Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Wanabodi vipi? mbona kimya!

Please, naomba maoni maelekezo na mwongozo ktk kipande hicho kilichotangulia. Mnajua tena mwenzenu hapa natumia elimu dunia ya madarsa.
 
Mkandara,
Nipe muda, nitarudi. Nimekuwa nje ya kituo kwa siku kadhaa so I have some catching up to do.
 
Mkandara,
Nimeisoma post yako. Kwa hakika imenikuna kichwa. Unajua katika kuandika njia bora ni kuandika kana kwamba unazungumza. You did just that na umeeleweka. Wazee wetu walipopigania uhuru kuna vitu walikuwa wanapingana navyo. Mojawapo ilikuwa ni indignity. Ukoloni haukujali dignity ya Mwafrika. Kwa hakika they even called us subjects. Wazee wetu pia walipigana kupinga raslimali zetu kutumika kwa ajili na manufaa ya Malkia. Kodi, maliasisi zetu zote zilikuwa ni mali ya Empire. Hizo infrastructure zilizojengwa hazikujengwa kumwendeleza Mwafrika. Zilijengwa kurahisisha the exploitation of the territory. Nadhani hii ndiyo ilikuwa kero iliyowapa founding fathers dira ya kupambana na ukoloni.
Tulipopata uhuru tulijikuta tukiwa totally dependent on our former masters. Kuna wakati Mwalimu Nyerere alisema ili kwake kuweza kuzungumza na Kenneth Kaunda line za simu zilikuwa zikipitia London. Hakukuwa na direct connection kati ya Tanzania na Zambia. Kwa kiasi fulani Mwalimu alijaribu kupunguza hii dependency. Unakumbuka hata ile reli ya Tazara. World Bank na Western countries walishauri kuwa si viable. Ilichukua muda kwa Mwalimu kumshawishi Kaunda kwamba watafute msaada China. That is where we were coming from. Hatukutaka kutawaliwa na nchi za magharibi lakini mind set zetu zilikuwa "pro-western."
Mimi nilidhani kuwa hiki kizazi kipya cha uongozi, baada ya Nkrumah na Nyerere, wangechukua mazuri yote waliyotuachia founding fathers, especially sisi Tanzania, na kuyaendeleza na si kuzika kila kitu alichosimamia. Nakumbuka hata during the dying days of ujamaa Mwalimu always held that Mtanzania should be the first consideration when it comes to uwekezaji. Lakini nashangaa hii kasi ya kumkaribisha mgeni badala ya kutafuta njia za kuwawezesha Watanzania. Hata pale ambapo Watanzania wanaweza serikali imekimbilia kumkumbatia mgeni. Kuna hii kasumba kuwa mgeni (read mzungu) anaweza zaidi ya Mswahili. Sijui kama nimechangia ya kutosha kukupa changamoto ya kuendelea?
 
Mkandara,
Kwanza umeleta changamoto kwetu wote kufuatilia kwa ukaribu kuhusu hii mada yako.Nadhani inamuelekeo chanya katika kutukumbusha wajibu wetu Wananchi katika jamii tunayoishi chini ya kivuli Mama Tanzania.
Kiutawala:- Je, dhumuni hasa lilikuwa kumwondoa mtawala mlowezi na badala yake kumweka mzawa tukitumia falsafa inayofanana na nguvu ya milki iliyowekwa na mkoloni?
Hili halikuwa dhumuni kuu la waasisi wetu bali walikuwa na nia ya dhati yakutaka kujikomboa kutoka katika makucha ya wakoloni na kuleta ustawi wa kila mwananchi na Hawakuwa na falsafa inayofanana ya miliki iliyowekwa na ukoloni.Ndiyo maana Awamu ya kwanza chini ya mwalimu iliweka dira kwa mtazamo wa kila mwananchi aweze kupata Huduma Bora na mahitaji ya muhimu na Kuanzisha mfumo au itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea wakiamini kwamba huo ungeweza kuleta tija kwa kila mwananchi na kufaidi matunda ya kuwepo Uhuru kutoka kwa mkoloni na Wakimaanisha kuwa katika mahitaji ya muhimu Hakuna kitakachotolewa kwa masharti ya aina yeyote au kwa matabaka. Mwalimu alipochukua nchi alikuwa na wakati mgumu kwani Tanganyika wakati huo Haikuwa na wasomi wa kutosha kuweza kushika kila Idara nyeti na Ujinga,Adui Maradhi, Umasikini vilikidhiri na Fedha na mali nyingi zilikuwa Chini ya wageni.Hapa ndipo alipokuja na Fikra ya Kutaifisha mali zote na njia kuu za uchumi kuziweka mikononi mwa wananchi(Azimio la Arusha).
Nitaendelea nitakapopata wasaa Lakini unaweza ukaendelea kutupa vitu vyako! nasi kila tutakapopata muda basi tutachangia!
 
kaka Mkandara,

Nashukuru umeanza kuweka hoja zako. Lakini nashauri uzifungulie thread tofauti au ziweke kwenye lile thread ya "Tanzania tunayoitaka. Hii thread hapa ya "Mbowe vs Chifupa+CHADEMA..." Nadhani tuiache iwe na masuala yanayoshabihiana na hayo.

Bado nipo "Msamvu". Nikirejea mjini nitachangia kuhusu katiba na huu mjadala ulioufungua.

JJ
 
Eeh bwana we, Msamvu ndio wapi tena? Ni pale Morogoro au? Ee bwana kama ni pale umenikumbusha mbali mwenzako, nataka kuruka lakini kamba imenishika, duh! Pana nyama ya kuchoma nzuri pale na nanihi!
 
Mwanasiasa:

Naam, "Msamvu" is a figurative word i use to represent that I am in Morogoro.

Indeed, nikitoka hapa nitaelekea huko kupata nyama choma.

JJ
 
Jasusi na kazi ndio Kipimo cha Utu,
Shukrani nyingi sana kwa mchango wenu na hizi points zenu zote nimezitafutia sehemu ndani ya kipande hicho cha mwanzo kilichotangulia.

Wanabodi wenzangu,
Nachojaribu kufanya hapa ni kukusanya comprehensive vision, ideas na ushauri ili tuweze kuleta mabadiliko ya kifkra. Nina imani through normative thought process tunaweza kabisa kuzua Ideology mpya ya kiuchumi na kisiasa inayopingana na ile ya kisiasa peke yake.

Nasubiri bado mchango wa waungwana wengine. pia ikumbukwe kabla sijanzisha kipande cha pili. naomba mawazo hata kama yanapingana na maelezo yaliyotangulia maadam mchango huo utasaidia kuendeleza hii mada in a form of organized collection of ideas.
 
J.J Mnyika,
Maneno yako kweli lakini ndio nimekwisha potea! Labda tumwombe ADMIN arekebishe!

Nasubiri bado mawazo ya Admin na wengineo... pleaseeeee!
 
Mkandara hii ilinipita kidogo,

Ni kweli inabidi uitafutie mahala pake mahususi, naendelea kukusoma
 
Hapa ndipo alipokuja na Fikra ya Kutaifisha mali zote na njia kuu za uchumi kuziweka mikononi mwa wananchi(Azimio la Arusha).Tafadhali Nilikomea hapa jana endelea..........................................!
Hapa haswa ndipo tulipoingia katika itikadi na mfumo wa ujamaa kamili kama ilivyoanishwa katika misingi ya azimio la rushwa na kuweka bayana katika katiba ya Chama kimoja na ya Nchi kwa wakati huo kama ilivyokuwa vikishahabiana Chama na serikali katika uongozi na utendaji.Madhumuni ya mfumo huu yalikuwa mazuri tu kinadharia na vitendo Lakini watendaji wengi ambao Kielimu hawakuwa wamekamilika(yaani hawakuwa na elimu ya kutosheleza) walianza kupewa dhamana kuendesha Nchi kama watendaji kwa kushika nafasi mbalimbali za kiutendaji huku wakiongozwa na wasomi wachache kufikia malengo.Tukumbuke njia kuu zote za uchumi zilishikwa na serikali chini ya kivuli cha azimio la arusha ambalo ni msingi mama wa chama kuwaletea wananchi tija,maisha bora na usawa wa kumiliki ,serikali ambayo ndiyo iliongoza uchumi na mikakati yake ya kuukuza huo uchumi haikuwa na wasomi wa kutosha na kama hilo halitoshi wengi wao walipewa nyadhifa za kiutendaji ndani ya serikali na mashirika ya umma.Nyadhifa nyingi za kiutawala na uendeshaji wa mashirika ,mabenki na njia nyingi za uchumi yalikabidhiwa kwa watendaji kwa muelekeo wa kisiasa zaidi na si kitaaluma hata pale ambapo tulikuwa na watu wachache ambao kwa uchache wao huohuo kielimu wangeweza kuendesha vyema na kwa ufanisi taasisi hizi za kiuchumi. Pamoja na kilimo kuwa ndiyo tegemeo la pato la Taifa.Tuliimbishwa wimbo wa kilimo ni utu wa mgongo kidhana walikuwa sahihi lakini kiutekelezaji hakukuwa na mipango endelevu ya kukifanya kilimo kweli kuwa ndiyo uti wa mgongo au mhimili mkuu wa uchumi wetu.
 
Kazi ndio kipimo cha Utu,

Mada hii imehamishiwa tayari kule - Tanzania Tuitakayo.
 
Taarifa Ya Kuhudhunisha Kwa Wanabodi.

Mheshimiwa Mbowe Amepata Bahati Mbaya Ya Kufeli Mitihani Yake Miwili Kati Ya Minne.

Jee Wanabodi Tatizo Ni Nini? Au Kuchanganya Masomo Na Siasa? Kuna Kipindi Alitoroka Shule Jee Hilo Limechangia? Naomba Tumshauri Wataalam Kama Mwalimu Augustino Moshi Na Kichuguuu Tunaomba Baraka Zetu Kwa Kiongozi Wa Kitaifa Wa Chadema.

Au Mshika Mawili Moja Humponyoka? Najiuliza Sipati Jibu.

Anatia Huruma Mheshimiwa Mbowe. Kila Anayemtakia Heri Mheshimiwa Aje Na Idea Au Mtumieni Pole Kwenye Pm Kumfariji Kuwa Kuchanika Kwa Jamvi Sio Mwisho Wa Maongezi Kasema Choki Na Wana Twanga Pepeta.

Cha Muhimu Ni Kumfariji Mtanzania Mwenzetu. Mambo Ya Chuki Za Kisiasa Au Kikabila Hapa Si Mahala Pake. Aliyekumbwa Na Tatizo Ni Mtanzania Mwenzetu Naomba Tuweke Uzalendo Mbele.

Natanguliza Pole Yangu Kwa Mbowe Na Wanachadema Wote Bila Kuisahau Familia Yake Na Hasa Baba Mkwe Wake Mzee Mtei. Napenda Mkono Wangu Wa Pole Uwafikie Akina Lucy, Ndesamburo. Muhonga,zitto Kabwe Na Mnyika.

Najua Mko Katika Hali Ngumu Kipindi Hiki Basi Mtambue Chinga Niko Nanyi Na Hii Inadhihirisha Wazi Mimi Ni Rafiki Wa Kweli Ambaye Kipindi Cha Shida Niko Nanyi.

Naomba Mfute Subira Na Kumshauri Mheshimiwa Ashike Moja Kwa Wakati.na Ikifika July Atulie Na Asome Vizuri Atapasi Tu. Hakuna Uchawi Kwenye Kusoma Ni Msuli Tu Kama Anavyofanya Mwanasiasa.

Na Mwanasiasa Acha Kuwa Mchoyo Mshauri Na Mpe Mbinu Mheshimiwa Za Kusoma. Au Unataka Nae Aharibikiwe Kama Mnyika? Na Unajua Kila Kikao Cha Conservative Inabidi Apewe Mkalimani. Kuwa Na Huruma Mwanasiasa Kwa Mwenyekiti Wako.
 
This is real a big BS . Kufeli Mbowe ni wa kwanza ?Una uhakika kwamba kafeli ? je kafukuzwa chuo kwamba kafeli ?Mbona unaumia sana na personal life ya Mbowe ?
 
Natoa mkono wa pole kwa mheshimiwa Mbowe nakuhusia ukaze uzi kwani kuteleza si kuanguka. kilichotokea umeteleza tu haujaanguka. na kufanya kosa si koza bali kurudia kosa. tumia nafasi hiyo ya kurudia mitihani mwezi wa saba kufanya kweli.

pole mkuu ndio maisha. sijui niseme fungu la kukosa? kura za urais mheshimiwa umeanguka na masomo ndio hivyo tena.
 
Nungwi: upo ndugu yangu; vipi masomo yako ya pacific western university (PWU) yanaendeleaje?
 
Chinga:

Naona umerudi kimya kimya. Last time tulipoachana ulikuwa hujajibu hoja na maswali mengi sana niliyoonyesha toka kwenye post zako kwamba umemua kupotosha. Naona umerudi tena!

Kama kawaida umekuja na staili zile zile za Chinga na Mtalii na Mswahili. What I like in you is that you are good at provoking! Lakini mara nyingi unatumia hoja ambazo zikishajibiwa unalazimika kuingia mitini au walau kujifunika kwa viganja...

Umesema Mbowe anahitaji mkalimani kwenye vikao vya kimataifa..teh teh what a mockery, binafsi nimesafiri naye kwenye vikao kadhaa ya kimataifa..fluence yake katika lugha ya kiingereza is admirable. Nadhani wewe mwenyewe umeshawahi kumuona kwenye mahojiano ya vipindi vya Kiingereza hapa nyumbani z likes of Hamza Kasongo Hour- Je alikuwa akitumia mkalimani?

Kwa taarifa tu ni kwamba Mbowe yuko Hull na anaendelea na masomo yake kama kawaida........

Nadhani kuna mambo ya muhimu zaidi ya kujadili kuliko Mbowe na Mnyika! Nakushauri uijadili CHADEMA

JJ
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom