Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Kwa akili za mtu asiyefikiria vizuri,kuna usawa katika hawa wanasiasa wawili.Ila ukifikiria kwa undani utaona vizuri.Tujadili mambo ya msingi sana.

Undani upi unaozungumzia? Maana hii thread imeanzishwa mwaka jana, na leo hii ilitakiwa useme ni nini umekiona baada ya muda wote huo, au ndiyo umekutana nayo leo hii?
 
Kwa akili za mtu asiyefikiria vizuri,kuna usawa katika hawa wanasiasa wawili.Ila ukifikiria kwa undani utaona vizuri.Tujadili mambo ya msingi sana.

Of course, one is dead, one is alive. That is the only difference I see. And, yes, tujadili mambo ya msingi sasa.
 
Mie naona mada hii ifungwe kutokana na mmoja wao kufariki.

At least hapa mzee wangu Nungwi umeongea point. Hata kama posts zinazowekwa kwenye thread hii hazimhusu marehemu kipenzi chetu Amina, jina lake kuonekana kwenye title kunaaishira kama bado tinamjadili badala ya kumwach apaumzike kwa amani, jambo ambalo siyo kweli. Naungana na Nungwi kumwomba Admin ama abadili kichwa cha thread hii au aifunge kabisa.
 
Mii pia,
Admin tafadhali ondoa hii mada imekuwa too much yaani watu wanakosa kabisa utu wao kwa sababu ambazo hazina msingi. Jamani huyu mtu marehemu mpeni staha na heshimuni mauti!.. Please!
Ikiwa issue hapa ni Zitto, Freeman ama Chadema basi naomba iwekwe mpya yenye maelezo hayo tu.
 
JF Admin pleeeaase!!

Kama walivyotangulia wenzangu Nungwi, Kichuguu na Mkandara kusema hapo juu, jaribuni kuondoa hilo Jina la marehemu...................Mwaweza kuiacha na Title CHADEMA Vs FAMILY BUSINESS

Shukran
 
NB: Huu ujumbe nimeupokea kutoka kwenye email yangu muda si mrefu. Sio mimi niliouandika! Waraka huu umetumwa na Wana Mabadiliko Chadema

CCM wanasafisha Chama chao na sisi tusafishe chetu, tusibweteke na umaarufu binafsi wa baadhi ya viongozi wetu.


Hatua ya kwanza ni kumbadilisha Mwenyekiti Freeman Mbowe. Historia, rekodi na uchafu wa Mbowe huko nyuma utatupa wakati mgumu siku za usoni kwasababu atakuwa easy target wa mafisadi.

Kwanini nasema hivyo?

1. Mbowe ni mla rushwana anashirikiana na wana-CCM kwa ajili ya maslahi yake. Mfano: Mgombea wetu wa Ubunge kule Singida Mjini alitoa malalamiko kwamba Mbowe hakumsimamisha na kumtambulisha kwenye mkutano wa kampeni Singida Mjini kama inavyotegemewa. Ukweli ni kwamba aliomba hongo kwa Mohammed Dewji, Mgombea wa CCM, na kupewa shilingi milioni 6 ili asifanye hivyo. Kwa wanaobisha wakatazame kanda ya video ya mkutano wetu pale Singida waone kama mgombea wetu alitambulishwa. La sivyo, Mbowe atoe maelezo kwenye Kamati Kuu.

2. Mbowe ana madeni mengi na hadi sasa anayo "arrest warrant" ya Mahakama Kuu kwa kushindwa kuwalipa wadeni wake na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu . Oda ya kukamatwa kwa Mbowe imetolewa tarehe 5 Desemba 2006 na Jaji Manento, kwa hukumu iliyosomwa na Jaji Rwakibarila tarehe 27 Oktoba 2006. Arrest Warrant ameandikiwa OCD wa Central na imesainiwa na Bwana Lyimo, Msajili wa Mahakama . Hizi rekodi zote zipo Mahakama Kuu. Bahati yetu tuna Serikali ya hovyo ndio maana Mwenyekiti hajakamatwa mpaka leo kwasababu CCM wanaogopa wakimkamata itaonekana ni siasa lakini siku yoyote Mwenyekiti atakamatwa kwa uchafu wa biashara zake binafsi. Salama yetu ni kuachana naye ili tusije umbuka siku za usoni.

3. Mbowe anahusishwa na biashara za hovyo. Kwenye uchaguzi wa 2005 watu wa CCM waliweza kutumaliza kwa hoja kwamba tutakuwaje na Rais mwenye kilabu cha pombe na muziki ambacho ni makao makuu ya machangudoa na wauza unga. Mwenyekiti aamue kikutumikia Chama au kufanya biashara ya Billcanaz.

4. Mwenyekiti ana historia chafu ya ufuska na uasherati . Hili ni tatizo kwa maadili lakini ni tatizo zaidi kwa Mwenyekiti Mbowe kwasababu analeta hizi tabia kwenye kazi na kuleta mifarakano.Nitatoa mifano kadhaa:
  • amevunja ndoa ya Mbunge Grace Kiwelu ambaye alikuwa ameolewa na mtoto wa Mzee Ndesamburo anayeitwa Sindato. Mwenyekiti alikuwa na ujasiri wa kulala na Grace kwenye ziara za Kichama wakati Mzee Ndesamburo anaona kwa macho yake . Mzee Ndesa alilileta hili suala Kichama, rekodi zipo hadi leo, lakini Mbowe akawa anaendelea. Kesi ilifika mahakamani na talaka kutolewa.
  • Mwenyekiti alitia aibu katika ziara tuliyofanya Newala. Grace Kiwelu na Chiku Abwao walipigana usiku saa 7 kwenye nyumba tuliyofikia kwasababu kila mmoja alitaka kulala na Mbowe. Ugomvi ulikuwa mkubwa baadaye Chiku Abwao akafanikiwa kulala na Mbowe. Msafara ulipofika Nachingwea, Grace akawahi kuingia chumbani kwa Mbowe mapema, kwahiyo Chiku akafukuzwa. Ilikuwa ni fedheha kubwa kwa walioshuhudia. Kwa kifupi, kama tunataka kujenga Chama makini, huyu hatufai kama Mwenyekiti. Tunao viongozi wengi ambao hawana historia ya uchafu wa biashara na uchafu binafsi.
  • Mwenyekiti alipigana na kiongozi mwenzake wa Chama Kawe kwenye sherehe ya kikundi cha sanaa cha Chama kinachoitwa Malongo Sanaa Group kwasababu Mwenyekiti alimtaka msichana mmoja kwenye kikundi anayeitwa Subira Waziri (au Koku) ambaye ni bibi wa kiongozi huyo. Ugomvi huo ulikuwa mkubwa na Mwenyekiti alichaniwa shati, lakini alimpiga na kumuumiza kiongozi mwenzake. Kesho yake Mwenyekiti akaenda kwa Mzee Makani kuomba radhi na kutoa 300,000 kwa kiongozi mwenzake asiseme na kuchukua hatua.
  • Mwenyekiti pia amevunja ndoa ya Mwanamrisho Abama wa Zanzibar ambaye bado anaendelea naye mpaka leo. Pia ameingilia ndoa ya Sophia Khatau wa Lindi ambaye mume wake anafanya kazi TTCL. Pia alivuruga ndoa ya Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Hai anaitwa Helga.
  • Kuna mengine mengi ambayo hayapaswi kusemwa hadharani lakini wao CCM wanayo, rekodi zipo hata za ubakaji miaka ya 1980 na 1990 uliokuwa unafanywa na Mbowe na rafiki yake Dudley Mawala enzi hizo na wanangoja wakati muafaka tu. Ni lazima sisi wenyewe tuchukue hatua kuwapreempt sasa.
Kwahiyo wanachama wenzetu, baadhi yetu sisi wa matawi ya Mikoa ya Ruvuma, Dar, Kigoma, Manyara, Shinyanga na Arusha tumeamua tuangalie mwelekeo wa mbele zaidi wa Chama chetu. Mnyika na Kabwe wanafanya kazi nzuri sana za kurecruit vijana wenzao wasomi kwenye Chama chetu. Wameanzisha mtandao wa vijana ambao una matumaini ya kutuvunia wanachama na viongozi wasomi makini kwa siku za usoni. Tusiache mtu mmoja atuvurugie hii future nzuri ya Chama chetu iliyo mbele yetu.

Wakati ni huu. Tunaweza kabisa kuwatoa mafisadi madarakani kama tutakuwa makini. MPAKA KIELEWEKE!
 
haya kumekucha weeee!!!


njooni mukanushe na kumtetea huyu FISADI wa kweli, au njooni museme mbinu chafu za CCM.

huyu wenu wa ndani nakatoa tuhuma hizo nzito, mzee kavuka maji kafika hadi zenji na kuchafua huyu mmhhhhhhh.

njooni mjibu hoja kwa hoja.

mwaka huuu wa kilioooooo na kichekoooooooo heeeeeeeee heeeeeeeeee
 
These are too light ukilinganisha na ufisadi wa CCM!

"Mbowe ni mla rushwana anashirikiana na wana-CCM kwa ajili ya maslahi yake. Mfano: Mgombea wetu wa Ubunge kule Singida Mjini alitoa malalamiko kwamba Mbowe hakumsimamisha na kumtambulisha kwenye mkutano wa kampeni Singida Mjini kama inavyotegemewa"
not justifiable

"Mbowe ana madeni mengi"
Hata serikali zinadaiwa hii haina uzito sana.

"Mwenyekiti ana historia chafu ya ufuska na uasherati"
haina uzito sawa na jinsi wananchi wanavyoteseka kwa ufisadi wa viongozi wa CCM. Na hata hivyo ni kiongozi gani wa CCM asiye na historia ya ufuska??

Labda mama Lwakatare mbunge mtarajiwa hatuna evidence zake za hili eneo!!

Tafuta yanayolingana na kuanzisha kampuni hewa za kuiba mabilioni ya walala hoi hadi tunakosa hata chanjo za watoto wasi na hatia yoyote. Ukiyapata yaweke tuyajadili hapa JF kam ulivyoleta hili
 
Tuna hakika na hizi kweli maana zile za Mengi tunakubali kwani ni dhahiri na wazi kuwa ametengana na mama Rodney na amekuwa na Mnyalu Ritta ;sasa hili faili la mbowe mbona liko swam swam
 
Labda mama Lwakatare mbunge mtarajiwa hatuna evidence zake za hili eneo!!

Tafuta yanayolingana na kuanzisha kampuni hewa za kuiba mabilioni ya walala hoi hadi tunakosa hata chanjo za watoto wasi na hatia yoyote. Ukiyapata yaweke tuyajadili hapa JF kam ulivyoleta hili
Tunachotaka ni maboresho ya kiushahidi ktk shutuma hizo
 
Ama kweli kupambana na mafisadi kunahitaji kuwa na moyo wa chuma.

Nani anataka kuamini kuwa ujumbe huo umeandikwa na wanachadema?

Naona hoja za ufisadi zimekuwa nzitto kiasi kwamba hawa jamaa sasa wanafanya character assasination na watakia kazi njema ila tunahitaji majibu juu ya ufisadi .

Huyu Mbowe ambaye mahakama haimkamati amekuwa mkapa?ama analindwa na katiba ?

Haya kazi kwelikweli naam kumekucha , na mafisadi na vibaraka wao hawana pa kwenda kwa wakati huu ila ni mpambano mapka kieleweke.

Nahitaji ushahidi wa maneno mazito kama haya kwani huu sasa kama sio udaku basi ni udadaku....
 
Well mimi simfahamu Mbowe kibinafsi kama mwandishi anvyodai au anavyotaka ionekane. Na pia sio chadema na wala sijitokezi kutetea maovu kama yapo. Mwandishi huyu anajikanyaga kanyaga na ni dhahiri ana nia isiyo njema juu ya mwenyekiti wa chadema. Kama kweli yupo chadema na ana nia ya dhati ya chadema mpya, itapatikana mtandaoni? Nimejaribu kupambanua kwa maandishi mekundu kwenye huo waraka hapo chini (Please read).


Subject: Hatima Yetu: Tuchukue Hatua

From: Wana Mabadiliko Chadema [mailto:chademampya@gmail.com]
Sent: Monday, 29 October 2007 10:37 PM
To: chademampya@gmail.com
Subject: Hatima Yetu: Tuchukue Hatua

CCM wanasafisha Chama chao na sisi tusafishe chetu, tusibweteke na umaarufu binafsi wa baadhi ya viongozi wetu.

Hatua ya kwanza ni kumbadilisha Mwenyekiti Freeman Mbowe. Historia, rekodi na uchafu wa Mbowe huko nyuma utatupa wakati mgumu siku za usoni kwasababu atakuwa easy target wa mafisadi.

Kwanini nasema hivyo?

1. Mbowe ni mla rushwa na anashirikiana na wana-CCM kwa ajili ya maslahi yake. Mfano: Mgombea wetu wa Ubunge kule Singida Mjini alitoa malalamiko kwamba Mbowe hakumsimamisha na kumtambulisha kwenye mkutano wa kampeni Singida Mjini kama inavyotegemewa. Ukweli ni kwamba aliomba hongo kwa Mohammed Dewji, Mgombea wa CCM, na kupewa shilingi milioni 6 ili asifanye hivyo
(Hili lina ushahidi gani maana hata mwandishi angesema sh. milioni 10, 20, 30 nani atabisha au kukubali. Mimi binafsi siamini kama Mbowe ni that cheap na hata hivyo kampeni za huyo mgombea mbona mwandishi hasemi chadema au mbowe mwenyewe alitoa kiasi gani kwa hiyo kutokumsimamisha mtu kwamba ni rushwa ni tuhuma za kitoto maana hata Geita Kikwete alishindwa kumsimamisha mgombea Mabina kwani alikuwa akizomewa kila mahali, Mabina alishinda lakini).
Kwa wanaobisha wakatazame kanda ya video ya mkutano wetu pale Singida waone kama mgombea wetu alitambulishwa. La sivyo, Mbowe atoe maelezo kwenye Kamati Kuu.

2. Mbowe ana madeni mengi na hadi sasa anayo "arrest warrant" ya Mahakama Kuu kwa kushindwa kuwalipa wadeni wake na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu . Oda ya kukamatwa kwa Mbowe imetolewa tarehe 5 Desemba 2006 na Jaji Manento, kwa hukumu iliyosomwa na Jaji Rwakibarila tarehe 27 Oktoba 2006. Arrest Warrant ameandikiwa OCD wa Central na imesainiwa na Bwana Lyimo, Msajili wa Mahakama
(Mwandishi anatakiwa afahamu kuwa na madeni si kosa maana hata Tanzania yenyewe inadaiwa kinoma, hata mwandishi mwenyewe very likely anadaiwa pia. Hili la kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu mbona haliko substantiated, ni fedha ngapi, kwenye dili ipi na wakati gani? - Rekodi kuwa mahakama kuu au arrest warrant haimaanishi kwamba wewe ni mhalifu- mwandishi nina wasi wasi sana na uelewa wako na hii ni dalili tosha kwamba mwandishi ni kada wa CCM).
Hizi rekodi zote zipo Mahakama Kuu. Bahati yetu tuna Serikali ya hovyo ndio maana Mwenyekiti hajakamatwa mpaka leo kwasababu CCM wanaogopa wakimkamata itaonekana ni siasa lakini siku yoyote Mwenyekiti atakamatwa kwa uchafu wa biashara zake binafsi. Salama yetu ni kuachana naye ili tusije umbuka siku za usoni.

3. Mbowe anahusishwa na biashara za hovyo. Kwenye uchaguzi wa 2005 watu wa CCM waliweza kutumaliza kwa hoja kwamba tutakuwaje na Rais mwenye kilabu cha pombe na muziki ambacho ni makao makuu ya machangudoa na wauza unga. Mwenyekiti aamue kikutumikia Chama au kufanya biashara ya Billcanaz.
(Hivi mwandishi amesahau kwamba Bilicanas ni klabu halali kisheria na vile vile kwamba viongozi na wachangiaji wakuu wa cham sisiem ndio wamiliki wa klabu, baa zinazokesha na uchangudoa nchi nzima mfano mzuri ni Villa Mwanza, AIRPORT NIGHTPARK dAR, HATA cORNER BAR dAR - wELL SILINGANISHI ILA NAJARIBU KUPAMBANUA KWAMBA HIYO HOJA NI BUTU)

4. Mwenyekiti ana historia chafu ya ufuska na uasherati
( Pamoja na kwamba kimaadili siwezi kulitetea hili lakini nadhani hao mabosi wa mwandishi CCM ni mahiri sana kwenye haka kamchezo) .
Hili ni tatizo kwa maadili lakini ni tatizo zaidi kwa Mwenyekiti Mbowe kwasababu analeta hizi tabia kwenye kazi na kuleta mifarakano.Nitatoa mifano kadhaa:

amevunja ndoa ya Mbunge Grace Kiwelu ambaye alikuwa ameolewa na mtoto wa Mzee Ndesamburo anayeitwa Sindato. Mwenyekiti alikuwa na ujasiri wa kulala na Grace kwenye ziara za Kichama wakati Mzee Ndesamburo anaona kwa macho yake
(Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini hili Baba kuona kwa macho mwanawe akizini) .
Mzee Ndesa alilileta hili suala Kichama, rekodi zipo hadi leo, lakini Mbowe akawa anaendelea. Kesi ilifika mahakamani na talaka kutolewa.
(Mwandishi pale juu ametueleza majina ya majaji, tarehe za kesi lakini hapa anageneralize, in short taarifa imekaa kiudaku udaku)
Mwenyekiti alitia aibu katika ziara tuliyofanya Newala. Grace Kiwelu na Chiku Abwao walipigana usiku saa 7 kwenye nyumba tuliyofikia kwasababu kila mmoja alitaka kulala na Mbowe
(Hii pia imekaa kiudaku udaku mwandishi habari kama hizi ni za kiu, ijumaa, nk) .
Ugomvi ulikuwa mkubwa baadaye Chiku Abwao akafanikiwa kulala na Mbowe. Msafara ulipofika Nachingwea, Grace akawahi kuingia chumbani kwa Mbowe mapema, kwahiyo Chiku akafukuzwa. Ilikuwa ni fedheha kubwa kwa walioshuhudia. Kwa kifupi, kama tunataka kujenga Chama makini, huyu hatufai kama Mwenyekiti
(Hili nadhani ni suluhisho linalotolewa na mwandishi ambaye kama kweli yuko chadema na ana hamu na hiyo chadema mpya alipaswa kuliwakilisha kiofisi na ofisi ingepuuza basi alikuwa na haki ya kuwasilisha hoja hii mtandaoni akiwa na nakal ya barua kama ilivyotokea kwa mzee Butiku) .
Tunao viongozi wengi ambao hawana historia ya uchafu wa biashara na uchafu binafsi.

Mwenyekiti alipigana na kiongozi mwenzake wa Chama Kawe kwenye sherehe ya kikundi cha sanaa cha Chama kinachoitwa Malongo Sanaa Group kwasababu Mwenyekiti alimtaka msichana mmoja kwenye kikundi anayeitwa Subira Waziri (au Koku) ambaye ni bibi wa kiongozi huyo.
(Huu pia ni udaku daku maana tarehe, haitajwi, sherehe ilikuwa inahusu nini? viongozi wa chadema kwa nini walialikwa au kuhudhuria haisemwi pia)
Ugomvi huo ulikuwa mkubwa na Mwenyekiti alichaniwa shati, lakini alimpiga na kumuumiza kiongozi mwenzake. Kesho yake Mwenyekiti akaenda kwa Mzee Makani kuomba radhi na kutoa 300,000 kwa kiongozi mwenzake asiseme na kuchukua hatua.

Mwenyekiti pia amevunja ndoa ya Mwanamrisho Abama wa Zanzibar ambaye bado anaendelea naye mpaka leo. Pia ameingilia ndoa ya Sophia Khatau wa Lindi ambaye mume wake anafanya kazi TTCL. Pia alivuruga ndoa ya Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Hai anaitwa Helga.
(Hivi kwenye hii angesema pia amevunja ndoa ya mkurugenzi kahama, bosi wa wizara ya fedha nk how can it be proved. huu ni udaku otherwise they have to be well substantiated)
Kuna mengine mengi ambayo hayapaswi kusemwa hadharani lakini wao CCM wanayo (Wao sisiem au nyie sisiem- Hii inahitimisha kwamba si kweli maana hawa jama especially mtandao walivyokuwa mahiri kwa kuchafuana wasingelimwacha mbowe hivi hivi ile 2005, na after all hivi kumbe sisiem ina hako ka kitego ka udaku na kufuatilia maisha binafsi ya watu?) , rekodi zipo hata za ubakaji miaka ya 1980 na 1990 uliokuwa unafanywa na Mbowe na rafiki yake Dudley Mawala enzi hizo na wanangoja wakati muafaka tu
(Hivi upi ulikuwa wakati muafaka, na kama chama chenye serikali kinasubiri muda muafaka kumsema au kumuumbua mbakaji badala ya kumpeleka mahakamani hii ni hatari) .
Ni lazima sisi wenyewe tuchukue hatua kuwapreempt sasa.

Kwahiyo wanachama wenzetu, baadhi yetu sisi wa matawi ya Mikoa ya Ruvuma, Dar, Kigoma, Manyara, Shinyanga na Arusha tumeamua tuangalie mwelekeo wa mbele zaidi wa Chama chetu
(Mwandishi anathibitisha kwamba yeye ni mwoga na mpika majungu, kwa nini asijitokeze hadharani ndani ya vikao vya cahama kama hizi tuhuma zake ni za kweli?) .
Mnyika na Kabwe wanafanya kazi nzuri sana za kurecruit vijana wenzao wasomi kwenye Chama chetu. Wameanzisha mtandao wa vijana ambao una matumaini ya kutuvunia wanachama na viongozi wasomi makini kwa siku za usoni. Tusiache mtu mmoja atuvurugie hii future nzuri ya Chama chetu iliyo mbele yetu.

Wakati ni huu. Tunaweza kabisa kuwatoa mafisadi madarakani kama tutakuwa makini. MPAKA KIELEWEKE!
 
Kikubwa tuhuma zilizotolewa zijibiwe then waanze sasa kuchafua nafikiri huu ni udaku, mnaonaje wanaJF? Hakuna mwanachadema mwenye muda wa kushughulikia trivial issues km hizi na kuna makubwa ya usalama na uchumi wa taifa yanamngoja?

hawa watakuwa vibaraka wanajaribu kudestroy attention ya watu tuache mambo ya kimsingi tuendee mambo binafsi!! wanajaribu kuwaokoa mabosi wao kwa njia yoyote sasa!

wajibu ya BOT, Richmonduli, Buzwagi, Kampuni hewa etc tutawaelewa
 
Mapambano na mafisadi ni kazi inayohitaji moyo na kujituma na pia kukabidhi roho kwa Mungu.

Hawa wanafikia kuanzisha e mail za kufoji ili watu tuache kujadili uchaguzi mkuu wa ccm huko dodoma kesho kutwa na jinsi mafisadi wanavyoenda kukichukua chama kizima ,

Ole wako Tanzania maana kila mtu anakutenda na hata wenye nia safi kwa sababu ya njaa na kuogopa kupoteza kitumbua wako tayari kutetea maovu ili mradi watoto wao waende kusoma ulaya.

Vijana mliosoma kumbukeni kuwa vijana wenzenu waliokosa elimu wanahasira juu yenu kwani nyie ndio mnawatenga na kuanza kuwatetea mafisadi , jueni kuwa watakapoanza kudai haki zao hata nyionyi mtadaiwa .

Au hii inatokana na usalama wa taifa kuwekwa hadharani kuwa hata wao walilipwa milioni miambili nini? THINK THIS TOO.
 
Admin. naomba uchukue hatua...

Tufikie mahali tukubaliane kuwa mijadala inayohusu watu binafsi ianzie kiunoni kwenda juu, na mambo yote yanayohusu kiunoni kwenda chini ni mambo binafsi. mimi hainisaidii kusikia kua kiongozi fulani kalala na fulani, kiongozi fulani kavunja nyumba ya fulani.....

Tujadili mustakabali wa Taifa letu, mambo ya chumbani tusiyalete jamvini.

Hii character assassination ikiruhusiwa kuendelea, zitamwagwa hapa taarifa na zenye ushahidi 100% patakuwa hapatoshi.
 
Ni kweli kabisa wanataka kuondoa attention ya watu kwenye mambo muhimu ili watu wasahau kuwa nchi inaliwa na wachache walioko madarakani.
 
Mimi binafsi nadhani ni ishara nzuri, kumbukeni Republican party walivyomwandama Bill Clinton? Mpaka walitaka impeachment! Sasa mi nasema tukianza kuandika kesi za Mwungwana na wasichana aliowaharibu si list haitakuwa na mwisho? Nakumbuka hili suala lilipoibuliwa eti wanasisiem wakasema kwamba ni proof kwamba ni handsome boy, wakakimbilia kumfananisha na Bill Clinton. Sasa imekuaje ghafla wanaanza mudslinging kwa Mbowe. Wanaogopa sana! That's my view!
Hamna haja ya Mbowe kujibu kitu, mbona issue ya Slaa ilikufa kiaina! And if sisiem wants it that way, basi naomba kila mtu achangie kwa kueleza uchafu alioufanya mwungwana na marafiki zake, maana data ziko nyingi! Kweli hapatatosha nchi hii!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom