Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Yourname, wakati mwingine unazungumza kama uko very naive... hivi Majira.. wanaposema "Mtandao" hamkuuliza ni mtandao gani? Sometimes natamani ungeweza kuona ninayoyaona mimi... hii vita ni kubwa kuliko na kesho moto utawashwa zaidi..!!
 
Asante Msee, nipo skeptical kuliko imaginations........i have been fighting these kind of fights since when I was 11 years old. Ktk ka-dunia kangu kila story ina version mbili, ukweli na uongo na ni zero kuchukulia vitu for granted..........kumbuka haya ni mapambano ya kifikra.
 
NB: Huu ujumbe nimeupokea kutoka kwenye email yangu muda si mrefu. Sio mimi niliouandika! Waraka huu umetumwa na Wana Mabadiliko Chadema

CCM wanasafisha Chama chao na sisi tusafishe chetu, tusibweteke na umaarufu binafsi wa baadhi ya viongozi wetu.


Hatua ya kwanza ni kumbadilisha Mwenyekiti Freeman Mbowe. Historia, rekodi na uchafu wa Mbowe huko nyuma utatupa wakati mgumu siku za usoni kwasababu atakuwa easy target wa mafisadi.

Kwanini nasema hivyo?

1. Mbowe ni mla rushwana anashirikiana na wana-CCM kwa ajili ya maslahi yake. Mfano: Mgombea wetu wa Ubunge kule Singida Mjini alitoa malalamiko kwamba Mbowe hakumsimamisha na kumtambulisha kwenye mkutano wa kampeni Singida Mjini kama inavyotegemewa. Ukweli ni kwamba aliomba hongo kwa Mohammed Dewji, Mgombea wa CCM, na kupewa shilingi milioni 6 ili asifanye hivyo. Kwa wanaobisha wakatazame kanda ya video ya mkutano wetu pale Singida waone kama mgombea wetu alitambulishwa. La sivyo, Mbowe atoe maelezo kwenye Kamati Kuu.

2. Mbowe ana madeni mengi na hadi sasa anayo "arrest warrant" ya Mahakama Kuu kwa kushindwa kuwalipa wadeni wake na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu . Oda ya kukamatwa kwa Mbowe imetolewa tarehe 5 Desemba 2006 na Jaji Manento, kwa hukumu iliyosomwa na Jaji Rwakibarila tarehe 27 Oktoba 2006. Arrest Warrant ameandikiwa OCD wa Central na imesainiwa na Bwana Lyimo, Msajili wa Mahakama . Hizi rekodi zote zipo Mahakama Kuu. Bahati yetu tuna Serikali ya hovyo ndio maana Mwenyekiti hajakamatwa mpaka leo kwasababu CCM wanaogopa wakimkamata itaonekana ni siasa lakini siku yoyote Mwenyekiti atakamatwa kwa uchafu wa biashara zake binafsi. Salama yetu ni kuachana naye ili tusije umbuka siku za usoni.

3. Mbowe anahusishwa na biashara za hovyo. Kwenye uchaguzi wa 2005 watu wa CCM waliweza kutumaliza kwa hoja kwamba tutakuwaje na Rais mwenye kilabu cha pombe na muziki ambacho ni makao makuu ya machangudoa na wauza unga. Mwenyekiti aamue kikutumikia Chama au kufanya biashara ya Billcanaz.

4. Mwenyekiti ana historia chafu ya ufuska na uasherati . Hili ni tatizo kwa maadili lakini ni tatizo zaidi kwa Mwenyekiti Mbowe kwasababu analeta hizi tabia kwenye kazi na kuleta mifarakano.Nitatoa mifano kadhaa:
  • amevunja ndoa ya Mbunge Grace Kiwelu ambaye alikuwa ameolewa na mtoto wa Mzee Ndesamburo anayeitwa Sindato. Mwenyekiti alikuwa na ujasiri wa kulala na Grace kwenye ziara za Kichama wakati Mzee Ndesamburo anaona kwa macho yake . Mzee Ndesa alilileta hili suala Kichama, rekodi zipo hadi leo, lakini Mbowe akawa anaendelea. Kesi ilifika mahakamani na talaka kutolewa.
  • Mwenyekiti alitia aibu katika ziara tuliyofanya Newala. Grace Kiwelu na Chiku Abwao walipigana usiku saa 7 kwenye nyumba tuliyofikia kwasababu kila mmoja alitaka kulala na Mbowe. Ugomvi ulikuwa mkubwa baadaye Chiku Abwao akafanikiwa kulala na Mbowe. Msafara ulipofika Nachingwea, Grace akawahi kuingia chumbani kwa Mbowe mapema, kwahiyo Chiku akafukuzwa. Ilikuwa ni fedheha kubwa kwa walioshuhudia. Kwa kifupi, kama tunataka kujenga Chama makini, huyu hatufai kama Mwenyekiti. Tunao viongozi wengi ambao hawana historia ya uchafu wa biashara na uchafu binafsi.
  • Mwenyekiti alipigana na kiongozi mwenzake wa Chama Kawe kwenye sherehe ya kikundi cha sanaa cha Chama kinachoitwa Malongo Sanaa Group kwasababu Mwenyekiti alimtaka msichana mmoja kwenye kikundi anayeitwa Subira Waziri (au Koku) ambaye ni bibi wa kiongozi huyo. Ugomvi huo ulikuwa mkubwa na Mwenyekiti alichaniwa shati, lakini alimpiga na kumuumiza kiongozi mwenzake. Kesho yake Mwenyekiti akaenda kwa Mzee Makani kuomba radhi na kutoa 300,000 kwa kiongozi mwenzake asiseme na kuchukua hatua.
  • Mwenyekiti pia amevunja ndoa ya Mwanamrisho Abama wa Zanzibar ambaye bado anaendelea naye mpaka leo. Pia ameingilia ndoa ya Sophia Khatau wa Lindi ambaye mume wake anafanya kazi TTCL. Pia alivuruga ndoa ya Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Hai anaitwa Helga.
  • Kuna mengine mengi ambayo hayapaswi kusemwa hadharani lakini wao CCM wanayo, rekodi zipo hata za ubakaji miaka ya 1980 na 1990 uliokuwa unafanywa na Mbowe na rafiki yake Dudley Mawala enzi hizo na wanangoja wakati muafaka tu. Ni lazima sisi wenyewe tuchukue hatua kuwapreempt sasa.
Kwahiyo wanachama wenzetu, baadhi yetu sisi wa matawi ya Mikoa ya Ruvuma, Dar, Kigoma, Manyara, Shinyanga na Arusha tumeamua tuangalie mwelekeo wa mbele zaidi wa Chama chetu. Mnyika na Kabwe wanafanya kazi nzuri sana za kurecruit vijana wenzao wasomi kwenye Chama chetu. Wameanzisha mtandao wa vijana ambao una matumaini ya kutuvunia wanachama na viongozi wasomi makini kwa siku za usoni. Tusiache mtu mmoja atuvurugie hii future nzuri ya Chama chetu iliyo mbele yetu.

Wakati ni huu. Tunaweza kabisa kuwatoa mafisadi madarakani kama tutakuwa makini. MPAKA KIELEWEKE!

Duuh! jamaa kumbe kidume hivyo? anakula kondoo zake.Huyu anaweza kuwa fisadi nae.Aje ajibu kama atashindwa atajibiwa na wapambe wake hapa.
 
Admin,

Wengi wape, irudishe kwenye siasa, itakuwa hujamtendea haki Mengi .....

Mtanzania usiondoke, Admin naamini atairudisha.
 
Admin,

Wengi wape, irudishe kwenye siasa, itakuwa hujamtendea haki Mengi .....

Mtanzania usiondoke, Admin naamini atairudisha.

FD,

Wala tatizo sio mada kuwa sehemu flani, suala ni mtu kuwa na mawazo negative always over JF. Yani hata wale usiowategemea wanakuwa kwenye mkumbo! Hakuna aliye mkamilifu. Hata mods wakikosea vp kwa mwendo huo nitalazimika kuvaa viatu vyao kuwatetea. Tuwe tunawasilisha maoni kwa njia nzuri na si kwa kuanzisha thread za lawama kwenye Siasa.

Thanks and done!
 
FD,

Wala tatizo sio mada kuwa sehemu flani, suala ni mtu kuwa na mawazo negative always over JF. Yani hata wale usiowategemea wanakuwa kwenye mkumbo! Hakuna aliye mkamilifu. Hata mods wakikosea vp kwa mwendo huo nitalazimika kuvaa viatu vyao kuwatetea. Tuwe tunawasilisha maoni kwa njia nzuri na si kwa kuanzisha thread za lawama kwenye Siasa.

Thanks and done!

Invisible shukran kwa uamuzi wako wa busara, mimi ni miongoni wa wanaoamini sana hikma na busara zako. Kwa mara nyingine umedhihirisha hilo kwa vitendo.

Binafsi naamini kuwa mada isiyo na mashiko hufa kifo cha asili, hii haya matendo ya kuburuzana yanaharibu jamvi hili.

Once again, brilliant intervention bravo mkuu
 
Hii style imepitwa na wakati sana. Ilitumika kudhoofisha upinzani baada ya uchaguzi wa 1995, lakini sio leo. Non starter, hii kashfa imekufa kabla haijaiva. Hawa wanaojiita wana-chadema makini kwa nini wasitoke hadharani na waka-lodge allegations zao kwenye chama zijadiliwe. Kwa mfano, huyu mgombea wa Singida ambapo mimi natoka alikuwa hana chochote; mgombea aliyekuwa na nguvu za kushindana na Dewji angalau kwa mbali alikuwa ni wa CUF. Wala Dewji alikuwa hana sababu ya kuhonga ili ashinde ubunge Singida, hilo linajulikana.

Chama chetu kipo makini. Mwenyekiti wetu yupo makini na tunampenda. Kashfa hizi zinalenga kutukatisha tamaa, lakini haturudi nyuma, tulishaamua na bahati nzuri wananchi nao walishaamua. Njia pekee ya kudhoofisha upinzani ni kwa serikali kutekeleza wajibu wake wa msingi. Kashfa kama hizi hazisaidii, zaidi ya kutuchochea zaidi katika mapambano.
 
Kashfa kama hizi hazisaidii, zaidi ya kutuchochea zaidi katika mapambano.

Lakini hazikwepeki mkuu; ndiyo hali ya sasa. Kama ni kichocheo cha mapambano kwenu basi ni nzuri kwakuwa zinaamsha ari ya mapambano na maanake zinasaidia au sio?
 
hii mada inaweza kuwa ni ya kutungwa moja kwa moja na asipenda maendeleo ya upinzani, lakini watanzania tusiwe wapuuzi wakusema kuvunja ndoa ya mtu na kumpiga mtu hadharani ni sawa kwa kuwa viongozi wa ccm wanafanya.

ikiwa viongozi wa upinzani wana tabia za namna hizi, na waziache mara moja.
 
hii mada inaweza kuwa ni ya kutungwa moja kwa moja na asipenda maendeleo ya upinzani, lakini watanzania tusiwe wapuuzi wakusema kuvunja ndoa ya mtu na kumpiga mtu hadharani ni sawa kwa kuwa viongozi wa ccm wanafanya.

ikiwa viongozi wa upinzani wana tabia za namna hizi, na waziache mara moja.

Giga, ni kweli kabisa waziache mara moja.lakini kwa sasa hiyo siyo kipaumbele chetu cha kuzingumzia maisha ya watu,kipaumbele chetu ni kuendeleza mapinduzi ya fikra kuweza kuwafikia wengi zaidi.ni kweli usiofichika kuwa ili tuweze kufikia hapo,kuna wapinzani kama hao wanaolete mambo ya mtu binafsi na kuweka kama kipaumbele.
 
Lakini hazikwepeki mkuu; ndiyo hali ya sasa. Kama ni kichocheo cha mapambano kwenu basi ni nzuri kwakuwa zinaamsha ari ya mapambano na maanake zinasaidia au sio?

yap! Katika ulingo wa siasa, haya yanatarajiwa! Cha msingi ni kuwa tayari kukabiliana nayo.
 
"hii story nzima ni uwongo,tena uwongo mweupe.Hizi tuhuma hazijatolewa kisayansi na zinaonekana kabisa ni za kutunga,na aliyeandika hawezi kuthibitisha".
 
Huyu atakuwa anafanya kazi kwenye gazeti la udaku, nadhani aliyemtuma alikosea kumtumia!
 
FD,

Wala tatizo sio mada kuwa sehemu flani, suala ni mtu kuwa na mawazo negative always over JF. Yani hata wale usiowategemea wanakuwa kwenye mkumbo! Hakuna aliye mkamilifu. Hata mods wakikosea vp kwa mwendo huo nitalazimika kuvaa viatu vyao kuwatetea. Tuwe tunawasilisha maoni kwa njia nzuri na si kwa kuanzisha thread za lawama kwenye Siasa.

Thanks and done!

Nimekuelewa, kweli nimeshtushwa na Mtanzania kuwa pia na fikra kama hiyo, ninafahamu ni mtu makini sana. Sijui kwanini amefikiria hivyo!
 
This email or shauri of Wachanganyikiwa wa Chadema is total garbage, similar to allegations against Slaa.

Court summons on debts are common, you are required to go and declare when will you settle your debts. The difference is CCM has enjoyed using Hazina money because it is in power. Even when Sukita was mufuilisi, hazina bailed it out and so are Meremeta, Tangold, Deep Green and Mwananchi Green.
Using tax payer money to offset political debts is a sin.

I do not see a sin with Mbowe as a person having debts, he needs to restructure them or file for bankcruptcy!

On Bilicanas, how many scrupoulos business does CCM and ite leaders hold? Look at the illegal hunting, logging, drugs and even arms trafficing that led to big disaster in Congo, Rwanda and Burundi.

He owned a business before he joined the politics, once he is a president, he will have to let his trust run the damn club. Is it dhambi to own the club, does he have choice in who gets in?

On Ufuska, lets not even get there! Start with the top team of CCM and Serikali! When whomever is dishing out this laundry can tell me why Kikwete allowed Karamagi to take John Mongella wife and other nonsense we hear, then I will shut up.

No one is perfect and ni human being is a Saint! Watanzania tunatafuta miujiza, Yesu atarudi at his own time.

Nchi inaongozwa na wezi, mafuska, walevi na majitu yenye roho katili!

However, it will be a great thing for Mbowe and Slaa to come out in public and clean up this mess and not end up like CCM folks who are using threats!
 
Nimekuelewa, kweli nimeshtushwa na Mtanzania kuwa pia na fikra kama hiyo, ninafahamu ni mtu makini sana. Sijui kwanini amefikiria hivyo!


Hii ilinipita; kwani Mtanzania ameamua nini katika hili. Huyu ni mwana JF makini sana, labda alighafilika tu!
 
Kitila,

Alisema amekasirika hii thread kuhamishwa kutoa hapa ilipo, akasema kikundi kinaiendesha JF na kusema kuwa haandiki tena hapa kwenye siasa.
 
Hii ilinipita; kwani Mtanzania ameamua nini katika hili. Huyu ni mwana JF makini sana, labda alighafilika tu!

Hata mimi naamini ni hasira tu, ni mmojawapo ya ASSET za ukumbi huu, yupo makini sana. Naamini atarudi.
 
Hii ilinipita; kwani Mtanzania ameamua nini katika hili. Huyu ni mwana JF makini sana, labda alighafilika tu!

Ni mtu makini YES, lakini alikuta topic hii ime-movuzishwa kwenda "Vibweka vya Wakubwa" akasema huko ni sawa na kuifuta na JF inamtetea Mbowe. Ingawa anaweza kuwa sahihi lakini alitakiwa kuwafahamisha mods wafanye kazi yao kwa lugha nyepesi ya kiungwana. Wote tuna mapungufu na tunaweza kujirudi (though sikuona ubaya wa topic hii kuwa kule).

BTW: Freeman anaweza kuja hapa ku-clear up this stuff? Au utamsaidia mkuu?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom