hauna maana lakini kadri nilivyoendelea kuusoma ndio nikagundua kuna madai makubwa
na majina kutajwa hasa upande wa UFUKSA. Hapo kuna issue inabidi
Mbowe au wapambe mutuambie kama hayo mambo ni ukweli au uwongo.

Masuala ya madeni na mengine yote siyapi uzito maana Mbowe ni mfanyabiashara na kukopa ni sehemu ya biashara.

Ila hayo ya ufuksa, tena sio mara ya kwanza kutolewa na majina pia yanatajwa hapo, hapana lazima tujadili.

Mnaosema tusijadili naona mna yenu. Hivi ni kweli huyu mama Kiwelu kaachana na bwanake? Haya madai yalitokea hata wakati ule wa kuteua wabunge wanawake kupitia CHADEMA.
 
Admin. naomba uchukue hatua...

Tufikie mahali tukubaliane kuwa mijadala inayohusu watu binafsi ianzie kiunoni kwenda juu, na mambo yote yanayohusu kiunoni kwenda chini ni mambo binafsi. mimi hainisaidii kusikia kua kiongozi fulani kalala na fulani, kiongozi fulani kavunja nyumba ya fulani.....

Tujadili mustakabali wa Taifa letu, mambo ya chumbani tusiyalete jamvini.

Hii character assassination ikiruhusiwa kuendelea, zitamwagwa hapa taarifa na zenye ushahidi 100% patakuwa hapatoshi.

Hivi mtajifunza lini kwamba hapa JF jambo halizuliliwi kwa kutumia nguvu ya admin?

Jambo kama ni la kipuzi litakufa lenyewe, kama sio la kipuuzi waacheni wana JF wachangie.

Nawasahangaa watu ambao kila wakiona ambacho hawakubaliani nacho ni kukimbilia kwa admin. Bahati tuna maadmin makini.
 
Now this is beneath contempt...and anybody who will fall for this kind of nonsense is the epitome of foolishness. I call for all of us, in the future, to ignore these kind of posts.
 
Tusiizuie jamii ambayo imeamua kujiangalia nje ndani.

Inavyoonekana sasa ni kwamba jamii imeanza kugundua kwamba uchafu wetu wa nje haukuanzia nje, bali unatoka ndani yetu, unatoka ndani ya mioyo yetu na akili zetu.

Kwa kuanza kuanika wazi habari za matendo ya aibu ya viongozi wetu ni dalili ya awali kwamba jamii imeamua kupambana na ufisadi kwa nguvu zote.

Kumbuka ilianza ufisadi wa ujambazi, jamii ikapiga kelele weee, sasa matokeo yake yakaonekana.

Jamii haikuishia hapo, ikasema na madawa ya kulevya nayo hatuyataki nayo yapigwe vita, Watu kama kina Marehemu Amina wakajitokezawakakemea sana.

Likaja tatizo la wizi wa ubadhirifu wa fedha za umma, jamii ikapiga kelele na inaendelea kupiga kelele.

Sasa naona jamii inazidi kuugongelea msumari katika kitovu cha ufisadi, ufisadi-ngono. ni nani atakayeizuia jamii iliyoamua kupambana na ufisadi?

Jamii imesoma chanzo cha ufisadi secondaryna imegundua unachangiwa sana na ufisadi primary(ufisadi-ngono).sasa jamii inaelekea inawataka viongozi wake wajisafishe.

No way!, shoka limeshawekwa kwenye mti bwana, kila mti usiozaa matunda lazima utakatwa tu.
 
Mzee wa propaganda RA najua yuko nyuma ya hii scandal ya kutengenezwa zidi ya mh Mbowe..... tutaendelea kujadili mafisadi bila woga aluta cont...
 
Mimi naunga kwa nguvu zote UFUKSA wa viongozi wetu uanikwe tu.

Tumeomba sana civil servants watoe siri za serikali ili tupambane na mafisadi wanaotuibia.

Sasa tunaomba pia wanaowajua viongozi hovyo kwenye UFUKSA waseme hapa JF, au watume hizo mails za siri. Tunataka kusafisha jamii yetu na lazima tutumie kila njia.

I don't care hiyo habari inatoka wapi, ninachojali ni kama kuna ukweli kwenye jambo husika.

Kila mtu anajua ile Good Stuff ilikuwa imeandikwa na mtu ambaye wala sio yule anayedai ndio ameandika, lakini pamoja na kuwa forgery imetusaidia mno kueleza ufisadi mkubwa unaoiandama TZ.

Mtu anavunja ndoa ya mtu mwingine, eti watu wanasema hiyo sio issue, kweli watanzania tumefilisika kimaadili.

Jana hapa UK kwenye Dail mail kulikuwa na issue moja, mwalimu mwanamke kavunja ndoa ya mwalimu mwenzake. Wazazi wameshika bango
mpaka huyo mwalimu jana kalazimika kuachia ngazi. Walisema watawaambia nini watoto wao ambao wanaona hao walimu ndio role models wao?

Mwaka huu haogopwi mtu hapa JF, tutawakoma nyani giladi tu.
 
Kwa kuzingatia mantiki na wakati ambao hoja hii inayodaiwa ya "ufisadi wa Mbowe" imetolewa, naona mleta hoja amejiharibia mwenyewe. Sijui kama ni ya kweli au ya kuzua, lakini hata kama ingekuwa na ukweli, yeyote atakayeisoma ataona tu ni mbinu za kuchafuana ili kufifisha zile hoja za Dr Slaa dhidi ya ufisadi. Ni ku-divert attention. Ni kama kudai "kama sisi mafisadi, ona hata mwenyekiti wao pia ni fisadi". Sioni tofauti yoyote kati ya madai haya na lile tukio nililowahi kulishuhudia mahakama ya Buguruni ambapo mahabusu mmoja alikuja na kinyesi rojorojo katika mfuko wa nailoni, akamrushia mwendesha mashtaka wakati kesi inaendelea, sijui alitaka kuvuruga kesi! Matokeo yake alikamatwa tena na mashtaka yakaongezwa. Majibu ya tuhuma si kuzua tuhuma.

Labda wangewahisha hii habari kabla ya tuhuma za ufisadi kuwekwa hadharani pengine tungeifikiria, lakini saa hizi naona wamechelewa. Bila kujali kama ni za ukweli au za uongo, naona hoja imedoda!
 
NB: Huu ujumbe nimeupokea kutoka kwenye email yangu muda si mrefu. Sio mimi niliouandika! Waraka huu umetumwa na Wana Mabadiliko Chadema

CCM wanasafisha Chama chao na sisi tusafishe chetu, tusibweteke na umaarufu binafsi wa baadhi ya viongozi wetu.


Hatua ya kwanza ni kumbadilisha Mwenyekiti Freeman Mbowe. Historia, rekodi na uchafu wa Mbowe huko nyuma utatupa wakati mgumu siku za usoni kwasababu atakuwa easy target wa mafisadi.

Kwanini nasema hivyo?


1. Mbowe ni mla rushwana anashirikiana na wana-CCM kwa ajili ya maslahi yake. Mfano: Mgombea wetu wa Ubunge kule Singida Mjini alitoa malalamiko kwamba Mbowe hakumsimamisha na kumtambulisha kwenye mkutano wa kampeni Singida Mjini kama inavyotegemewa. Ukweli ni kwamba aliomba hongo kwa Mohammed Dewji, Mgombea wa CCM, na kupewa shilingi milioni 6 ili asifanye hivyo. Kwa wanaobisha wakatazame kanda ya video ya mkutano wetu pale Singida waone kama mgombea wetu alitambulishwa. La sivyo, Mbowe atoe maelezo kwenye Kamati Kuu.

2. Mbowe ana madeni mengi na hadi sasa anayo "arrest warrant" ya Mahakama Kuu kwa kushindwa kuwalipa wadeni wake na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu . Oda ya kukamatwa kwa Mbowe imetolewa tarehe 5 Desemba 2006 na Jaji Manento, kwa hukumu iliyosomwa na Jaji Rwakibarila tarehe 27 Oktoba 2006. Arrest Warrant ameandikiwa OCD wa Central na imesainiwa na Bwana Lyimo, Msajili wa Mahakama . Hizi rekodi zote zipo Mahakama Kuu. Bahati yetu tuna Serikali ya hovyo ndio maana Mwenyekiti hajakamatwa mpaka leo kwasababu CCM wanaogopa wakimkamata itaonekana ni siasa lakini siku yoyote Mwenyekiti atakamatwa kwa uchafu wa biashara zake binafsi. Salama yetu ni kuachana naye ili tusije umbuka siku za usoni.

3. Mbowe anahusishwa na biashara za hovyo. Kwenye uchaguzi wa 2005 watu wa CCM waliweza kutumaliza kwa hoja kwamba tutakuwaje na Rais mwenye kilabu cha pombe na muziki ambacho ni makao makuu ya machangudoa na wauza unga. Mwenyekiti aamue kikutumikia Chama au kufanya biashara ya Billcanaz.

4. Mwenyekiti ana historia chafu ya ufuska na uasherati . Hili ni tatizo kwa maadili lakini ni tatizo zaidi kwa Mwenyekiti Mbowe kwasababu analeta hizi tabia kwenye kazi na kuleta mifarakano.Nitatoa mifano kadhaa:
  • amevunja ndoa ya Mbunge Grace Kiwelu ambaye alikuwa ameolewa na mtoto wa Mzee Ndesamburo anayeitwa Sindato. Mwenyekiti alikuwa na ujasiri wa kulala na Grace kwenye ziara za Kichama wakati Mzee Ndesamburo anaona kwa macho yake . Mzee Ndesa alilileta hili suala Kichama, rekodi zipo hadi leo, lakini Mbowe akawa anaendelea. Kesi ilifika mahakamani na talaka kutolewa.
  • Mwenyekiti alitia aibu katika ziara tuliyofanya Newala. Grace Kiwelu na Chiku Abwao walipigana usiku saa 7 kwenye nyumba tuliyofikia kwasababu kila mmoja alitaka kulala na Mbowe. Ugomvi ulikuwa mkubwa baadaye Chiku Abwao akafanikiwa kulala na Mbowe. Msafara ulipofika Nachingwea, Grace akawahi kuingia chumbani kwa Mbowe mapema, kwahiyo Chiku akafukuzwa. Ilikuwa ni fedheha kubwa kwa walioshuhudia. Kwa kifupi, kama tunataka kujenga Chama makini, huyu hatufai kama Mwenyekiti. Tunao viongozi wengi ambao hawana historia ya uchafu wa biashara na uchafu binafsi.
  • Mwenyekiti alipigana na kiongozi mwenzake wa Chama Kawe kwenye sherehe ya kikundi cha sanaa cha Chama kinachoitwa Malongo Sanaa Group kwasababu Mwenyekiti alimtaka msichana mmoja kwenye kikundi anayeitwa Subira Waziri (au Koku) ambaye ni bibi wa kiongozi huyo. Ugomvi huo ulikuwa mkubwa na Mwenyekiti alichaniwa shati, lakini alimpiga na kumuumiza kiongozi mwenzake. Kesho yake Mwenyekiti akaenda kwa Mzee Makani kuomba radhi na kutoa 300,000 kwa kiongozi mwenzake asiseme na kuchukua hatua.
  • Mwenyekiti pia amevunja ndoa ya Mwanamrisho Abama wa Zanzibar ambaye bado anaendelea naye mpaka leo. Pia ameingilia ndoa ya Sophia Khatau wa Lindi ambaye mume wake anafanya kazi TTCL. Pia alivuruga ndoa ya Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Hai anaitwa Helga.
  • Kuna mengine mengi ambayo hayapaswi kusemwa hadharani lakini wao CCM wanayo, rekodi zipo hata za ubakaji miaka ya 1980 na 1990 uliokuwa unafanywa na Mbowe na rafiki yake Dudley Mawala enzi hizo na wanangoja wakati muafaka tu. Ni lazima sisi wenyewe tuchukue hatua kuwapreempt sasa.
Kwahiyo wanachama wenzetu, baadhi yetu sisi wa matawi ya Mikoa ya Ruvuma, Dar, Kigoma, Manyara, Shinyanga na Arusha tumeamua tuangalie mwelekeo wa mbele zaidi wa Chama chetu. Mnyika na Kabwe wanafanya kazi nzuri sana za kurecruit vijana wenzao wasomi kwenye Chama chetu. Wameanzisha mtandao wa vijana ambao una matumaini ya kutuvunia wanachama na viongozi wasomi makini kwa siku za usoni. Tusiache mtu mmoja atuvurugie hii future nzuri ya Chama chetu iliyo mbele yetu.

Wakati ni huu. Tunaweza kabisa kuwatoa mafisadi madarakani kama tutakuwa makini. MPAKA KIELEWEKE!

We need some authentication of these allegations. Please provide us with some photos showing fornication behaviour of the elleged, debt receipts, case judgments etc so that we can honestly and shamelasly judge Mbowe. No one will be let free, all shall be juegde accordingly.
 
CCM inajua wazi kwamba muda wake wa kuishi kwenye dunia ya madaraka umekwisha na kwamba muda si muda CCM kuwa chama tawala itakuwa ni historia.

Kama mfa maji anavyotapatapa ndivyo na chama hiki kinavyotapatapa. Wanadhani wanaweza kuhamisha mawazo ya wananchi hivihivi. Wana JF mnaodai mjadala na ushahidi ni haki yenu.Mwenye wajibu wa kutoa ushahidi ni waandishi wenyewe wa kashfa hii kama walivyofanya akina Slaa na mzee Butiku. Lakini pia ni lazima kutumia common sense tu. Kwamba CCM wanazo hizi record muda mrefu na zingine za miaka ya 1980 na 1990 tena crimes, halafu wanasubiri muda muafaka? Muda gani muafaka zaidi ya 2005 Mbowe alipowachachafya kwa helkopta?

Kwani kilichowafanya CCM waibe mabilioni yote hayo ndani ya BOT ni nini? Si ni kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa Mbowe? Na kama walikuwa nazo hizo nyeti wakati huo kwa nini hawakuzitumia eti wasubiri uchaguzi ujao, walijuaje kwamba katika uchaguzi mkuu ujao ndio atakuwa tishio zaidi na ndipo watazitumia? Na hawa wanaojiita wanachadema, August 2006 tulikuwa na mkutano mkuu ambapo Mbowe, Mzee Ndesamburo, Grace Kiwelu,Chiku Abwao, wote walikuwepo na waandishi wa habari waliondolewa wote kwenye kikao, mbona hawakulileta jambo hilo kwa manufaa ya chama wanasubiri hadi leo?

Waandishi wanasema, "sisi wanachama wa Kigoma, Arusha, Dar, n.k, tumeamua". Mimi nimekuwa katibu wa wilaya ya Arusha (V) tangu 2006 na niko karibu sana na viongozi wa wilaya ya Arusha (M) ambao pia wanakaimu kama viongozi wa Mkoa. Hata mwezi uliopita tulikuwa na kikao cha pamoja kama mkoa lakini hakuna hata mmoja aliyegusia jambo hilo. Hawa wanachama wa chadema wasiojitambulisha kwamba wana vyeo gani wanaendesha Arusha ipi hizo propaganda zao?

Ukweli ni ule aliousema Mnyika na mimi narudia kwamba ni mara nyingi sana CCM mmetumia mbinu hii chafu bila mafanikio. Mmewahi hata kutangaza Dr. Slaa kafumaniwa na mkewe, uchaguzi uliofuata akashinda. Mmewahi pia kusema Zitto ana love affairs na Amina Chifupa, ikafa. Mkasema Dr. Slaa aliacha uaskofu kwa kumpa binti mimba hata Ze Commedy wakaigiza, imekufa. Na hii ya Mbowe itakufa.

Mwaka 2005, mgombea wa CCM akiwa Mererani, alisema hatuwezi kuongozwa na mmiliki wa Club ya Disco. Mgombea wa Chadema alipofika akawauliza wananchi wa Mererani, mjanja anayefaa kuwa rais ni yupi, wa chadema anayemiliki ukumbi wa disco na kufanya biashara au wa CCM anayechukua pesa na gari la uwaziri na kwenda kuingia disco na kujimwaga na vimwana? Wote mnaweza kujua wananchi walijibu nini labda kama wote mmegeuka kuwa kada mpinzani.

Wana CHADEMA popote mlipo msibabaishwe na propaganda kama hizi. Chama kiko imara na inshallah, mapambano yanaenndelea.
 
sasa tumeingiliwa kweli,lakini hicho kibanda walichojificha kimeshachoka muda wowote kitaanguka,sijui aibu watakayokuwa nayo pale wazee wazima wakikimbia bila nguo
 
NB: Huu ujumbe nimeupokea kutoka kwenye email yangu muda si mrefu. Sio mimi niliouandika! Waraka huu umetumwa na Wana Mabadiliko Chadema

Tarishi hauwawi.
 
Jamani tusichanganye hoja hapa, hakuna aliyekataa Wabadhirifu wa fedha za umma wasizidi kupewa kibano. lakini vile vile Tusikatae kwamba kuna tatizo la msingi la UFISADI-NGONO unaozidi kuwatafuna waliopewa dhamana na jamii .

Kwa hiyo hili fagio la kusafisha nyumba yetu Ya tanzania Halina budi kusafisha uchafu wa Ufisadi wowote ule,uwe wa Rushwa ,wizi, au Ufisadi-ngono

Iwapo sasa hili fagio limefika katika chumba cha wapinzani tulipe nafasi lifyagiefyagie, Maana Masterbedroom kule kwa watawala inaelekea linafanya kazi nzuri japo bado halijamaliza

Halafu tuhuma ni tuhuma iwe zimetoka CCM au popote, cha msingi ni kuzichunguza je hizo Tuhuma ni za kwel?i na kuzipa uzito unaostahili.Hiyo ndiyo pointi.

Ni Lazima jamii ihoji Matendo ya viongozi wake, either wawe wa CCM au wa Upinzani.

Tuhuma za kuvunja ndoa za watu si tuhuma ndogo, ni tuhuma nzito sana, yule aliyedhulumiwa penzi la ampendaye kwa sababu ya Fisadi ngono anatambua uchungu wake.

Halafu eti jamii ipuuzie uharibifu huu!
What a nonesense!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom