Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Niliposema Bunge nilitaka kumaanisha Bunge ama Baraza la Katiba(constitutional assembly)

Mfano wa Intergrated federalism ni shirikisho la UJERUMANI
 
J.J Mnyika,

Shukran nyingi sana kwa kunipa somo moja zuri sana ambalo hakika litawafungua na wengine kuweza kulichukulia swala hili kwa Uzito mkubwa.

Nakubali sana ulivyoichambua serikali iliyopo sasa hivi inavyozua mikoa na wilaya bila ridhaa ya wananchi... Na nina hakika hii mikoa na wilaya inaweza kuwa inavumbuliwa kutokana na hesabu ya kura ama wabunge kama walivyofanya Visiwani.

Na kibaya zaidi ni kwamba sisi tukijiuliza FOR WHAT? hatuwezi kupata jibu isipokuwa wao wanafahamu kinachoendelea kwa manufaa ya Chama. Hii inatihsa sana na ndio maana nimekuwa nikiwashukuru sana Chadema kwa kujiweka wazi na hata kukubali kuchukua maswali mazito ambayo hayana ufumbuzi wa karibu. Kwa hiyo basi bado narudi palepale kwenye WHAT FOR?

Ndugu J.J Mnyika kuna vitu viwili hapa ambavyo napenda sana uvifahamu na imekuwa vigumu sana kwa ndugu yengu Eric kufahamu tofauti zake.

Kwanza kuna hili la MIPAKA ya MAJIMBO Kiutawala peke yake..
Hapa unaweza kuweka MIPAKA ya MAJIMBO bila kubadilisha mfumo wa UTAWALA wa MAJIMBO, na mfano ndio kama huo wa South Afrika ambao waliongeza majimbo mengine 5 kufikia 9 hali viongozi na ngazi za viongozi zilibaki vile vile.

By the way, South Afrika walikuwa na kila haja ya kuondoa majimbo manne kwa sababu majimbo haya yalikuwa ya kibaguzi toka mwanzo - mawili ya kaburu na mawili ya Muingereza - hakuna jimbo la mtu mweusi isipokuwa hizo homeland!.

Majimbo manne bado yangewatenga weusi na haki zao maanake hiyo homeland hazikuwa sehemu zenye rutuba wala uzuri wowote zaidi ya kuwa mwitu.

Kulikuwa na kila sababu ya kuvunja mipaka hiyo pamoja na kwamba bado waliendelea kutumia utaratibu wa Uongozi ule ule yaani Premier, Executive council ya mawaziri na Bunge. Kwa hiyo mageuzi yao umuhimu wake ulikuwa ni MIPAKA, ili kuvunja ule utaratibu mbaya uliowapa wazungu majimbo na weusi wakabakia na vi doa ndani ya ramani kama territories ambazo hazikuwa na utaratibu mzuri wa kiutawala unaoendana na katiba ama kutambuliwa na serikari kuu.

Hapa, kulingana na mapendekezo ya Chadema nimekuwa nikijiuliza maswali - WHAT FOR? maanake tusiwe tunaiga kuweka kitu hali hatuna sababu kabisa ya kufanya hivyo! ama tumeweka mipaka hiyo kwa sababu ya kukamilisha hili la Pili ambalo nitalizungumzia baada ya hili.

Ndio sababu hizo hizo leo tunajiuliza kuhusu CCM wanavyoweka mipaka mipya hali haina malengo ya kuboresha wananchi ila kukidhi mahitaji yao ya kiutawala.

Kisha kuna hili la pili, UTAWALA WA MAJIMBO ambao utaanzisha utaratibu mpya wa kiutawala. Mipaka na upana wake sio issue hasa kwa sababu unachotafuta hapa ni mabadiliko ktk jinsi ya kuongoza. Hapa ndipo unapowakuta, hao akina Premier, mawaziri na bunge kwa majimbo na pia kuwepo kwa serikali kuu, tofauti na utaratibu huu tuliokuwa nao wa kuwatumia RC, DC, bunge moja na serikali moja.

Sasa ukiweza kuyarudia maswali yangu mengi huko nyuma utakuta kuwa yamechangia zaidi kuwepo na mabadiliko ya sehemu zote hizi mbili..na maswali yangu mengi yamelala ktk hilo la kwanza yaani MIPAKA ya MAJIMBO kiutawala.

Hili la Pili, sio maswali mengi isipokuwa najaribu kuangalia hiyo What for?
mliyoitoa na kuangalia hali halisi. Nimekuabaliana sana na kuwaondoa RC na DC lakini sio sababu ya kuondoa utitiri wa viongozi ama hakika ya utendaji mzuri wa kazi.

Hili nitarudia tena trust me J.J, chini ya Majimbo hata yawe vipi hayawezi kuwa na wizara chache kuliko leo hii ambapo tumesimama kuwa na wizara 26. Hata kama useme serikali kuu iwe na 4 bado haya majimbo yatakuwa na wizara zisizopungua 15 kila moja... bado hatujagusa wabunge na wawakilishi wa hizi serikali ndogo. Now, tutaweza vipi kuzikata wizara na wabunge ktk majimbo hali hilo ni swala la ndani ya jimbo?

Kisha tukienda ktk ufanisi ndugu yangu mimi siwaamini viongozi wetu hata kidogo. Viongozi wetu NJAA na kwa bahati mbaya hawana shibe hata kidogo. Ni sawa na jambazi linaloingia benki halijali kuwepo na mlinzi wala sheria!.. Napata taabu sana kuwa convinced kuwa mfumo wa majimbo unaweza kuleta ufanisi kwa sabau ya kutazama nchi zenye majimbo hali nchi hizo kwanza zinajali sheria, Uzalendo na upendo wa nchi yao.

Watanzania wengi wetu mapenzi yapo mdomoni wakati tuna shida kama vile mwanaume malaya. anavyoweza kuwahadaa dada zetu. Wakati wa shida hakuna mzuri kama yeye lakini akimkupa mgongo tu...hata jina hulikumbukwi.

Nina imani kubwa kuwa hawa viongozi wanaotuongoza leo ndio watakao shika nafasi hizohizo tunazo jaribu kuwafunga. Ndanio ya CCM leo hii kuna utitiri wa viongozi wanaosubiri nafasi kama hii kwa sababu mfumo uliopo una limit number za viongozi wetu. Nje ya uongozi hakuna malipo na ndio sababu hata ma prof wetu wamekimbilia siasa.

Kuwepo kwa majimbo ni kuongeza pia nafasi zaidi za kisiasa kwa wale waliokosa nafasi.

Ni sawa na mfumo wa MKAPA na JK kujenga mashule mengi hali walimu wenye uwezo hawatoshi, vifaa vya kufundishia hakuna. Kifupi hakuna utaratibu unaoendana na ujenzi wa shule hizo.

Mwisho, J.J Mnyika nina mengi sana ya kusema na kweli tunaweza kuandika kitabu maanake hoja zinazidi kila siku tunayokwenda mbele. Lakini ndugu Mnyika kuna maswali mengi sana ktk mfumo huu uliopo kuliko huo wa majimbo na sidhani kama kuna hata harufu ya ufumbuzi ktk mfumo huu wa leo.

Nafikiri uliwahi kumsikia mwenyekiti wa Global Organization of Parliamentarians Against Corruption (GOPAC) alipokuwa kizungumzia kuhusu Umaskini wetu pindi alipotembelea Tanzania. Bila marekibisho makubwa ndani ya katiba na Utekelezaji wake hatuwezi kwenda popote ndani ya mfumo huu ama mfumo mwingine wowote!
Ikiwa hukuweza kuyaona maoni ya Williams (GOPAC) nitakuwekea hapa uyatazame na nadhani ni bora kwanza vitu hivi virekebishwe!
 
Mnyika, Asante kwa michango yako, haswa ile link,imeshiba na kuna mengi ya kujifunza toka South Afrika,Canada na Geremany na nchi zingine pia. Ninakili hi michango na kuhifadhi, ni muhimu sana.



Mkandara heshima kwako, wembe ni ule ule



Nakumbushia swali langu juu ya kinga ya ukabila tulionayo katika mfumo wa kiutawala tulionao katika mfumo wetu wa sasa.



Kuhusu gharama tangu mwanzo nilisema hili linazungumzika,angalia ofisi za mikoa zina watumisi wangapi? wakusanye wapeleke katika jimbo, mmoja wao awe waziri na wawli watu hivi wasaidizi wake.Tuseme maafisa elimu mkoa wako 26(kila mkoa), ambao ni ghrama kuwa nao kwa kuwa hawana nguvu ya kimaamuzi(wao ni watekelezaji wa maazimio ya Dar).Chini ya maafisa elimu wapo wasaidizi wao katika kila mkoa, kuna maafisa taaluma, mitala, michezo,ukaguzi n.k. Chukulia Jimbo moja linaonganisha mikoa 4, hapa unaleta maafisa elimu wa mokoa wanne na wasaidizi wasiopungua watano, hawa ni watu 24!Unaweza kuunda wizara ndogo ya elimu ya jimbo yenye mamlaka kutokana na idadi ya hawa watu 24 au pungufu ya hapo. Tutafakari kwa kina suala la ongezeko la gharama.



Pia, si sawa kuangalia ongezeko la gharama pekee, halipaswai kusimama peke yake,pamoja na gharama tuonganishe na ongezeko la tija/uzalishaji.Ubaya utakuja pale gharama zitakapoongezeka pasipo kuwa na tija. Je kutokana na kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi katika sera na ushindani wa kiutendaji baina ya serekali za majimbo, ufanisi utaongezeka au utapungu?



Hofu yako juu ya uongozi, ya kwamba hata kama tukibadilisha muundo wa kiutawala, bado viongozi watakuwa ni wale wale! Cha msingi cha kujiuliza hawa viongozi kwanini hawaondoki miaka na miaka? Tunaondakana nao vipi?



Suluhisho ni nguvu ya umma. Sauti za wananchi kupewa nguvu, watawala dhaifu wa sasa wapo kutokana na udhaifu wa mfumo wa utawala(kuteuwana) ambao majimbo itaondokana nao na sababu ya pili ya ung'ang'anizi wao ni upenyo wa kikatiba uliopo, wanatumia vibaya katiba dhaifu ya sasa kuhakikisha uwepo wao. Mabadiliko ya katiba na sera ya majimbo(ushiriki wa wananchi) ni suluhisho maridhawa la aina hii ya viongozi.
 
Eric Ongara, tatizo langu sio watumishi wa serikali. hawa wakiwa wengi sii hoja kwangu zaidi ya viongozi wanasiasa ambao kazi yao kubwa ni kuchuma. Na kama nitafuata mfano wako ina maana kuwa majimbo latasababisha unemployment wa watumishi wa serikali. Kwa hiyo umekata watumishi na kuongesha viongozi wanasiasa!

Na pili, Ikiwa Lowassa leo ama Karamagi leo hii wameshindwa ktk ngazi ya Taifa huyu mtu kweli ataweza ktk majimbo?..kuchaguliwa kwao ni lazima maanake huwezi kunipa sababu iliyomfanya JK achaguliwe ama wabunge wote waliopo CCM leo. Hofu inazidi pale viongozi hawa wa CCM watakapo shika kila jimbo... uwezekano upo kwa sababu wananchi bado wanachagua watu kwa sura zao
 
J.J Mnyika na Eric,

Mtanisamehe nitakutoweni nje kidogo ya mada hii ili tuagalie mawazo yangu ambayo nadhani yanatangulia kabisa swala hili la Majimbo na hata hiyo Katiba.
Je, mmeweza kukusanya mawazo ya wananchi ktk kuifanyia marekebisho KATIBA?... na yapi muhimu mliyoyakubaliana na mnayawakilisha.
 
mwana mukandara, mtani hali ya nyumbani kanyigo!

nafikiri mnaendelea kula matoki na huku mkikamua elimu.salamu kwa proffessor na mwambie nimependezwa sana na uamuzi wake wa kukubali kuwa mkuu wa chuo.

nimeona umetoa uelekezo mzuri wa hoja zetu.mambo mengi yamekuwa yanatokea na niseme kwamba ni mazuri kwa upande mmoja na mabaya kwa upande wa pili.

vijana wa chadema wamekuwa wanaomba sana sera ya majimbo.nataka niwaambie kitu. hiii sera sio mpya na wala si ngeni hasa kwa wakina sisi twene umri mkubwa hapa jambo.

ikumbukwe katika miaka ya 1950 , jamii ikiwa katika harakati za kudai uhuru wa mwafrika wa kweli. baba yangu pamoja na wakina cheyo waliomba sana suala hili la majimbo. lengo likiwa kama ambalo leo chadema wanaliomba. kugawa maendleo na watu wawe na demokrasia ya kweli ikiwemo hata kuchagua watu wanaojulikana kama magavana ambao ni sawa na wakuu wa mikoa, katika tanzania ya leo.

mimi nilikuwa napendana sana na wazazi wangu na hata nilipomuuliza baba kwa maelezo yake nilifarajika kuona kwamba tutakuwa na maendeleo yetu wenyewe.mwalimu kipindi hicho alitwambia jambo muhimu sana. '..............tunachotafuta ni maendeleo na si kugawanya maendeleo........',

nilichukua muda kuelewa lakini baadaye nilikuja kujua nini siri ya haya maneno.

tukae tujiandae , sera yao sio mbaya/.
 
Chief Masanja,
Habari nzuri mzee wangu ila tu napenda kukufahamisha kuwa Prof. Mukandara sina ujamaa naye, majina tu yamefanana kidogo.

Hilo neno alilosema Nyerere kweli zito sana na upeo wake ni mkubwa sana!
Tunachotafuta ni maendeleo na si kugawanya maendeleo........',

Hili ndilo jibu kubwa la puzzle nzima ya majimbo!.. yaani pale nfugu J.J Mnyika aliposema WHAT FOR? basi tumepata jibu na kila kitu kiundwe ktk misingi hiyo. Leo hii kweli Tanzania tunachotafuta ni maendeleo sasa tutagawana vipi maendeleo hali hayajapatikana?.. Mnnnnhhhhh! kazi mpya!

Chief, nafurahi sana kuwa umejiunga nani ktk kijiwe hiki na karibu sana. Bado wavaa ile kofia yako ya kimafia?

Eric na Mnyika,
Tafadhali nakuombeni kama mnaweza kutupa kwa kifupi mapendekezo yenu ktk kuibadilisha kati maanake nina baadhi ya hoja na michango ambayo niliikusanya toka zamani. Michango hii kama itaweza kufanya kazi nina hakika kabisa kuwa demokrasia ya kweli itaweza kusimama.
 
Mkandara,

Nashukuru. Hii ni ishara kwamba tumefikia pazuri kwenye mjadala kuhusu sera ya majimbo. Sasa tunaweza kuuacha mjadala huu kwa muda. Lakini kwa kuwa hii thread imeilenga CHADEMA sana nashauri ufungue thread nyingine ya mjadala kuhusu katiba. Binafsi nitakuwa mchangiaji mzuri katika mjadala wa katiba. Ni mjadala muhimu kupindukia. Kwa leo nimekuja kukusabahi tu.

JJ
 
Mnyika.
utanataka thread ifungwe kwavile imeilenga chadema hiyo sio fair.jibuni hoja tu mbona chinga mmeshamfukuza?
 
Mswahili soma vizuri mchango wa Mnyika, hakuna sehemu aliyotaka thread ifungwe! Ameshauri tu Mkandara afungue thread nyingine ya katiba ili kuiswe na mchanganyiko wa mambo!!
 
Mswahili,

Kuna document fulani naiandaa kuhusu Utawala bora kwa malengo ya kiuchumi. Nitakuja iweka hapa tupate kuijadili bila kutumia vyama ama majina ya watu.. Kidogo inaiba kote yaani toka CCM, CUF, Chadema, TLP na NCCR- Mageuzi..
Patamu hapo!
Imani yangu ni kwamba hata Demokrasia ni Ilani ya kitaifa ambayo haihitaji chama kimoja kutumia kama mwongozo wake. Tunachukua muda mrefu sana kutazama kitu kuelewa nafasi yake ktk jumuiya au chama!...

Utanisikia!... nipe mji tu.
 
As I said before, I believe on freedom of speech but do not forget that can turn up to be very very destructive to the society. As the family, we have our philosophy so called forum's philosophy. If you have decided to write your gabages in this forum you have to answer to it. If you have decided to be hermaphrodite just because your lord will pay you, fire will be upon you. If you can not control your bladder and let the forum sink in and marinate, sam will never allow you to do so.
I real respect all of you but I will not be afraid to be terminated out of the forums because of the fools. Let us talk about issues and if you want us to play a dirty game of character assassination you should know better that I am good on that.

well, i don't think that all that Chinga put down was critically analyzed neither do i think all was misrepresentation.

i there think what we have here is character revelation as oppose to assassination.
 
Mkandara:

Hiyo document kuhusu utawala bora na malengo ya kiuchumi ni wazo zuri. Naomba ikiwa tayari iweke kwenye ile thread ya Tanzania tunayoitaka. Ukiiweka hapa kwenye thread ya CHADEMA inaweza kutazamwa vivyo sivyo!!!

JJ
 
J.J. Mnyika,
Unajua hii mada imekatikia pabaya sana kiasi kwamba naeleweka kuwa mpinzani wa Majimbo!..ila nilichotaka kusema ni kuwa - MAJIMBO ni last option baada ya kushindikana kabisa kupata uongizi bora. Bado zipo nafasi za kuitengeneza katiba hasa ktk uwajibikaji kiasi kwamba itawalazimu watawala wawajibike kisheria. Policy za uzalishaji kuwatanguliza wananchi mbele kama wao ndio watakao leta maendeleo na sio kinyume.

Naomba ieleweke kuwa MAJIMBO sio option ya sasa hivi kama vile baadhi ya wabunge wa Marekani waliokataa kuivamia Iraq. Hawa watu hawakupinga kabisa swala la kuivamia Iraq lakini waliona bado kuna nafasi ya suluhisho kwa kupitia njia za amani. Uvamizi kuwa last option haina maana hakuna nafasi kabisa!
Huyu CCM anayeshika mirathi yetu ndiye mbadhilifu na kuna kila haja ya kumwondoa ktk usimamizi wa mali yetu. Ama bado naamini kuna viongozi wazalendo ambao wanaweza kutumia mfumo huu ULIOTANGULIA kugawa raslimali zetu vizuri ikiwa kutakuwepo na msisitizo fulani toka ktk sheria zetu. Ikishindikana kabisa basi hakuna hila zaidi ya KUIGAWA nchi ktk majimbo na hapo ndipo huyu mjomba CCM atajikuta kapoteza uaminifu wake!...
That's my all point!
 
J. J Mnyika,

Ndugu yangu lazima nikubali kitu kimoja!.. Nilidhani hadithi yangu ya uandishi wa hiyo document ungekuwa mfupi lakini mzee kila napoandika vitu vinazidi kumwagika kichwani na sasa hivi imekuwa kitabu maanake!..duuuh ama kweli uandishi mgumu sana.

Kisha naona ukumbi huu ni wa majadiliano, maswala ya kuandika risala ndeeefu hua inachosha hata kusoma na ukweli ni kwamba it is boring!. Sasa wewe just imagine mimi hapa Mkandara nimesha choka kusoma kurasa chache nilizokwisha ziandaa itakuwaje kwa wasomaji wengine?
 
Ndugu Mkandara, ziteremshe taratibu taratibu kama ule mfulilizo wa IPTL ulivyokuwa.
 
Sawa,
Labda nitangulize kipande hiki kisha nipate feed back za watu. Wapi nibadilishe ama kipi niongezee maanake unajua tunaweza kutunga kitabu cha pamoja hapa?..mengi yaliyotangulia umewahi kunisikia nikiyasema siku za Bcstimes, TEF na mijadala iliyotangulia ya JF. Kisha lugha ya uandishi mjomba mimi bado kabisa sijaenda shule! ila nakuombeni jaribuni kuipata message!..naandika kama nanyoongea, kazi kweli kweli!
Hata hivyo itachukua miezi kukamilisha kwa hiyo tuanze na kipande hiki kulingana na mawazo yangu mimi binafsi - MJAMAA mimi!

Nimeondoa kichwa cha habari kinachotangulia.

UTANGULIZI

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikisumbuka kuelewa hasa dhumuni la nchi yetu na hasa nchi za kiafrika tulipodai uhuru wetu toka kwa mkoloni ikiwa matokeo ya uhuru huo umekuwa na matunda mabaya sana kwa raia wake kisiasa na kiuchumi. nachopenda kujiuliza kila mara ni kati ya maswali haya:-
Kiutawala:- Je, dhumuni hasa lilikuwa kumwondoa mtawala mlowezi na badala yake kumweka mzawa tukitumia falsafa inayofanana na nguvu ya milki iliyowekwa na mkoloni?
Kiuchumi:- Je, ilikuwa mategemeo ya wengi viongozi kubadilisha mkono wa mtawala wa uchumi toka mlowezi na badala yake kushikwa na mzawa pasipo kuwa na dira yenye malengo ya kumkomboa mwananchi kiuchumi ama tulitegemea kwamba zimwi likujualo halikuli likakwisha!..

Nini hasa maana ya neno UHURU ikiwa wananchi wengi wa nchi zilizo huru wamekuwa na maisha mabaya zaidi chini ya utawala wa mzawa. Adui mkubwa wa maendeleo ya mwafrika imekuwa mwafrika mwenyewe. Umaskini wa mwafrika umezidi kukua baada ya Uhuru na ujenzi wa matabaka baina ya wananchi kiuchumi umeshamiri zaidi ktk siasa zetu.
Leo hii imefikia kuwepo na watu wanaosema - Afadhali ya mkoloni!
Hili ni neno zito sana na lenye uchungu mkubwa kwa mwenye kufikiri, kwa sababu umaskini wa mwafrika ni maradhi ya kujitakia zaidi ya hali halisi na yawezekana kabisa kuwa UHURU wetu umetafsirika vibaya hivyo kupoteza malengo ambayo yalikusudiwa toka awali kwa sababu ya tamaa ya baadhi watu wachache walioshika ama wanaendelea kushika madaraka aidha kwa kuchaguliwa ama kuteuliwa.

Pamoja na maswali yote haya, sio rahisi kupata majibu yake ikiwa tutashindwa kutambua kwanza - Sisi tumetoka wapi na yapi yalikuwa malengo yetu! Kwa kifupi tumetoka wapi na tunakwenda wapi!..Nini madhumuni ya ubunifu wa falsafa ambayo ingetuongoza kama dira katika kila hatua ya maendeleo yetu. Nje ya hapo Uhuru kwa mwafrika utakuwa hauna tofauti kabisa na mabadiliko ya sura ya mtawala. Kiongozi mwafrika ni binadamu mwenye tamaa na hisia zote za kibinadamu kama watawala wengine na kuna kila sababu ya mtawala mwafrika kuwa mbaya sawa ama zaidi ya mtawala mgeni. Kwani mtawala mgeni hutegemea zaidi nguvu ya silaha kuendesha utawala wake wa mabavu, wakati mwenyeji anaweza jificha chini ya rangi yake kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo.


Umaskini wa mwafrika ni maradhi ya kujitakia na yawezekana kabisa kuwa UHURU wetu umetafsirika vibaya toka mwanzo hivyo kupoteza kabisa dira ya uhuru huo. Hii vita kubwa ya kumkomboa mwafrika ktk Umaskini itawezekana tu ikiwa sisi tutaweza kutambua dira na malengo yetu na wapi tumekwama. Na Katika kuyatazama hayo ndipo tutaweza kuweka maazimio mapya, maazimio ambayo yataambatana na uboreshaji wa KATIBA katika vitengo muhimu vya UTAWALA, SHERIA na UWAJIBIKAJI kulingana na hitlafu zitakazo jitokeza.
Katika kifungu hiki nitazungumzia zaidi dira ya kitaifa kwa kuzingatia zaidi msukumo uliotufanya sisi kuchagua dira ya kitaifa baada ya uhuru kuwa ya UJAMAA na KUJITEGEMEA.
1. UJAMAA ikiwa na maana ya ujenzi wa UMOJA wa Watanzania wote ktk maendeleo na usatawi jamii hiyo.
2.KUJITEGEMEA ikiwa na maana ya ujenzi wa Uchumi wetu ili kutupa uwezo wa kuendesha maendeleo yetu bila kutegemea misaada toka nchi nyingine.

Haya ni maelezo ya uchache kama sababu za kimsingi ambazo zimetokana na historia ya nchi yetu, historia ambayo imetufanya tujifunze mengi mabaya na mazuri chini ya utawala wa mkoloni. Na kutokana na sababu hizo tulipata msukomo wa kupitisha dira hii ya kitaifa ambayo tuliijengea maazimio na mikakati ili tuweze kwenda mbele kama taifa huru. hayo Maazimio na Mikakati kwa kiasi ilitusogeza mbele lakini ilifika mahala tukakwama, hazikuweza kuzaa matunda tena kitaifa tofauti na madhumuni yaliyotangulia. Hapa nikiwa na maana kwamba kwa kiasi kikubwa Tanzania iliweza kujenga nguzo za ujenzi wa UJAMAA kiasi kwamba Tanzania ilikuwa moja ya nchi chache maskini duniani zilizosimamisha UJAMAA wa kweli baina ya wananchi wake lakini tulikuja shindwa baada ya nguzo hizo kuanza kuachia kutokana na kutokuwa na msingi mzuri wenye uwezo wa kubeba uzito wa jumba zima la UJAMAA na KUJITEGEMEA. Kushindwa kwa nguzo hizi kusimama, kumetokana na uzito mkubwa uliobeba kipengele cha pili cha dira yetu yaani KUJITEGEMEA. Kipengele ambacho wakati wote hakikupewa muda kutazamwa kwa makini zaidi ama kutenganishwa na imani yetu ktk siasa zilizokuwa zimetawala dunia. Ujamaa badala ya kuwa ni UMOJA wa wananchi wake ktk maendeleo ya pamoja ukajengwa kwa kuiga kiutendaji itikadi za wageni zenye malengo ya kujenga ama kuboresha bado uchumi wa dola zao. Baada ya Wakoloni kuondoka, mfumo mpya wa kiutawala ulivumbuliwa, utawala ambao ulizua falsafa mpya ya ujenzi wa makoloni ya kiuchumi kwa njia ya mawasiliano badala ya dola ama milki lakini bado nchi za kiafrika na nyingine maskini ziliendelea kuwa tegemezi wa falsafa za utawala huo wa Kibepari na Kimmunist.
Ukitazama kwa makini utakuta kwamba Wamarekani, Warusi, Wajarumani, Wareno, Wahispania, Wajapan, Wachina na Waingereza wote walisimama kama mataifa yenye kutaka kutawala, kudumisha na kulinda tawala zao nje ya mipaka yao kwa kutumia mawasiliano ya kiuchumi ambayo haitofautiani na dhumuni la mwanzo la dola ya mkoloni ambalo lilikuwa ni uwezo wao kumiliki uchumi wa nchi nyingine kwa kuweka utawala wa dola ndani ya nchi hizo kuhakikisha mafao ya nchi hizo yanarudi kujenga nchi zao.
Hii ndiyo azma kubwa ya siasa zote za nchi za Ulaya, azma ambayo ilikuja zua vita kubwa baina yao wakitutazama sisi kama ngo'mbe jike linalohitaji fahari wa kumiki zizi. Kila fahari akaingia na rangi zake, makeke na kila vitisho ambavyo vinaweza kumvutia ngo'mbe jike. Ni tofauti hizi za umilikaji wa uchumi nje ya mipaka yao ndio chanzo kikubwa kilichowasha vita zote kuu za dunia. Tofauti ambazo sisi tulikuja kuzikumbatia na kuzitangaza kwa kuzipigia debe hali misingi ya ujenzi wa rasimu na hata ilani yake haikuwa kwa manufaa ya nchi zetu au kuboresha mazingira yetu bali sisi kutumiwa kama watumishi watawaliwa mithiri ya mchwa wanavyojenga makazi yao kwa manufaa ya malkia. Ukimwondoa malkia mchwa hana maisha tena kwa hiyo uhai wake unategemea kuwepo kwa malkia ambaye ni unique ktk kizazi.

Tanzania na baadhi ya nchi maskini tukajikuta tukifuata mkondo wa Urusi bila kufahamu kwamba wao walijenga itikadi hii pingamizi kwa nchi za magharibi wakati wakizitawala nchi zote za USSR na ulaya ya mashariki kiuchumi na hata China wakizitawala nchi nyingi za Asia ya mbali kiuchumi. Kwa kifupi Ujamaa na Ubepari ni mifumo ya kiuchumi iliyojengwa ktk mazingira ya kuboresha nchi zao wakizitumia nchi maskini kama shamba la kuvuna kwa mapana ya mipaka kulingana na mbegu za kisiasa walizopandikiza. Ni katika kuiga hizi siasa Maazimio yasiyo kuwa na hesabu yalijengwa kwa kupotosha madhumuni yaliyotangulia kabla na baada ya uhuru. Matokeo yake tulipoteza kabisa dira na malengo yetu ya awali na kujitwika utumwa wa fikra za kupachikwa ambazo zimedumu hadi leo hii.

Tanzania imebaki kama uwanja mtupu uliojaa tope bila nyasi baada ya vita ya hao mafahari ambao bado hadi leo hii wanatafuta mabaki ya nyasi ktk malisho yao. Vita ya kwanza ya dunia na ile ya pili, zote zilitokea nchi zetu zikiwa bado chini ya utawala wa mkoloni isipokuwa vita hii baridi ya kisiasa kati ya Marekani na Urusi ndio vita pekee ambayo nchi zetu za kiafrika zimeweza kuusikia uzito wake kiuchumi kwa sababu vita hiyo imetukuta tukiwa huru na wenye kuwajibika ktk maendeleo ya nchi zetu. Matokeo ambayo yamekuwa jaribio jipya kwa nchi yetu kiasi kwamba tunadiriki kudai kuwepo kwa mabadiliko ya kiuchumi duniani hali ukweli umesimama kuwa ni mabadiliko ya kisiasa yaliyotangulia mabadiliko ya kiuchumi. Misingi ya kiuchumi iliyotumika zamani bado ni ile ile toka mkoloni isipokuwa hatukuchukua muda kutafakari mchango wa siasa hizo ktk uchumi wa nchi maskini kama kikwazo kikubwa kilichopotosha malengo ya awali ktk kudai uhuru wetu. Pamoja na mabadiliko yote, misingi ya kiuchumi bado inaendelea kutazama maslahi ya nchi za Ulaya. Hakuna tofauti kubwa za Kiuchumi kwa nchi maskini kati ya Ukoloni wa kilowezi na Ukoloni mamboleo ila mabadiliko yote ya kiuchumi yalitokana na ukweli kwamba nchi nyingi zilizokuwa zimetawaliwa kuwa huru. Sheria na masharti ya biashara yalipanuliwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa teknologia na hasa kulinda soko kubwa la nchi hizo. Hata hivyo bado nchi maskini tunatumiwa kama tulivyokuwa tukitumiwa wakati wa Mkoloni, wakati wa vita baridi na leohii ktk mfumo mpya wa Ukoloni mamboleo.
Huko ndiko tulikotoka!..

Haya waungwana nasubiri dondoo zenu kabla sijaendelea! nadhani mnaelewa naelekea wapi mjamaa miye!

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom