Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Mlalahoi.
nilikuwa najibu hoja ya udini aliyokuja nayo Lunyungu. lakini kama kawaida yako ya kuvamia wanaume umeanza kamchezo kako.nitakushughulikia.
Tunajua umekuja kuuvuruga huu mjadala wa Mbowe ili ufutwe kama wa Mengi.
hilo nimekushtukia mtu haumwi na nyoka mara mbili.na wengine kuweni macho na huyu Mgalatia (bishop mlalahoi). kama mnakumbuka amesoma chuo kisicho na wahadhiri wenye sifa cha Iringa.

Huna hoja zaidi ya udini.Kwanini usiende kuwasaidia mujahidina wenzako wanaopewa kibano huko Somalia? Sifa mojawapo ya hoja zako ni kutoa point pumba,kupindisha topiki na kukwepa mada za moto.

Historia imeonyesha kuwa mara nyingi wavivu wa kufikiri hukimbilia kutoa majibu rahisi kwenye maswali magumu, na wewe mzembe wa kufikiri unakimbilia udini kwa vile uwezo wako wa kufikiri na kupembua hoja ni critically limited.
 
Tafitithenjadili uliandika hivi: "Ukabila unaozungumziwa hapa ni Chadema tangu kianze wenyeviti wake wote ni wakaskazini na ni uchaga tu hakuna cha zaidi, wabunge wa kuchaguliwa ni wana ndugu tu sio mtu mwingine. Chadema ndio mnatakiwa mkue na muache utoto".


Jibu langu ni kuwa: Hapo umedanganya tena makusudi. Sio kweli kwamba tangu CHADEMA ianze wenyeviti wote wametoka Kaskazini. Kama ndivyo unavyoishauri serikali ya JK basi hamna ajabu kwamba wanafanya madudu wanayoyafanya!
 
Asante Bishop Mlalahoi.
wewe umechangia nini humu kwenye mada hii? kama sio kuvuruga.
utasubiri sana na Mwandosya wako.
 
EO
Kichwamaji

Ukabila unaoongelewa hapa ni wa Chadema toeni mboni zilizo machoni mwenu.

kazi kwenu

Kama huu ndio mtazamo wenu wa dhana ya ukabila, basi tumekwisha! Ukabila ni nini? Una uhusiano na ubaguzi? Una uhusiano na upendeleo? Je, tunawezaje kuyahusisha haya na hilo na viongozi wawili ndani ya CHADEMA? Kura zilizowaweka madarakani zilipigwa na kabila lao? Je, walishindanishwa na wenye uwezo zaidi wa makabila mengine WAKAPENDELEWA wao?

Ninavyojua, mmoja alikuwa mwasisi. Wala hakutumwa na watu wa kabila lake kuasisi hicho kitu. Wa pili je? Wa tatu, pamoja naye kuwa mmoja wa waasisi, hakuchaguliwa na wanakabila lake. Alishindanishwa na nani kikabila? Tutajie. Na tangu amechaguliwa, mnaona hawezi kazi?

Ukabila, ukabila...sioni ukabila hapa. Ni upeo mdogo wa wanaojadilii ukabila. Rudini vitabuni kwanza mje na tafsiri halisi ya dhana ya ukabila, na mtoe ufafanuzi wa jinsi tafsiri hiyo ilivyotumika kuhalalisha hoja zenu. Vinginenvyo naona watu wanakariri maneno ya wengine kuhalalisha kauli zao dhidi ya wengine. U-KABILA?
 
chadema.
jifunzeni umuhimu wa shule kama ya migiro imemfikisha huko.pelekeni shule mnyika na mbowe, au uteuzi wa mnyika kwenye jumuia ya vijana ya kimataifa ndio sawa na Migiro?

jamani shule!!!
 
Migiro ana shule sawa lakini Migiro hajafika hapo kwa hilo bali shule imeongezea . Nilionya kwamba soon CCM wataanza kumtumia Migiro na kulipwa fadhila kama maendeleo ya CCM kwa wananchi.

Shule iko CCM sana lakini Nchi iko wapi? Migiro anatoka kwenye Serikali Corrupt ya CCM nalo ni jambo la kujivunia . Hivi hii si takrima baada ya TZ kumuunga mkono kwenye UN na alisha ahidi kwamba atalipa fadhila akisha kuwa Katibu Mkuu ?

Aliyasema haya Ikulu ya Dar na ndicho kafanya kwamba takrima na Migiro kapata nafasi ile ?
 
chadema.
jifunzeni umuhimu wa shule kama ya migiro imemfikisha huko.pelekeni shule mnyika na mbowe.
au uteuzi wa mnyika kwenye jumuia ya vijana ya kimataifa ndio sawa na Migiro?
jamani shule!!!


Ndugu yangu, acha utoto. Kwani Migiro kuteuliwa UN kuna uhusiano gani na Mnyika kuteuliwa DUA?

Wapi Chadema au CCM? Ukweli kwamba Migiro kawa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo, au tuseme hata Tibaijuka pale alipo, ina maana Tanzania ndiyo ina wanawake bora walisoma kuliko wote duniani? Kuna watu wana bahati zao.

Wapo wasomi kuliko Migiro hawajateuliwa. Kama unapenda mpongeze Migiro, usilete UCCM na Uchadema hapa. hauhusiki.

Zungumza issues, si ushabiki wa kitoto!
 
Eric Ongara,
Wewe mwenzangu Mwanasiasa hali mimi ni mlalahoi!.. jambo ambalo itanipa kazi sana kukuelewa.

Hapo juu sijaona kabisa ukijibu maswali yangu zaidi ya kuyapindisha kisiasa.
Kwanza kabisa kuhusu Mirathi!..
Kuna tofauti kubwa kwa mali inayorithiwa na watoto kwa pamoja wakigawana mishahara kutokana na uzalishaji wao... na ile ambayo kila mtoto atakuwa na mali zake akichangia pale familia itakapo mhitaji kuchangia!..

Majimbo ni mfumo unaotaka tugawane mali zetu hali upo uwezekano mkubwa wa kutimiza la kwanza bila kugawana hizo mali ila tunagawa MAPATO yanayotokana na rasilimali hizo. Kuweka masiliasili chini ya serikali za majimbo ni kugawa mirathi!... period!
Pili, mlipokuwa mkitangaza hii serikali ya Majimbo, sii mara moja wala mara mbili Freeman na wengineo wametupa mifano ya Marekani,sijui India na hata Nigeria na majibu yangu ktk hoja hiyo pia sipendi kurudia!..

Kifupi hakuna nchi hata MOJA duniani ambayo imegawa majimbo yake Kiutawala kwa sababu ya kuboresha uchumi wa sehemu husika. Na nchi zilizojaribu kufanya hivyo matokeo yake yalikuwa kuvunjika kwa serikali kuu!..
Ebu nambie ikiwa Freeman hawezi kuja na plan ila sisi wananchi basi Tanzania haitakuwa Taifa tena, ila majimbo kujenga Taifa kiasi ambacho majimbo yatakuwa na sauti kuliko rais!..Then swali litakuja tunamhitaji rais wa nini?
Hadi sasa nachosema mimi ni kwamba kuna njia nyingi sana za kuweza kurekebisha UTAWALA huu uliopo na kujenga VIONGOZI. Kuwapa Wabunge nguvu ya kupanga na kuamua maendeleo ya wilaya zao hakuondoi nguvu ya rais ama plan ya rais ktk maendeleo ya taifa zima.

Uchumi utabakia chini ya wataalam wa Uchumi kama ni ruzuku kwa wananchi hili jambo linaweza kabisa kurekebishwa kitaifa bila kubadilisha mipaka ya taifa letu. Tamaduni na mazingira yetu imejengwa kwa mipaka yetu...Unaposafiri kwenda Marekani, Ukifika New York utarudi nyumbani na kuwambia watu ulikuwa Marekani na wao watakuelewa hivyo kwa sababu USA imejengwa kwa majimbo... huna haja ya kutembelea majimbo yote lakini huwezi kwenda Eritrea akawambia watu ulikuwa Ethiopia wakakuelewa..hawa jamaa walivunjika kutokana na kuwepo kwa majimbo ya kiutawala ktk kujenga uchumi wa sehemu husika...

Sasa sielewi kabisa hilo la Mkapa kutembelea majimbo kuwa na uhusiano gani na Utawala wa majimbo!

Tatizo kubwa la sera ya majimbo ni KUIBADILISHA ramani yetu kiutawala kwa sababu ya kurekebisha mapato ya Uchumi wetu. Hii hainingii akilini kabisa. JK ameweza kuongeza baraza la mawaziri, kesho Freeman akaondoa baadhi ya wizara, kata baadhi ya watumishi na matumizi yake na hata kuondoa ma DC, RC bila kubadilisha mipaka ya nchi.

Hizi ndizo tofauti za vyama vya kisiasa kiutawala ktk nchi moja yenye dira moja. Ikiwa leo CCM wameshindwa kuzijenga wilaya zetu, mikoa yetu kwa udogo wake itakuwa vipi kama Ukubwa wa eneo utaongezeka kuwa majimbo kwa rasilimali zilezile zilizopo!..
Eric, problem ni sera za CCM ambazo hazilingani na maandishi yake. CCM ni waumini wanaosali kila siku na kumwomba Mungu huku usiku wapo mitaani wakijiuza na kucheza Uchi.

Hii ndiyo promise ambayo naitegemea toka Chadema ama chama cha upinzani kuwa badala ya wao kwenda kujiuza na kucheza uchi watakuwa na familia nzima kuhakikisha MATENDO yao wote yanafuata maadili ya dini.
 
Eric Ongara,
Ebu nambie ikiwa Freeman hawezi kuja na plan ila sisi wananchi basi Tanzania haitakuwa Taifa tena, ila majimbo kujenga Taifa kiasi ambacho majimbo yatakuwa na sauti kuliko rais!..Then swali litakuja tunamhitaji rais wa nini?

Hivi Mkandara unataka kutueleza kwamba Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini hana mamlaka eti kuwa magavana wa majimbo wana mamlaka katika majimbo yao? Tafakari.
 
Kichwamaji,

Jamani lini mtaweza kuelewa nachozungumza!

South Africa ilijengwa kwa majimbo kwanza! yaani majimbo yake kuunda nchi na sio kuwepo kwa nchi (South Afrika) kisha wakaigawa kwa majimbo. Mbeki, Mandela, Botha wote wameyakuta majimbo.

Je, sio sisi waafrika tunaowalaumu wazungu kwa kutugawa kwa kuweka states za kiutawala?..kisha leo hii unanambia its OK! hali tunajaribu kuiweka Afrika moja jambo ambalo limekuwa gumu zaidi na pengine haliwezekani.

Je, Unajua kama Rwanda na Burundi zilikuwa part of Tanganyika hadi pale tulipogawanywa na hawa wazungu kiutawala?. Leo hii sii rahisi kurudisha Umoja (as one country) huo zaidi ya shirikisho la kiuchumi...Hilo la mipaka haliwezekani tena na hiyo ni hadithi nyingine kabisaa.

Pili kuna tatizo la Kiuchumi ambalo pia muungano ni muhimu zaidi!... nimekupeni mfano wa EAC ambayo ilivunjika kutokana na siasa zetu za kiutawala!...Kujitenga kwetu kumedhoofisha nchi zote kiuchumi tofauti na dhana yetu ya awali kuwa tutajijenga zaidi.

Nakuombeni nyie mnipe mfano unaofanana na kile mnachokusudia kukifanya!.

Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kuunda majimbo baada ya Uhuru lakini hakuna kati ya nchi hizo imeweza kudumisha UHURU wake kwa zaidi ya miaka 20. Kwa hiyo tukianza leo na majimbo, possibility kubwa ni kuigawa nchi.. Hakuna mfano, unaopinga dhana hiyo kama upo nitoleeni!..
 
Nafurahi kuona wachangiaji tele toka zile zama za BCSTimes wapo humu - haswa akina Mkandara et al.

Kuna hoja nzuri nyingi tuu. Majimbo au Status Quo. Kila moja na merits zake. Sitaingi ahuko kwa sasa. If I were to confess, nimependa mchanganuo wa Mtei, ingawa sijapata bahati kuona "malalamishi" ya Nesario in original format.

Pia ni faraja kuona kuna viongozi wa Vijana humu 'nadhani ni JJ' kutoka chadema ambapo nahisi watakuwa wanaongea kama sauti ya Chadema, tena kwa kuweka na real names plus photos... Uwazi umekomaa kwa kweli. Well done...

Kinachonisumbua mimi, ni kuwa tunapenda sana malumbano bila kufikia maamuzi. Inaishia kuwa kama mazingaombwe halafu hakuna kinachoeleweka baada ya mada husika. Labda manufaa hapa ni kwa wakubwa kupata nafasi ya kuona maoni yanaendaje on the ground so to speak.

Mimi nionavyo dosari kubwa kabisa iko kwa VIONGOZI WETU WOTE - VYAMA VYOTE pamoja na sie tunaowachagua kwa kupiga kura. Sasa kama chama MBADALA chenye (chadema sio?) kinakodisha helikopter kwa kutembelea Tanzania nzima (ni wananchi wa Tanzania sio South Africa au Switzerland) kwa gharama zote hizo na kujustify, ni nani ataweza kuhoji Serikali ya CCM inapospend kwenye radars, presidential jet plus other white elephants projects? Priorities zetu ziko wapi? Huu uongozi tunaufuata kwa ajili ya nini haswa na ajili ya akina nani? Alafu sie wapiga kura tunapokaa kimya au kuuliza juu juu tu bila majibu na kuridhika maisha mbele kwa mbele au kuona kuwa ndio ujanja kama wasemavyo if you canbeat them join them... basi hapo ndipo unapoanza kuona kuwa tuna safari ndefu sana.

To be honest, kabla Chadema hajaongelea mambo ya majimbo au la, kuigia ikulu au la, inabidi watoe maelezo ya kueleweka kuwa kwa nini helicopter approaches ni better and any different from what CCM are currently doing. Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kufurahi vilivyo endapo nchi yetu iishie kuwa na vyama vichache sana lakini viwe makini haswa and holding the incumbent ruling party fully accountable kwenye kazi za serikali na maamuzi ya kila siku.

Without this post ending sounding like a rant, naomba wana Chadema wanielimishe pamoja na wengine waliohoji juu ya maamuzi ya matumizi ya fedha kama hizo za helikopter (bear in mind ndizo figures zilizopo public) badala ya kutumia mbinu zingine za kidemokrasia na maendeleo kama jina la hicho chama kisemavyo.

Nawasilisha!.

Taasisi.
 
Nikiongezea, mtu asisome somo la swali la helicopter as a ticket to majimbos au ikulu as re-reading my thread - posted hasitly - somone could easily interpret it that way, huo ni mfano tuu ambao unaweza kutupa the kind of thinking iliopo kwenye highest party leadership ya chama mbadala.
 
Taasisi
hilo la helikopta mbona limeshaongelewa mara nyingi. Kama unataka tafuta mada ya JJ alivyofafanua. Hapo uamue mwenyewe kama kunajustification au hakuna badala ya kuendelea kutaka watu watoe majibu yaleyale. Kuongezea Mbowe kakwambia ameweza kufika mikoa kumi katika kipindi kifupi kabisa kiasi ambacho asingeweza kufanya kwa hali ya sasa ya barabara na muda.
Mkandara,
Majimbo yanajitokeza kama hoja mbadala kutokana na ukubwa wa nchi na hivyo uwezo wa serikali kuu kushughulikia maendeleo unapwaya.
Hebu tazama article hii kutoka Daily News:
House committee suspends Mwanza contract
PATI MAGUBIRA in Mwanza
Daily News On Saturday; Saturday,January 06, 2007 @00:06

THE visiting Parliamentary Committee on Regional Administration and Local Governments has suspended construction of Misasi Health Centre valued at over 50m/- in Misungwi District, Mwanza Region, following allegations of the contractor's incompetence and non-registration.

"The Misasi Health Centre project is being implemented by government funds, and should abide by the law and rules governing government funds expenditure," remarked the Chairman of the committee-cum-Member of Parliament for Korogwe Rural, Engineer Laus Mhina, after the committee had inspected the project on Thursday.

Misungwi residents have contributed 7m/- into the project, while the government has put up 52m/-. Engineer Mhina cautioned, on behalf of the upset members of the Committee, that it was a criminal offense for an unregistered contractor to implement such a project, stressing that the government already had insisted that only registered contractors should be assigned such important projects.

The legislatures pointed an accusing finger at the Misungwi District engineer and economist, allegedly for allowing a bogus contractor to implement a government project.

"Failure to enforce laws vividly indicates that district experts are not useful to the residents of Misungwi," said Mr Gosbert Blandes, a legislature from Karagwe constituency, stressing that the district economist was not performing his duties well. Of all the district councils they visited, they had never come across such an offense being committed in the eyes of experts, he said.

About 40m/- has so far been spent on the implementation of the project, including 4m/- contributed by residents.

Kweli kwa staili hiii tutafikia maendeleo tunayoota ikiwa hata zahanati (siyo hospitali) inabidi ijengwe na Serikali kuu?
 
Tabasamu... na wengine, si nia yangu kurudia mjadala uliomalizwa - nilikuwa tuu nafuatilia hii thread ndio maana nimeweka maoni yangu hapa.

Pia nimeona maelezo ya Mwenyekiti wa Chadema "Mbowe pia alitetea matumizi ya helikopta katika ziara yake hiyo ya shukrani, kwa kusema wanaohoji "wana upeo finyu wa kufikiri." Katika mvua hii ningekuwa wapi katika siku 10, alisema na kuzungumzia jinsi ziara hiyo ilivyomfikisha wilaya kadhaa za mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
".

Utanisaidia zaidi ukiweka the link hapa ya hiyo thread yenye majibu yote badala ya mie kutafuta kwenye forum nzima.

Nina shauku ya kujadili hiyo comment ya Leader wa Chadema.
 
Waliokuwa wanamtafuta mwana CCM naona sasa wamempata. Aluta continua!
 
John Mnyika na akina wanachama wa Chadema.

Kwanza kabisa, ni bora nitoe sifa zifuatazo (very simple but very effective in my opinion):

1. Mmeingia kwenye hizi forums kwa uwazi na mnapata mawaidha direct from the ground. This is an excellent move and haina maficho. Ni wazi kuwa, mko wazi zaidi kuliko wengine.

2. Mnajibu hoja zinazorushwa kwa ufasaha kabisa
3. Mna uwakilishi wa vijana
4. Maelezo ya Mtei ya misingi ya chama ni swafi kabisa kwa upande wangu.

Pale sasa nionavyo mimi kuwa mnakosea:

1. Kwanza kabisa, mnajilinganisha na miuondo mibovu pale unaposema mbona JK and Shain kafanya hivi au vile. Nyie mnajenga chama Mbadala. Fanyeni mara 1000 vyema kuliko wao. Hao wamekalia hatamu. Chadema will stand a far better chance morally, politically, ideologically and hata internationally kama mkiweka yenu hivyo hivyo bayana ila kama ulivyosema kupanga ni kuchagua, ila mchague vizuri.

2. Katika hilo la helikopter, umeelezea jinsi coverage inavyofanyika lakini pia sijui kama mmejiuliza Mtanzania kule amefaidika aje? Nikupe mfano, kujenga shule au kituo cha huduma fulani kwa sehemu fulani fulani - strategically mkiangalia kura sio mbaya - ila mfanye kitu ambacho kionozi akiondoka pale alipotembelea hata miaka 2 mbeleni mmeacha kitu halisi. Jengeni mashule, fanyeni vijisherehe vya kufungua shule etc, zahanati - hata kama ni cheap kipesa impact yake ni kubwa mno kwa mtanzania. Binafsi naona kung'ang'ania helikopter kwa mambo ya coverage kwa chama kama cha Chadema kwa nchi kama ya Tanzania, ni uchoyo kwa upande wa Chadema kwa naona inaweka kuwa vile mnachotaka hapa na kukimbilia Ikulu. Sawa lengo ni Ikulu ili muweze kugovern better than CCM kwa manufaa ya nchi na Mtanzania, ila mwananchi awekekwe mbele na kuwe na track record of such deliveries hata kabla hamjaingia madarakani. Bila kujadili siasa zao - mfano ni akina Hamas walivyoweka network kali kwenye huduma za jamii kiasi kwamba walipoingia kwenye ulingo wa kura wamekuwa serious threat to the establishment. Ukweli ndio CCM must be worried now and will use any possible angle kufanya Chadema ichekeshe - kama kurubuni viongozi wahame etc, ila nyie don't play their game.

3. Talking of playing CCM games, Mwenyekiti Chadema he is falling on this trap . Mnamkumbuka Kaka Ben Mkapa ambavyo alikuwa na utawala wa Kibabe hata kwenye kutoa maelezo? Sasa mambo kama :

"Mbowe pia alitetea matumizi ya helikopta katika ziara yake hiyo ya shukrani, kwa kusema wanaohoji “wana upeo finyu wa kufikiri.” Katika mvua hii ningekuwa wapi katika siku 10, alisema na kuzungumzia jinsi ziara hiyo ilivyomfikisha wilaya kadhaa za mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Shinyanga, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.
"

Kama hiyo quote ni ya kweli, hizi ni lugha za kibabe za kushindwa hoja. Ukimwambia mwenzio ambaye ana hoja tofauti eti yeye ana "upeo finyu wa kifikiri" huku ni kujaribu kutoa intimidations. He is expected to talk and act like a President in waiting. Achangie hoja tuu bila kutoa kashfa. Sasa kwenye opposition lugha ndio hii (kama CCM!) sasa madarakani itakuwaje? Si maanishi kuwa nice nice tuuu, ila Tanzania inahitaji completely different ways of doing and conducting politics za nchi kwa maendeleo ya nchi. Hapo Chadema itakuwa very distinct. Ukweli ni kuwa, binafsi napenda kuona alternative National party ambapo naamini Chadema are in the right track, but we need to be totally different na wananchi wataona.

Senti Mbili zangu kwa leo.

Taasisi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom