Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Februari:

Wapendwa,

Kama ilivyoada naomba niwatake radhi kwa kuogelea kwenye bahari ya ukimya. Nilikuwa nafuatilia mijadala inavyokwenda japo mara chache ingawa muda wa kutoa nami mawazo yangu ulikuwa kiduchu. Leo nimepita hapa kijiweni japo nidondoe machache.

Mara ya mwisho kuandika nilisema nikija nitaanza na family business, lakini naona DrWHO alinijia juu kuhusu swali lake la kama Mbowe ni realist au la na akasema mengi kuhusu CHADEMA na conservative.

Kwa upande mwingine ligi ya Mkandara na Eric kuhusu majimbo ilikuwa ndefu kweli kweli. Very critical, very informative!. Kwa hiyo nimeona nianzie na masuala haya.

Nikiri pia kwamba nimepitwa muda mrefu kwa hiyo sijasoma neno kwa neno. Nitachangia kwa ujumla na kama kuna suala mahususi litakuwa limesalia basi mnidokeze nalo nilijadili.

Mosi nianze kwa kutambua wote waliochangia hoja ya CHADEMA;REALISM na CONSERVATISM.

DrWHO:

Disemba 8; umehoji kwa nini kwenye website ya CHADEMA hakuna maelezo kuhusu uhusiano wa CHADEMA na conservative na republican-Si kila kitu kinawekwa kwenye tovuti; hivi umeona kwenye website ya taifa uhusiano wa Tanzania na kila nchi ambayo tuna uhusiano nayo? Nadhani hii haikuwa hoja ya muhimu. Cha msingi ni kuwa website imeeleeza mkakati wetu kuhusu mahusiano ya kimataifa nk. Hata hakuna sehemu inayoeleza uhusiano wetu na CUF etc. Unapaswa kujua CHADEMA ina uhusiano na vyama mbalimbali duniani.Nitajadili hili kidogo chini.

Mzee Es:

Disemba 9; umeuliza kwamba Je, Freeman anapata pesa kutoka ile charity ya blair. Jibu, ni hapana. Kuhusu conservative nitajadili chini.

DrWHO:

Disemba 9;Je, CHADEMA inauza nchi kwa waingereza mara ya tatu? Hapana, labda serikali ya CCM inayoendeshwa kwa misaada toka nje huku uingereza ikiwa ni mtoaji namba moja. Zaidi ya asilimia 95 ya bajeti ya CHADEMA inatokana na ruzuku na michango ya wanachama.

Jasusi ;

Disemba 9 : Does it mean CHADEMA will swallow the policies of conservative ? hapana, nitajadili hapa chini.

DrWhO:

Disemba 9; DrWHO; umesema CHADEMA haiko transparent. Hapana, CHADEMA imekuwa ikiweka uhusiano wake na vyama mbalimbali bayana. Tofauti na vyama vinavyoleta wageni wa nchi mbali na kufanya programu kwa siri. Sisi tumefikia mpaka hatua ya kusema wazi kwa vyombo vya habari tumepokea shilingi ngapi toka conservative kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya wagombea! Tumeweka wazi matumizi yetu ya kampeni. Mbona vyama vingine viko kimya mpaka leo?

Disemba 9; ndabita alifafanua mambo kadhaa sijui kama DrWHO uliyasoma. Yasome!

Mwanasiasa:

Disemba 9,thanks for clarifaction you sought from DrWHO


Ndabita;

Disemba 9; asante kwa mchango wako wa nyongeza

DrWHO:

Disemba 10; ni kweli CHADEMA ina uhusiano kamili na conservative lakini si kweli kwamba kwa sasa tuna uhusiano kamili na republican. Na ni ukweli ni kuwa hatujawahi kupokea hata senti moja mpaka sasa toka republican. Kwa hiyo chama hiki tukiondoe kabisa kwenye huu mjadala

Ni kweli alama ya torries/conservative sio tena ule mwenge kama wa CCM siku hizi-wana alama ya mti na rangi za kijani kama CCM!

Lakini uchambuzi wako hauna maana sana kwa conservative ya sasa-facts zipo tofauti sana: Soma conservative renewal!

(Lakini huu mjadala sio muhimu, why should we discuss a party in UK? Ni kama kuwa mwanachama wa Manchester na kuacha kushabikia Simba ya jirani kwako)

Umeuliza is the alliance based on ideology? Watu kadhaa humu wametoa maoni yao, nami nitatoa maoni yangu chini!(this is the principal question).


Tafiti then Jadili:

Disemba 10, nimependa uchambuzi wako. Kuna element kidogo za ukweli. Soma kitabu cha smelling the coffee kwenye www.lordashcroft.com utajua sababu ya wao kufanya walioyayafanya.

Umemtaja Ndesamburo kuwa ni SG wa CHADEMA. Umekosea, SG ni Dr Slaa.

Is CHADEMA a gentlemen club that no poor can benefit as you have said? Another ideological question, I will discuss!

Mwanasiasa:

Umesema uhusiano wa CHADEMA na conservative sio necessarily ideological. Nakubaliana nawe kiduchu!, Nitajadili.

Umesema pia kwamba trend duniani ni kuwa vyama vina-ideological bankruptcy. No, sikubaliani nawe. Labda Afrika, vyama kama CCM kwa kauli ya Mwanri aliyoitoa bungeni kuwa CCM haina itikadi kinachoendelea ni shughuli tu!. Vyama katika nchi zilizoendelea vina itikadi bado. But I agree with you kwamba kuna overlaps za policies sometimes!.

Conservative UK wameamua kuchukua NHS, na Education ambazo traditionally ni issue za labour lakini angalia watazitazama kwa sura gani na kutumia approach gani. Hivi karibuni watazindua content ya policies zao. Maana mwaka jana walizindua package tu. They differ.

Sweden chama cha conservative cha huko kimechukua dola, kinaitwa moderaterna-wakati wa kampeni walikuwa wanajiita wajamaa wapya; just because waliiteka policy ya afya; but angalia approach yao-tofauti, wao sio pro welfare-wamechochea huduma za afya kupatikana kwa upana zaidi kwa njia tofauti kwa mujibu wa itikadi yao! Ni habari ndefu. Anyway, tatizo la vyama vya Afrika vingi havina itikadi. CHADEMA tumejizatiti kuwa tofauti. Nitajadili.

Nimependa ulivyo-link mtazamo wa CHADEMA kuhusu ubinafsishaji na peoples power-hiyo ndio sera kuendana na itikadi/falsafa sasa!

DrWHO:

Disemba 10: Umezungumizia uhusiano wa tax cut na inflation! This is a sweet ideological debate. Tujadili nikishaweka bayana msimamo wa CHADEMA kiitikadi!

DrWHO:

Disemba 22, umenitaka tena ni clarify kuhusu uhusioano wa CHADEMA na conservative na kunitaka niseme kama Mbowe ni Realist au la. Nitajadili hapa chini. Dhima ya maswali haya umeirejea tena Disemba 23,24 na 26! Hongera kwa kushikilia jambo

Baada ya kutambua michango yao sasa nijadili hoja:

Is Freeman a realist?

Layman Swahili translation tells us realism is uhalisia hence realist is enye uhalisia. But according to philosophy REALISM (from Low ' Lat. realis, appertaining to res, things, as opposed to ideas and imaginations), a philosophical term used in two opposite senses. The older of these is the scholastic doctrine, traceable back to Socrates, that universals have a more "real" existence than things. Universals are, in scholastic language, ante res, in rebus and post res. Behind all numerous types of chairs there is in the mind the ideal chair of which particular chairs are mere copies. In the most extreme form realism denies that anything exists in any sense except universals. It is opposed to nominalism and conceptualism.

For the history of the doctrine, see Scholasticism. Realism in this sense has been called "an assertion of the rights of the subject" (cf. the Protagonean maxim, "Man is the measure of all things"). The modern application of the term is to the opposing doctrine that there is a reality apart from its presentation to consciousness. In this sense it is opposed to idealism, whether the purely subjective or that more comprehensive idealism which makes subject and object mutually interdependent. In its crude form it is known as "Natural" or "Naive" Realism. It appears, however, in more complex forms, e.g. as Ideal Realism (or Real Idealism), which combines epistemological idealism with realism in metaphysics.

Again, Kant distinguishes "empirical" realism, which maintains the existence of things in space independent of consciousness, from "transcendental" realism, which ascribes absolute reality to time and space. (thats why I did not want to give DrWHO a quick answer on this matter!!!!, its a big discourse). Simply, realism is commitment to independent of mind!.

I know the context in which DrWHO posed the question. Basically, idealism vs realism on issues such as Iraq war. Bushs camp is said to be realist. But my answer on Mbowe is far from this context.

I must submit before hand that there is no person on earth that is pure idealist or pure realist. It all depends on circumstance of someone or perception on the other who is judging the person in question!

As far as I know Mbowe is an idealist-he sees what some may not see, and I think majority of visionaries share this attribute. But sometimes he is a realist, especially when it comes to doing things. In any case, usually I dislike discussing personalities but sense DrWHO has pondered this question time and time again I have decided to share these few thoughts.
 
What is relationship between CHADEMA and conservative?

If it were mere operational affinity, the framing of the question would have sufficed but since central to it is an ideological discussion the framing of the question should have been what is the relationship between CHADEMA and conservatism?

Before giving my position, let me highlight a couple of issues:

1. The word conservatism has a lot of connotations and denotations just like the words KABURU, BEPARI and likes. And all this branding has been done during the ideological warfare worldwide. So what we are discussing now is being discussed elsewhere around the world.

2. CHADEMA has relations with various other parties apart from Conservative of UK such as the NPP of Ghana(ruling) and Hoyre of Norway. We are also in close contact with parties such as DP of Kenye, Liberal of Australia (ruling)..the list is long. Focusing this discussion on conservative party of UK lives a lot to be desired. But for the sake of satisfying the zeal of those who have raised the issue I will focus on the torries and zoom to other parties were important.

3. I am very disappointed that I had started a discussion on party ideologies early next last year before the beginning of this debate but it was not given a requisite attention. But once it has been put in the context of CHADEMA and conservative then it has become juicy!. My humble submission is we open another thread as well to discuss party ideologies of CCM, CUF etc…..the objective is eventual to have parties which are built and identified upon policies rather than mere personalities and events.

CHADEMA has bilateral relations with Conservative Party of UK just like various other parties. And this bilateral cooperation has been cherishes and Ndabita pointed out because the two parties belong to the same international alliance-the center, center right parties. This Union is called International Democratic Union and in Africa it is called Democratic Union of Africa.

These are parties which share some few similar values such as a freedom, individual responsibility and opportunity, enterprise and entrepreneurship, low taxation and small government. There are parties with a lot of diversities in terms of their background and policies but they are some few core values that are shared.

So is it an ideological relation- overall I must say YES. Because they are parties with ‘center, center right ideology', do the have the same ideology. NO. For instance while CHADEMA has a center ideology parties such as the conservative party of UK has a center right ideology. So the bottom line is –these parties have similar ideology, they have some few shared values.

Why is CHADEMA in this union? Have we decided to dance a tune we do not know? Are we a flag that is following the wind? The answer is no!. Our choices are deep rooted to the party origin and objectives, which has informed the philosophy and ideology and the later has made us realize that we have some shared values.

In order to understand let me raise some issues from the five minutes remarks a presented in a certain forum recently on ‘what makes us who we are', I quote:

Tanzania is located in eastern Africa with a population of over 35 million people with more than 120 tribes. Tanzania has landmarks such as Kilimanjaro Mountain, Ngorongoro crater, Lake Victoria and Zanzibar Islands. The country is endowed with diverse of natural resources including minerals and national parks.

Despite this the country is among the poorest country with more than half of the population living in less than a dollar a day.

Tanzania (then Tanganyika) obtained independence from United Kingdom in 1961(before the second world war it was under Germany colonialism) and formed a Union with Zanzibar in 1964 to form the United Republic of Tanzania.

In 1967 the country adopted socialist centralized economy through Arusha Declaration that promoted the policy of Ujamaa na Kujitegemea (Socialism and self reliance).

The first ten years recorded some success in terms of promoting equality, provision of services and development of some key sectors of the economy. But as times went by the system limited social and political values of personal freedoms and human rights. Various rights were limited/controlled such as freedom of speech, organization, free elections, freedom to organize effective opposition including in parliament, right to free and independent media and individual opportunity . Hence the country was driven to social and economic crisis.

Meanwhile, there were groups of people opposing this policies among of those leading critics of these policies that were pioneered by the sole party(CCM) was Mr. Edwin Mtei, the founder of CHADEMA. He had to resign as Minister of Finance during in the government of the Late president Nyerere after differing with him regarding state monetary control .Mtei was pro socially oriented market economy.

This internal pressures together with changes in the world politics such as the decline of socialism as evident by the fall of USSR forced the CCM regime to adopt multi party politics in 1992.


Origin of CHADEMA

CHADEMA is abbreviation and brand name for Chama cha Demokrasia na Maendeleo(a Swahili name which literally translates into Party for Democracy and Development).

CHADEMA was established in 1992 and permanently registered in 1993 as a political party in Tanzania.

CHADEMA was formed with a belief that democratic society provides individuals with conditions for political liberty, personal freedom and equality of opportunity under the rule of law.

The party was formed to promote a culture of pluralistic competition and socially oriented marked economy.

Values

CHADEMA has been guided by the following values:
• Socially oriented market economy that provides opportunities and encourages entrepreneurship/self initiatives
• Right of each individual nation to preserve identity and safe guard vital self interest
• The need for smaller yet effective government
• Greater personal freedom and human rights
• Morality, through supporting institutions such as family and the right of belief.
• Low taxation
• Open society where power is distributed among institutions


Evolution of CHADEMA

CHADEMA is a growing party that has recorded a double increase in both membership and the number of seats over the past elections although the overall opposition seems to be declining. CHADEMA has been able to distinguish itself and its policies in an environment where there are no clear policy and ideological distinctions among the other 18 registered political parties.

Despite these achievements the party had decided to undergo some changes in order to position itself better hence the Re-launched in August 2006.

These changes include:

• Promoting the party message and new party slogan :
The re-launch is branded TUMAINI JIPYA, "NEW HOPE", the party slogan that is currently used is MABADILIKO YA KWELI UHURU WA KWELI "REAL CHANGE, REAL FREEDOM".
• The constitution of the party has been amended to have effective structure from grass root and to enhance the party philosophy and ideology.

This includes values such as maintaining state secularism but promoting freedom of belief as a foundation for morality;

Promoting opportunity and ownership of resources among citizens as a means to promote freedom;

Improving the economy through available resources;

Promote patriotism and encourage the practicing of good and morally apt Tanzanian customs and traditions and


• Change of party flag to include two more colors hence representing better the tenets of the party.

Originally the party color was light blue (which represented justice). The party logo was in black to represent African continent and the philosophy of peoples' power.

The color White has been added to represent truth, transparency and accountability.

Color Red has been added to honor the heroes of the country who had waged resistance against the colonial rule of the Germans, these include Chief Mkwawa and all those who died during the Maji Maji war in 1905.

• Organizations for special social groups have been established: Women, Youth and Elderly councils are being established as semi autonomous/independent organizations of the party.

• Five years party program(strategic plan) has been adopted: This is being implemented focusing on re-registering member and recruit more members(new cards have been created); improving party organization and communication; reviewing party policies; conduct trainings particularly on party philosophy, ideology, policies and organization.

Conclusion:

1. Tanzania like most of the African countries is still under the reminisces of socialism and socialistic culture. Up to now the constitution of the country is maintaining that the country is following the policy of socialism and self reliance. Ideological differentiation are not evident among most of the parties, there is low personal initiative and the culture of competition.

2. However, the government under the ruling party CCM in actual sense is pursuing open market policy that is very dependent on foreign countries at the expense of increasing grand corruption, unemployment, decline of social services and poverty. The ruling party being the state party is also using various means to suppress the opposition.

3. Meanwhile, CHADEMA is working to position itself and promote the philosophy of people' power and center ideology in Tanzania. The focus is to make the party philosophy, ideologies and policies known to the people, be able to provide alternative positions and leadership and promote FREEDOM and UNITY in DIVERSITY." End of the quote.

English is boring! Although DrWHO has directed his questions in English, let me now shift to the language I am comfortable with.
 
Sasa huu ni mwelekeo wa CHADEMA toka awali. Na hata ukiangalia sera zetu wakati wa uchaguzi zilijikita katika maeneo hayo. Pamoja na kuwa vipaumbele vilikuwa mfumo mpya wa utawala(ikiwemo sera ya majimbo); elimu, kilimo, uchumi, afya na vita dhidi ya rushwa utaona kuwa ndani yake masuala tuliyokuwa tukiyajadili yalikuwa yanatokana na misingi hiyo ya asili ya chama.

Taja ahadi na kauli zetu katika kampeni na nitakuonyesha zimetokanaje na misingi hiyo.

Kwa hiyo hatuwezi kuwa dictated to sera za conservative ama chama kingine chochote. Tunakwenda kwa kadiri ya misingi ya chama; visheni ya viongozi na nini ambacho wananchi wanataka(katika muktadha wa misingi yetu kama chama).

Mtakumbuka kwamba mwaka 2003-2004 palifanyika mabadiliko ya katiba ya chama na ndani ya chama falsafa na itikadi ya chama ikabainishwa kuwa ni " Nguvu na mamlaka ya umma" na chama kikafafanua kuwa:

FALSAFA YA CHADEMA:

1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.

2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.

3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.

4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.

5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi.

Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.

6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.

7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.

8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

Kwa kweli ukiisoma hii falsafa inafanana kidogo na ujamaa ama ukomonisti. La hasha!. Tofauti hapa ni tafsiri ya neno UMMA. Wakomunisti na wajamaa kwao umma ni dola mbele ya wananchi na dola kuwa na mamlaka zaidi. Lakini kwetu umma ndio wenye mamlaka zaidi. Kwa maneno mengi huku ni kuunganisha nguvu za watu binafsi binafsi.m Lakini suala moja ambalo liko wazi ni kuwa chini ya falsafa hii suala la KUJITEGEMEA liko bayana!

Hii ndiyo iliyotuongoza wakati tunaekea mabadiliko ya uongozi ndani ya chama yaliyomuingizia Freeman madarakani na hata harakati za mwanzo za kujenga chama ikiwemo marejeo ya sera. Hata ilani ya uchaguzi ilijengwa katika msingi huu. Wakati wa kampeni tuliposema falsafa na itikadi yetu ni "NGUVU YA UMMA" wengi mlitishambulia mkasema hiyo sio itikadi-ni falsafa ama kauli mbiu.

Uchaguzi ulipokwisha kama sehemu ya kuboresha zaidi mwelekeo wa Chama tukalijadili suala hili. Tukaona kuna hoja. Tukaunda kamati ya kuchambua kwa kina malengo/madhumuni ya chama, falsafa/itikadi na sera za chama na kutenganisha bayana falsafa na itikadi ya CHADEMA. Kamati ilikuwa chini ya uenyekiti wa Profesa Baregu, mimi nilikuwa katibu wa kamati.

Baada ya kuchambua kwa kina tukapendekeza kwa kamati kuu, baraza kuu na hatimaye mkutano mkuu ukapitisha na kuingiza kwenye katiba kutenganisha bayana falsafa na itikadi. Tumebaki na falsafa yetu ile ile ya nguvu ya umma kama ilivyohapo juu. Kwa kuchambua kwa kina malengo, sera nk, tuliamua kwamba CHADEMA ni chama cha mrengo wa kati kama inavyofafanuliwa hapa chini.


Itikadi ya CHADEMA

1. CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).
2. CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.

3. CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.

4. CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.

5. CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.

6. CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.

7. CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.

8. CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.

9. CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.

10. CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.

11. CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.

12. CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.

Hii haikuwa kazi rahisi katika chama chenye watu wa misimamo mbalimbali. Wako wa kushoto kama Profesa Baregu, wa kulia kama Mzee Mtei nk, lakini ‘tukakubaliana kukutana kati kati'. Hii inamaanisha nini-kila tunachokifanya kama chama, iwe ni sera ama matamko lazima isadifu falsafa na itikadi yetu.

Kwa mantiki hiyo basi thaathira ya conservative ama kundi lingine lolote itaenda sambamba na sisi kama tu inasadifu hii misingi yetu ama sivyo tutakuwa tofauti kabisa. Na huu ni ukweli, tunatofautiana na vyama vyetu rafiki katika masuala mengi.

Na hii ni wazi kwani hata nchi zetu zinatofautiana kihistoria,hali nk hata watu nao wanatofautina kwa kiasi kikubwa.

Lakini ukweli utaendelea kubaki pale pale kwamba CHADEMA ni chama ambacho kinajitegemea. Zaidi ya 95 ya bajeti ya chama kwa sasa inatokana na ruzuku na michango ya chama. Hawa wenzetu tukishirikiana nao wanaotoa michango kidogo tu hususani kwa ajili ya kuendesha mafunzo. Na tumedhamiria kupanua mtandao zaidi wa kimataifa na kuwa na ushirikiano na vyama vingine duniani. CHADEMA ni serikali inayosubiri.

Nawaomba pia mchambue ushirikiano kati ya CCM na vyama mbalimbali vya kijamaa duniani, ama CUF na vyama vya kiliberali duniani. Mtakuta kwamba ulimwengu wa siasa za kimataifa na diplomasia una madudu mengi sana ndani yake!. Cha msingi ni chama kuwa na misingi, uongozi makini/thabiti na mwelekeo.

Nimalizie hapa kwa leo kuhusu ushirikiano wa CHADEMA na conservative.
 
Kuhusu Sera ya Majimbo:

Kuhusu sera ya majimbo.

1.Narejea tena kuwashukuru Eric na Mkandara kwa mjadala wa kina kuhusu sera hii. Lakini nasikitika kuwa mjadala umenipotea kati kati ila kama kuna masuala mahususi ambayo natakiwa kuyazungumzia nitaomba mnirushie.

2. Chimbuko la sera ya majimbo ni falsafa ya CHADEMA ya nguvu ya umma. Kwa umma ndio unapaswa kuwa na mamlaka lakini pia umma ndio unapaswa kunufaika na raslimali za nchi.

4. Niweke pia bayana kwamba katika uchaguzi CHADEMA haikuwa na ajenda ya majimbo kama ajenda inayosimama peke yake. Ilikuwa ni sehemu ya ajenda nyingine. Tulisema wazi kwamba tatizo la CCM ni kuwa huwa inakuja na ilani ya kuahidi kila kitu na hatimaye kutofanya chochote. Sisi tulisema pamoja na kuwa na sera nyingi lakini tutakuwa na vipaumbele vitano tu: Moja; Mfumo Mpya wa Utawala; Pili; Elimu; Tatu; Kilimo; Nne; Uchumi Tano: Afya. Na hata katika vipaumbele hivi bado tulichagua maeneo machache mahususi mathalani katika uchumu tulilenga KODI(Kupunguza ukubwa wa kodi na kuhakikisha kuwa kodi zinakusanywa ipasavyo);

AJIRA na RASLIMALI hususani MADINI. Katika MFUMO MPYA WA UTAWALA: Hapa tulikuwa na masuala matatu- Mosi, Uongozi mpya kwa maana ya wananchi kuwaondoa viongozi walioko madarakani kwa maana wameshiriki ufisadi wa nyuma hivyo hawawezi kufanya mabadiliko yoyote ya maana; Pili; kusafisha mfumo wa utawala kwa maana ya kupambana na rushwa na ufisadi na Tatu; kutengeneza muundo mpya wa utawala ikiwemo kuanzisha muundo wa majimbo.

Lakini kwa kuwa suala la majimbo lilipata ladha zaidi na mashambulizi mengi SERA/AJENDA MAMA ya MFUMO MPYA WA UTAWALA ikafunikwa kabisa. Niliwahi kujadili wakati fulani kwa nini hali hii ilitokea, mnaweza kutazama kwenye michango yangu ya nyuma.

5. Kwa kuwa mmeshazoea kutumia neno sera ya majimbo nami katika mjadala huu nitatumia jina hili ili twende vizuri kwa pamoja. Suala la sera ya majimbo ni suala la kikatiba. Chama chochote cha siasa kinauza kwa wananchi matakwa yake kama kikipewa ridhaa na wananchi; matakwa hayo yanaweza kutokana na misingi ya chama husika ama matakwa wa wananchi ama matakwa ya viongozi wa chama husika.

Lakini baada ya uchaguzi zipo sera ambazo utekelezaji wake lazima urudi tena kwa wananchi kupata ridhaa ya pamoja mathalani CCM wamejikuta suala la mahamakama ya kadhi linapaswa kurudi kwa wananchi. Lakini mambo mengi chama hutekeleza kwa kwenda kwa wawakilishi wa wananchi yaani bunge.

Kadhalika, suala la kuunda kwa majimbo ni suala la mabadiliko ya katiba hivyo kwa vyovyote vile CHADEMA ingepaswa kurudi kwa wananchi. Hata ndani ya chama kwenyewe; misingi ya sera ilikubaliwa kwa pamoja lakini tafsiri ya kina kila mtu alikuwa anaifanya kwa mujibu wa mahali.

Kwa vyovyote vile, kama tungechukua dola tungepaswa kukubaliana kuhusu masuala kadhaa kwa ndani kabisa kabla ya kwenda kwa wananchi kuomba ridhaa. Je, hii ni ishara ya kutoifanyia kazi sera kwa undani? Hapana. Ni kawaida ya ilani ya uchaguzi.

Huwa inatoa ahadi ya ujumla. Mathalani; tutahakikisha kila mwanafunzi anapata nafasi ya kusoma shule ya msingi-suala la nani atafanya nini kutekeleza ahadi hii linakuwepo kwenye programu ya utekelezaji ambayo inaingia kwa kina kuweka mikikakati na shughuli mbalimbali.

6. Suala la sera ya majimbo sio geni duniani. Nchi kadhaa za Afrika zinafuata mfumo huu mathalani Afrika ya Kusini, Nigeria, DRC, Ethiopia nk. Ulaya nchi nyingi zinafuata mfumo huu. Marekani ya Kaskazini, Australia.

Kwa kweli dunia kwa ujumla wake inatambua umuhimu wa majimbo. Wengine wamekuwa na majimbo kutokana tofauti za kimbari /kinasaba(ethnic federalism); wengine ni sababu tu za kurahisisha utendaji(functional federalism) na wengine ni umbali tu wa kiographia(geographical federalism).

Kwa hiyo Eric na Mkandara kwa kuwa mmeamua kuchambua suala hili kwa kina chambueni pia ufiderali unafanyaje kazi katika nchi hizi. Faida na hasara zake. Ukiangalia hata muungano wa tanganyika na Zanzibar ni aina ya ufiderali ingawa ni ufiderali tenge!.

7. Kwa hiyo cha msingi hapa ni kuijadili misingi ya Sera ya majimbo ya CHADEMA na kuangalia ni vipi ni sehemu ya falsafa ya nguvu ya umma na kwa vipi inaendana na misingi ya CHADEMA, kwa vipi inaweza kusaidia utekelezaji wa sera za CHADEMA na kwa ujumla ni namna gani ni silaha ya nyongeza katika kukabiliana na ujinga, umaskini na maradhi.

8. Msingi wa kwanza: Kujenga uwezo wa kisiasa,uongozi na uwajibikaji: Sera ya majimbo inaelekeza taifa kuwa na viongozi wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi katika ngazi mbalimbali.

Hii ina maanisha kwamba kwa muktadha wa sera ya majimbo vyeo vya mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, katibu tarafa vitafutwa. Hawa uzoefu unaanyesha kwamba wamekuwa wakiongeza mzigo wa gharama kutokana na mwingiliano kati yao na wakurugenzi mathalani wa halmashauri ambao ni waatalamu wanaofanya kazi chini ya viongozi wa kuchaguliwa.

Uzoefu unaonyesha kwamba kwa kuwa mikono ya mhimili wa serikali ngazi ya chini viongozi hawa wamekuwa sababu ya serikali kuu kuingilia serikali zingine na kimaamuzi na kimwelekeo. Matokeo yake ni kuwa nchi nzima inaendeshwa na ikulu ya DSM hata katika mambo ya kawaida kabisa. Urasimu huu umukuwa kikwazo cha maendeleo.

Nguvu ambayo viongozi hawa wamepewa toka wakati wa muundo wa kikoloni wa kutawala kwa kutumia mawakala umewafanya wawe miungu watu na wananyanyasaji. Kwa kifupi ni watu wasiohitajika. Kwa upande mwingine, Sera ya majimbo inataka mameya wachaguliwa na wananchi moja kwa moja badala ya mabaraza ya madiwani ili kuongeza uwajibikaji. Kwa kifupi, msingi huu wa sera unachochea hamasa ya uongozi na kuweka viongozi wenye kuwajibika kwa watu. Hii ndiyo falsafa ya nguvu ya umma katika vitendo.

9. Msingi wa pili: Kushusha na kugawanya madaraka(devolving and separation of powers): Kwamba uzoefu unaonyesha kuwa majimbo yanapopewa madaraka nayo yanatoa madaraka kwa ngazi ya nchini yake na kuendelea mpaka chini. Serikali kuu inapohodhi mamlaka kadhalika ngazi za chini zinahodhi mamlaka ya ngazi za chini. Hoja inatolewa kwamba je kwa nini njia isingekuwa serikali huru za mitaa?

Hiyo ni njia moja lakini mandate ya serikali ya mtaa huwa katika maeneo machache tofauti na mfumo wa majimbo. Mfumo wa majimbo unahusisha ni masuala gani ambayo majimbo inaweza kuyashughulikia moja kwa moja kama ambavyo masuala yanavyogawanywa kwa misingi ya yale ya muungano na yasiyo ya muungano.

Lengo ni kuuifanya serikali ya fideresheni ishughulike na mambo machache na kila eneo lisimamie mambo yake kwa mujibu wa mazingira ya maeneo husika. Hii ndio nguvu ya umma!

10. Msingi wa tatu: Kupanua umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania na kuvunja dhana ya ukabila: Mfumo wa sasa wa kugawa wilaya umejikita katika kugawa wilaya kwa mujibu wa makabila-mfano rombo ya warombo, ukurewe ya wakerewe-mifano ni mingi kweli kweli.

Sera ya majimbo imelenga kuvunja mshikamano wa kiwilaya na badala yake kutengeneza fungamano la kimajimbo- mathalani jimbo la Kaskazini linajumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na tanga-hii ni jimbo la wamasai, wairaq, wabarabaig, wachaga, wapare, wabondei nk. Jimbo la Ziwa ni mikoa ya karagwe, Mara, Mwanza nk., hii ina maanisha wasukuma, wahaya, wakurya nk.

Lengo ni kutengeneza kizio(unit) mpya ya utambulisho chini ya Taifa(tanzania) yaani raia wa Jimbo Fulani na kufanya watu wajinasabishe kabisa na majimbo yao. Hii ni kwa sababu majimbo yanakuwa na upekee wake ambao mtu anapenda kujinasabisha nao. Mathalani jimbo moja linaweza kuwa na sheria za ajira zenye kuvutia zaidi n.Hii ndio nguvu ya umma!

11. Msingi wa nne: Kuweka utamaduni wa ushindani na upekeen ndani ya nchi: kama ambavyo nchi zinavyoshindana ndivyo ambavyo majimbo yenye taratibu tofauti za kibiashara, ajira, uwekezaji, makazi na kadhalika zitakavyoshindana.

Serikali ya majimbo inatoa mwanya ya majimbo kujiamulia mwelekeo wake katika masuala fulani fulani. Mathalani jimbo moja linaweza kupiga marufuku uvutaji sigara; majimbo mengine yanaweza kuiga ama yanaweza kutofuata. Hata katika michezo nakadhalika, ushindani utaongezeka maradufu.

Kila jimbo litataka kujifananisha na mafanikio fulani fulani. Dhana ya ushindani na upekee imeshindikana katika mazingira ya sasa ambapo kila halmashauri inaongozwa na maelekezo ya DSM na inajivunia mafanikio ya nchi kwa ujumla wake. Hata binadamu, ukipewa uhuru wa kujiamulia una uwezo wa kufanya vitu vya pekee zaidi kuliko ukiwa sehemu ya mfumo mpana. Hii ni saikolojia ya maendeleo.Hii ndio falsafa ya nguvu ya umma!

12. Msingi wa sita: Kupanua vyanzo vya mapato: pindi majimbo yanapopaswa kujitegemea kwa aina fulani moja kwa moja yanapaswa kuanza kutafuta njia za kujitegemea. Hii itasaidia vyanzo vya mapato kupatikana.Hii ni kutokana na kanuni ya mwitu(the law of the jungle).

Sasa hivi kila mahali wanaitazama DSM ikusanye pesa nchi nzima na kutoka kwa wahisani na kila eneo lina achama mdomo kwa ajili a kupokea! Wapinzani wa hoja hii wanaotoa hoja kwamba lipo jimbo ambalo halina raslimali na wanatolea mfano wa jimbo la kusini. Hawa ni watu ambao pengine hawajui kwamba tanzania ina raslimali kila mahali.

Wananchi wengi wamekuwa wakilalamika kuwa mikoa ya kusini haina maendeleo. Ukweli ni kwamba tafiti zinaonyesha mikoa ya kusini ina rasilimali na mali asili nyingi sana tatizo kubwa ni miundo mbinu. Jimbo la Pwani ya Kusini kwa mfano lina mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya za Kisarawe na Kibiti. Jimbo hili lina rasilima kama madini, bandari, uvuvi, nishati ya gesi,kilimo cha korosho, mikoko pamoja na utalii.

CHADEMA ina kil;a sababu ya kuwaeleza wananchi umuhimu wa majimbo kwani kila jimbo lina rasilimali za kutosha ila kwa kuwa serikali ya CCM imekuwa ikiwahadaa wananchi na kuwadhibiti ili wasijiletee maendeleo, imekuwa ikipinga vikali serikali ya majimbo. Hata kama kungekuwa hakuna maliasili: ukweli unabaki kwamba nchi duniani ambazo hazina maliasili lakini zimeneemeka kutokana na kutoa huduma tu!

Lakini kwa upande mwingine kama sehemu ya sera ya majimbo lipo pato ambalo litakusanywa serikali kuu na kusaidia katika maeneo ambayo yanamapungufu.
 
13. Msingi wa saba: Wanannchi kunufaika kutokana na matunda ya raslimali za eneo lao; Mfumo wa sasa ambapo raslimali zote zinamilikiwa na DSM unafanya wananchi wasinufaike na raslimali za maeneo yao kikamilifu.

Mathalani kodi za madini, mbuga za wanyama nk sehemu kubwa inakuja serikali kuu na ama kugawanywa katika mfumo ambao haunufanishi maeneo husika ama kutumika katika matumizi ya anasa ya serikali kuu. Mathalani pamoja na kuchimba madini yenye thamani Geita ni moja ya wilaya maskini kabisa. Wanaofaidi madini ya Geita wako DSM.

Serikali ya majimbo itakuwa na sehemu ya mamlaka ya ugawanyaji wa mapato yanayotoka katika eneo husika.Pamoja na kukusanya mapato ya pamoja ya serikali kuu. Hii ndio nguvu ya umma !

14. Msingi wa nane: Kupunguza ukubwa na gharama za uendeshaji wa serikali: Serikali ya majimbo haiongezi ngazi yoyote ya utendaji kwa kuwa inavunja ngazi ya mkoa(ambayo ni mikoa mingi zaidi takribani 26) na kutengeneza ngazi ya jimbo(majimbo ni machache 4 mpaka 8 kutegemea na makubaliano ya kikatiba).

Wakati huo huo ukubwa wa serikali kuu utapunguzwa kwa kuwa wizara zitabaki chache za mambo ya federesheni mathalani ulinzi, mambo ya nje, fedha. Wizara nyingine zote zinakuwa katika ngazi ya majimbo husika kwa mijibu wa utaratibu wa majimbo husika. Kutokana na ukaribu wa utoaji huduma na utendaji mwishowe gharama za utendaji zitakuwa ndogo kuliko DSM inavyoendesha nchi mzima katika kila jambo.

Mathalani utoaji wa passport, vibali vya elimu na mambo mengine mengi. Serikali ya majimbo itahakikisha mfumo wa utendaji unatukuwa mdogo kwa kujenga mifumo iliyokaribu zaidi. Hii ndio nguvu ya umma!

15. Msingi wa tisa: Muundo mpya unasaidia utekelezaji wa majukumu. Hapa ni mjadala wa kipi kinaanza muundo ama majukumu(stucture or function). Sera ya majimbo inachukua mtazamo wa kwamba yote yanakwenda pamoja.

Suala la Mkandara wakati wote limekuwa: tatizo la msingi la mwananchi ni hali mbaya ya maisha, kipato duni, uchumi mbovu, elimu duni nk. Na anachotaka mwananchi ni suluhisho la haya matatizo ya msingi sio porojo za sera ya majimbo. :Lakini ukweli ni kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja na kimatokeo baina ya masuala haya(Direct and causality relationship).

Kwa mfano, asili ya wananchi wa Geita kuwa na uchumi mbovu ni sera mbovu ya madini iliyopitishwa na DSM lakini pia mfumo mbovu wa mgawanyo wa mapato ulipitishwa na DSM. Pengine wananchi wa Geita na Jimbo lao wanajua zaidi ni ambacho wanataka; sehemu ya tiba ni kuwapa sehemu ya tiba ya kujiamulia mambo yao. Wajikaange kwa mafuta yao.

Tatizo la elimu pengine ni maagizo ya waziri toka DSM ambaye hajui kabisa hali ya Mwanza ni tofauti na Mtwara. Sasa hata elimu aamue waziri DSM? Tatizo la nchi yetu ni wananchi kukosa inititiative na umiliki. Ujinga, Umaskini, Maradhi ni matokeo tu, chanzo ni uongozi.

Kushughulikia mfumo na muundo wa uongozi/utawala ni sehemu ya suluhisho. Upo wasi wasi wa kufanya hivi kwamba kuna kutengeneza matabaka. Hata sasa matabaka katika nchi yetu yapo, tena mabaya zaidi. Maana haya ni ya mtu na mtu. Afadhali utofauti wa kisera kati ya jimbo na jimbo kuliko mtu na jirani yako!.

Kuna hofu kwamba yapo majimbo yatakayojitenga. Katika muundo wa Tanzania ya sasa jimbo lenye makabila mbalimbali haliwezi kujitenga ilihali jeshi, mambo ya nje na masuala kadhaa nyeti yako kwenye kapu moja. Huku ni kuhofia kivuli!

Haya ni maoni yangu kwa leo, rusheni maswahali mahususi-nitarejea siku nyingine..

JJ
 
J.j Mnyika,

Nimesoma maelezo yako kwa kina na bahati mbaya hapa pia nimemaliza kusoma yote bila kupata jibu la waswali yangu yote. Kifupi nimejikuta kila mara nikieleza zaidi ya nyie mnaotakiwa kujibu.

Nimekubali sana kipengele ambacho umesema swala hili lazima lingerudi kwa wananchi kupata mawazo yao na nadhani hapa mimi nachokifanya ni kuwakilisha mawazo ya wale wanaopinga Majimbo.

1. Sii kweli kabisa kuwa majimbo mengi yameundwa kwa sababu ulizozitaja hapo juu ila moja na linalofahamika zaidi ni KUJENGA UMOJA -yaani kuunganisha nchi zilizokuwa huru kuzifanya nchi moja na Majimbo yametumika kama mipaka ya kutambua na kuheshimu sovereignty iliyotangulia Ufederali.

Nitarudia kusema sijaona nchi hata moja iliyojenga Majimbo baada ya kujitangaza wao kuwa huru na bado kukawepo na Amani kati ya Majimbo haya maanake majimbo haya yametokana na tofauti zao za kikabila, kidini ama ubaguzi wa aina yoyote ile.

Hivyo basi swali langu bado linabaki pale oale WHY? sisi tuwe mfano wa mgawano huo ambao hakuna kati yetu anafahamu hatima yake wala hakuna mfano wa kuigwa.

Jambo jingine ni hilo la kupunguza mikoa... nitarudia kusema hata kama leo hii tuna mikoa 26 na tuseme wilaya 200, ndani ya Miajimbo bado tutakuwa na wilaya 200 kwa sababu mikoa yote ni jina tu, kila mkoa ni wilaya vilevile. Kinachobadilika hapa ni ramani sio utendaji kazi.

Mkoa wa Dar-es Salaam una wilaya tatu, Ilala, Temeke na Kinondoni hizi bado zitabaki wilaya ila kinachoondoka hapa ni neno mkoa wa Dar-Es Salaam ambao huduma zake zipo wilaya ya Ilala. Hapa tunaondoa Ma - RC 26 tu, lakini wilaya na wards zitabaki idadi ile ile na zote zitahitaji viongozi.

Utitiri wa viongozi utazidi ktk majimbo kwa sababu mbali na wilaya kuwa na viongozi wake kila jimbo litakuwa na wizara zake iwe 10 ama 20 lakini kwa kifupi kutakuwepo na wizara zisizopungua 100 ktk nchi nzima (majimbo na federali) na kila jimbo litakuwa na bunge lake kuweza kupanga miundo yao ya kiuchumi. Umewaondoa Rc 26 na kuweka viongozi wengine 200.

Nimeshindwa kumwelewa Eric aliposema Wabunge waliochaguliwa watakuwa ktk bunge la taifa sasa hapa sielewi majimbo yataweza vipi kupanga bajeti yake ikiwa wabunge wake hawatahusishwa kimajimbo pekee. Hii ina maana bado majimbo yatategemea serikali kuu (federal) kupanga bajeti zao jambo ambalo halina tofauti kabisa na kutegemea Dar isipokuwa sasa tutategemea Dodoma.

Sioni tofauti ya swala la majimbo na lile la serikali Tatu ikiwa lengo ni kupunguza utitiri wa viongozi. Zanzibar ina wizara zake, bara nayo itakuwa na wizara zake 26 au less kisha kutakuwepo na wizara za serikali kuu - Federali sijui ishirini na ngapi.. ukiweka jumla utapata utitiri wa viongozi zaidi kuliko hivi tulivyo sasa.

Muhimu na mwisho, nachopinga mimi kuhusu majimbo ni hiyo theory behind it!

Mnyika, my all point is this:-
Timu yetu ya soccer Tanzania ni nzuri sana lakini tuna tatizo moja kubwa, Uongozi...Uongozi ambao unatufanya kila siku tusipate kwenda mbele ktk ligi hali quality zote zipo.

Tumekubali kufanya marekebisho ndani ya Uongozi -jambo zuri sana na kila mtu analiafiki...
Tatizo langu ni pale sisi tunapoamua kuongeza ama kupunguza Ukubwa wa goli ama kiwanja ili kurahisisha/kupunguza ufungaji wa magoli.

Hapa nasema ikiwa mnataka kurekebisha goli basi kuna uwezekano kuwa kosa sio la Utawala uliopo ila ukubwa wa goli. Na Utawala uliopo unaweza kusema kama goli lingekuwa na ukubwa huo siku za nyuma hata sisi tungeweza kuipeleka timu mbele...
Pili, swala la kuongeza ukubwa wa goli sio swala la timu moja, hili ni swala la ligi ya taifa zima.

UAMUZI sio wetu hata kidogo na kwa sababu ni swala la kitaifa lazima kuwepo na muafaka toka vyama vyote kwa sababu hatuwezi leo kuwa na majimbo chini ya Chadema , kesho wakichukua CUF ama CCM waondoe Majimbo.

Na tatu, lazima tukumbuke kuwa upo uwezekano mkubwa kuzua madhara mengine zaidi kwetu sisi wenyewe. Kupunguza/kuongeza kwa goli kunaweza kuwa ni advantage kwa timu nyinginezo hali sisi tumetazama mapungufu yetu ktk kupata ushindi (Offense) kurekebisha goli bila kufahamu nasi tuna goli ambalo linaweza kufungwa na wapinzani (defence).

Badala yake turekebishe viongozi na mipaka yao ya utawala kisha wachezaji na mipaka yao ya kulisukuma ndinga.

Hakuna asiyekubali kuwa viongozi wa CCM sii wajuzi wa mpira na wachezaji wengi bora wako bench, CCM leo hii hawana formation wala mpangilio mzuri. Goalkeeper mara kenda piga kona akiacha goli wazi. haya ndiyo marekebisho tunayoyataka wanamchi sio kurekebisha goli na wala sidhani kama ni kazi ya timu (Chama).
 
  • Thanks
Reactions: amu
Kaka,

Mosi, sijasema kwamba hiyo misingi tisa ni misingi ya ufiderali duniani. Nimesema hii ni misingi ya ufiderali ambao CHADEMA inapendekeza kwenye sera yake. Kwa maneno mengine, ipo ambayo ipo nchi nyingine na ipo ambayo haitumiki kwingine.Kumbuka nilisema awali kuwa wetu ni ufiderali wa kiutendaji(functional federalism). sio wa kimbari(ethnic federalism). Hivyo hii misingi ni yetu.

Pili; umesema kwamba hakuna nchi zote zimeunda ufiderali kwa kuunganisha sovereignities kuwa dola moja. Hapa napo sikubaliani nawe- hivi nchi kama Majimbo ya Afrika ya Kusini yalikuwa ni nchi zinazojitegemea. Je majimbo yote ya Nigeria yalikuwa ni nchi zinazojitegemea kabla? ethiopia je? Mifano iko mingi duniani. Nakuomba ufanye uchambuzi kwa kina kuhusu hili. Nami nitakupa uchambuzi wangu.

tatu, umesema kwamba ufiderali unaongeza idadi ya wizara kwa kufanya replication. Hebu soma tena mchango wangu utabaini kwamba ngazi ya federation inakuwa na wizara chache za mambo ya federation. Wizara nyingine zinakuwa katika maeneo husika kwa mujibu wa vipaumbele vya eneo husika. Zanzibar si mfano mzuri wa federation, as I said Muungano wetu ni ufiderali tenge ambao una matatizo mengi sana.

Nne; umesema tatizo la msingi ni uongozi. Hapa nakubaliana nawe, ndio maana nilianza kwa kukwambia kwamba sera hapa ni mfumo mpya wa utawala; ambayo ina aspect tatu: uongozi mpya(nakubaliana nawe 100%); utawala safi(vita dhidi ya ufisadi) na muundo mpya wa utawala(ufiderali-hapa ndipo tunapotofautiana. Unapaswa kujua uongozi haupaswi kuwa empty container-pamoja na falsafa ya nguvu ya umma, tunadhani kwamba muundo mwafaka wa utawala ni zana muhimu ya kutimiza ajenda tunazozisimamia!Hili ni suala la kikatiba sasa. Ndio maana nataka tuendelee kujadiliana.

tano; umetumia mfano mzuri wa kiwanja na magoli. Nahitaji kuutafakari kwanza, lakini just food for thought-kama je tulikuwa tumepelekwa kwenye kiwanja ambacho hakina vipimo sahihi? Katiba yetu na mfumo mzima wa utawala una matatizo ya msingi. This we have to admit tutofautiane tu katika kujadili ni katiba gani mpya tunaitaka!

Bottom line, Nakubalina nawe suala moja kwamba tatizo la Msingi ni UONGOZI, the rest will follow-but what we are saying is, at least we should give indication on how its is to follow!

otherwise, tutaweka uongozi mpya halafu ndio tutaanza kujiuliza. For what?

Endeleeni kuchangia kwanza!

JJ
 
JJ, mchango wako umeshiba

Naendelea kutafakari ili ntoe mchango wenye afya zaidi juu ya sera ya majimbo.

Kazi nzuri sana.
 
hali Zenu Ndugu Zangu Na Wana Forum,

Kwa Wale Wa Mahsariki Ya Mbali , Nafikiri Ni Usiku Na Kwa Wale Wa Marekani Kama Sintokosea Ndiyo Mnaamka. Mimi Nina Langu Jambo Nataka Weka Sawa.

Kaka Mnyika , Amezungumza Mengi Lakini Nataka Nikuambie Kitu Nafikiri Kitakusaidia Kwa Siku Za Usoni. Jambo Forum Sio Jukwaa Au Bunge Ambalo Utaanza Kwa Kushukuru Kila Mtu Hata Mpishi Wako Nyumbani.sio Ukumbi Wa Siasa Kama Wanavyofanya Wakina Jakaya,mbowe Na Wengineo Nawe Sidhani Kama Hupo!

Kwa Nini Nasema Hivyo......kaka Umeandika Vitu Vingi Sana Kiasi Kwamba Mimi Kama Mmoja Kati Ya Wale Wafanyakazi Nafikiri Sintokuwa Na Muda Wa Kuyasoma Yote. Na Ninavyoendelea Kuacha Kiporo Yanazidi Ongezeka.

Tunaipenda Jambo Forum Kwa Hoja Zenu Na Pia Tuanendelea Kuandika Ili Kuleta Ufahamu Wa Mambo. Umeandika Vitu Vingi Labda Nikuambia Vya Hoja Lakini Umebore Kwa Kutojua Nini Unaandika Na Wakina Nani Unawaandikia.

Am Sorry Kukuambia , Weka Internet Nyumbani Au Jiunge Kwenye Zile Wireless Service Za Zantel Ili Uweze Kuandika Kila Unapojisikia. Tuna Mambo Ya Kufanya Na Sio Kusoma Maandishi Yako.

Nb: Tafuta Nafasi Gazeti La Rai.
 
Maneno,

Samahani kwa kukuchosha na maandishi marefu. Niliulizwa maswali kwa muda wa miezi kadhaa nilikuwa sijayajibu hivyo ilibidi nianze kwa kukumbusha nani aliuliza nini.

Kama ningejibu mapema kama ninavyokujibu wewe hivi sasa nisingeandika maandiko marefu hivyo.

Nakushauri uyanakili(copy) na kuyahifadhi mahali uyasome ukiwa likizo.

Nitazingatia ushauri wako wa kuandika mara kwa mara ingawa inakuwa ngumu sana hasa ninapokuwa DSM kutokana na mazingira ya kazi zangu.

Hata hivyo usiwasemee watu wote kwa kuwa wapo wanaopenda michango mirefu na ya kina. Kama watu kama Mtanzania wanataka kitabu kizima cha Ndesa kiwekwe hapa wakisome itakuwa huu mchango wangu wa kurasa kadhaa!

lakini naheshimu mchango wako kwamba niangalie targets-ikiwemo watu kama wewe msiokuwa na muda wa kusoma maandiko marefu.

Changamoto ni jinsi ya kuwianisha(balancing) kati ya maswali yanayoambana na hoja ndefu kama yanavyoandikwa na Mkandara na Ongara na haja ya kujibu kwa ufupi kama anavyohitaji Maneno.

Umenishauri nitafute nafasi RAI. Rai imepoteza uhuru wake, mara kadhaa nimepeleka maandiko yangu wameepa kuyachapa.

Mahali pekee tunapoweza kuandika kwa uhuru ni kama hapa. JF kwa sasa ni moja ya vyombo vya habari huru kabisa Tanzania.

cha muhimu ni kuwafanya wasomaji wa RAI waje hapa, na kutafuta jinsi ya kuwafikia wasomajiwa RAI walioko katika maeneo ambayo hakuna internet.

JJ
 
Nb: Tafuta Nafasi Gazeti La Rai.

Kaka/Dada Maneno,

Si kila mmoja anaweza kulipata RAI. Lingekuwa linapatikana Online ingekuwa rahisi kwa sisi tusio Tanzania kuweza kulisoma. Aidha anachoandika Mnyika na wengineo (wanasiasa) ni kitu muhimu sana na kama umefuatilia vema wengine badala ya kuhangaika kutafuta alichosema FLANI wanafika hapa wananakili (copy and paste) tatizo hawaweke source.

Nadhani mtandao ni sehemu moja huru sana na ambayo mtanzania yeyote anaweza kuweka wazi mawazo yake, sera zake n.k.

Tatizo kama ni muda wa wewe kusoma kilichoandikwa nakushauri uangalie kwenye Archives au pale chini kwenye Kabrasha letu utakuta mada za siku nyingi ziko packed.

Mheshimiwa Mnyika; nakushukuru kwa michango yako ya kila mara. Aidha nakutakia uchangiaji mwema wa makala/mijadala mbalimbali inayoendelea hapa JamboForums.com.

Kumradhi members; sikuwa hewani kwa muda kutokana na matatizo ya mtandao niliko.

Mbaki salama
 
Bwana utawala wa JF:

Nashukuru.

Ila kuna kitu kimoja nime-note chini ya jina langu sasa kuna maneno "Expert from CHADEMA". Naomba yaondoke, yananikwaza na kunitweza!

Nilikuwa junior member, nikiwa member-nadhani kama ni kupandishwa daraja basi niwe senior member!. Mimi sio Expert from CHADEMA!

Tuendelee kujadili hoja na kuitangaza JF...

Inawezekana kila mmoja akitimiza wajibu wake.

JJ
 
ndugu watanzania,
kwa mtazamo wangu, ili tuweze kupata maendeleo ya kweli tunahitaji kuwa na characteristic fulani ambazo ni "uncomprimise".

we need to set goals and to explore ways/methods to archieve those goals.
once those goals are set and the best method/way is determined,in other words after we have our road map, we need to be commited on following the road map, day by day, our by our and second by second.

there is no doubt that there will be challenges, which will shift our attention toward archieving that success, therefore everytime we need to review our plan and stay focused, we shold never comprise or give any excuse to justfy failures.

kwanini nimeanza na hayo maneno hapo juu?
ni baada ya kusoma maandishi ya ndugu maneno aliyoyaelekeza kwa kijana john mnyika.
nimekuwa nikiobserve kwa makini sana jinsi gani watu wanavyojibu hoja humu ndani na kwa kweli hii ina reflect the charachteristics of majority of tanzanians

WE ARE NOT SERIOUS PEOPLE, WE ARE NOT SERIOUS IN ANYTHING,
EVEN IN THING WHICH CONCERNS OUR LIVES AND THIS IS DANGEROUS!!
ANY SOCIETY WHICH IS NOT SERIOUSLY CONCERNING WITH ITS OWN WELL BEING IS A DOOMED SOCIETY.

THE QUESTION IS BEING ASKED AGAIN AND AGAIN IS
WHY IS THIS COUTRY POOR? WHY AFRICANS CANT DO THIS, WHY THEY CANT DO THAT?
WHY AFRICANS ARE FREEING THEIR BEUTIFULL CONTINENT AND MOVING TO THE WEST WORKING AS SLAVES!!

FOR US WHO ARE LIVING IN WESTERN COUNTRIES HAVE ALREADY A CLUE WHY OUR FELLOWS ARE GETTING DEVELOPED,
IT IS BECAUSE THEY ARE SERIOUS, THEY ARE VERY SERIOUS AND COMMITTED TO THEIR WELL BEING AND THEY ARE WOKRING HARD TO ARCHIEVE THEIR GOALS.

kijana mnyika amejitahidi sana kujibu hoja za watu, pamoja na muda mdogo aliokuwa nao lakini inaonekana watu wanania ya kumkatisha tamaa, mara ohh hujajibu hoja, mara ohh wewe hauko huku, mara huko kule, hii yote inaonyesha watu hatupo serious,
mimi kwa upande wangu naona mnyika amejitahidi na amejibu kwa nyongeza au zaidi ya matarajio, ukiacha hiyo kuna links ambazo mnyika alitoa zilikuwa zina majibu mengi na mimi nilisoma makara moja aliyoileta hapa ya mtei ilikuwa na majibu mengi sana ya watu waliyouliza,
sasa samahani kama mtanielewa vibaya ila nilianza kueleza kuwa matatizo ya msingi ya watanzania wenyewe,narudia tena kusema KWA UCHUNGU SANA;

WE ARE NOT SERIOUS PEOPLE, WHILE AOUR FELLOWS TANZANIANS ARE DYING IN THE HOSPITALS BECAUSE THERE IS NO DOCTORS,EQUIPMENT, AND MEDICINES; ONE TANZANIAN CAN TAKE 12MUSD KWENYE ACCOUNT YAKE NA MPAKA WATU WA NJE WASEME NDIO NA SISI TUNAAMKA,

WAKATI VIJANA WETU WA MLIMANI WANAKOSA PESA YA KUSOMA SHULE,SERIKALI INA INGIA KWENYE ANASA NA MIKAKATABA KUNUNUA VITU VISIVYO NA KIPAUMBELE NA KICHWA WALA MIGUU;

BUT I AM CRYING FOR MY COUTRY AND I AM CRYING FOR THE SUFFERRING OF TANZANIAN PEOPLE WHO WE KNOW THEY ARE CAPABLE PEOPLE BUT BECAUSE OF THE ACTION OF THE FEW WHICH HAS HINDER THE CAPABLE PEOPLE TO TAKE THE AUTHORITY AND LEAD THIS COUTRY IN THE RIGHT DIRECTION.
 
J.J Mnyika,

Shukran sana tena sana kwa kunipa hoja nzito ambazo zimenichukua muda mrefu sana kuzieleza huko nyuma. Labda kwa kifupi nitasema nakubali neno lako la mwisho hasa pale uliposema;-

Bottom line, Nakubalina nawe suala moja kwamba tatizo la Msingi ni UONGOZI, the rest will follow-but what we are saying is, at least we should give indication on how its is to follow!

Kisha nakuomba sana unielewe kuwa nakuwa mbishi wa hoja kulingana na jinsi Watanzania wengine watakavyo utazama huu mfumo na ichukulieni nafasi hii kutufahamusha zaidi maanake hili sii swala dogo hata kidogo kama wengi wanavyofikiria. najaribu kufikiria kila angle ya swala zima na wapi kuna penyo za mapungufu. It's up to you guys to fill up!

Tuendelee,
Ndugu Mnyika nadhani huko nyuma hukusoma maelezo yangu kwa nchi ambazo mnataka kuzichukulia mfano. Na siku zote nasema tusifanye kitu kwa kuiga ila kwa sababu zetu - For what?
Kila nchi imeyafanya majimbo yake kwa sababu zake na muhimu ambazo zimefanikiwa sana ni zile zilizoungana majimbo kuleta UMOJA. wa nchi moja chini ya seruikali kuu (Federali).

The most improtant question kwetu kujiuluza ni KWA nini tunahitaji mabadiliko fulani?.. hapo mwisho kuna kipande kidogo umesema:-
Otherwise, tutaweka uongozi mpya halafu ndio tutaanza kujiuliza. For what?

Hii ndiyo sababu kubwa ambayo imenisukuma mimi ktk mada hii ili tuweze kujiuliza For what? kabla hatuja ji commit ktk majimbo.

South Afrika unajua vizuri kuwa walikuwa na kila haja ya kuwa na majimbo kwa sababu majimbo yaliyokuwepo walikuwa wametawaliwa na Apartheid.. kabla ya 1994 walikuwa na majimbo manne, mawili chini ya Kaburu - Boers na mawili chini ya Muingereza kisha kuna viji territories ndani ya haya majimbo vya watu weusi wakiviita homelands.

Kwa hiyo hawa South hawakufanya majimbo kwa sababu ya Uongozi, Uchumi ama mipaka ya Utawala ila kuondoa mikapa ya nchi inayomfunga mtu ktk apartheid na ndipo walipounda hayo majimbo 9 kuondoa kabisa mikapa ya kiutawala wa Apartheid.

hapa wamejibu swali zima la for what!
Sasa tukirudi ktk kesi yetu siwezi kukubaliana na wazo kuwa Tanzania mipaka yetu ina ubaguzi wa aina fulani kwa sababu ni mipaka hiyo hiyo iliyotufanya leo tuwe hapa tulipo!....The best of them all (Ubaguzi hakuna), na mshkaji hatuwezi kusema kwamba kiwanja hiki (Tanzania) hakina mistari wakati tunafahamu kuwa mistari ipo ila sio wanayoitaka baadhi ya wachezaji na viongozi. Kinachotisha isije kuwa unazungumzia mistari ya basketball hali tunacheza soccer bob!.. heee heee hee! kila wakati unapigiwa filimbi kuunawa mpira.

Kumbuka pia hao maadui wanafiki ninaowazungumzia kama wazua side effects - yaani hiyo timu wa wapinzani ni watanzania vile vile ambao pia hucheza mazoezi yao uwanja huu huu na wameisha zoea mistari iliyopo. Ukibadilisha mistari kumbuka kuwa kuna uwezekano wa kubishana kuwa mpira ulitoka nje kabla ya goli ama ulikuwa ndani ya uwanja, na kama unavyowajua kiboko msheri watakuchumieni fimbo za mchongoma. hapo hakuna tena cha msalie mtume...fimbo tu na mpira umekwisha.

Haya Ukiangalia nchi kama Nigeria na hata Uganda ni majimbo yaliyotengenezwa kwa sababu ya Kiuchumi lakini hawa watu walishindwa kuweka kinga ya kufungwa magoli (UKABILA). Kwa hiyo pamoja na kwamba wameweza kwenda mbele sehemu moja wamerudishwa maili kumi nyuma kwa Ukabila na vita ya kiuchumi.. imekuwa sio mashindano tena ila kuuana!.Nigeria ni matajiri kuliko nchi nyingi sana za magharibi yaani haitakiwi kabisa kuwa hapo ilipo na trust me, utengano wa majimbo is one of the main cause.

Ukitazama Ethiopia kuna majimbo hata hayakaliwi na watu kabisa!... haya yamesahaulika kutokana na kuwa hayana rasilimali kabisa na hakuna anayetaka kuyatazama. Hii ndio hofu aliyokuwa nayo ndugu Sam kama unakumbuka siku za mwanzo tulipozungumzia majimbo akagusia sehemu kama Singida!

Kwa hiyo nachozungumza mimi ni kuwepo na sheria, mbinu ama vitu muhimu kuhakikisha makosa yaliyotokea nchi nyingine hayawezi kutokea kwetu na kibaya zaidi ndugu Mnyika utafiti ulioufanya ktk majimbo ni katika nchi zilizofanikiwa badala ya kwenda pia ktk nchi zilizo-fail.

Mwisho, Mnyika sikupenda kabisa kuzungumzia hilo la serikali kuu kuwa na wizara chache sijui tatu ama nne. Hapa yanishinda kabisa kuelewa uhusiano kati ya majimbo na serikali kuu na inatisha zaidi kuwa na matokeo kama ya Yugoslavia!

Yaani sikufichi hii imenishtua zaidi kuona majimbo kuwa na nguvu kuliko serikali kuu!.. sioni kabisa maisha ya hiyo serikali kuu.
 
Mkandara
Tatizo langu na majimbo ya CHADEMA bado lipo pale pale kama ulivyolieleza ila niliamua kukaa mbembeni niwe nasoma na kuwasikiliza maelezo yao labda kuna siku na mimi nitaelewa au kukubaliana nao.
 
Ndugu Mkandara,

Ile tuwe pazuri naomba uanishe kinga dhidi ya ukabila Tanzania tulionao katika mfumo wa sasa.Mimi bado naamini ukabila ni suala/hofu ya kubuni.

Suala la Singida, kwanza huu ni ushahidi kwamba mfumo wa sasa ni mbovu ndio umesababisha maeneo kama haya kusahaulika. Ndio maana, inakuwa rahisi kwako kuonyesha maeneo yaliosahaulika kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala. Si sahihi, kutumia udhaifu wa mfumo wa sasa na kuuweka kwenye sera ya majimbo.

Kanda ya kati, kama Dodoma na Singida zinaweza kugeuzwa kuwa visima vya wataalam nchini. Wakati wa kampeni, Mbowe aliwambia wakazi wa Dodoma atawafanya kuwa makao makuu ya elimu nchini.Singida na Dodoma wanaweza kuwa matajiri wa rasilimali watu.Cha muhimu ni mipango.

Isitoshe, CHADEMA inasema sehemu ya mapato yatabaki kwenye majimbo husika na sehemu iliyobaki yatakwenda serekali kuu. Sehemu ya mapato yanayokwenda serekali kuu yatasaidia kuweka uwiano wa mtiriko wa mapato ya rasilimali kwenye maeneo yenye rasilimali kidogo(hakuna eneo lisiwakuwa na rasilimali!)

Unaposema serekali za majimbo zitakuwa na nguvu zaidi ya serekali kuu unamaanisha nini? Serekali kuu kushikilia mambo ya ulinzi(majeshi yote), mambo ya nje,fedha, kuwa na sehemu ya mapato kutoka majimbo yote una maanisha nini kusema serekali za majimbo zitakuwa na nguvu zaidi ya serekali kuu?

Nguvu ya serekali haiwezi kupimwa na idadi ya wizara, tuangalie rasilimali itakazo kuwa nazo na uzito/unyeti wa maeneo itakayokuwa inayashikilia.
 
Kaka Mkandara:

Nakushukuru sana kwa michango yako kuhusu MAJIMBO/UFIDERALI

Nafurahi unakuwa mbishi si kwa sababu tu ya kubisha, ila umeingia katika viatu vya watanzania wenye hofu kuhusu majimbo ama wanaopotoshwa kuhusu majimbo. Na ni kweli kabisa. Na hasa baada ya technical mistake kufanyika ya kuzindua sera heavy kwenye uchaguzi na tena kuanzia kuitambulisha Kilimanjaro(nimewahi kulijadili hili mwaka jana).

Washindani wetu wakaitumia hii fursa kupotosha sera hii na kuwatia hofu wananchi. Uzuri ni kwamba hakukuwa na hoja zilizotolewa, zaidi ya kauli tu ni UKABILA, italeta vita kama Nigeria, Ni Ubaguzi, wengine watakosa RASLIMALI nk. Sasa tuna miaka mitano ya kubishana kwa hoja. Na niliwahi kusema huko nyuma ukweli ukitamalaki aliyesema uwongo hutamani kujifunika kwa kiganja kama adili na nduguze. Na hii ndiyo itawakumbuka viongozi wa juu wa CCM miaka mitano toka sasa.

Changamoto kwetu sasa ni kuuhamisha mjadala huu kwa wananchi ili wafahamu undani wa mambo haya. Na ninavyoona sasa kuna masuala ambayo tumeanza kuelewana. Sina wasaa wa kuiweka hii michango yenu na yetu pamoja ili itoke kama kitabu ama ianze kuchapwa kama makala katika magazeti ya nyumbani. Eric Ongara, kama unawasaa naomba uikusanye hii michango yote pamoja uihifadhi mahali. Pindi nikipata wasaa nitakutafuta unipatie. Narudia tena kukushukuru kwa kuamua kutazama kila angle! Endelea kutazama.

Umesema kwamba tusifanye kitu kwa kuiga!. Nataka ni kuhakikishie kwamba hii haikuwa sera ya kuiga. Ilizuka kama idea tu, kwamba kwa kuwa falsafa yetu ni nguvu ya umma, kwa nini tusipeleke mamlaka kwa umma.

Tukajiuliza ni kwa njia gani, likaja wazo la kuwa na mfumo mpya wa utawala-ikiwemo suala la muundo mpya wa utawala(majimbo). Na kwa kweli ilikuwa ni fresh field kiasi kwamba kulikuwa na mitazamo tofauti kuhusu mfumo uweje. Katika harakati hizo ndio tulipoanza kuangalia pia je nchi nyingine zinafanyaje?(hii inakaribia na kuiga).

Lakini hatukuingia kiundani sana kuchota mifano ya nchi nyingine kwa kuwa hata muda huo hatukuwa nao. Kwa hiyo tukafikiria kwa kadiri ya mazingira yetu. Tukaingia kwenye uchaguzi.CCM wakaanza kupotosha kwa kutumia mifano ya nchi mbalimbali.

Hapo sasa ikabidi kuingia kiundani hiyo mifano wanayoitoa kwa nia ya kuwajibu, hapo ndipo mjadala sasa kwa pande zote ukaanza kutawaliwa na mifano ya nje(hapa ndipo hisia za kwamba tunaiga zikaanza kujengeka). But I said this a repeat-sisi tulikuja na dhana ya functional federalism (uliberali/umajimbo wa kiutendaji).

Umesema kwamba wengine wanachukua ufiderali kwa sababu ya kutafuta UMOJA. Nakubaliana nawe. Lakini UMOJA ni sababu moja tu. Hata sisi ni moja ya sababu kama msingi mmoja wapo(rejea mchango wangu wa awali). Lakini kila nchi ni zaidi ya hapo, pitia misingi ya ufiderali ya nchi mbalimbali utakubaliana na mimi.

Umechukua muda mrefu sana kuzungumzia mfano wa South Afrika na Apartheid. Kwa kufanya hivyo, nami hapa chini nitakupatia uchambuzi wangu kuhusu afrika ya kUsini na kukupa rejea. Umesema kwamba South Afrika wamechukua muundo wa majimbo ili kukabiliana na apartheid, na kwamba palikuwa na majimbo manne afrika ya kusini ambayo yapo divided.

Nakubaliana nawe kuwa palikuwa na majimbo manne(kwa hiyo kama ingekuwa ni kwa lengo la kuunganisha majimbo kuleta umoja na kuondoa ubaguzi pekee kwa nini Afrika ya kusini imeamua kuwa na majimbo tisa badala ya hayo manne?). Haya majimbo mengine matano yametoka wapi?Yameundwa kwa vigezo gani? Nitajadili suala hili kiasi hapo chini.

Umesema hukubaliani nami kama mipaka yetu imewekwa kiubaguzi. Kwanza niseme kwamba sijatamka bayana kwamba mipaka yetu imewekwa kiubaguzi. Nilichosema ni kwamba imetokea mara kadhaa watawala wetu kuweka mipaka ya kiwilaya kwa misingi ya ukabila ama makabila.

Unaweza ukaniambia ni kwanini kikwete ameigawa wilaya ya Tarime kuwa wilaya mbili za Tarime na Rorya? Au unaweza kuniambia kwa nini wilaya ya Hai ambayo ni ndogo iligawanywa kuwa wilaya mbili za Hai na Siha(wilaya ambayo kwa idadi ya watu ni ndogo kuliko hata kata moja ya jimbo la Ubungo)?

Umesema kwamba tunataka kuweka mistari ya basket court hali tunacheza football(huwa napenda unavyozungumza kwa mifano). Lakini hapa kuna mambo mawili-Mosi, ni kwamba hii mistari tunayoita mistari hivi sasa ilichorwa na watu kama wewe(ila wao tunawaita watawala). Mistari ya nchi ilichorwa na wakoloni. Baadhi ya mistari ya mikoa na wilaya tukairithi toka kwao.

Na mistari mingine watatawala wakaanza kuichora. Na mingine wanaendelea kuichora. Mwaka juzi wakachora mstari kukatokea mkoa unaitwa Manyara. Na sasa nasikia wanataka kuichora zaidi. Wasiwasi wetu ni kwamba wanaichora vibaya, bila shabaha(hawajibu swali FOR WHAT). Sisi tunataka ichorwe na wananchi kupitia mchakato wa kuunda katiba mpya.

Iwe mistari ya wananchi kwa ujumla wao na kwa matakwa yao. Tunaweka wazi misingi ya ufiderali. Halafu kwa pamoja tuamue uweje na mipaka yake iweje. Tunapotaja mipaka ya maeneo hivi sasa mathalani ya Jimbo la Ziwa ama Jimbo la Kaskazini nk tunataja kama mawazo yetu tu na ili kurahisha uelewa.

Mipaka itakuwa ipi hili ni suala la wananchi kuamua. Tofauti na sasa ambapo Rais anaweza akalala akaamka akatangaza kugawa mkoa..na akateua anayemtaka kuwa mkuu wa mkoa ama akafanya hivyo kwa wilaya..No checks, No balance, No participation.FOR WHAT, anaweza tu kuwajibu kwamba URAIS HAUNA UBIA, AMA NIMEFANYA HIVYO KWA MASLAHI YA UMMA, AMA NIMEFANYA HIVYO KWA MAMLAKA MLIYONIPA!

Umerejea tena kumtaja SAM na Singida yake. Na yeye ameingia na kusema kwamba bado Singida ni concern kwake. Nadhani hii ni symbolic ikimaanisha maeneo ambayo hayana raslimali. Nisema mambo kadhaa hapa.

Mosi, SAM unataja Singida-hakutakuwa na Jimbo linaitwa Singida, Singida ni mkoa wa hivi sasa ambao utavunjwa na kuunganishwa na maeneo mengine kuwa na JIMBO LA KATI(central province). Itajumuisha maeneo gani itategemea idadi ya majimbo nchi nzima kwa mujibu wa uamuzi wa wananchi. Lakini kama tukiwa na majimbo 8 au 9 basi Jimbo la Kati linaweza kuwa na Maeneo ya DODOMA, SINGIDA, MTERA, KILOSA nk. Sasa wakazi wa maeneo haya watuambie je, kanda hii itakuwa haina raslimali?

Huku kuna Zabibu, Mabwawa ya Maji, Mito, Mbuga za wanyama, Ardhi ya Kilimo etc. Lakini nirudie ambacho niliwahi kukisema, Eric amekirudia na nakirudia tena-duniani kote RASLIMALI ni zaidi ya MALIASILI. Kuna states hazina MALIASILI lakini zinatumia RASLIMALI watu na upekee wake kufanya kwenda mbele. Kadiri Singida inavyoendelea kuwa tegemezi kwa DSM(I mean serikali kuu msitegemee maajabu ya Mussa).

Hivi mpaka sasa DODOMA imetumiaje fursa ya kuwa Mji Mkuu wa Bunge kuleta maendeleo?(I mean what I have written, dodoma sio mji mkuu wa Tanzania-kama kuna kuna asiyekubali afungue mjadala separate na atuambie ni wapi katika katiba pameandikwa kwamba DODOMA Ni mji mkuu ama ni lini sheria ilipitishwa kubadili makao makuu ya nchi zaidi ya sheria pre mature ya CDA?)

Umesema natumia mifano ya nchi zilizofanikiwa. Nadhani ni kitu kizuri kutumia mifano mizuri na kujifunza kutoka katika mifano mibaya. Nipe nchi ambazo zimeshindwa kutokana na Mfumo wa Ufiderali(per se). I mean federalism being a source of the specif country problems nami nitakupa mifano ya nchi nyingi zaidi zilizofanikiwa kutokana na ufiderali na nchi zilizoshindwa kutokana na serikali kuu kuhodhi kila kitu(unitary).

Umesema Nigeria haiendelei kutokana na majimbo. Hapa umefungua mjadala na watu waojua historia na mwelekeo wa Nigeria. Watakujibu. Ukweli utasimama kwamba yanayotokea Nigeria si kwa sababu ya majimbo, tena ukweli ni kwamba kuna majimbo ambayo yamepitisha progressive laws zinazowapa wananchi wake manufaa ya raslimali.

Kuna majimbo ambayo hayana msalie mtume na rushwa. Struggle za Niger Delta si kati ya wananchi kwa wananchi, ni kati ya wananchi na watawala waliofunga ndoa na makampuni ya kinyonyaji. Ni struggle ambayo hata Tanzania inakuja,tuwe na mfumo wa ufiderali, tusiwe nayo hatuwezi kuwazuia wananchi kudai raslimali zao.

Njia pekee ni kutambua hili kama tatizo la kiungozi na kulishughulikia. In fact muundo wa sera ya majimbo(in herent) unatambua suala la wananchi kumiliki ama kunufaika na raslimali.(Rejea misingi niliyoandika awali).

Umetoa mfano wa Ethiopia kwamba kuna majimbo hayakaliwi- You mean Majimbo au maeneo fulani fulani katika majimbo? Toa mifano wa hayo majimbo tujadili. Na ukweli ni kuwa-hata Marekani, Canada, Germany, kuna utofauti wa idadi ya watu baina ya majimbo-ni suala la kijiografia na kijamii.
 
Kaka Mkandara:

Nakushukuru sana kwa michango yako kuhusu MAJIMBO/UFIDERALI

Nafurahi unakuwa mbishi si kwa sababu tu ya kubisha, ila umeingia katika viatu vya watanzania wenye hofu kuhusu majimbo ama wanaopotoshwa kuhusu majimbo. Na ni kweli kabisa. Na hasa baada ya technical mistake kufanyika ya kuzindua sera heavy kwenye uchaguzi na tena kuanzia kuitambulisha Kilimanjaro(nimewahi kulijadili hili mwaka jana). Washindani wetu wakaitumia hii fursa kupotosha sera hii na kuwatia hofu wananchi.

Uzuri ni kwamba hakukuwa na hoja zilizotolewa, zaidi ya kauli tu ni UKABILA, italeta vita kama Nigeria, Ni Ubaguzi, wengine watakosa RASLIMALI nk. Sasa tuna miaka mitano ya kubishana kwa hoja. Na niliwahi kusema huko nyuma ukweli ukitamalaki aliyesema uwongo hutamani kujifunika kwa kiganja kama adili na nduguze. Na hii ndiyo itawakumbuka viongozi wa juu wa CCM miaka mitano toka sasa.

Changamoto kwetu sasa ni kuuhamisha mjadala huu kwa wananchi ili wafahamu undani wa mambo haya. Na ninavyoona sasa kuna masuala ambayo tumeanza kuelewana. Sina wasaa wa kuiweka hii michango yenu na yetu pamoja ili itoke kama kitabu ama ianze kuchapwa kama makala katika magazeti ya nyumbani.

Eric Ongara, kama unawasaa naomba uikusanye hii michango yote pamoja uihifadhi mahali. Pindi nikipata wasaa nitakutafuta unipatie. Narudia tena kukushukuru kwa kuamua kutazama kila angle! Endelea kutazama.

Umesema kwamba tusifanye kitu kwa kuiga!. Nataka ni kuhakikishie kwamba hii haikuwa sera ya kuiga. Ilizuka kama idea tu, kwamba kwa kuwa falsafa yetu ni nguvu ya umma, kwa nini tusipeleke mamlaka kwa umma.

Tukajiuliza ni kwa njia gani, likaja wazo la kuwa na mfumo mpya wa utawala-ikiwemo suala la muundo mpya wa utawala(majimbo). Na kwa kweli ilikuwa ni fresh field kiasi kwamba kulikuwa na mitazamo tofauti kuhusu mfumo uweje. Katika harakati hizo ndio tulipoanza kuangalia pia je nchi nyingine zinafanyaje?(hii inakaribia na kuiga). Lakini hatukuingia kiundani sana kuchota mifano ya nchi nyingine kwa kuwa hata muda huo hatukuwa nao. Kwa hiyo tukafikiria kwa kadiri ya mazingira yetu.

Tukaingia kwenye uchaguzi.CCM wakaanza kupotosha kwa kutumia mifano ya nchi mbalimbali. Hapo sasa ikabidi kuingia kiundani hiyo mifano wanayoitoa kwa nia ya kuwajibu, hapo ndipo mjadala sasa kwa pande zote ukaanza kutawaliwa na mifano ya nje(hapa ndipo hisia za kwamba tunaiga zikaanza kujengeka). But I said this a repeat-sisi tulikuja na dhana ya functional federalism(uliberali/umajimbo wa kiutendaji).

Umesema kwamba wengine wanachukua ufiderali kwa sababu ya kutafuta UMOJA. Nakubaliana nawe. Lakini UMOJA ni sababu moja tu. Hata sisi ni moja ya sababu kama msingi mmoja wapo(rejea mchango wangu wa awali). Lakini kila nchi ni zaidi ya hapo, pitia misingi ya ufiderali ya nchi mbalimbali utakubaliana na mimi.

Umechukua muda mrefu sana kuzungumzia mfano wa South Afrika na Apartheid. Kwa kufanya hivyo, nami hapa chini nitakupatia uchambuzi wangu kuhusu afrika ya kUsini na kukupa rejea. Umesema kwamba South Afrika wamechukua muundo wa majimbo ili kukabiliana na apartheid, na kwamba palikuwa na majimbo manne afrika ya kusini ambayo yapo divided.

Nakubaliana nawe kuwa palikuwa na majimbo manne(kwa hiyo kama ingekuwa ni kwa lengo la kuunganisha majimbo kuleta umoja na kuondoa ubaguzi pekee kwa nini Afrika ya kusini imeamua kuwa na majimbo tisa badala ya hayo manne?). Haya majimbo mengine matano yametoka wapi?Yameundwa kwa vigezo gani? Nitajadili suala hili kiasi hapo chini.

Umesema hukubaliani nami kama mipaka yetu imewekwa kiubaguzi. Kwanza niseme kwamba sijatamka bayana kwamba mipaka yetu imewekwa kiubaguzi. Nilichosema ni kwamba imetokea mara kadhaa watawala wetu kuweka mipaka ya kiwilaya kwa misingi ya ukabila ama makabila.

Unaweza ukaniambia ni kwanini kikwete ameigawa wilaya ya Tarime kuwa wilaya mbili za Tarime na Rorya? Au unaweza kuniambia kwa nini wilaya ya Hai ambayo ni ndogo iligawanywa kuwa wilaya mbili za Hai na Siha(wilaya ambayo kwa idadi ya watu ni ndogo kuliko hata kata moja ya jimbo la Ubungo)?

Umesema kwamba tunataka kuweka mistari ya basket court hali tunacheza football(huwa napenda unavyozungumza kwa mifano). Lakini hapa kuna mambo mawili-Mosi, ni kwamba hii mistari tunayoita mistari hivi sasa ilichorwa na watu kama wewe(ila wao tunawaita watawala). Mistari ya nchi ilichorwa na wakoloni. Baadhi ya mistari ya mikoa na wilaya tukairithi toka kwao. Na mistari mingine watatawala wakaanza kuichora.

Na mingine wanaendelea kuichora. Mwaka juzi wakachora mstari kukatokea mkoa unaitwa Manyara. Na sasa nasikia wanataka kuichora zaidi. Wasiwasi wetu ni kwamba wanaichora vibaya, bila shabaha(hawajibu swali FOR WHAT). Sisi tunataka ichorwe na wananchi kupitia mchakato wa kuunda katiba mpya. Iwe mistari ya wananchi kwa ujumla wao na kwa matakwa yao. Tunaweka wazi misingi ya ufiderali. Halafu kwa pamoja tuamue uweje na mipaka yake iweje.

Tunapotaja mipaka ya maeneo hivi sasa mathalani ya Jimbo la Ziwa ama Jimbo la Kaskazini nk tunataja kama mawazo yetu tu na ili kurahisha uelewa. Mipaka itakuwa ipi hili ni suala la wananchi kuamua. Tofauti na sasa ambapo Rais anaweza akalala akaamka akatangaza kugawa mkoa..na akateua anayemtaka kuwa mkuu wa mkoa ama akafanya hivyo kwa wilaya..No checks, No balance, No participation.FOR WHAT, anaweza tu kuwajibu kwamba URAIS HAUNA UBIA, AMA NIMEFANYA HIVYO KWA MASLAHI YA UMMA, AMA NIMEFANYA HIVYO KWA MAMLAKA MLIYONIPA!

Umerejea tena kumtaja SAM na Singida yake. Na yeye ameingia na kusema kwamba bado Singida ni concern kwake. Nadhani hii ni symbolic ikimaanisha maeneo ambayo hayana raslimali. Nisema mambo kadhaa hapa. Mosi, SAM unataja Singida-hakutakuwa na Jimbo linaitwa Singida, Singida ni mkoa wa hivi sasa ambao utavunjwa na kuunganishwa na maeneo mengine kuwa na JIMBO LA KATI(central province).

Itajumuisha maeneo gani itategemea idadi ya majimbo nchi nzima kwa mujibu wa uamuzi wa wananchi. Lakini kama tukiwa na majimbo 8 au 9 basi Jimbo la Kati linaweza kuwa na Maeneo ya DODOMA, SINGIDA, MTERA, KILOSA nk. Sasa wakazi wa maeneo haya watuambie je, kanda hii itakuwa haina raslimali?

Huku kuna Zabibu, Mabwawa ya Maji, Mito, Mbuga za wanyama, Ardhi ya Kilimo etc. Lakini nirudie ambacho niliwahi kukisema, Eric amekirudia na nakirudia tena-duniani kote RASLIMALI ni zaidi ya MALIASILI. Kuna states hazina MALIASILI lakini zinatumia RASLIMALI watu na upekee wake kufanya kwenda mbele. Kadiri Singida inavyoendelea kuwa tegemezi kwa DSM(I mean serikali kuu msitegemee maajabu ya Mussa).

Hivi mpaka sasa DODOMA imetumiaje fursa ya kuwa Mji Mkuu wa Bunge kuleta maendeleo?(I mean what I have written, dodoma sio mji mkuu wa Tanzania-kama kuna kuna asiyekubali afungue mjadala separate na atuambie ni wapi katika katiba pameandikwa kwamba DODOMA Ni mji mkuu ama ni lini sheria ilipitishwa kubadili makao makuu ya nchi zaidi ya sheria pre mature ya CDA?)

Umesema natumia mifano ya nchi zilizofanikiwa. Nadhani ni kitu kizuri kutumia mifano mizuri na kujifunza kutoka katika mifano mibaya. Nipe nchi ambazo zimeshindwa kutokana na Mfumo wa Ufiderali(per se). I mean federalism being a source of the specif country problems nami nitakupa mifano ya nchi nyingi zaidi zilizofanikiwa kutokana na ufiderali na nchi zilizoshindwa kutokana na serikali kuu kuhodhi kila kitu(unitary).

Umesema Nigeria haiendelei kutokana na majimbo. Hapa umefungua mjadala na watu waojua historia na mwelekeo wa Nigeria. Watakujibu. Ukweli utasimama kwamba yanayotokea Nigeria si kwa sababu ya majimbo, tena ukweli ni kwamba kuna majimbo ambayo yamepitisha progressive laws zinazowapa wananchi wake manufaa ya raslimali. Kuna majimbo ambayo hayana msalie mtume na rushwa.

Struggle za Niger Delta si kati ya wananchi kwa wananchi, ni kati ya wananchi na watawala waliofunga ndoa na makampuni ya kinyonyaji. Ni struggle ambayo hata Tanzania inakuja,tuwe na mfumo wa ufiderali, tusiwe nayo hatuwezi kuwazuia wananchi kudai raslimali zao. Njia pekee ni kutambua hili kama tatizo la kiungozi na kulishughulikia. In fact muundo wa sera ya majimbo(in herent) unatambua suala la wananchi kumiliki ama kunufaika na raslimali.(Rejea misingi niliyoandika awali).

Umetoa mfano wa Ethiopia kwamba kuna majimbo hayakaliwi- You mean Majimbo au maeneo fulani fulani katika majimbo? Toa mifano wa hayo majimbo tujadili. Na ukweli ni kuwa-hata Marekani, Canada, Germany, kuna utofauti wa idadi ya watu baina ya majimbo-ni suala la kijiografia na kijamii.
 
Sasa nirudi kwenye mjadala kuhusu Afrika ya Kusini ambao umeufungua:

Afrika ya Kusini wamepitia mchakato wa kuwashirikisha wananchi katika kuunda katiba yao tofauti na katiba ya Tanzania hivyo uamuzi wa majimbo ni wa wananchi. Nao ndio walioamua kuwa na majimbo 9 badala ya 4. Na ni kwa kuangalia sababu za ukubwa wa kimaeneo, raslimali, historia, mamlaka nk. Na hili si suala geni, Canada kwa mfano ilibuni mfumo wake wa majimbo mwaka 1867(kwa sababu za umoja zaidi), lakini majimbo ya Canada yamekuwa yakibadilika, ama kuongezeka au wajibu wake kubadilika kutokana na mageuzi ya kijamii, ukubwa, dhima ya serikali na maamuzi ya kimahakama. Hii inathibitisha kwamba functional federalism(majimbo ya kiutendaji) sio ndoto. Ni kitu kinawezekana kwa lengo la kukidhi matakwa fulani(the FOR WHAT). Matakwa ambayo mimi nimeyaanisha kwenye misingi tisa niliyoitoa.

Chama ambacho kilikuwa kinapambana na apartheid South Africa ni ANC. Kwa hiyo kama nia ya kuunda majimbo ingekuwa ni kupambana na apartheid per se. ANC ingekuwa ya kwanza kutaka mfumo wa MAJIMBO/UFIDERALI. Lakini ANC ilikuwa inapinga majimbo(kama walivyo rafiki zao CCM wa Tanzania). Na walikuwa wanasema wanataka Unitary government ili serikali kuu ya chama tawala ANC iweze kutoa huduma kwa wananchi kila mahali mathalani hospitali, shule na kuondoa tofauti za kiuchumi(sounds sweet).

Na ANC(kama ambavyo CCM inasema) imekuwa ikisambaza propaganda kwamba neno FEDERALISM ni la kibaguzi na kimbari na kwamba linafanana na HOMELANDS(No wonder kwenye katiba ya South Africa hakuna neno FEDERALISM ingawa nchi imeundwa na inatambua kufuata mfumo wa UFIDERALI). Nakubaliana nawe pia kwamba katika yale majimbo manne yapo ambayo yalikuwa yakitaka kujitenga mathalani KwaZULU Natal. Lakini mwisho wa siku wananchi waliuopenda zaidi mfumo wa ufiderali.

Mwalimu alitaka unitary government-hoja zake zilikuwa hizo hizo za serikali kuu kupeleka huduma kila mahali. He has done his part. Kuna mahali amefanikiwa, kuna mahali ameshindwa. Now, gone are the days of state centralized economy. Now it's the time for people(I mean wazawa as opposed to foregnization) centered economy. Na huu ndio msingi wa falsafa ya nguvu ya umma na itikadi ya mrengo wa kati!. Na hili nimelichambua katika misingi ya ufiderali ambao CHADEMA inapendekeza Tanzania tuufute. Ndio maana naendelea kusisitiza kuwa pamoja na kuwa kipaumbele ni UONGOZI kuna uhusiano mkubwa baina ya MFUMO/MUUNDO WA UONGOZI na UONGOZI wenyewe. Wananchi wanapaswa kujulishwa mapema kwamba wakichagua CHADEMA wanachagua falsafa ya NGUVU YA UMMA kutumika katika utawala na UFIDERALI kuwa muundo- labda kama wananchi(ambao sio wote wanaunga mkono sera za CHADEMA) au bunge(ambalo halitakuwa la CHADEMA peke yake)-WAKATAE wakati wa mjadala wa KATIBA MPYA!

Wakati huo tutaamua kama tufuate Ufiderali uliogawanyika(divided federalism) kama ilivyo Canada ama tufutate Ufiderali uliounganika(integrated federalism).

Mambo ni mengi kwa kweli, unaweza kupata picha kidogo ya jinsi Afrika ya Kusini ilivyofikia katika mfumo wa ufiderali kwa kusoma andiko hili..http://www.iigr.ca/pdf/publications/145_Considerations_on_the_De.pdf

Tuendelee kujadili, ila nawaomba pia waandishi wahamishie mjadala huu kwenye vyombo vya habari ili wananchi wengi zaidi wafahamu ukweli. Na ukweli uwafanye huru.

Na nitaendelea kuandika kwenye huu mjadala wa majimbo mpaka kaka mkandara na Sam mtakaponiambia kama ama tumekubaliana au tumekubaliana kutokukubaliana ndipo nitaanza kujibu maswali kuhusu family business na viti maalumu.

JJ

NB: Eric amekutaka ueleze kinga ya ukabila katika mfumo wetu wa sasa. Ukishajibu nami nitachangia; kinga zipi CCM(read Nyerere) ameziweka, zipi ameshindwa. Hali ikoje hivi sasa, je kuna ukabila hivi sasa hapa nchini?Ni fear au fiction. Je, mfumo wa majimbo utaleta ukabila ama utaondoa ukabila ? Haya ni maswali tete ambayo nashauri yafunguliwe mjadala wake wa peke yake !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom