Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Mwanasiasa,
Ni kweli kabisa demokrasia ni Universal - Principal are the same. Hata dira ya Uongozi kati ya vyama - Principal ni moja isipokuwa kila nchi kina tofauti zake ya njia zake kufikia Malengo yaliyokusudiwa.

Kiuchumi na hilo Soko huria ni moja ya mifumo ambayo imerudisha bara letu la Afrika miaka 30 nyuma ktk ukoloni mamboleo. Nchi nyingi za kiafrika zimerudi nyuma sana kimaendeleo kuliko wakati ule ila zimekuwa kifikra ktk biashara hii. Sababu kubwa tulikubali soko huru bila kuangalia nguvu ya soko letu nje kama TZ tulivyoukubali Ubwanyenye bila kujiandaa na athari zake.

Leo hii Tanzania inauza nje mara mia zaidi ya wakati wa Ujamaa lakini ni asilimia 5 tu ya mauzo hayo yanawagusa wananchi moja kwa moja. Kumbuka tanzania unakadiliwa kipato cha mwananchi ni dollar moja kwa siku!.. ONE DOLLAR sasa haya kweli maendeleo?

Big Corparates ndio wanazidi kuimarika zaidi wakitujengea sisi magorofa tujisikie. Vitu vya anasa, simu za mkono na kadhalika ambazo hakuna hata nchi moja ya kiafrika inatengeneza.
Tanzania leo hii hakuna mfanyakazi hata mmoja anayeweza kununua kiwanja kwa mshahara wake kwa urefu wa ajira yake acha uwezo wa kujenga hiyo nyumba.

Wazazi wetu waliweza kujenga kwa mishahara yao! wakalisha familia na sisi watoto tukapata muda wa kwenda shule Not today!

Kwa nini wewe na mimi tumesimama hapa kupinga uongozi wa CCM?... Yote haya nadhani yanatokana na mifumo mibaya ambayo imetekelezwa na CCM. lakini kutokubaliana kwetu na CCM haina maana tunapinga Principals za Soko huria.

Kwa hiyo mjomba sikatai kabisa kuwepo kwa Demokrasia Afrika isipokuwa zipo mbinu kubwa ambazo zinatakiwa kujengwa kwanza kabla ya hiyo demokrasia. Na mojawapo kubwa ni hiyo aliyoifanya Nyerere - Kuondoa Ukabila na Udini kwanza kisha tumeweza kusimamisha vyama vingi.
Hii ni moja ya tuzo ama faida kubwa alotuachia mwalimu na ubora huo unaanza kupotoshwa na baadhi ya makada wa vyama vyetu.

Mwanasiasa,
Napopinga ufugaji wa ng'ombe wa kizungu sina maana kuwa Afrika haturuhusiwi kufuga ng'ombe wala ati Afrika hatuna utamaduni huo bali nasisitiza unapogeza kitu chochote kile ni muhimu utazame kwanza mazingira yako!..Ndio yalee ya Sarakikya na ufugaji wa Farasi!.

Na Mkapa kusifia mtu kwa kuwa na shamba la ng'ombe wa kizungu hali kuna Wasumbwa akina Ngosha wana ng'ombe aina ya Zebu na Ankole 4000 bila shamba, hawapewi sifa zao wala kufikiriwa kutajirishwa.

Principal za Ufugaji hazibadiliki.
 
Kichwamaji,

Mimi nakuelewa vizuri sana labda wewe ndio bado.. ebu rudia kusoma maelezo yangu taratibu...

Tunapojenga hii hoja ya Majimbo, sioni kabisa kama itapunguza nguvu ya huyu rais ambaye kila wilaya itakuwa na Mbunge wake (most likely CCM) hata tuseme toka chama tofauti. Kwa nini kila mbunge asiwe ndiye DC na serikali kuu ipitishe matumizi ya wizara zake ki wilaya kulingana na mapendekezo ya mbunge? Do we have to form JIMBO kuweza kukamilisha huduma hizi kwa wananchi hata wa vijijini?. I don't think so! hawa watu mbunge hadi Gavana kutakuwa na patashika jingine pia!... we are Poor hilo msilisahau ULAJI ni kitu cha kwanza kwa kila Mdanganyika. Next election? who cares 5 years after nimeisha chota mtaji wa kutosha!
Ukimwondoa RC ambaye ni mwakilishi wa rais na kuweka Gavana ambaye machoni mwa watu atakuwa mwakilishi wa kule alikotoka! Huja solve kitu... Mhaya hawezi kukubali kuona Gavana Mkurya ati anamwakilisha yeye!..Wala hatuwezi kusema Gavana Mzaramo aliyehamia kanda ya juu (Moshi na Kilimanjaro) atapokelewa kama Mtanzania na ati yupo pale kuwaendeleza Wachagga, Kimajimbo!..

..

Mukandara,

Tusaidiane hapa. Magavana (au vyo vyote watakavyoitwa) wa Majimbo tunayojadili, HAWATATEULIWA na mtu yeyote; WATACHAGULIWA. Tunazungumzia viongozi wa kuchaguliwa na wananchi, wanaowajibika kwa wananchi. Ndiyo dhana yetu kwa sera ya majimbo. Na hii haiwezekani katika mfumo wa sasa. Hivyo, dawa ni kuuvunja huu na kutengeneza mwingine. Hakuna dhambi hapo.

Nadhani hoja hii inasaidia kumaliza nguvu za woga wako kuhusu ukabila. Mtu atachaguliwa kwa kukubalika kwake, kwa uwezo wake...pale anapoomba kura. Si kuletwa na kupachikwa cheo. Tunaogopa nini?

Kumbuka wakati nyie mnakataa na kuogopa majimbo kwa sababu yametetewa mno na Chadema, CCM wanazungumzia KANDA, ila wanakwamishwa na mfumo uliopo. Wazo lile lile, approach tofauti. Ndiyo maana nadhani pa kuanzia ni kufumua mfumo na kuweka mwingine utakaoruhusu hoja hizi kupenya na kutekelezwa.
 
Kichwamaji,

Rudia tena kusoma hoja yangu hapo juu vizuri na taratibu utaelewa vizuri kuwa nimesema hawa Magavana watachaguliwa na wananchi sikusema kuteuliwa hata kidogo.

Ila basi uloshindwa kuliona ni kwamba ktk kila jimbo kuna mikoa na makabila yake.

Mathlan, kanda ya ziwa:- haiwezekani kabisa kwa hali tuliyokuwa nayo Mhaya akamchagua Gavana toka usukumani akamwacha mgombea Mhaya mwenzake. Hivyo hivyo kwa Mjita wa Mara. Kwa hiyo hapa mshindi siku zote atakuwa mgombea toka kabila lenye watu wengi (population kubwa)ambalo ni mkoa wa Mwanza na Shinyanga (wasukuma).

Amini maneno yangu kuwa hii itakuwepo kama tunavyoona sasa hivi ktk uchaguzi wa wabunge.
Hivyo basi sidhani kama Mhaya na Mjita watakubali mfumo huu kuwa ni demokrasia baada ya muda wataanza matatizo!. Vile vile ni vigumu kwa Mchagga mkazi wa jimbo la Ziwa kugombea Ugavana watu wakamtazama kama Mtanzania kwa sababu Majimbo itaondoa kabisa Utanzania ambao mwalimu alisha ujenga.

Mchagga ataonekana kama mgeni anayekuja kuchuma mali (dhahabu za msukuma), Unless nyie Chadema mtakuja na mbinu ya kuhakikisha majimbo hayatakuwa na maana ya kuwaendeleza watu wa sehemu hizo mkianzisha Utawala wa majimbo.
Now, swali langu linakuja mtafanya nini?..mbinu gani imetayarishwa kuhakikisha mambo haya hayawezi kutokea.

Acha maswali mengi niliyowahi kuuliza huko nyuma ambayo bado hayana mbinu za kukomesha Utengano zaidi ya ahadi na hope. Hope bila vision sidhani kama ni utaratibu mzuri.

Vita ya siku hizi mshikaji sio kuwa na silaha tu bali hata zana za kujikinga ni muhimu sana. Tusje jidangaya kuwa Tanzania hatuwezi kuwa kama nchi nyingine kwa sababu tu ati hakuna Ukabila.. well hata baada ya Ujamaa wengi walifikiria kuwa hatuwezi kuwepo na mabepari weusi wasiokuwa na uzalendo wa mali ya Umma.

We were wrong!
 
Mwenyekiti Vijana NCCR aenda masomoni



na Happiness Katabazi


MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha NCCR-Mageuzi - Taifa, Bahati Tweve, wiki ijayo anatarajiwa kwenda nchini Uingereza kuchukua shahada ya pili katika fani ya sheria.


Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam, jana, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mafunzo wa NCCR, George Kahangwa, alisema akiwa nchini Uingereza, Tweve atasoma katika Chuo Kikuu cha Coventry, kwa kipindi cha mwaka mmoja.


Kahangwa alisema, kuondoka kwa mwenyekiti huyo, kunafanya nafasi yake kuwa wazi na Evaristo Haule, ambaye ni Katibu wa Idara ya Itikadi na Mfunzo –Taifa, atakaimu nafasi hiyo.


Mwaka juzi, Tweve, alihitimu shahada ya kwanza ya sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na kuajiriwa na Kampuni ya Uwakili ya Southern Law Chambers.
 
Elimu ni bora kuliko mali. ELIMU INAKULINDA, MALI UNAILINDA,elimu inaongezeka kadri unavyoitumia, mali inapungua kadri unavyoitumia.

Elimu haina mbadara. Chadema somesheni vijana.
 
Kwanza natanguliza pongezi zangu za dhati kwa wachangiaji wote katika kuchambua,kueleza, kudadisi na kuelimishana kuhusu mustakabali wa nchi yetu.La msingi ni kwa hao tuliowapa (au basi waliojitwalia) dhamana ya kutuongoza kuchukua na kuyaweka katika vitenda haya tuwaambiayo.

Naomba niongelee hayo matatu hapo juu (Majimbo, demokrasia na ukabila Tanzania ) bila ushabiki wa kivyama...yaani nitajaribu kuwa as neutral as neutral itself.

Sera ya Majimbo
Kulingana na mapungufu ya kiutendaji katika muundo wa serikali tulionao, sera ya majimbo inaonyesha inaweza kutoa suluhisho mbadala kwa hilo. Nisemapo upungufu wa kituendaji ninamaanisha ule wa kijiografia na kimiundombinu.Yaani kutokana na na ukubwa wa nchi yetu na ubovu wa miundombinu (barabara, reli,viwanja vya ndege n.k) huu mfumo wa Central Gov ya Dar es Salaam kuamua na kuongoza shughuli zote (mambo ya Halmashauri za miji/wilaya ni danganyatoto tu), unasababisha kudorora kwa maendeleo kusiko na lazima.

Tatizo:Hatajawahi kuwa na mfumo wa majimbo katika Tanzania huru. Hivo jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.Tena basi mfumo huu kokote duniani (kuna tofauti za kimiundo though) ulikojaribiwa umetoa success and failures (US, Germany, Japan, Nigeria and even Uganda) karibu sawa bina sawia. Hivo it is logical to worry of it!! Lakini ukichunguza kwa makini hatuna sababu za kuuogopa maana sababu zinazofanya mfumo huu ushindwe kuleta ufanisi (mfano Nigeria) ni za ukabila, udini, historia ambavo kwa pamoja tunasema geopolitics; tatizo ambalo kwetu sio kubwayou could say its marginal.

Katika suala zima la power struggle kati ya vyama vya siasa Tanzania (kama ilivo kokote duniani) lazima kutafuta mbinu za kumpaka matope mpinzani wako ili uendelee kukalia madaraka au uingie madarakani. Kwa hili CCM inatumia hii hali ya raia kutojua vizuri muundo na mafanikio wa utawala wa majimbo kuipaka matope CHADEMA.

Na zaidi ya hapo the political landscape of neighbouring countries na elimu hafifu ya wananchi walio wengi inainufaisha CCM katika campaign yake hii. Na huwezi kusema it is unfair a game!! Hiyo ndo power struggle yenyewe although it tends to go too far hapa kwetu!!

Suluhisho: Ni jukumu la CHADEMA (proponents of the MAJIMBO) kukaa chini na kudesign ni jinsi gani sera ya majimbo itafanyakazi ,faida inazotazamia kutuletea (zaidi ya huu mfumo wa sasa) na possible pitfalls zake na jinsi ya kukabiliana nazo...in black and white, cut and dry!!! Liwe tamko rasmi la chama na iwe ni sehemu ya manifesto ya 2010 campaign.

Onyesheni yatakuwepo majimbo mangapi, makao yake makuu yatakuwa wapi na ni mikoa au maeneo yepi yataunda majimbo yepi. Kutakuwa na viongozi wepi, watapatikanaje, mipaka madaraka yao na uhusiano wa majimbo na Central Gov. Na onyeshi pia kuwa hiyo ni subject to baraka za wananchi.

Najua mlieleza vya kutosha 2005 lakini nachelea kusema hamkueleweka au basi hamkutarajia such a negative connotation!! Inatakiwa kujipanga upya!! Kumbuka neno JIMBO halina tofauti sana kwa tafsiri na neno KANDA na au hata MKOA
Tumieni hizi blunders na hali ngumu ya maisha ya awamu hii for your gains

Demokrasia
Hili sintoliongelea sanaila napenda kuclear suala moja; nalo ni kuhusu mbinu za watawala wengi wa kiafrika kusema ati demokrasia ya nchi za magharibi haitufai au haiwezi kutekeleza Africa!! Huu ni uongo wa mchana kweupe.

Hapa nakubaliana kabisa na ndugu mwanasia (hapo juu). Misingi ya demokrasia ni ile ile kwa binadamu wote. Democrasy is all about respect to peoples decision, the right to choose and be chosen as a leader, freedom of expression, accountability of those in power, transparency ya watawala na mengine kama hayo na sidhani kama Africa (tofauti na kwingine koote duniani less Middle East) hatuyahitaji hayo!!!

Ukabila
Dhana ya ukabila imekuwa ikitumika kama cover up ya failures za serikali zetu na imekuwa silaha madhubuti katika kushambulia sera ya CHADEMA ya majimbo.

Yes makabila yapo na huwezi kuzuia watu kutambulikana kwa makabila yao maana kwanza ni sehemu ya utamaduni Na nakubali chembechembe za ukabila bado zipo Tanzania (e.g kwenye opportunities za ajira, elimu etc) lakini kwa kiasi kikubwa mtanzania hufikiri na hata kutenda kama mtanzania na wala sio kwa kabila lake. Kwanza unakuta watoto wengi (hapa sina statistics) hawajui lugha za makabila yaoKwa mtoto kama huyo ni vigumu sana kumweleza habari za ukabila akakuelewa.

Hivo kwa kuhitimisha katka hili, CHADEMA no hili lazima kulipa kipaumbele stahili; welezeni wananchi nao wakuelewenithat the ethnic landscape in Tanzania can not jeopardize the implementation of Majimbo.
 
Verily Verily,

Ndugu yangu haimchukui mtu kuwa mwanasayansi kuelewa kwamba wewe umaesimama upande gani?...
Nitagusia baadhi ya sehemu ulizoziweka kwa lugha yetu tuliosimama upande huu wa Upinzani wa Majimbo.

Kwanza nakupinga katika swala hili kwa sababu umechanganya mambo hapa. Umesahahu kuwa ni Central Government inayojenga miundombinu ya nchi nyingi kama sio zote na katika bajeti za majimbo hayohayo unayoyazungumzia hutegemea fedha kutoka serikali kuu. Miundombinu haijengwi kwa fedha za kodi ndogo inayopatikana ktk majimbo. It's billions of dollars inachukua dhamana ya taifa zima hasa nchi maskini kama Tanzania.

Pia inaonyesha wazi kuwa Majimbo tajiri yataweza kujijenga kwa kiwango fulani kuliko yale maskini kwani ujenzi wa barabara moja kuu ni mtaji (bugdet) wa Jimbo kwa miaka 20.

Pili, Ni huo huo mfumo uliopo wa serikali kuu ambayo umeondoa kabisa Ukabila na Udini nchini, jambo ambalo Nyerere kasifika na mataifa yote!Na leo hii tumesimama hapa tunajivuni ila kilichopungua ktk ujenzi wa taifa zima ni Uchumi wetu. Then why scrap mfumo uliojenga UMOJA wetu hali tatizo ni Uchumi?

Binafsi, naunga mkono kabisa mpango wa CCM leo hii wa kuunda Majimbo ya kiuchumi (Economic zones). Lakini hauwezi kubadilisha kitu ikiwa wanasiasa wataendelea kuweka mikono yao ktk maamuzi ya haya Majimbo ya kiuchumi badala ya kuacha Policy zao zifanye kazi yake..
Pia mimi nitakubaliana na mfumo wa Chadema ikiwa Wabunge na wilaya zao ndio watakuwa wawakilishi wa wananchi toka Bungeni hadi ktk maendeleo ya wilaya husika.

Mbunge ataondoa vyeo vya hao ma RC, DC (nguvu ya rais) na hata huyo Gavana, hali umeacha imara nguzo ya Utawala wa Nyerere ulioondoa Ukabila na udini. Pungufu la mfumo huu ni kwamba utapunguza tu matumizi mabaya ya fedha za umma, Kuondoa nguvu ya rais zaidi ya kujenga misingi mizuri ya Kiuchumi. More work ktk structure nzima inatakiwa.

Kinachonishangaza hapa ni kwamba Umaskini wetu umewekwa kama sio tatizo la TAIFA zima. Kwa mantiki ya hoja yako inaonyesha kuwa umaskini wetu unatokana na Ukubwa wa nchi kiutawala hali mapato ni yale yale yanayotakiwa ku-solve umaskini wa nchi nzima ktk mganawnyo wowote ule. Hapa sielewi kabisa mahesabu yanakwenda vipi zaidi ya kukisia kuwa kuna mikoa inayopendelewa!.

Nadhani hii sio kweli zaidi ya kusema kuwa viongozi wetu ndio wezi wetu. Utajiri wetu unaibiwa na VIONGOZI, viongozi ambao kesho watakuwa Magavana wetu na uwajibikaji wao utakuwa mgumu kutokana na hivi viji mila vyetu - Mwenye nacho ndiye mwenye sauti! lakini sio ukubwa wa nchi ama majukumu.

Kwa hiyo, ninakubaliana na hoja ya Chadema kuwa tatizo lipo ktk Utawala wa CCM na kikubwa zaidi ni - RUSHWA. Pili, nguvu ya rais ni kubwa sana kiasi kwamba wananchi hawana sauti chini ya hao ma RC na DC - Tumeyaona wenyewe ya Ditto. Hivyo basi, panga pangua mipaka ya nchi (giografia) bado tatizo ni kwamba JIZI ndiye kashika madaraka! -That's One.

Pili, kikubwa zaidi kinachotakiwa kuangaliwa ni mbinu ambazo zitatufanya, kuondoka ktk hii mikataba feki (Katiba) na Tatu - Kuongeza UZALISHAJI wetu (Utajirisho) ili kuwawezesha wananchi kujiendesha wenyewe na kuwasaidia kupata masoko nje bila wao kupitia kwa hawa wageni waliojazana nchi.

Sasa hivi exposure ya nje tu ni soko kubwa Tanzania kiasi kwamba ma - Nigeria matapeli wamejazana nchini kuwafunga kamba wananchi na serikali imeacha uwanja wazi. Tanzania imekuwa Killing zone ya KIUCHUMI.
Democrasy is all about respect to peoples decision, the right to choose and be chosen as a leader, freedom of expression, accountability of those in power, transparency.
.

Tunaelewa wote nini maana ya Demokrasia lakini kuna sehemu imeshindikana kusimama hata kama hatua zote zimechukuliwa. Ebu jiulize why umesema less middle east?

Ni kwa sababu unafuata demokrasia ya Mzungu! na hasa hiyo Freedom of expression lazima iwe ktk values zenu sio za mzungu. i.e. Mkristu anaweza ku-question aya ya Biblia lakini sio defamation of the name of Jesus ukasema bado ni Freedom of expression. Hiyo ni Blasphemy...Lakini hapo hapo kwa Makafiri demokrasia kwao ni kwa Nyamuhanga!

Principals ni zile zile hazibadiliki. Now, la kujiuliza sisi ni what are our values? then tujenge hoja kulingana na misingi hiyo!

Mwisho, ndugu Verily unataka Watanzania wavuke msitu wa Serengeti kwa mguu wasitegemee kuliwa na Simba ati kwa sababu msitu kama huo Huko nchi za Ulaya hakuna Simba wala wanyama wa hatari!

Nipe kinga kwanza tutaelewana lakini hujanivusha kwa miguu mitupu hali wewe umekaa Ikulu.
 
Mh Mkandara,

Nashukuru kwa maelezo yako ya haja nitajaribu kuyachambua kinagaubaga hapo baadae ila kama umesoma vizuri maelezo yangu utangundua kuwa tunaongea kitu kimoja katika mitazamo tofauti kidogo.Na natanguliza sahamani kama nimeonekana kuchukua upande--basi halikuwa lengo langu kabisa.Mpaka hapa nitaendelea kuwa as neutral as neutral itself.

Kwamba mfumo wa majimbo is unprecedented in post-colonial Tanzania, kwamba hatujui risks zake na faida zake in our own environments etc hayo tunakubaliana. Na ndio maana nimewataka/washauri CHADEMA watupatie muundo na utekelezaji wake ili sisi tupime potentials and risks.

Kwamba madaraka ya raisi (tusisahau na watendaji wake kuanzia PM, mawaziri, RC,DC all the way mpaka ngazi ya vijiji na vitongoji) ni makubwa mno kwa muundo uliopo sasa hilo tunakubaliana.

Japo sikugusia habari za RUSHWA (wasn't my topic of discussion) ila nakubaliana na wewe kwa asilimia zote kuwa rushwa itaendela kuwa STUMBLING BLOCK kwa serikali zote bila kujali ni ya chama gani na mfumo gani.

Tena hilo la rushwa litahita mjadala wa peke yake maana rushwa ina even broader definition, hutakiwa na hutolewa kwa mbinu nyingi, huchukuwa sura nyingi sana zaidi ya wengi tunavoichukulia.
Nitarudi baadae mkuu
 
Verily Verily,
Na mimi nasema pia samahani...Kumradhi kwa kukupa upande hali wewe huoni hivyo. Yote imetokana na kusoma maoni yako ktk Majimbo inayosema:- Sera ya majimbo inaonyesha inaweza kutoa suluhisho mbadala.
Pia ktk makabila:- Dhana ya ukabila imekuwa ikitumika kama cover up ya failures za serikali zetu na imekuwa silaha madhubuti katika kushambulia sera ya CHADEMA ya majimbo.

Utangulizi huo ulinipa picha, kwanza tunapinga ndio haooo upande wa CCM hali unaelewa kuwa hili sio swala dogo la CCM na tupuuze kabisa tukitegemea miujiza ya Mungu toka upande wa pili.
Anyway, wakati wa mitume umekwisha, miujiza ya leo ni Ubunifu wenye vision na nafasi ya kufanya makosa ni ndogo sana.

Wewe tazama kama huo mradi wa Rada mhindi kaingiza USd 12/m kupitia waziri mkuu!..hapa majimbo yatasaidia kitu gani? ndege za rais, Richmond, IPTL, Mabenki, ATC, City Water, misafara ya rais zaidi ya arobaini kwa muda wa mwaka mmoja tu. Yote haya yapo nje ya nguvu ya bunge letu acha huko kwenye Majimbo. na mbunge aliuliza huambiwa - Kaa pembeni kijana bunge umelikuta! na ukizidi sana utaitishiwa kikao na kubabikwa kesi.

Mbinu ni kuondoa kabisa penyo zote hata maji yasiweze kupita kirahisi.
Kiutawala:- Changes lazima zianze ktk katiba, nguvu ya Bunge na madaraka ya wawakilishi ya Wananchi. Solution zake nimezisema wazi sio kupinga tu mfumo wa CCM - Huo ndio Uhuru tunaopigania leo sio wa bendera (mikapa)

Kiuchumi:- Hapa lazima tukubali kwanza kuwa Umaskini wetu ni wa Taifa zima. Mizizi yake ndiyo hiyo...Rushwa, mikataba feki, na Kubebana!... Dawa yake naweza kukubali kuwa inaanza juu kwa RAIS kushuka chini..Kwanza tunahitaji kiongozi Mwana mapinduzi - Freeman ana fit kabisa nafasi hiyo isipokuwa bado zinatakiwa mbinu nzito za kuwavuta wananchi.. MIUJIZA ya Kileo!

Labda baada ya kushika serikali kama mkijaaliwa miaka hiyooo ndipo mnaweza kufikiria Majimbo na project nzima itakuwa ktk majaribio kwa miaka kumi kama ilivyokuwa madaraka mikoani. nacho waasa - msitumie kabisa Majimbo kama moja ya sera zetu!... ni kosa kubwa sana sawa na CUF wanadai Uhuru wa Zanzibar wakiwa na makada waarabu wa Pemba kisha wanadai wao chama chenye makao yake makuu bara.

Wananchi sio wajinga kushindwa kuona Upemba (ukabila) ndani yake na hata kuchuliwa kuwa CUF ni chama cha waislaam. They (CUF) could be very right on the money lakini wanafanya makosa kuanika na kutangaza sera za Utenganishi wakati wa uchaguzi. Wanakunywa sumu yao wenyewe!

As Political party should stick to your goals as - Conservative! Tena basi kwa kuongezea kama alivyosema Mwl. Nyerere na Siasa yetu ya Ujamaa kuwa ina mfumo wa kiafrika basi nyie mtakuwa Conservative wenye mfumo wa Kiafrika.
 
Mkandara,
Nimerudi si unajua tena at the end of the day lazima mkono uende kinywani?
Wewe kweli kiboko lazima nikiri. Wakati najiandaa kujibu post yako ya kwanza tayari umeishashusha na ya pili tena iliyoshiba nondo haswa.

Narudia kuweka bayana kuwa naongea kwa maslahi ya taifa wala si kwa chama chochote kile cha siasa. Umesema kuwa nilionekana kutake side kwa vile niliandiaka:
Sera ya majimbo inaonyesha inaweza kutoa suluhisho na pia Dhana ya ukabila imekuwa ikitumika kama cover up ya failures za serikali zetu na imekuwa silaha madhubuti katika kushambulia sera ya CHADEMA ya majimbo

Lakini kama umeangalia kwenye hiyo hiyo post mahali fulani nimendika

Hatujawahi kuwa na mfumo wa majimbo katika Tanzania huru. Hivo jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.Tena basi mfumo huu kokote duniani (kuna tofauti za kimiundo though) ulikojaribiwa umetoa success and failures (US, Germany, Japan, Nigeria and even Uganda) karibu sawa bina sawia. Hivo it is logical to worry of it!!

Na nikaendelea pia

Na zaidi ya hapo the political landscape of neighbouring countries na elimu hafifu ya wananchi walio wengi inainufaisha CCM katika campaign yake hii. Na huwezi kusema it is unfair a game!! Hiyo ndo power struggle yenyewe although it tends to go too far hapa kwetu!!


Kwa hiyo ukiangalia vizuri nilikuwa naagalia pande zote za shilingi. Na kama nimeonekana kuwa upande wa CHADEMA (implied meaning of your post) basi ni katika kutafuta kona nyingine isiyojaribiwa bado au exploring other options. Na hapa nasema wazi kwamba mpaka hapo CHADEMA itakapotuconvince beyond reasonable doubt kwamba sera ya majimbo itatutoa hapa tulipo na kutupeleka hatua kadhaa mbele, bado sera ya majimbo itaendelea kuwa kitendawili na bakora mahsusi itakayotumiwa na chama tawala na hata vyama vingine against CHADEMA. Ushauri tumeishaweka wote.

Kumbuka hapa sijagusia sababu kuu zinazotufanya maskini wa kutupwa (hili jina wajameni linaudhi!!) pamoja na baraka zote za maliasili tulijaaliwa na muumba.

Umeongea kwa kirefu sana kuonyesha kuwa RUSHWA ndo adui wetu mkuu wa maendeleo. Kwa hilo niko pamoja na wewe asilimia zote!! Lakini pia usisahau kuwa zipo sababu nyingine ama synergistically ama independently zinaturudisha nyuma kiuchumi;mojawapo likiwa hilo la muundo wa kiuongozimaamuzi yote kufanywa na Rais na watendaji wote. Mfumo usioshirikisha wananchi.

Mkandara najua wewe ni muumini mkubwa sana wa Mwalimu na sera zake. Sote tuanakiri kuwa wakati wa Mwalimu hizi grand corruptions zilikuwa nadra kwa kiasi kikubwa (ukiachilia mbali uzembe na kutokuwajibishwa kwa viongozi ambayo pia ni form mojawapo ya rushwa!). Lakini unakumbuka pia kuwa kipindi hiko hatukuwa na neema sana kiuchumi kwamba rushwa ilikuwa chini basi uchumi wetu ulikuwa imara. Hapa najua hatukubaliani sana ila ndo hali halisi yenyewe kwamba watu hawakuwa na uwezo wa kununua hata chumvi, sabuni wala mafuta ya kibatari. Ukivaa kiatu basi wewe ni motto wa mzito Fulani. Lakini pia nikiri kuwa kwa kiasi fulani uchumi wetu ulikuwa imara say thamani ya shillingi, uwezo wa kusomesha watoto wote elimu ya msingi,hatukuwa tegemezi kiasi tulivo leo hii n.k. Kwa maelezo haya nataka nieleweke kuwa zipo sababu nyingi zinazoturudisha nyuma na RUSHWA ikiwa at the top of the list.

Mfumo wa utawala unaweza kuwa chanzo cha ufanisi mdongo wa utendaji wa serikali lakini zipo sababu nyingine lukuki. Nyingi katika hizo zikiingiliana na kuwa na multiplicative effect.

Mfano mdogo hapa:
Centralized gov (tatizo mojawapo say namba moja, japo sio kwa umuhimu) inasababisha ushindani mdogo wa ujenzi wa mashule na kuajili walimu wa chache (hapa elimu hafifutatizo namba mbili) hili tatizo namba mbili linasabisha kuwa na taifa la watu mbumbumbu wasio na uelewa wala uwezo wa kuhoji blunders za serikali yao (hapa Rushwa and unaccountable governmenttatizo namba tatu) hili linasababisha kuwa na elimu hafifu (tatizo namba mbili hilitayari ni vicious cycle).

Tatizo namba mbili pia linababisha low human capital (tatizo namba nne) ambayo in turn inababisha low income nayo inarudi kwenye tatizo namba mbili pamoja na taifa la watu wagonjwa (tatizo namba tano). Matatizo nne na tano yanarutubisha tatizo mbili, na tatu). Yote hayo yanasababisha tatizo namba sita nalo ni watu maskini wa mali, fikra na matumaini. I can go on and on with this aligorithm...
Kwa hiyo kwa ufupi ndugu yangu matatizo yetu ni mengi, yana such intricated and inspissated profile but one thing for sure they can be solved, definitely tukianzia na hilo la RUSHWA!!

Masuala ya uzembe (hili ni kwa wote wawe watawala ama watawaliwa mfano angalia huko ughaibuni Wanigeria, Waghana na hata Wakenya walivo aggressive na wanavo-own ventures kubwa kubwa), ubinafsi (ndo lile la Dr Bundala la fikra jumuiya), globalization na negative forces za mabwanyenye wanaotawala hii dunia, historia ya ukoloni na fikra tegemezi ni masuala mazito sana yanayotufanya tupige marktime tu bila kwenda mbele au sana sana kudidimia zaidi.

Mwisho, Bw Mkandara najua una upeo mkubwa sana wa masuala haya ya uchumi, maendeleo na siasa. Naomba mtazamo wako katika haya mawili:

1) Miaka ya mwanzoni mwa 60s uchumi na vipato vya mataifa mengi ya kiafrika ulikuwa sawa sawa kabisa (au tofauti kiduchu) na wa mataifa kama ya Korea kusini, Japan, China, Thailand n.k lakini leo hii sijui wametutupa karne ngapi vile Unasemaje tatizo hasa ni nini kwa upande wa Afrika na ufanisi hasa unatokana na nini kwa hawa waasia? Je utumwa na ukoloni peke ndo vikwazo kwetu? Kama ni ubnafsi wa watawala na watawaliwa, je tatizo ni la maumbile au? Au kuna sababu gain nyingine?

2) Tuchukuwe mfano nchi yetu ya Tanzania. Kama ungetokea kuwa rais wa nchi au tungetokea kumpata rais makini, hebu tupe maoni yako ni nini kingeweza kufanyika kwa priorities zipi na kwa measurable actions zipi ili kuleta ahueni ya maisha na maendeleo kwa ujumla.

Kama kuna short term na long term measure usisite kutuhabarisha katika mtazamo huo

Du kwa leo naishia hapa naona tumeivamia thread ya wenyewe wakati wanafunga mahesabu!!
 
Verily Verily,

Duuuuh ama kweli umenizidi kete hapa, hayo maswali nitakujibu pamoja na kwamba ni mambo mazito sana. Kwanza kabisa inabidi niweke sawa maelezo yako kwamba wakati wa Nyerere - Watu walikuwa hawana fedha..Sii kweli!

Wakati wa Nyerere watu walikuwa na fedha isipokuwa vitu ndivyo vilikuwa adimu. Kumbuka wakati ule Nyerere alihakikisha kila mwanafunzi aliyemaliza kidato cha sita anapata kazi acha hao wa University. Mfumo huu kiuchumi haukuwa mfano mzuri kwani serikali ililipa mishahara mingi hali returns yake ndogo sana.

Tatizo kubwa sana lilikuwa kushindakana kwa kuijenga nchi yetu ktk viwanda... Viwanda vingi vilivyoanzishwa vilianza vizuri sana lakini kwa sababu havikuwa na ushindani pia soko dogo vilianza kuchemsha!. Sukari,matairi na hata chunvi zilikuwa zikipelekwa kwa magendo nchi za jirani.

Kila kilichozalishwa nchini toka viwanda hivi kilikuwa hotcake nje na walanguzi waliikausha nchi kabisa bila kujali ndugu zao wanakula nini.

Again wakati pato la taifa linashuka watu hawakupunguzwa kazi kwa sababu JUWATA yenyewe ni serikali acha mbali kutafuta mbinu mpya za kujikwamua. Yaani Nyerere ktk uchumi alichemsha sana na wasomi wake wote mimi bado nawaona Malimbukeni tu kwani ukiwasikia maoni yao wengi ilikuwa tukubali madai ya IMF na masharti ya mikopo yake badala ya kumshauri rais wetu kuwa serilkali kuachana kabisa na miradi yote inayohusiana na biashara na kujikita zaidi ktk Miundombinu na huduma.

Kuwatajirisha wananchi hasa (wazawa) ili waweze kushindana nje. Mimi siwezi kuumwa roho kabisa ikiwa mzawa (Mengi) atakuwa tajiri wa kutupa lakini mwajiri mzuri wa Watanzania 2,000 analipa kodi na fedha zake zinakwenda benki zetu kuanza mzunguko mpya!
Hapa nitarudi nyuma kumpa pongezi mzee wetu Mtei kwa ujasiri wake pamoja na kwamba swala la IMF aliliweka mbele kama mkongojo wa kilema chetu cha uchumi, hapo kidogo naona walakini! -Nitaelezea mbele ya safari.

Ulipaji kodi pia ulikuwa kilema kingine kwani waliolipa kodi halali walikuwa wafanyakazi tu lakini sii wafanya biashara.

Wakenya, Nigeria na wengineo wametuzidi hapo kwani serikali zao zilikuwa tayari zimeisha weka sawa vitu hivi na hadi leo zinawaendelea kuwatajirisha wananchi wake pamoja na kuwepo chaochao la nguvu (petty corruption).

Turudi ktk maswali yako!
Kwa maoni yangu, swali lako la kwanza halina jibu zaidi ya viongozi wetu na hasa CCM kukurupuka na Utandawazi kabla ya kujiandaa. Viwanda vyetu viliisha kufa, kilimo ktk hali ya chini na wananchi kielemu ndio usiseme.

Sasa wewe nambie kweli uliisha ona mtu akiingia ktk mashindano akiwa mgonjwa ama ana kilema!..Utandawazi sii mchezo mdogo ni mchezo mchafu sana wa biashara, ni uwanja wa Darwin's hilo moja ilikuwaje sisi tuingie ktk Utandawazi hali kiuchumi tulikuwa wagonjwa wa kulazwa hospitali..IMF sii daktari mzuri hata siku moja! -Hakuna daktari mzuri atakaye tibu mgonjwa akaomba one night stand na mkeo hiyo sii tiba tena! Na anajua mkeo akisha onja ndio imetoka tena..Mali yake!

Pili, ni kwamba tukitazama kwanza nchi zote za Kijamaa hakuna hata moja ambayo leo hii uchumi wake haukuwi zaidi ya asilimia 6 hadi 7. Kwa sababu hiyo hiyo milango ilikuwa imefungwa na sasa imefunguliwa.. hesabu lazima itakuwa kubwa ikipanda kila mwaka maanake umetoka zero au Minus!

Tofauti kubwa kati yetu na wao ni kwamba wenzetu waliisha jiandaa na hawakufuata uchumi wa vitabu peke yake!.. Ujanja wa biashara.

Chukulia China, kabla ya wao kujiingiza katika Utandawazi karibu 70% ya viwanda vyake vilikwisha lala kabisaaa! Viwanda vya nguo havikuwa na kazi kama Bongo lakini walipoingia tu kwanza walianza na kutoa vitu fake kuyajaza masoko ya Ulaya.. na hivi viwanda viko chini ya serikali hivyoo!.

Kuna nchi za Ulaya zilipiga marufuku kabisa mali za China lakini ndi hivyo soko linapokuwa wazi huwezi kuzuia kila kitu. Wachina walimiminika kwa Mamillioni nchi za nje (program za serikali kupitia mafia zao) kwenda kusoma na kufungua miradi ya wizi wa teknologia. Haya yote ni ktk kuelewa kuwa Utandawazi ni uwanja wa mashindano!..Bongo hadi leo hii hatuelewi lugha hii kabisa zaidi ya kufikiria kuwa Utandawazi ni uwezo wa kuajaza nchi mali toka nje! na benki zetu zinasisitiza mikopo ya uagizaji badala ya ile ya uzalishaji...kumbuka tu hizi ni benki zilizotoka nje. kaliwa nani?

Ulimbukeni na elimu ya kushikiwa nadhani pia ni adui mkubwa sana wa maendeleo ya Mdanganyika.
Tatizo la Afrika nzima ni UBINAFSI - ambao umeambatana na RUSHWA... Ni kawaida kabisa kwa kiongozi wa kiafrika kuiba USd 2/m ktk deal moja tu tena mradi mbovu tulio bambikwa na kitu used.

Kuna viongozi wana worth USd 200/m in cash ktk benki za Ulaya jambo ambalo huwezi kabisa kuona nchi za wenzetu ambao utajiri wao ni pamoja investment na Assets lakini sio cash bank hali mtu huyu hana kampuni ya kimataifa. Sii kiongozi mmoja tu bali viongozi wetu wanashindana accounts zao nje ukubwa.

Who is the man na kicheko kikubwaaa! Naweza kusema kuwa marais wa Afrika wote wana fedha benki in cash kuliko Bill gates lakini hawana investment za uhakika kuliko P. Diddy... utachoka mwenyewe na akili za wasomi wetu.
Swali la Pili, majibu ya swali hili yamo humu mjomba... humu JF... kumetolewa majibu kibao ya kila aina na uzito!

mada nyingi zimeeleza mengi mazito na yenye kutia moyo..pia hutuba za baadhi viongozi na wataalam zinaweza kuwa mwanga mzuri sana kwa kiongozi.
 
Mkandara na Mzee Verily Verily,

Kazi nzuri, kunako mwisho wa wiki nitaweza kuwajoin nitoe angalau senti 2 zangu kwa sasa nimetingwa ila ninawasoma wote na ninawapa big up!

FD
 
Mkandara,
Asante sana kwa uchambuzi wako murua kabisa. Mkuu FD karibu tena na pole na kutingwa, kwanza weka mambo sawa na ukishakuwa tayari unakaribishwa tujaribu kutafuna huu mfupa (siasa na maendeleo) uliwashinda “fisi” wote wa Afrika!!

Mkandara,
Bado natafakari majibu yako, kuwaza na kuwazua matatizo yetu kama watanzania na waafrika kwa ujumla wetu.Unajua a problem known is half solved! Ila kwa sasa kama mzee FD nami nimetingwa kiasi ila panapo majaliwa nitashuka na uchambuzi wangu hapo baadae. Nondo zako hakika zimetulia lililobaki ni kwa hao watawala kuyaweka katika vitendo.

Matatizo yetu ni mengi sana. Ni mengi katika hesabu yake na ngeli zake. Yanaingiliana sana na kurutubisha kama tulivosema katika post zilizotangulia kiasi mpaka inakuwa vigumu kusema kwamba ufumbuzi wake uanze na hili au lile. Na baya zaidi ngeli zake ni nyingi kiasi nyingine hatufahamu marefu na pana yake. Mfano mdogo tu ukimwuliza msomi aliyebobea katika fani ya kilimo na uzalishaji mali kama hali ya hewa ya bara la afrika ni balaa au ni baraka katika kilimo huwezi kupata jibu mwafaka au jibu lenye kutoa mwelekeo wa namna ya kutatua tatizo.Na walio wengi watakwambia hawajui kama wana guts kuweza kukiri! Na mtaalamu wa mifugo vivo hivo hana hakika kama zebu au hao wa kizungu wanaweza kufaa katika kuongeza mazao yatokanayo na mifugo.

Ukimwuliza daktari aliyebobea kwenye Disease Control and Prevention kwa nini hatuwezi kutokomeza malaria utapigwa lecture mpaka ukimbie mwenyewe but at the end nothing tangiable!! Au je kama elimu ndo msingi wa hayo maendeleo, kama watoto wote watapatiwa elimu mpaka chuo kikuu ni solution ya tatizo bado hutapata quantifiable estimates. Hapo Mzee Moshi itabidi atusaidie. Hiyo ni michache katika mingi ya mifano hai ya mnyumbuliko wa matatizo yetu.

Katika mkanganyiko huo inakuwa ni vigumu kuweka priorities. Baadae nitatoa mchango wangu katika mkabala huo.
 
Verily Verily na Mkandara, Nafurahia michango yenu. Wakati naendelea kutafakari juu ya changamoto mlizo toa, na post makala ya BW. Masinde(MwanaCHADEMA) ambayo inatoa uchambuzi wa kina wa sera ya Majimbo.
Tembelea:http://www.chadema.net/nyaraka/sera/majimbo1.php

WATANZANIA TUKUBALI KUWA KUNAHITAJIKA KUWEPO MABADILIKO KATIKA MFUMO NA MUUNDO WA TAWALA ZA MIKOA!

TUONDOKANE NA “MAZOEA TU”








Mheshimiwa Sylvester K. Masinde anafafanua Sera ya Utawala wa Majimbo na kutoa mtazamo wake juu ya Sera hii baada ya kufuatilia kwa makini malengo ya Chama na maoni ya Watanzania.






Miaka 44 sasa baada ya nchi yetu kuwa huru, hatuna haja wala ulazima wa kuendelea kukumbatia mfumo na muundo wa Tawala za Mikoa tuliorithi kutoka kwa wakoloni. Ni muundo wa kuwa na mamlaka (Rulership) juu ya watu kama ilivyokuwa wakati wa Tanganyika ya Ukoloni. Utawala wetu sasa unatakiwa kuwa wa kuongoza watu (Leadership).


Nyakati za mfumo wa siasa za Chama Kimoja na Dhana ya Chama kushika hatamu za utawala wa nchi, muundo wa tawala za mikoa uliendelezwa kwa maslahi ya kiitikiadi. Wakati huu wa zama na udikiteta wa kisiasa, muundo huu ulitumika kuunganisha mamlaka na madaraka ya utawala na shughuli za chama. Kwa ajili hii chama kiliweza kudhibiti Nguvu ya Umma kwa kuwanyima watu fursa ya kupata na kujua maoni na mitazamo tofauti ya kisiasa. Chama kilichukua nafasi ya kuwa kiunganishi cha jamii ya Watanzania badala ya serikali. Serikali ilifanywa chombo cha kutumiwa na chama badala ya kuwa chombo cha watu, raia huru wa nchi.


Leo CCM na Serikali zake vinatetea na kuukumbatia mfumo na muundo huu kwa maslahi ya kisiasa tu na siyo kwa sababu ya ufanisi wa kuwaendeleza wananchi kimaisha. Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kama watu binafsi hawawezi kuwaendeleza watu zaidi ya kuwatawala.

Serikali za Mitaa na siyo Tawala za Mikoa ndilo jibu sahihi katika kuleta ufanisi wa kuwaendeleza Watanzania. Wakuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya wako na wanajishughulisha zaidi na maslahi ya kisiasa ya chama chao na ndio maana uteuzi wao ni wa kiitikadi zaidi ya taaluma, ujuzi na uzoefu wa maswala ya utawala. Ni vema ikumbukwe kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ndiyo nguzo za kuwezesha CCM kushinda uchaguzi. CCM na Serikali zake hawako tayari kuzifanya nyadhifa hizi kuwa za kitendaji katika utumishi Serikalini. Hii ni kwa sababu wanaogopa kupoteza nguvu hii kubwa ya kisiasa.


MANENO “JIMBO” NA “MKOA”
Maneno “Jimbo” na “Mkoa” kimsingi yana maana moja. Yote yana maana ya “eneo” katika mgawanyo wa nchi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za Serikali/utawala. Maneno haya yanatumika kwa kubadilishana (Interchangeably).


Katika lugha ya kiingereza neno “Jimbo” lina tafsiri ya “Province” na neno “Mkoa” lina tafsiri ya “Region” lakini kiutawala yote yana maana ya aina moja ile ile ya eneo la kiutawala. Wakati Tanganyika (Tanzania Bara) inapata uhuru, neno “Jimbo” ndilo lilikuwa linatumika na Tanganyika ilikuwa imegawanywa katika majimbo nane. Neno “Jimbo” lilibadilishwa baada ya uhuru na neno “Mkoa”. Huenda kubadilisha matumizi ya neno “Jimbo” kuwa “Mkoa” ulikuwa uamuzi wa kisiasa tu ili kuondoa fikra za “utawala” wa kikoloni. Kwa bahati mbaya kubadili neno “Jimbo” kuwa “Mkoa” hakukuenenda na mabadiliko ya misingi ya utawala wenyewe, yaani misingi ya mamlaka juu ya jamii chini ya mtu mmoja. Hiyo mtu anaweza kutumia “Tawala za Mikoa” au “Tawala za Majimbo” kwa maana moja ile ile.

“UONGOZI” DHIDI YA “UTAWALA”
Kabla ya kujadili misingi na malengo ya dhana ya “Uongozi wa Kijimbo” dhidi ya “Tawala za Mikoa” ni budi tuelewe tofauti ya kuongoza na kutawala. Kuwatawala watu au jamii fulani ya watu kunaweza kutokana ama kutotokana na ridhaa ya watu hao. Lakini kuwaongoza watu au jamii wakati wote kunahitaji na kunatokana na ridhaa ya aina fulani ya watu husika.

Machifu wetu na wakoloni walitutawala bila ridhaa yetu. Majeshi yanapotumia nguvu ya mtutu wa bunduki kushika mamlaka na madaraka ya kuendesha nchi hayapati kwanza ridhaa ya watu. Husimika “utawala” wa kijeshi bila ridhaa ya watu. Gavana wa Kiingereza na Makamishena wa Majimbo yake manane ya Tanganyika walikuwa watawala wa Watanganyika kwa niaba ya mamlaka ya utawala wa Uingereza, utawala wa Kifalme.


Kutawala, kimsingi, ni kuwa na mamlaka na madaraka juu ya watu wengine hata kama watu hao hawahiari hivyo. “Utawala” ni kuwa na madaraka juu ya jamii na mtawala anaweza kuwa mtu binafsi au kundi la watu. Kwa lugha ya kiingereza “utawala” wa aina hii ni “Rulership”, Lakini neno “utawala” linatumika pia kwa maana ya “uendeshaji” (Administration). Ndiyo maana sheria ya Tawala za Mikoa kwa kiingereza inaitwa “Regional Government Administration Act".

Kwa upande mwingine, neno “Uongozi” unatokana na ridhaa ya watu au jamii husika. Mamlaka na madaraka ya kiongozi yanatokana na ridhaa ya watu/jamii moja kwa moja ama kupitia uwakilishi wao. Watawala wa aina ya Rulership huendesha mambo kwa kutumia zaidi sheria na kanuni walizoziweka wao wenyewe. Lakini viongozi watawala huendesha mambo kwa kutumia sheria na kanuni zilizowekwa na jamii yenyewe kwa utaratibu maalumu, uliokubalika.

Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya kidemokrasia. Kwa mantiki hii Watanzania wanaongozwa, hawatawaliwi tena.


Rais wetu ni “Kiongozi Mkuu” wa Nchi, siyo “Mtawala Mkuu” kama alivyokuwa Gavana wa Kiingereza. Hii ni kwa sababu Rais anatokana na ridhaa ya Watanzania kupitia uchaguzi wa kidemokrasia. Rais wetu ana kofia mbili za uongozi. Ana uongozi wa kisiasa (Government Political Leadership) na ana uongozi wa uendeshaji Serikali (Government Administration Leadership).

Katika kuendesha uongozi wa nchi na watu wake, Rais huteua timu kuu mbili za kumsaidia. Timu ya kwanza inapewa jukumu la uongozi wa kisiasa. Timu hii ni “Baraza la Mawaziri”. Timu ya pili inapewa jukumu la uongozi wa uendeshaji shughuli za serikali. Hawa ni Makatibu Wakuu wa Wizara, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Idara na Wakala Kuu za Serikali zinazojitegemea/zinazojiendesha na Maafisa wengine waandamizi kama Makamishna na Wakurugenzi katika utumishi wa Serikali.

Baraza la Mawaziri huteuliwa kutoka miongoni mwa wabunge ambao wana ridhaa ya jamii kupitia uchaguzi. Rais pia ana ridhaa ya kuteua watu kuwa Wabunge na kisha kuwapa dhamana ya Uwaziri. Rais hufanya hivyo kwa kutumia mamlaka aliyopewa kikatiba na kisheria kupitia Bunge, chombo kinachotegemewa kuwakilisha sauti ya watu.


Rais anategemewa kuteua viongozi wa uendeshaji wa shughuli za Serikali kutoka miongoni mwa Watanzania walio katika utumishi wa umma kwa kuzingatia taaluma zao, uzoefu na ujuzi wao na uadilifu wao katika jamii na katika utumishi wa umma.

Kwa hiyo kimsingi mfumo wa uendeshaji shughuli za nchi yetu ni wa “Ki-uongozi” na siyo kwa “Ki-utawala”; Vivyo hivyo Mikoani kunahitajika kuwepo uendeshaji wa ki-uongozi badala ya utawala wa Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya.
UKAMISHNA WA MAJIMBO NA WILAYA WAKATI WA UKOLONI NA
UKUU WA MKOA NA WILAYA WA LEO
Makamishna wa majimbo na wilaya waliteuliwa na mamlaka ya utawala wa Uingereza kupitia Ofisi ya makoloni. Makamishna wa majimbo waliwajibika kiutendaji kwa Gavana. Makamishna wa majimbo walikuwa na mamlaka na madaraka ya kisiasa, ya kiuendeshaji/kiutendaji, ya kipolisi na hata ya kimahakama. Walikuwa watawala wa kweli kweli.


Wakuu wa Mikoa wanateuliwa na Rais. Kiutendaji wanawajibika kwa Rais kupitia Waziri Mkuu. Kama walivyokuwa Makamishna wa Majimbo, Wakuu wa Mikoa pia wana mamlaka na madaraka ya kisiasa na kiuendeshaji/kitendaji na ya kipolisi (kama kutoa amri mtu kukamatwa na kushtakiwa) ila hawana madaraka ya kimahakama tu. Kwa hiyo nao ni watawala tu siyo viongozi.


Kama alivyo Waziri kwa Wizara yake ndivyo alivyo pia Mkuu wa Mkoa kwa Mkoa wake. Wote wanamwakilisha Rais katika maswala ya kisiasa na ya uendeshaji shughuli za Serikali. Lakini tofauti na Waziri, Mkuu wa mkoa hatokani na ridhaa ya wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia. Hii ndiyo kasoro ya kwanza kubwa na ya msingi sana inayokusudiwa kuzibwa na Dhana ya Uongozi wa Kijimbo.

UTAWALA WA KIJIMBO NA TAWALA ZA MIKOA
DHIDI YA SERIKALI ZA MITAA
Serikali za mitaa zilikuwapo hata kabla na wakati wa ukoloni. Wakoloni wa Kijerumani walikuta tawala za Jadi nchini Tanganyika. Hawakuziamini na kwa hiyo wakaweka mawakala wao walioitwa MAAKIDA.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya Dunia, wakoloni wa kiingereza walichukua nafasi ya Wajerumani. Lakini tofauti na Wajerumani, wao walizitambua Tawala za Jadi za Machifu. Wakoloni hawa wa Kiingereza walithubutu hata kusimika machifu wa Jadi pale ambapo hawakuwepo. Mwaka 1926, Gavana Donald Cameron aliyetawala Tanganyika kati ya mwaka 1925 na 1931 alipitisha sheria ya Mamlaka ya Wenyeji (SURA YA 72). Mnamo mwaka 1947, kutokana na vuguvugu za kudai uhuru zilizoendeshwa na waafrika waliorejea kutoka vitani, Waziri wa makoloni wa Serikali ya Kiingereza, Bw. A. Creech Jones, alitoa waraka maalum kwa magavana wa kiingereza na kuwaagiza waanzishe mfumo wa kidemokrasia wa Tawala za Serikali za Mitaa katika makoloni yao. Kwa kuzingatia waraka huo mnamo mwaka 1950 Gavana wa Tanganyika aliifanyia marekebisho sheria ya mamlaka ya wenyeji ya mwaka 1926, marekebisho ambayo yaliunda MABARAZA YA MACHIFU kama mamlaka ya kuwashauri wakuu wa majimbo na Wilaya.


Mamlaka hizi za Mabaraza ya Machifu zilipewa kibali cha kutumia mapato yao kwa shughuli za utawala, maendeleo na ustawi wa Jamii. Kamati za Fedha ziliundwa kusimamia mapato na matumizi ya mamlaka hizo.


Mwaka 1953, sheria ya serikali za mitaa (sura ya 333) ilipitishwa kwa kufuta sheria ya Mamlaka ya wenyeji (Sura ya 72) ya 1926 na kuanzisha “Halmashauri za Serikali za Mitaa” zenye madaraka kamili ya utendaji juu ya watu ndani ya maeneo yake. Sheria hii ilianzisha pia utaratibu wa uchaguzi wa madiwani na kutoa uhuru zaidi wa utendaji kwa Halmashauri zilizoundwa.

Kwa hiyo chimbuko la Tawala za Serikali za mitaa za sasa ni Serikali za aina hiyo za wakati wa ukoloni.

Kuwepo kwa makamishna wa mikoa na wilaya wakati wa ukoloni kama wawakilishi wa utawala wa kikoloni chini ya Gavana, lilitokana na wakoloni kutowaamini wenyeji kujiongoza. Kwa hiyo Tawala hizi za Serikali za Mitaa ziliwajibika kwa wakuu wa majimbo na wilaya. Hata sisi leo bado wakuu wa mikoa na wa wilaya wamepewa mamlaka na madaraka fulani juu ya Serikali za Mitaa. Tumeendeleza mtazamo huo huo wa kikoloni wa kutokuwaamini wananchi kujiongoza. Hii ni kasoro kubwa ya pili ya mfumo wa Tawala za Mikoa.


Leo Watanzania ni watu huru. Serikali za Mitaa na watu chini ya Mamlaka hizi ni sehemu ya Jamii ya Tanzania huru. Ni kweli kuwa uendashaji na utendaji wa Serikali za mitaa vinahitaji kuratibiwa na kudhibitiwa kwa kiasi fulani na Serikali Kuu. Lakini hii haihalalishi kuendeleza mfumo wa Tawala za Mikoa wa enzi za ukoloni kama ulivyo sasa. Uratibu na udhibiti unaweza kuendeshwa bila ya kuwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika mfumo wa sasa. Rais siyo mtawala kama Gavana wa Kiingereza na Serikali ya Muungano wa Tanzania siyo sawa na Serikali ya Mfalme wa Kiingereza iliyoitawala Tanganyika. Uongozi wa Kitaifa na ule wa Serikali za mitaa unatokana na jamii ile ile ya Watanzania katika mtandao wao Mkoani na Wilayani.
 
MFUMO NA MUUNDO WA UONGOZI WA MAJIMBO
DHIDI YA TAWALA ZA MIKOA

MAENEO YA KIJIMBO


Tunahitaji mfumo mpya wa kidemokrasia ngazi ya Mkoa na hili ndilo lengo la Dhana ya Uongozi na Utawala wa Kijimbo.


Ibara ya 2, Ibara ndogo ya (2) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977 ndiyo inayotoa madaraka kwa Rais kuunda mikoa.

Kwa bahati mbaya katiba haikuainisha vigezo vya msingi vya kuzingatiwa katika kuamua eneo fulani kutamkwa kuwa Mkoa. Aidha mkoa kama taasisi haukupewa majukumu mahsusi ya kikatiba. Badala yake ni Mkuu wa Mkoa binafsi anayepewa majukumu kikatiba na majukumu hayo kufafanuliwa zaidi katika sheria ya Tawala za Mikoa No. 19 ya 1997. Uundaji wa wilaya nao hauna vigezo vya msingi vinavyoeleweka kisheria.

Kwa utaratibu huu suala la kuunda Jimbo jipya halitakuwa tena la utashi tu wa Rais aliyepo madarakani, au la mtazamo tu wa kisiasa, na kwa maslahi ya kisiasa yasiyozingatia utashi na maslahi ya kitaifa na wananchi kwa ujumla.

Dhana ya uongozi wa kijimbo inapaswa kulenga kwanza Katiba itamke idadi ya majimbo kwa kuanzia na pili iainishe vigezo vya msingi vitakavyotumika katika kubadili idadi hiyo kwa kuongeza majimbo mapya. Kwa maana hiyo itabidi serikali ya wakati huo kupeleka muswada Bungeni na utekelezaji kufanyika tu kutokana na uamuzi wa Bunge wa kubadili katiba. Aidha Dhana ya uongozi wa kijimbo inalenga pia kuwezesha majukumu ya msingi ya kijimbo yatamkwe kikatiba na kisha kufafanuliwa zaidi katika sheria itakayounda mamlaka ya uongozi wa Jimbo

Kwa utaratibu huu suala la kuunda Jimbo jipya halitakuwa tena la utashi tu wa Rais aliyepo madarakani, au la mtazamo tu wa kisiasa, na kwa maslahi ya kisiasa yasiyozingatia utashi na maslahi ya kitaifa na wananchi kwa ujumla.

Na kwa mantiki hii mamlaka na madaraka ya sasa ya Mkuu wa Mkoa, yaani yale ya kisiasa na ya uendeshaji serikali yatahamishiwa kisheria kwa mamlaka ya uongozi wa Jimbo na siyo tena kwa mtu au ofisi binafsi katika utumishi wa serikali kama ilivyo sasa kwa Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya.




MUUNDO WA UONGOZI WA KIJIMBO DHIDI YA TAWALA ZA MIKOA

Dhana ya uongozi wa kijimbo ilenge kuendeleza lengo la dira ya uboreshaji wa Serikali za mitaa na mikakati ya utekelezaji wa mfumo mpya wa Serikali za mitaa unaondelea sasa, yaani "uhuru wa watu kujiamulia" na kutekeleza mambo yao "chini ya mfumo wa serikali zao za mitaa". Dhana ya uongozi wa kijimbo ni kwa kufanya mkoa kuwa ngazi ya uongozi wa kidemokrasia, chini ya mfumo wa Serikali za Mitaa.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika Ibara ya 6, inaainisha "Dhana ya Serikali" kwa kujumuisha Serikali ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali za Mitaa. Lakini Ibara hii inajumuisha katika dhana hii mtu binafsi anayetekeleza madaraka na mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali yoyote. Bila shaka Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni miongoni mwa watu hawa binafsi wanaotekeleza kazi kwa niaba ya Serikali Kuu ya Muungano wa Tanzania katika maeneo ambayo yamo ndani ya mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Dhana ya uongozi wa majimbo haulengi wala hauzalishi kitu kipya kabisa katika mfumo na muundo wa utawala nchini.

Lengo kuu la dhana hii ni kubadilisha muundo wa Tawala za Mikoa na kuunganisha na muundo wa Talawa za Serikali za Mitaa.

Kwa kifupi, ni kuendeleza, kupanua na kuimarisha dhana ya "Madaraka ya Umma" kama ilivyokusudiwa na kuainishwa katika Ibara za 145 na 146 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.


Kwa hiyo chini ya uongozi wa kijimbo kunatakiwa kuwepo na chombo cha mkoa cha uwakilishi wa watu na kitakachotokana na utashi wa wananchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia. Hatua hii itaboresha ushiriki wa jamii na kwa hiyo kuongeza mamlaka na madaraka ya umma katika kushawishi na kuridhia maamuzi ya uendeshaji wa shughuli za kiserikali kimkoa.


Kwa kuwa na chombo chenye ridhaa ya jamii, majimbo yataweza kusimamia vizuri zaidi maendeleo ya jamii ya kimkoa na Taifa kwa ujumla. Chombo cha namna hii ni muhimu sana katika kusimamia rasilimali za nchi na katika jitihada za kulinda na kuhifadhi mazingira ya ki-ikolojia ndani ya Mkoa kwa kushirikisha jamii.

Baada ya kulifanya Jimbo sehemu ya muundo wa serikali za mitaa kwa mujibu wa Ibara za 145 na 146 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano, hakutakuwa na haja tena ya kuwepo na ngazi za Wilaya na Tarafa katika muundo wa Serikali Kuu kama ilivyo sasa. Hii ni kwa sababu maeneo yote ya Kiwilaya na Tarafa kwa sasa yamo katika mipaka ya mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mujibu wa sheria Na. 7 ya 1982 na Na.8 ya 1982 ya mamlaka za wilaya na za mijini.

Majukumu ya Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tarafa, hususani yalivyofafanuliwa katika Ibara ya 14 na 17(2) ya Sheria ya Tawala za Mikoa yatatekelezwa na mamlaka za serikali za mitaa chini ya Ibara ya 146(2) (6) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara za III (a) na III(2) (a) ya Sheria Na. 7 ya 1982 ya mamlaka za wilaya na Ibara ya 54(1) (a) ya Sheria Na. 8 ya 1982 ya mamlaka za mijini. Kwa hiyo hapatatokea pengo lolote la utendaji wa kisheria, wala la kiutawala.



MUUNDO WA UONGOZI NA MAMLAKA YA JIMBO

Dhana ya uongozi wa majimbo inalenga kuondoa nyadhifa hizi kwa kugeuza Mkoa kuwa ngazi ya juu ya Serikali za Mitaa yenye Uongozi na Utendaji wa kutekeleza majukumu ambayo kwa sasa yamekabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

Kutokana na mabadiliko haya, muundo wa uongozi wa majimbo utaimarisha upelekaji wa madaraka zaidi ya Serikali Kuu kwa Umma. Aidha mfumo na muundo wa Serikali za Mitaa sasa utakuwa wa ngazi kuu tatu za:-
1. Kijiji/Mtaa yaani ngazi msingi
2. Wilaya/Miji yaani ngazi kati
3. Mkoa yaani ngazi kilele
Mamlaka ya Jimbo yatapewa kisheria madaraka ya kusimamia na kuratibu kwa ukaribu zaidi, shughuli za mamlaka za chini za Serikali za Mitaa ndani ya Mkoa. Serikali Kuu, kupitia wizara husika na Serikali za Mitaa, mawasiliano yake kuhusu Serikali za mitaa sasa yatapitia Mamlaka za Majimbo ambazo zitakuwa viungo kati yake (Serikali Kuu) na Mamlaka za chini za kati za Serikali za Mitaa.

Mpango wa uboreshaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara unaainisha maeneo manne ya kimkakati ya kuzingatiwa katika kuimarisha Serikali za Mitaa. Maeneo haya ni:-
 
1.1. Kukabidhi Serikali za Mitaa madaraka zaidi ya kiutawala na watumishi.
2. Kukabidhi Serikali za Mitaa madaraka ya kifedha.
3. Kukabidhi Serikali za Mitaa madaraka ya kisiasa.
4. Kubadili uhusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa wa ''kutoa Amri'' kuwa wa ''Uwezeshaji''.
5. Serikali za Mitaa kuwa vyombo vya msingi vya vita dhidi ya umaskini.





Dhana ya uongozi wa majimbo inalenga kuimarisha malengo haya ya mpango wa uboreshaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa kwa kuwa na ngazi ya mkoa kama ''ngazi kilele'' ya mfumo wa Serikali za Mitaa nchini. Ngazi hii itawajibika kusimamia utendaji wa mamlaka za chini ambao kwa sasa umekabidhiwa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa mujibu wa vifungu vifuatavyo vya sheria vilivyotokana na Sheria Na. 6 ya 1999 ya marekebisho mbalimbali ya Sheria za Serikali za Mitaa za 1982 na Sheria ya Tawala za Mikoa.
◊ Sheria Na 19 ya 1997 kifungu 5(3) Tawala za mikoa
◊ Sheria Na 9 ya 1982 ya fedha za Serikali za Mitaa Ibara ya 44
◊ Sheria Na 7 ya 1982 Ibara ya 174A
◊ Sheria Na 8 ya 1982 Ibara ya 78A
◊ Sheria Na 19 ya 1997 Ibara ya 14(3)










MFUMO WA TAWALA ZA MIKOA NA MFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA





Dhana ya Uongozi wa Majimbo ilenge kuondoa kabisa hali hii ya migongano ya kiitikadi kwa sababu chombo cha ngazi ya mkoa kitakuwa cha kidemokrasia chenye kuwajibika kwa jamii badala ya mtu mmoja mwenye itikadi ya chama kimoja tu. Misingi ya kidemokrasia ndiyo yataongoza maamuzi na utendaji kazi wa chombo husika.






Nchi yetu imo katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Kwa hiyo vyama tofauti vitaweza kuongoza Serikali za Mitaa tofauti. Pia vyama tofauti vitaweza kuongoza serikali kuu na baadhi ya serikali za mitaa. Katika mazingira ya aina hii siyo rahisi Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyechaguliwa na Rais wa chama kimoja kwa misingi ya kiitikadi kutoa ushirikiano kwa Serikali za Mitaa zinazoongozwa na vyama tofauti na kile cha Rais wa nchi. Historia imedhibitisha hivyo na mfano halisi ni wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu inayoongozwa na CHADEMA tangu kipindi cha 2001 hadi 2006. Kiini cha mgogoro katika Wilaya hii ni mitazamo ya kiitikadi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ambao ni wana-CCM.
Kwa mfumo wa sasa timu za Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ni sawa na timu ya Mawaziri. Itakapotokea CCM kushindwa uchaguzi na chama kingine kushika madaraka, wakuu wote wa mikoa na wilaya ambao wote ni wenye itikadi ya CCM watafutwa kazi na wapya wenye itikadi ya chama kilichoshinda kuteuliwa. Hatua hii ina athari kubwa mbili. Moja ni mzigo wa kuwalipa mafao ya utumishi wao. Pili ni kupoteza uzoefu walioujenga kupitia mafunzo mbali mbali ya kiutawala kwa gharama za umma. Hivyo kuingiza timu mpya isiyo na uzoefu wa uendeshaji wa shughuli za kiserikali na za kiutawala kwa ujumla ni kurudisha maendeleo ya jamii nyuma.





Dhana ya uongozi wa majimbo ilenge kurekebisha hali hii kwa kujenga mfumo wa uongozi na utendaji wa kudumu hata kutokeapo mabadiliko ya kisiasa yanayoletwa na matokeo ya uchaguzi wa ushindani wa kisiasa wa vyama vingi vya siasa. Kitakachokuwa kinabadilika ni uwakilishi wa kisiasa katika mamlaka yenyewe, na siyo utendaji. Tunahitaji kujenga mfumo imara wa kitendaji na uendeshaji wa shughuli za kiserikali ili kulinda Taifa kutokana na mishtuko ya mabadiliko ya uongozi wa kisiasa baada ya chaguzi kuu.



MAHUSIANO NA MGAWANYO WA MAJUKUMU

Lengo kuu la Serikali za mitaa ni kusogeza mamlaka ya maamuzi ya kisiasa na kiutawala karibu na watu. Kusudi ni kuwezesha ushirikishwaji wa jamii kwa ufanisi mkubwa. Aidha jukumu kubwa la Serikali za Mitaa ni utoaji huduma kwa jamii, hususani huduma zinazowagusa moja kwa moja kimaisha.





Dhana ya uongozi wa majimbo ilenge kuwezesha kupanua wigo wa utendaji wa mfumo wa Serikali za Mitaa na kuipunguzia Serikali Kuu, kwa maana ya wizara za kisekta, majukumu mengi ya kiuendeshaji na kitendaji ngazi ya mkoa. Dhana ya uongozi wa majimbo itapunguza urasimu wa kufikia maamuzi na kuongeza ufanisi kwa kuwa na usimamizi wa karibu zaidi na maeneo ya utoaji huduma kwa jamii.






Mahusiano ya kisheria na kiutawala kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa yanatakiwa kuondokana na mtindo wa AMRI NA MAELEKEZO na kuwa ya UWEZESHAJI ZAIDI. Yanatakiwa kuwa ya uwezeshaji wa Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yake kwa uhuru zaidi. Hii ndiyo njia pekee ya kuwezesha kufikiwa lengo la msingi la mpango wa uboreshaji wa mfumo wa serikali za mitaa ambalo ni "kuziwezesha Serikali za Mitaa kutekeleza masharti ya uongozi/utawala bora unaozingatia uwajibikaji, uwazi, demokrasia na ushirikishaji wa umma ili kuinua ubora na kiwango cha utoaji huduma muhimu kwa wananchi wote". Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zinatakiwa kuwa washirika katika kutoa huduma kwa jamii ya Watanzania.

Aidha utaratibu wa sasa wa kutoa mamlaka ya kisheria moja kwa moja kwa Waziri unatakiwa kurekebishwa pia ili nia za Serikali Kuu za kikatiba za kudhibiti shughuli za Serikali Mitaa ziwe zikipitia bungeni kwa njia ya hoja maalum na utekelezaji wake utokane tu na azimio la Bunge. Hii itakuwa njia ya pili ya kupunguza au kuondoa kabisa maamuzi ya Waziri binafsi kwa misingi ya kiitikadi pale ambapo mamlaka husika ya Serikali za Mitaa inaongozwa na chama tofauti na cha Waziri huyo mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa.





Dhana ya uongozi wa majimbo ilenge kupunguza mikondo ya utoaji amri kwa serikali za mitaa kutoka mikondo mitatu, yaani Waziri, Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya hadi mmoja tu wa Serikali Kuu kupitia Waziri.






Lakini kunahitajika kuwepo chombo mathubuti cha kitaaluma ambacho kitatoa ushauri wa kitaalam kwa mamlaka kuu zote za Serikali za Mitaa. Chombo hiki ndicho kitapewa jukumu la kuongoza mijadala yoyote baina ya mamlaka za Serikali za mitaa na Serikali Kuu. Kwa maneno mengine Serikali za Mitaa zinatakiwa kuwa na sauti moja katika kujadiliana na Serikali Kuu.
 
MFUMO MPYA WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

Kwa kuunganisha ngazi ya Tawala za Mikoa na Tawala za Serikali za Mitaa, muundo mpya wa mfumo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na mahusiano ya kimuundo kati yake na Serikali Kuu unatarajiwa kuwa Ifuatavyo:-.
Serikali
Kuu
Mamlaka
za
Majimbo
/ Mikoa
Mamlaka
za sasa za
Serikali
za Mitaa
(Mamlaka za Wilaya na za Mijini)
Mamlaka za Vijij / Mitaa
Jamii za Watanzania wa Vijijini na Mijini





Dhana ya uongozi wa majimbo ilenge kuifanya Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) kuwa chombo hiki cha ushauri wa kitaalamu na menejimenti, na mwakilishi wa mamlaka hizi katika majadiliano na Serikali Kuu hususani kuhusu vyanzo vya mapato, ukusanyaji wake, mgawanyo wake baina ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na mgawanyo wa mipaka ya utoaji huduma kwa umma, ambao itabidi uendane na mgawanyo wa rasilimali.






Kwa hiyo mbali na majukumu yaliyokwisha ainishwa na kugawiwa kwa mfumo wa sasa wa serikali za mitaa, kutatakiwa kuwepo na mgawanyo mpya wa majukumu, kwanza kati ya Serikali za Mitaa za sasa na Uongozi wa Majimbo na pili kati ya Uongozi wa Majimbo na Serikali Kuu, kwa maana ya wizara za kisekta.

Inatarajiwa kuwa chini ya uongozi wa majimbo watendaji wengi wa taaluma za kisekta ambao wako Wizarani na wanashughulikia majukumu ya kiwizara mikoani, watahamishiwa katika mfumo wa uongozi wa majimbo ili kuimarisha utendaji na usimamizi wa kitaaluma wa utoaji huduma zitakazosimamiwa na uongozi wa majimbo.

Kwa mfano inatarajiwa kuwa baada ya uongozi wa majimbo kuanza uendeshaji wa:
1. Elimu ya sekondari na ukaguzi wa elimu ya msingi zitakuwa chini ya Majimbo.
2. Hospitali za wilaya na mkoa zitakuwa chini ya Majimbo.
3. Barabara ziitwazo za mkoa, lakini zile tu zinazounganisha wilaya ndani ya mkoa zitakuwa chini ya Majimbo.
4. Shughuli za ugani katika kuendeleza kilimo na mifugo, shughuli za kusimamia usambazaji pembejeo, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima wadogo na wa kati nakuendelea, zitakuwa chini ya jimbo.
5. Usimamizi na hifadhi ya mazingira pamoja na usimamizi wa hifadhi za misitu vitakuwa chini ya Majimbo.





Dhana ya uongozi wa majimbo inatarajia kuwa katika kutekeleza dhamira hizo za serikali kuu. Mbali na bunge, itashirikisha pia serikali za mitaa kupata mawazo yake kabla ya kufikia maamuzi. Inatarajiwa kuwa mamlaka ya uongozi wa Jimbo, kama chombo kilele cha mfumo wa Serikali za mitaa, ndiyo itashirikishwa moja kwa moja. Aidha Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zinatarajiwa kuwa wabia katika kuwatumikia wananchi kwa sababu vyombo vyote viwili vipo kwa ajili ya jamii moja ile ile ya Watanzania. La msingi ni kuwepo mgawanyo mzuri wa majukumu na rasilimali.






Kwa vyovyote majukumu haya ambayo kwa sasa yako chini ya Wizara za Kisekta yatahitaji watendaji chini ya mamlaka ya uongozi wa majimbo.

Mgawanyo wa vyanzo vya mapato na usimamizi wa ukusanyaji wake nao itabidi uangaliwe upya ili kuainishwa wazi wazi, Halmashauri za Wilaya/Miji zihusike na nini, Jimbo lihusike na nini na Hazina Kuu ya Serikali ihusike na nini moja kwa moja. Aidha ugawaji wa mapato yanayo kusanywa na kila mamlaka utaangaliwa upya ili kuweka uwiano wa uwezo wa kifedha wa kutoa huduma katika kila mamlaka. Hii ndiyo njia ya kuhakikisha kuwepo kwa viwango sawa vya msingi vya utoaji huduma muhimu kitaifa.

Kimsingi Dhana ya uongozi wa majimbo, ilenge kuwezesha Wizara kuhusika zaidi na:
1. Uundaji wa sera za kitaifa kwa kushirikisha serikali za mitaa.
2. Uwekaji viwango vya huduma kitaifa.
3. Usimamizi wa Taasisi na miundo mbinu za kitaifa kama vyuo vikuu, Hospitali kuu za rufaa, Barabara kuu nak.
4. Ufuatiliaji wa uzingatiwaji wa sera, sheria, miongozo ya Kitaifa na viwango vya huduma kwa Umma.
Uongozi wa Majimbo unatazamiwa kuchukua majukumu kama yafuatayo:
1. Kusimamia utekelezaji wa sera za kitaifa kwa kuzingatia mazingira ya kila jimbo.
2. Kusimamia utoaji huduma kwa jamii katika Jimbo kwa kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa za ngazi ya kati.
3. Kusimamia ushirikishaji jamii katika mipango ya maendeleo na utoaji huduma kwa kushirikiana na mamlaka za Serikali za Mitaa za ngazi ya kati.
MFUMO MPYA WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

Kwa kuunganisha ngazi ya Tawala za Mikoa na Tawala za Serikali za Mitaa, muundo mpya wa mfumo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na mahusiano ya kimuundo kati yake na Serikali Kuu unatarajiwa kuwa Ifuatavyo:-.
 
Serikali
Kuu
Mamlaka
za
Majimbo
/ Mikoa
Mamlaka
za sasa za
Serikali
za Mitaa
(Mamlaka za Wilaya na za Mijini)
Mamlaka za Vijij / Mitaa
Jamii za Watanzania wa Vijijini na Mijini





Dhana ya uongozi wa majimbo ilenge kuifanya Jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT) kuwa chombo hiki cha ushauri wa kitaalamu na menejimenti, na mwakilishi wa mamlaka hizi katika majadiliano na Serikali Kuu hususani kuhusu vyanzo vya mapato, ukusanyaji wake, mgawanyo wake baina ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na mgawanyo wa mipaka ya utoaji huduma kwa umma, ambao itabidi uendane na mgawanyo wa rasilimali.






Kwa hiyo mbali na majukumu yaliyokwisha ainishwa na kugawiwa kwa mfumo wa sasa wa serikali za mitaa, kutatakiwa kuwepo na mgawanyo mpya wa majukumu, kwanza kati ya Serikali za Mitaa za sasa na Uongozi wa Majimbo na pili kati ya Uongozi wa Majimbo na Serikali Kuu, kwa maana ya wizara za kisekta.


Inatarajiwa kuwa chini ya uongozi wa majimbo watendaji wengi wa taaluma za kisekta ambao wako Wizarani na wanashughulikia majukumu ya kiwizara mikoani, watahamishiwa katika mfumo wa uongozi wa majimbo ili kuimarisha utendaji na usimamizi wa kitaaluma wa utoaji huduma zitakazosimamiwa na uongozi wa majimbo.


Kwa mfano inatarajiwa kuwa baada ya uongozi wa majimbo kuanza uendeshaji wa:
1. Elimu ya sekondari na ukaguzi wa elimu ya msingi zitakuwa chini ya Majimbo.
2. Hospitali za wilaya na mkoa zitakuwa chini ya Majimbo.
3. Barabara ziitwazo za mkoa, lakini zile tu zinazounganisha wilaya ndani ya mkoa zitakuwa chini ya Majimbo.
4. Shughuli za ugani katika kuendeleza kilimo na mifugo, shughuli za kusimamia usambazaji pembejeo, kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima wadogo na wa kati nakuendelea, zitakuwa chini ya jimbo.
5. Usimamizi na hifadhi ya mazingira pamoja na usimamizi wa hifadhi za misitu vitakuwa chini ya Majimbo.





Dhana ya uongozi wa majimbo inatarajia kuwa katika kutekeleza dhamira hizo za serikali kuu. Mbali na bunge, itashirikisha pia serikali za mitaa kupata mawazo yake kabla ya kufikia maamuzi. Inatarajiwa kuwa mamlaka ya uongozi wa Jimbo, kama chombo kilele cha mfumo wa Serikali za mitaa, ndiyo itashirikishwa moja kwa moja. Aidha Serikali Kuu na Serikali za Mitaa zinatarajiwa kuwa wabia katika kuwatumikia wananchi kwa sababu vyombo vyote viwili vipo kwa ajili ya jamii moja ile ile ya Watanzania. La msingi ni kuwepo mgawanyo mzuri wa majukumu na rasilimali.






Kwa vyovyote majukumu haya ambayo kwa sasa yako chini ya Wizara za Kisekta yatahitaji watendaji chini ya mamlaka ya uongozi wa majimbo.

Mgawanyo wa vyanzo vya mapato na usimamizi wa ukusanyaji wake nao itabidi uangaliwe upya ili kuainishwa wazi wazi, Halmashauri za Wilaya/Miji zihusike na nini, Jimbo lihusike na nini na Hazina Kuu ya Serikali ihusike na nini moja kwa moja. Aidha ugawaji wa mapato yanayo kusanywa na kila mamlaka utaangaliwa upya ili kuweka uwiano wa uwezo wa kifedha wa kutoa huduma katika kila mamlaka. Hii ndiyo njia ya kuhakikisha kuwepo kwa viwango sawa vya msingi vya utoaji huduma muhimu kitaifa.

Kimsingi Dhana ya uongozi wa majimbo, ilenge kuwezesha Wizara kuhusika zaidi na:
1. Uundaji wa sera za kitaifa kwa kushirikisha serikali za mitaa.
2. Uwekaji viwango vya huduma kitaifa.
3. Usimamizi wa Taasisi na miundo mbinu za kitaifa kama vyuo vikuu, Hospitali kuu za rufaa, Barabara kuu nak.
4. Ufuatiliaji wa uzingatiwaji wa sera, sheria, miongozo ya Kitaifa na viwango vya huduma kwa Umma.
Uongozi wa Majimbo unatazamiwa kuchukua majukumu kama yafuatayo:
1. Kusimamia utekelezaji wa sera za kitaifa kwa kuzingatia mazingira ya kila jimbo.
2. Kusimamia utoaji huduma kwa jamii katika Jimbo kwa kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa za ngazi ya kati.
3. Kusimamia ushirikishaji jamii katika mipango ya maendeleo na utoaji huduma kwa kushirikiana na mamlaka za Serikali za Mitaa za ngazi ya kati.
MAJIMBO YA UKOLONI NA MIKOA YA SASA
Tanganyika ilikuwa na Majimbo nane wakati wa kupata Uhuru, ambayo sasa yamegawanywa katika Mikoa ishirini na moja kama ifuatavyo:-
Wakati wa Ukoloni Hivi Sasa

i. Jimbo la Ziwa Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga (ukiondoa wilaya za Kahama na Bukombe zilizokuwa Wilaya moja ya Kahama katika Jimbo la Magharibi)

ii. Jimbo la Magharibi Mikoa ya Tabora, pamoja na Wilaya ya Mpanda ambayo sasa iko Mkoa wa Rukwa) na Kigoma.

iii. Jimbo la Kati Mikoa ya Dodoma na Singida.

iv. Jimbo la Kaskazini Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro (ukiondoa wilaya za Mwanga na Same zilizounda wilaya ya Pare chini ya Jimbo la Tanga).

v. Jimbo la Tanga Mikoa wa Tanga, kasoro wilaya za Mwanga na Same ambazo sasa ziko Mkoa wa Kilimanjaro.

vi. Jimbo la Mashariki Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar- es-salaam.

vii. Jimbo la Nyanda za Juu Kusini Mikoa ya Iringa na Mbeya, kasoro wilaya za Sumbawanga na Nkasi zilizokuwa zinaunda wilaya ya Ufipa na sasa ziko mkoa wa Rukwa.

viii. Jimbo la Kusini Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.

Kila Jimbo liligawanywa katika Wilaya kadhaa na kwa mfano wakati wa kupata Uhuru wa Tanganyika, Mkoa wa Ziwa ulikuwa na Wilaya kumi na moja tu za Mwanza, Ukerewe, Geita, Kwimba, Shinyanga, Maswa, Buhaya, Biharamulo, Ngara, North Mara na South Mara. Leo eneo lile lile limegawanywa katika Mikoa minne, Wilaya za Kiserikali ishirini na tatu na Mamkala za Serikali za Mtaa ishirini na tatu pia.

Kuyagawa majimbo ya kikoloni baada ya uhuru mwanzoni huenda kulilenga zaidi kurahisisha usimamizi wa utawala ili kuharakisha maendeleo, lakini kadri siku zilivyopita lengo hili halikuzingatiwa tena na badala yake maslahi ya kisiasa ya kupeana ajira na madaraka ya kisiasa yalipewa kipaumbele. Hili lilisukumwa hasa na uundaji wa Wilaya mpya na Majimbo mapya ya ubunge kisiasa zaidi. Uwingi wa Wilaya ukawa kigezo cha kuunda Mikoa mipya, na uwingi wa Majimbo kuunda Wilaya mpya.





Dhana ya uongozi wa kijimbo ilenge kuiangalia upya Mikoa na kwa kuzingatia lengo la kiuchumi. Vigezo vya ukubwa wa kimaeneo, uwingi wa watu kama rasilimali nguvu kazi, upatikanaji wa raslimali zingine wa kiuchumi vitapewa uzito wa kipekee katika kuiunda upya Mikoa na Wilaya mfanye kila Mkoa na kila wilaya mpya kuwa na uwezo wa kubeba gharama za utawala wake, na wakati huo huo kuharakisha maendeleo ya watu. Mitazamo ya kisiasa haipaswi kupewa nafasi katika kuunda mikoa itakayotumika kikatiba. Kila Mkoa msingi wake uwe wa kijitosheleza kijamii na kiuchumi (Socio-Economically Viable).






Kwa kuwa lengo kuu la utawala wa leo ni kukuza uchumi kwa maendeleo ya watu, kunahitaji mtazamo mpya kuhusu vigezo vya kuundwa kwa mikoa au wilaya.

Kwa mtazamo huu itabidi pia muundo wa Mamlaka za sasa za Serikali za Mitaa uangaliwe upya kwa lengo la kulifanya kila eneo la Mamlaka moja kuwa la kujitosheleza kijamii na kiuchumi (Socio-Economically Viable). Hii ni kwa sababu moja ya tatizo la msingi katika uendeshaji wa baadhi ya Mamlaka za sasa ni kutojitosheleza kwake kijamii na kiuchumi. Hayana rasilimali ya watu na mali ya kutosha.

Kuhusu jina hakupaswi kuwa na malumbano. Msamiati wa neno gani litumika kati ya "Mkoa" na "Jimbo" ni suala la mwafaka wa kijamii. Hoja ya msingi katika dhana hii siyo "Jina" ni "mfumo na muundo wa utawala." Mijadala yoyote ya kitaifa, katika vyombo vya habari au katika vikao mbalimbali, ilenge katika "mfumo na muundo wa utawala" na siyo jina.


Ninapenda kumalizia makala yangu kwa kuwaomba Watanzania wenzangu waione nakala hii kama changamoto katika kuboresha mfumo na muundo wa utawala wa nchi yetu.

Ninafungua upya mjadala kuhusu sera ya CHADEMA ya majimbo.





Ili kuliepusha Taifa kukumbwa baadaye na mgogoro wa kisiasa na kiutawala na ili kudumisha na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa ni wakati muafaka kwa nchi yetu kuangalia upya mfumo wa Tawala za Mikoa. Sasa tunahitaji kuwa na mfumo na muundo wa kuongoza jamii badala ya kuitawala jamii. Tunahitaji kuwa na chombo cha uongozi wa kimkoa kinachotokana na watu kwa misingi ya ushindani wa kisiasa. Tunahitaji mfumo na muundo endelevu utakaofanya kazi wakati wote bila kujali ni chama gani kinashika utawala wa nchi Kitaifa. Sote kwa pamoja tukubali kubadilika kwa maslahi ya Taifa kuwa tuliweza kufuta mfumo wa uchifu na Azimio Arusha tunashindwa nini kufanya hivyo kwa Tawala za Mikoa?






Ninawaomba wachangiaji wajadili dhana hii kwa mitazamo ya kuwezesha:
1. Kupunguza "contralism" na urasimu wa madaraka ya utendaji na ya rasilimali kutoka mawizarani.
2. Kuimarisha mfumo na muundo wa Serikali za Mitaa kwa kuingiza ngazi ya Mkoa katika muundo huu.
3. Kuimarisha utawala wa kidemokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.
4. Kuondoa kasumba ya watawala binafsi (Rulers) katika mfumo wetu wa uongozi na kidemokrasia na ushiriki wa jamii.
5. Kuyafanya maeneo ya kimkoa kuwa ya kudumu kwa kuyaainisha katika katiba na kwa hiyo kuondoa nafasi ya uundaji wake kwa kukidhi tu maslahi ya kisiasa ya vyama binafsi katika utawala.
6. Kuondoa migongano ya kitendaji kati ya Serikali Kuu (Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya) na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa pande zote kufanya kazi katia eneo moja la kijiografia na katika jamii ile ile moja.
Wazee wetu walitutoa katika ukoloni na kuanzisha mifumo ya utawala ambayo kwa sehemu kubwa iliiga mifumo ya kikoloni na baadaye mifumo ya kijamaa ya watu wachache kuhodhi madaraka. Miaka 49 inatosha kuviwezesha vizazi vya leo kuiboresha mifumo hii ili iendane na zama mpya za sasa na za miaka mingine hamsini ijayo. Tunahitaji mifumo ya kukidhi zama za kisiasa, kijamii na kiuchumi, kitaifa na katika jamii mpya ya kimataifa.
Ninauelewa ukweli wa usemi kuwa "Mazoea yana Taabu". Kwa wanasayansi ya jamii taabu ya mazoea ni kuwa:-
1. Udumaza uwezo wa watu kufikiri zaidi na kwa haraka.
2. Uwafanya watu waendelee kuridhika tu na hali waliyo nayo na waliyoizoea kimaisha miaka nenda.
3. Uwafanya watu waogope hali mpya yoyote ile wasioijua hata kama ni ya neema zaidi kuliko ile waliyomo.
4. Uwazuia watu kujifunza na kuiga kutoka kwa wengine kwa sababu tu ya kutokuwa na dhamira ya kubadilika.
Kwa hiyo mazoea usababisha kudumaa kwa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Yanadumaza ustawi wa watu kimaisha.


Siamini kuwa Watanzania wa leo wa miaka 18 hadi 41, yaani waliozaliwa katika mfumo wa chama kimoja kati ya 1964 na 1987 watakuwa wameathirika kiasi hicho na mazoea ya muundo wa Tawala za Mikoa tulio nao sasa. Kwa hiyo siwategemei nao kuwemo katika kundi la wapinzani kwa dhana hii ya utawala wa Kijimbo/Kimkoa. Nina wategemea waongoze utayari wa kuleta mabadiliko haya kwa manufaa na maslahi ya Taifa lao na ya kizazi cha chini yao na vile vitakavyofuata.

Ninawapa changamoto.
... mwisho ...
 
Ukitembelea ile link ndio utayaona vizuri, kuna majedwali na michoro ambayo nimeshindwa kuayaweka hapa, kwenye nafasi hapo juu kuna michoro/jedwali

Tujadili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom