Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 12
Kichwamaji,
Nashukuru kwa kujaribu kufafanua, japo nikiri bado hayajaniingia.
Huenda wengi wetu tunaojadiliana humu hatuelewi nini maana ya "MAJIMBO" na hivyo sera yake pia kuielewa inatuwia vigumu. Labda niulize zaidi ili uzidi kunifafanulia:
1. Kuna tofauti gani kati ya "Madaraka Mikoani" na hii sera ya MAJIMBO? Kumbuka tulijaribu hii sera huko nyuma tukakwama.
2. Mpaka sasa kila mkoa na hata wilaya una maafisa/wataalam/watawala kwa ajili ya maeneo/sekta mbalimbali, kama vile Elimu, nk. Kwa hiyo si kweli kwamba kila uamuzi wa suala la elimu, mathalani, lazima uamuliwe na Wizara ya Elimu kutokea Dar es Salaam. Sasa hapo kuna tofauti gani itakayoletwa na sera ya majimbo?
3. Hata sasa katika Halmashauri za Jiji/Manispaa na Miji tuna wawakilishi wetu madiwani (na wabunge) ambao hutuchagulia mameya na wenyeviti wa halmashauri hizo. Je, hiyo haitoshi kujibu hoja yako kuwa tuna viongozi wetu tuliowachagua wenyewe, kupitia kwa madiwani wetu, ambao tuliwapigia kura sisi wenyewe?
4. Hivi sasa wataalam mbalimbali katika halmashauri (wahandisi, madaktari nk) wanaajiriwa na halmashauri zenyewe baada ya halmashauri kuwasilisha mahitaji yao kwenye wizara ya sekta husika (mfano Wizara ya Afya kwa madaktari) na kupewa kibali na Utumishi (ofisi ya menejimenti ya umma). Je, hivyo ni sawa au si sawa na kutekeleza sera ya majimbo, kwani wenye madaraka "to hire and fire" ni halmashauri zenyewe?
5. Nafahamu pia, kuwa kuna sera ya kubakiza kiasi cha pesa katika eneo lenye rasilimali fulani badala ya kupeleka mapato yote Hazina. Hili lipo katika sekta ya maliasili na utalii ambapo inatakiwa asilimia 20 ibaki katika wilaya husika. Na ndiyo maana hata kwenye madini iliamriwa kuwa kila mgodi (kina Barrick) wazipe halmashauri walimo TZS 200m/- kwa mwaka, licha ya kushiriki katika miradi mingine ya kijamii. Je, hii inaelekea kwenye kutekeleza sera ya majimbo kwani mapato ya rasilimali katika eneo fulani yanabaki kwenye eneo husika?
6. Katika zama hizi za utandawazi-kidunia, inafaa pia tuhamasishe utandawazi wa ndani ya nchi, na hii pia ndiyo inasaidia kupunguza ukabila na kupanua uelewa wa watu wetu kuhusu nchi yetu kwa ujumla. Tupunguze ile hali ya Mtu kumaliza kidato cha nne Malangali, akaenda Chuo cha Ualimu Mkwawa, JKT Mafinga, na kuanza kufundisha shule ya msingi Tanangozi! Nadhani mfano wangu utaeleweka. Hapo ndipo utakubali kuwa kuna shule za msingi Kagera ambako wanafunzi masomo wanafundishwa masomo yote, ikiwemo Kiingereza na Kiswahili, kwa Kihaya! Nyerere na Marx bagamba ze seim! Yaani, "Nyerere na Karl Marx wanazungumza kitu kile kile kimoja."
Mawnagenzi,
1.Ipo tofauti kuba kati ya madaraka mikoani na sera ya majimbo. Madaraka mikoani ndio hizo serekali za mitaa, tumechanganya mifumo miwili kuna mrundikano na muingiliano wa kimajukumu na mgawanyo wa rasilimali baina ya viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa. Sera ya majimbo kama inavyopendekezwa na CHADEMA haijawahi kujaribiwa.
2.Ni kweli maamuzi yaamuliwa Dar-es-salaam, wao ndio wanatoa miongozo yote, maafisa elimu ni watekelezaji tu. Ndio maana tunawakaguzi wa kikanda huwa wanapita kuanagalia utekelezaji wa mipango toka Dar. Kwenye sera ya majimbo maamuzi ya elimu yatabaki majimboni, mipango itawekwa kuendeana na mazingira ya maeneo husika na sio kama sasa.
Ndio maana wakuu wa mikoa sita wameitwa na waziri mkuu Dar, kuhojiwa kwa nini wamehsindwa kutekeleza malengo/maagizo waliyopewa.Yaani Lowassa kapita wilaya kwa siku moja, akahoji kwa nini watoto hawaandikishi kwa wingi? Kwanini hamajenga madarasa? Hapo hapo anatoka na mpango ambao inabidi utekelezwe? Na nani? Ndio raha inapoaanzia waliochaguliwa wananchi wanaowajibika kwa wanachi au wateule wa raisi? Kwa rasilimali zipi? Toka serekali kuu au rasilimali za maeneo husika tokana na ushuru na mapato ya halamashauri? Ni mchanganyiko wa mambo.
3. Hawa viongozi tulio wachagua hawana nguvu kabisa. kumbuka wilayani tuna Meya(anachaguliwa na wawakilishi wa wananchi-madiwani na wabunge wa maeneo husika), madiwani(wachaguliwa na wananchi) Mkuu wa wilaya(anateuliwa na Raisi), Mkurugenzi wa manispaa(ambae huyu ni mtumishi wa manispaa lakini nae anateuliwa na raisi na sio kuajiriwa na halmashauri) tuna wataalam wengine kama Mganga mkuu wa wilaya(anapangwa na wizara husika) halikadhalika afisa elimu wa wilaya( anateuliwa na kupangiwa eneo la kazi na wizara husika). Halmashauri inaajiri maafisa mipango tu.
Ikumbukwe pia Waziri wa TAMISEMI na Wazira mkuu wana mamalaka ya kuzifuta hizi halmashauri na kueteu tume. Haya ndio yalifanyika Dar, wakati ule wa tume ya keenja! Viongozi wa kuteuliwa na nguvu kubwa mno dhidi ya wale wa kuchaguliwa.Pia sheria ndogo ndo zinazotungwa na halmashauri haziwezi kuwa sheria mpaka zipitishwe na Waziri wa TAMISEMI!!! Mfumo wetu ni kituko na kichekesho.
Ndio maana wilayani tuna: Mkuu wa wilaya(Mwanasiasa-Mteule wa Raisi), Meya(Mwanasiasa-Mteule wa wawakilishi wa wananchi), Mkurugenzi wa halmashauri(Mtaalaam na mteule wa rais), (Katibu tawala wa wilaya(DAS) Mtalaam na mteule wa raisi) mbunge(mwanasiasa-Anachaguliwa na wananchi) na Madiwani(Wanasiasa- wanachaguliwa na wananchi). Itakumbukwa kwamba ni wabunge na madiwani ambao hunadi mikakati yao ya kiamaendeleo(Ilani) na kupitishwa na wananchi. Kibaya ni kwamba baada ya uchaguzi hujikuta hawana rasilimali kutekeleza mikakati iliyopitishwa bali wateule(Wakuu wa wilaya) wasio na mikakati yoyote ya maeneo husika wala ridhaa ya wananchi. Ni kwa sababu hii wabunge na madiwani huamaua kuwa omba omba kwenye balozi na mashirika ya kimataifa ila kupata fedha kutekeleza mikakati yao iliyo kubaliwa na wananchi. AU wengine hugeuka mafadha Xmass kugawa misaada ya hapa na pale! Kwenye sara ya majimbo mameya wana nguvu na watakuwa na rasilimali kuetekeleza mikakati yao itakayokuwa imepitishwa na wananchi.
4. Hakuna haja ya ukiritimba na urasimu wa kupata ridhaa Dar-es-salaam juu ya waajiri wa halmashauri.
6. Barrick ni danganya toto, wanavuna kiasi gani? Na hizi halamshauri hazina nguvu na uhuru, bado zitakuwa zinaamuliwa toka Dar, zikataa kusalimu amri zinafutwa na kuundwa tume.
7. Sioni kwa jinsi gani majimbo yatazuia hali hiyo kuendelea. Na istoshe sasa hivi ndio kuna mtindo mbaya zaidi na wa kikabila. Wakati wa bajeti Mramba alitumia nafasi yake ya uwaziri wa miundo mbinu kupeleka UJENZI Barabara ya Bilioni 17 kugharimia barabara ilio chini ya halamshauri na sio serekali kuu huko jimboni kwao, Wasira nae akajibu mapigo kwa kupeleka zaidi ya milioni 250 kugharimia miradi ya maji jimboni kwake, ghrama ambayo ilizidi kiasi kilichotengwa kwenye mikoa kadhaa. Sasa huu ndio ukabali, uchoyo na ubinafsi. Chini ya mfumo wa majimbo mambo kama haya yanaepukwa.