kichwamaji
JF-Expert Member
- Dec 1, 2006
- 232
- 13
Taarifa Ya Kuhudhunisha Kwa Wanabodi.
Mheshimiwa Mbowe Amepata Bahati Mbaya Ya Kufeli Mitihani Yake Miwili Kati Ya Minne.
Du! Hii ya Chinga kali sana! Chinga ameingia na mpya, na wengine wakaingia mkenge....
Anavyoandika, utadhani yeye mwalimu wa Mbowe au ni staff katika chuo aliko Mbowe...na kwa baadhi yetu tunaojua jinsi mifumo ya elimu ya Ulaya inavyofanya kazi, tunabaki kujiuliza Chinga ni nani hadi ajue haya anayoandika juu ya Mbowe. Kayapata wapi? Tukisema CCM ni wakali wa propaganda chafu dhidi ya wenzao baadhi yenu mnakataa. Si mnaona wenyewe hapa? Kitu cha ajabu, wapo ambao tayari wamechotwa na mkumbo huu wa Chinga...wanataka kumchukulia Chinga kama authority kwa mambo yaliyo juu ya uwezo wake!
Ameulizwa maswali kadhaa na kina Lunyungu lakini hakuweza kuyajibu kuhusu vyanzo vya taarifa zake hizo. Uwongo mbaya, mjadala huu juu ya masomo ya Mbowe ambayo wengine hatuyajui, umenikumbusha mbali tangu ilipoandikwa thread ya kwanza kwamba Mbowe anakwenda kusoma Uingereza. Ni hawa hawa wenye mawazo kama ya Chinga walioanza kumzomea Mbowe na kukataa katakata kwamba hawezi kwenda kusoma chuo kikuu.
Sasa wanakuja na 'ujanja' wa Chinga wa kutunga uwongo kubadili mwelekeo wa mjadala, na kwa kufanya hivyo wansababisha mtu ahoji masuala mbalimbali yakiwamo haya:
1. Wenyewe hapa mliwahi kudai kwamba Mbowe hasomi. Sasa kama wenyewe mnaanza kusema 'amefeli' masomo kadhaa, si mnathibitisha kwamba anasoma kweli?
2. Mnaleta matokeo ya kutunga ya mitihani yake mkisahau kwamba na sisi wengine shule tulikwenda na tunajua mifumo ya utoaji matokeo... Chinga anataka kutuaminisha kwamba yeye ni mmoja wa staff wanaoshughulika na masomo ya Mbowe?
3. Chinga anasema amefeli masomo mawili kati ya manne? Kama hiyo ingekuwa kweli, basi Mbowe ni mkali, ana uwezoi mkubwa, maana kwa jinsi baadhi yetu wanavyomshambulia na kuonyesha hawezi kitu, na ikizingatiwa shughuli zake nyingi zinazoambatana na shule yake kwa wakati mmoja kama tunavyomjua na tunavyosoma na kusikia kwenye vyombo vya habari, na zaidi ya hapo ukizingatia na umri wenyewe alionao sasa, mtu huyu alipaswa kufeli masomo yote. Lakini kama maneno ya Chinga yangekuwa ya kweli, basi Mbowe angestahili sifa badala ya kubezwa na baadhii ya watu kama chinga.
4. Zaidi ya hayo, wote tuliokwenda shule tunajua kuwa kusoma, kufeli na ku-resit mitihani ni sehemu muhimu na nyeti ya usomi. Baadhi yetu tusingefika hapa tulipo bila kupitia misukosuko hiyo. Mtu anayefeli ndiye anayeweza kujifunza na kufunza wengine maana anajua maana ya kufeli na kushinda. Maprofesa wengi tunaowaheshimu leo waliwahi kufeli sana kabla ya kuhitimu. Naona Chinga yu gizani katika hili, vinginevyo asingetunga uwongo na kuwaletea watu wazima.
5. Mbowe, kama angetaka kupata elimu ya makaratasi ya kununua kama baadhii ya maswahiba wake Chinga, hao anaowahusudu, asingkosa - kwa gharama yo yote. Mbowe amektaa ulipuaji, natafuta quality, anatafuta elimu ambayo ni real. Mtu wa profle ya Mbowe kufanya hiki anachokifanya sasa, si jambo la kawaida, wala si mtu wa kubeza na kupaka matope huyu...wala hastahili kubezwa na watu ambao wanajikita katika kujadili very trivial issues - an indication that some of the discussants on this forum are merely weak, simple minds bent on character-assassinating people...Is this another mtandao in operation? Chinga, are you being used? Or are you 'using' yourself ignominiously?