Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Asante Eric ngoja tuyapembue kwanza najua mzee mzima Mkandara anayo mengi ya kusema juu ya makala hayo.
 
Verily Verily,
Kama ulikuwepo akini mwangu....nimeanza kwa vipande maanake ripoti ndefu sana na mwanzo tu nimeshtukizwa na bonge la mbata!..TUONDOKANE na MAZOEA tu.

Eric Ongara,
Mimi sintakuharakisha kabisa napenda tuwe pamoja kwa kila kipengele cha hoja za huyu ndugu yangu wa karibu sana Mh. Masinde... kwanza heshima mbele!..
Miaka 44 sasa baada ya nchi yetu kuwa huru, hatuna haja wala ulazima wa kuendelea kukumbatia mfumo na muundo wa Tawala za Mikoa tuliorithi kutoka kwa wakoloni. Ni muundo wa kuwa na mamlaka (Rulership) juu ya watu kama ilivyokuwa wakati wa Tanganyika ya Ukoloni. Utawala wetu sasa unatakiwa kuwa wa kuongoza watu (Leadership).
Ndugu Eric hapa kuna utata tena sio mdogo kwa sababu zilezile nilizozisema toka huko nyuma..Wakoloni walitugawa waafrika kwa MAJIMBO ili wapate kututawala kirahisi na wala haikuwa Ki -mkoa. Kabla ya uhuru mwenyewe amekiri kuwa tulikuwa na MAJIMBO manane kisha baada ya uhuru tukabadilisha na kuwa mikoa kumi na saba kama sikosei..Kwa hiyo sii kweli kwamba mfumo wa mikoa umetokana na Ukoloni.

Pili, Wakoloni walipotugawa kwa MAJIMBO ya kiutawala walikuwa nje kabisa ya fikra za kutuendeleza kiuchumi. Na hakuna nchi ambayo inaunda mipaka ya kiutawala kwa sababu ya kuwaendeleza watu kiuchumi bali ni Kiutawala, pia dhana ya kuwaendeleza wananchi huwa tu kwa wale wanaoona mzigo mkubwa wanaubeba kutoka ktk baadhi ya majimbo maskini!..Problem tuliyokuwa nayo Tanzania sio mipaka yetu kati ya mkoa na mkoa ama jimbo hadi jimbo.
Problem yetu ni UONGOZI MBAYA!

Hivyo basi dawa nyepesi na isiyo na gharama ni Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa wilaya Kuondolewa kama Watawala, jambo ambalo hakuna kati yetu anabisha tumeondoa dosari moja kubwa sana. Lakini hii dosari kuondoka haitakuwa na maana kama hapatakuwepo na UONGOZI wa kushika nafasi zao inavyotakiwa kuwa.. Tumependekeza WABUNGE wetu, madiwani na Meya ambo wote huchaguliwa na wananchi.

Kulingana na mchakacho wa Nd. Masinde ukiutazama vizuri utagundua kuwa:-
1. Mpango wa majimbo ni ubadilishaji wa lugha tu ya maeneo..serikali zitabaki vilevile ila kwa kuongezeka serikali moja ya JIMBO.

2. Dhumuni hasa la mfumo huu ni kuondoa viongozi wateule RC na DC na kuwapa nguvu viongozi waliochaguliwa.

Sasa ikiwa yote haya yanawezekana kwa kufuta vyeo vya RC na DC bila kubadilisha mikoa na wilaya zake why bother kuweka majimbo?

Serikali ya jimbo lazima itakuwa kubwa kuliko serikali ya Mkoa iliyopo sasa hivi maanake kuna mikoa mitatu hadi minne ktk kila jimbo. Paperworks zitakuwa bado matatizo kwani kazi nyingi za serikali kuu lazima ziwepo ktk majimbo. Kila jimbo litakuwa na vitengo vingi ktk kila fani hali wataalam hatuna wa kutosha.

Donda ndugu la Rushwa haliwezi kupungua kwa sababu sasa hivi tumeongeza ukubwa wa eneo la utawala wa Gavana mmoja kwa mikoa minne badala ya RC na mkoa mmoja.

Je, sio sisi tuliokuwa tukisema Tanzania ni kubwa sana kiasi kwamba JK hawezi kukidhi matatizo yote kwa wakati unaotakiwa?.. ikiwa haya maneno ni kweli na JK ama niseme rais ana wawakilishi wake kila mkoa kashindwa itawezekana vipi mattatizo yapungue kwa kumpa madaraka Gavana ashike mikoa mitatu hadi minne?

Guys, RC na DC wapo chini ya rais na kama kazi haifanyiki ina maana RC na hao DC ni wazembe na pengine wadhifa waliopewa haulingani kabisa na matakwa ya mikoa na wilaya hizo. Let wananchi wachangue viongozi wanaowafaa na sio kubadilisha mipaka ya nchi na pengine kuongeza marais wadogo (Ma-Gavana).

Majukumu ya uamuzi wa majimbo ktk maswala haya:-
1.Madaraka zaidi ya kiutawala na watumishi.
2. Madaraka ya kifedha.
3. Madaraka ya kisiasa.
4. Serikali za Mitaa wa ''kutoa Amri'' kuwa wa ''Uwezeshaji''.
5. Serikali za Mitaa kuwa vyombo vya msingi vya vita dhidi ya umaskini.
Hili ni tishio kubwa sana la Umoja wetu ukiondoa hilo la mwisho yaani namba

5. Tofauti kubwa kati ya bara na Zanzibar inatokana na hayo manne ya kwanza na kila mmoja humlaumu mwenziwe kwa sababu wananchi hadi leo ktk muungano huu hawafahamu mipaka ya utawala kati ya serikali hizi mbili.

Eric, Nitashuka chini baadaye kwanza tujadili kipande hiki kama inawezekana!
 
Ngugu Mkandara, Tupo pamoja

Ni vyema ukamaliza makala yote.

Alichojaribu kufafanua bwana Masinde, Kwanza ni neno Jimbo. Amejaribu kupambana na mawazo mgando. Amefafanua kuwa ni eneo la kiutawala kama ilivyo Mkoa.

Kuhusu Uwepo wa sera ya majimbo wakati wa ukoloni si kweli.Tunapaswa kutofautisha jina jimbo na mfumo au sera ya majimbo. Ukisoma vizuri uchambuzi wake, utafahamu mfumo uliotumika wakati wa Ukoloni ni sawa na unaotumika sasa.

Anafafunua kuwa mfumo wa kikoloni ulikuwa Ukitokea Dar-Es-Salaam. Viongozi wa mikoa waliwajibika moja kwa moja kwa Gavana kama livyo sasa kwa wakuu wa wilaya. Baada ya uhuru, kilichobadilishwa ni jina tu, mfumo ni uleule,unaanzia Dar. Ndio maana anajenga hoja kwamba huu ni mfumo mbaya usiowaamini wananchi, kwamba hawawezi kujiongoza. Tazama amefafanua hata mamlaka/Nguvu ya wakuu wa wliaya wakati wa mkoloni na sasa hivi, hazitofautiani,tofauti ni moja, uwezo wa kimahakama, hapa alikuwa anonyesha mfumo wa ukoloni hautofatiani na mfumo wa sasa! Kwa hiyo wakoloni hawakutugawa kwa mfumo wa majimbo bali kwa kutumia vibaraka.Pia sera ya majimbo, ambayo imejikita katika kuupa nguvu umma(Kama inavyotetewa na CHADEMA) haijawahi kuwepo Tanzania.

Hapa hata hoja ya wakoloni kuwagawa watanzania kwa majimbo inakufa! Hoja ya ukabila nayo ni mfu. Lazima tutafakari, Wanaharakati wa Uhuru waliwezaje kuliunganisha Taifa zima dhidi ya mkoloni kama kulikuwepo mfumo uliowagawa sana? Kwani miaka ya mwanzo wa uongozi wa Nyerere hatukusikia migongano ya makabila? Hata uchaguzi uliofanyika baada ya uhuru, Ambapo Nyerere na Mtemvu walichuana kwanini haikuwepo migongano ya kikabila ikiwa watu walikuwa wapo kwenye mfumo wa majimbo unatetea makabila? Maana hapa ndio tungesikia kila kanda au kabila limeanzisha chama chake na kusimamisha mgombea wake!! Pengine suala la ukabila Tanzania ni suala la kufikirika, tumelizusha wenyewe, halipo!

Kuhusu kuligawa taifa soma vizuri, amesema kabisa serekali kuu itakuwa na uwezo wa kudhibiti serekali za majimbo.Na mahala pengine sera kuu za kitaifa zitaungwa na serekali kuu Kanda/ Majimbo yatachuana kuzitekeleza kufuatana na mazingira ya eneo husika.

Serekali ya jimbo ni muhimo katika kupunguza utegemezi wa kimaamuzi tokea Dar. Kimantiki inawekana tukawa tuna punguza gharama, angalia idadi ya viongozi na maafisa katika mikoa jumlisha katika mikoa mitano tusema tutaunda jimbo kumbuka na utitiri wa viongozi wa wilaya tutakaowaondoa. Tutafakari upya hoja ya gharama.

Utendaji wa wakuu wa wilaya ni mbovu kwa kuwa hakuna mfumo wa wkuwajibishwa moja kwa moja na wananchi na pili vyeo hivi hugawiwa kama zawadi au njia ya kuwachota vigogo wa upinzani. Uteuzi katika mazingira kama haya hatuwezi kuwa na viongozi wawajibikaji.

Pia tuangalie changamoto nyingie kama mfumo wetu wa sasa unaendana na mfumo wa vyama vyingi. Rejea mfano aliotoa wa Halmashauri ya karatu ilio chini CHADEMA ilikwaruzana na Mkuu wa wilaya ambae anasimamia maslahi ya CCM.

Mjadala mzuri, tutafakari
 
Eric Ongara,
Shukran kwa kuweka sawa maelezo ya ndugu yetu Masinde...Na kusema kweli sikuona sababu kabisa ya yeye kusema Jimbo ina maana sawa na Mkoa - kwani yote ni maeneo ya Kiutawala... Hilo linakwenda hata kwa NCHI ama TAIFA yote ni maeneo ya KIUTAWALA. What was the point behind ukihusisha na Umaskini wa nchi? _ kwa nini jamani tusitumie lugha fupi?
Navyoona sasa hivi mnataka hata kunipotosha mimi ktk maswali yangu maanake tunazunguka mbuyu kiasi kwamba nashindwa kujua kaskazini wapi tena! nimesha anza kulewa!

My point is tatizo la nchi zetu sio ukubwa ma udogo wa MIPAKA bali mfumo wenyewe wa Utawala ktk Utendeaji kazi. WHO IS WHO hapo ndipo panapogomba.
Kwa lugha ya nd. Masinde anachotaka kusema muda wote ni makosa ya Nyerere na mkoloni ktk who is who ktk kushka madaraka na demokrasia ya kweli, lakini inanipa taabu sana mimi kuelewa kwa nini who is who itumike ktk kujenga hoja na Ulazima wa kuwepo MAJIMBO - Mikapa mipya!

Umezungumzia swala la UKABILA kisha nalo ukalihusisha directly na UTAWALA..na sielewi kabisa maana yako unacho hoji hapa!.. Je, huamini kuwa wazungu walitugawa! na imetokea vipi huo mgao wa wakoloni ufikie kusema ni wa Kimakabila na sio wa Kiutawala!
Well swali kama hili nadhani tunaweza kujiuliza hata kwa nchi nyinginezo kama Kenya Uganda, na nchi zote za kiafrika maanake zimepata UHURU wa taifa hali kuna makabila na UKABILA -waliweza vipi kuliunganisha taifa zima na kupata uhuru wao ikiwa nao waligawanywa. Tunachoogopa TZ ni mgawanyiko wa makabila kama ulivyo nchi hizo chini ya taifa moja -Huru.

UHURU wa nchi na UKABILA ni vitu viwili tofauti kabisa na kila nchi ina historia yake. Huko Zimbabwe, Washona na Ndebele walikuwa wakitoana macho lakini inapofikia Uhuru hawa watu walikuwa na adui mmoja tu KABURU kama vile Wasomali.. Ukimchokoza Msomali mmoja basi umetangaza vita kwa Wasomali wote hata kama ni clans tofauti.

Kabla na baada ya Uhuru ndugu Eric kila mkoa na wilaya zilikuwa zikitumia lugha zao mbele. nakumbuka mimi nilisoma shule ya msingi ya kimisheni na tulikuwa tukisoma biblia kwa kilugha!.. huendi kununua kitu sokoni kama huwezi kuzungumza lugha ya hapo. Na labda nikuchekeshe kidogo - mwenzako sikuwahi kumtia machoni Mchagga hadi nilipofika shule ya sekondari acha kusikia Wachagga wakizungumza!.. kwa hiyo unaweza kupima mwenyewe mambo yalivyokuwa miaka hiyo ya 60's.
Lakini basi utakuja gundua tu kwamba nguvu hizi zilikuja kufa kabisa baada ya UTAWALA wa Nyerere.
Nyerere aliweza kupandikiza mbegu za makabila mengine through AJIRA kila kona ya nchi na kisha akawaweka hawa ma RC na DC kama watawala wa maeneo hayo. Faida kubwa ya ma RC na hao ma DC ilikuwa kushika uongozi ambao kutokana na hali ya wakati ule ingeshikwa na Machief. Hawa machief walitumiwa na wakoloni muda wote kama kiunganisho kati yao na wananchi. Na ukitazama kwa makini utakuja gundua nguvu yao ilipotea kabisa baada ya intro ya hawa ma RC na DC kama watawala..na mpaka leo hawana Uchief tena imebaki jina tu.
Now, the good side ya hao ma - RC na DC ilikuwa ni ktk lengo la kuondoa utawala wa Kitemi na kutuunganisha sote kama taifa moja WATANGANYIKA - Mission Accomplished kama msemo wa Bush.
Problem inakuja tu kuwa hawa ma RC na DC kazi yao ilikwisha malizika KUTUUNGANISHA, sasa kwa nini Utawala bado unaendeleza mfumo wa Utawala ambao ulishindikana kutuendeleza IKUCHUMI?..
Binafsi siamini kuwa swala hapa ni Central Government. Zipo nchi kibao ambazo zina central Government na zinaendelea kiuchumi vizuri sana kuliko zile zenye Majimbo. Huu utawala wa Majimbo ni kuwatafuta marais wadogo ambao wanaweza kuwatesa wananchi wote...
Ebu nikuulize wewe Eric, Let's say Jimbo la Kaskazini Gavana aliyeshinda ni toka Chadema, Mkoa wa Arusha CCM na wilaya zake mikoa mingine Chadema na CUF na rais wa Jamhuri aliyeshinda kwa Popular vote ni CCM.. Hapa mpango utakwenda vipi?
kama ingekuwa nchi za wenzetu (wazungu) wala nisingeuliza kwani wao demokrasia imeisha simama - Hapa kwetu ambapo sheria ni Pochi kila mtu ana yake unategemea matokeo yapi?
 
Mkandara, Tupo pamoja

Tumefikia pazuri, kwamba kila nchi na mazingira yake na historia yake. Nilijaribu kuonyesha kwamba wakolni walitugawa kwa kutumia vibaraka wao na sio majimbo. Sioni ni kwa jinsi gani sera ya majimbo italigawa taifa au kuchochea ukabila.

Hamna tatizo kama majimbo yatakuwa yamechukuliwa na vyama tofauti. Tena itakuwa ni vizuri zaidi kwani kutakuwa na ushindani wa kimaendeleo.Yaani kama Halmashauri ya Karatu kuwa Chini ya Karatu, YA bariadi chini ya UDP na serekali kuu chini ya CCM!!!

Ikiwa chama fulani kitakuwa kimechukua jimbo, hio ni ishara kwamba wananchi wa eneo husika watakuwa wamekubaliana na mikakati ya kimaendeleo ya chama hicho kwenye eneo hilo. Chama kinaweza kuwa na sera nzuri kwenye serekali kuu na pia kikawa na sera mbaya katika ngazi ya wilaya au jimbo au mgombea mbaya. Cha muhimo ni kuwa na mgawanyo mzuri wa kimamlaka na wenye kueleweka katika ngazi zote.

Nime onganisha suala la ukabila na utawala kwamba halina uhusiano kama ambavyo sera ya majimbo isivyokuwa na uhusiano na Ukabila. Ukabila ni ubinafsi wa mtu na sio suala la mfumo.

Na tena tukitafakari zaidi utagundua Kwambe Watanzania hawana ukabila. Ikiwa waliungana kumuondoa mkoloni, baada ya uhuru tungekuwa na kinyang'anyiro baina ya makabila kugombea vyeo na pia isingekuwa raisi kwa watu kukubali kirahisi kupewa wakuu wa wilaya na Mikoa toka maeneo tofauti, wangepinga na pengine wangewadhuru wateule wa Nyerere wilayani na mikoani, ukabila usingeyeyuka kirahisi kwa kuchanganya tu maDC wa makabila tofauti katika wilaya yaani kama suala la kupuliuza filimbi!! Tanzania hakuna ukabila, hujawahi kuwepo na hautakuwepo.

Ingekuwa suala la lugha ya kiswahili na mfumo wa utawala ndio jibu la kuondoa ukabila, tungeharakisha kuwasaidia kuwafunda Kenya, Rwanda na Burundi kuondokana na ukabila.Unachagua tu mkuu wa wilaya mhutu kwenye wilaya inayokaliwa na watusi kisha unawafundisha kiswahili, ukabila unakoma!!!!

Tatizo la ukabila Tanzania ni la kubuni,sera ya majimbo kwa namna yoyote ile haiwezi kuleta ukabila haupo kwenye nyoyo za watanzania
 
Eric,

Sasa Nimekubali kuwa tatizo kubwa la Chadema ni UTAWALA..
Nimepata wasaa mzuri kuisoma report ya ndugu Masinde na hakuna sehemu imenipa picha kuwa GONJWA linalokusudiwa hapa ni - UMASKINI bali UTAWALA.
Sasa tazama nikupe picha nzuri...

Nakubaliana na wewe uliposema:-
Nilijaribu kuonyesha kwamba wakoloni walitugawa kwa kutumia vibaraka wao na sio majimbo
.
LENGO:- Lengo la mfumo huo wa mkoloni ilikuwa ni urahisi wa kututawala na sio kabisa kusaidia nchi hizi Kiuchumi.
MATOKEO:-
1.Mafanikio kwao:- Utawala wa Mjerumani na Muingereza wote waliweza kupunguza nguvu na Umoja wa mwafrika ktk Upinzani. Watawala wote hawa hawakufikiria kabisa kuijenga Tanzania kiuchumi na ndio maana walipoondoka Tanzania ilikuwa nchi maskini kuliko zote zilizokuwa huru wakati huo.
Tunaingia sehemu ya pili sasa:- UHURU.
Tulipopata Uhuru, mfumo mzima wa Nyerere ktk kuweka Mikoa na Wilaya ilikuwa kubadilisha Utawala ili KUTUMIA VIBARAKA WAKE...
LENGO:- Lengo la mfumo huu ilikuwa kuweza kuondoa Ukabila, nguvu ya Machief (Watemi) na kuifanya Tanzania iwe nchi isiyokuwa na matabaka ya kikabila..Nothing ktk Uchumi hadi hapo.
MATOKEO:-
1. Mafanikio kwa JKN:- Kuondoaka kwa Ukabila na leo Watanzania ni kabila moja la Waswahili.(our first language).

Nyerere alipotangaza - UJAMAA -1967, huu ndio mfumo uliotumika kujaribu kujenga Uchumi wetu na pengine kutuondoa ktk Umaskini.. Naomba ieleweke kuwa Ujamaa ni mbinu ya Kiuchumi ambayo ingeweza kutumika tukiwa na Majimbo ama Mikoa kama tulivyo leo na matokeo yake bado yangekuwa vilevile..So kubadilisha kwa Nyerere Majimbo kuwa mikoa na wilaya - has nothing to do with Uchumi wetu.

Nd. Eric naomba unifahamu hapa nimesimama wapi? siko ktk kabati la CCM wala Chadema nyote nakueleweni vizuri isipokuwa natazama faida na hasara za mabadiliko ya aina yeyote ile yatakwavyoweza kunigusa mimi.
Sasa tuingie sehemu ya tatu,
Chadema wameona dosari ktk Utawala Ule na hapa wanahitaji kubadilisha mfumo mzima wa Utawala mkianza na:-
1. Utawala wa Majimbo - lengo lake ni kupunguza nguvu ya Rais kiutawala
2. Kuondoa watawala wateule - lengo lake ni kuweza kuweka madaraka ya uongozi mikononi mwa wananchi wakiongozwa na Gavana chini ya serikali ya mitaa. n.k

Well and good - Chadema wana intention nzuri sana na hadi hapa hakuna kosa vitu hivi vyote ni positive vinakubalika kwa wananchi. na ni ktk mfumo huo tu ndipo mfumo mzima wa KIUCHUMI wa Chadema (Conservative) unaweza kufanya kazi vizuri ktk kuhakikishia maendeleo wananchi. Hii mshikaji inaweza kuwa dawa (psychotropic drug) nzuri sana kwa hili gonjwa letu la UMASKINI kama kweli tukianza na Watawala..Hiyo mikapa ya Majimbo ni part ya kubadilisha mfumo mzima wa Utawala (masaa ya kunywa dawa).
Je, tupo pamoja hadi hapo ndugu Eric!

Safi sana kwa sisi wagonjwa na kuvumbiliwa kwa hii dawa imejenga tumaini jipya kwetu, lakini je, hii dawa haina side effect yeyote?... hapo ndipo Panapo Gomba!..
Hapo ndipo Mkandara na wananchi wengine (doctors without Borders)tumeutazama huu mfumo (dawa) pamoja na UBORA wake wa ingrediance zake kama kuna dalili za kuzua gonjwa jingine. (side effects)..

Verily Verily, pia kaniondoa mimi ktk ulimwengu wa dhana na badala yake tuwasikie Chadema wamepanga kupambana vipi na hizi side effects zinazoweza kutokea kirahisi. Je, ni life threating?... - Yes, wengi (humu) wanaziona kama ni life threat lakini Chadema wanasema haiwezekani...
Now, question arise is How?... how nyie mnasema haiwezekani haiwezi kuwa life threat wakati wananchi tumekupeni kila maelezo yanayohusiana na uwezekano..(jinsi mwili wa binadamu unavyofanya kazi). Chadema hamjatupa jibu, ama sababu ya kutowezekana zaidi ya kusema hii ni dhana potovu!..Huyu mgonjwa hana kabisa cancer (ukabila) ilishapona na vitu hivi havihusiani... well side effects hii ndiyo inaweza kuwa chanzo cha gonjwa lililokwisha pona siku nyingi while nyie mkitazama tu huu ugonjwa mmoja wa Mtanzania na hamtazami side effects zake. Na kama mmeweza kuziona toka mwanzo mtaweza vipi kuziponya ama kuboresha dawa yenu ili zisiwepo hizi side effects!
Nadhani ni bora sana turudi kule tulikokuwa na ndugu Verily Verily tukisubiri mbinu zenu za kuzuia hizi side effects, laa sivyo inakuwa taabu kwa mtanzania kunywa dawa hii muhimu.
Eric, Ikiwa leo hii watu kama akina Mwinyi, Mkapa na sasa hivi JK wameweza kununua Radar, midege, IPTL, Richmond na mengine kibao ya kututoa damu za pua na kuhara - bado hatuna dawa hali watu hawa wamechaguliwa na wananchi! yet, wametumia wadhifa zao kujitajirisha why should I believe gavana atakuwa na Ubora wowote kwangu ikiwa RULE of the LAW hakuna nchini na pengine Afrika nzima. Why kuongoeza watawala zaidi ambao sasa kila jimbo watashindana - Uchief kama Nigeria na India ambako the most richest people are the Politicians waliochaguliwa kutokana na Populality zao - The CHIEFS.
 
Eric,

Ikiwa leo hii watu kama akina Mwinyi, Mkapa na sasa hivi JK wameweza kununua Radar, midege, IPTL, Richmond na mengine kibao ya kututoa damu za pua na kuhara - bado hatuna dawa hali watu hawa wamechaguliwa na wananchi! yet, wametumia wadhifa zao kujitajirisha why should I believe gavana atakuwa na Ubora wowote kwangu ikiwa RULE of the LAW hakuna nchini na pengine Afrika nzima. Why kuongoeza watawala zaidi ambao sasa kila jimbo watashindana - Uchief kama Nigeria na India ambako the most richest people are the Politicians waliochaguliwa kutokana na Populality zao - The CHIEFS.

HAPA ndipo tunapozungumzia mfumo. majimbo si tu maeneo. Ni dana nzima ya utawala na mfumo wa kuongozana. Kinachosumbue leo, katiba inawapa mamlaka makubwa hapo wezi. Hawawajibiki, na hakuna uwazi unaosimamiwa kisheria. Ndani ya mfumo wa majimbo hayo yanafumuliwa, katiba inawekwa upya, wananchi anapewa mamlaka ya kuwabana wakubwa wao. Huwezi kuwa na mfumo wa majimbo kwa katiba na utaratibu huu tulionao sasa. Hivyo dhana hii ya majimbo inakwenda mbali hivyo...Inaangalia failures za wengine na kuzifanyia kazi.
 
Kichwamaji,
Hapa bado kidogo.. Kipi kinatangulia Katiba au Majimbo?..

Trust me ikiwa mtaweza kubadilisha katiba leo hii kulingana na maelezo ya Mwanasiasa, huhitaji kabisa kuweka majimbo.
Kulingana na mabadiliko hayo yatawagusa hata hao ma RC na DC na nguvu ya rais itakwisha... Bunge litakuwa mbele na kuheshimika.. nguvu ya bunge ndiyo nguvu ya wananchi. Kwa nini tuchanganye dawa hapa na hayo Majimbo ambayo ni capsule isiyopimika kirahisi?..
Huwezi kuwa na majimbo bila kurekebisha KATIBA kwanza na hii ngoma nzito sana imeshindikana miaka!.. Zanzibar wamekula magongo, wengine wamefukuzwa uongozi na hata kupoteza roho zao. JM leo anazungumzia nje kwa sababu ya katiba hiyohiyo!
Hii ndio dawa nayoweza kuikubali kirahisi. Ikiwa mnaweza kupambana na hilo basi nadhani nguvu zaidi iende huko kuliko Majimbo. Tufanikishe hilo moja kisha likiwa bado lina tobo labda ndio mnaweza kufikiria Majimbo kwa kuziba nyufa na tobo!.. Dose ya majimbo ni kubwa sana kwa maradhi yetu na side effects zake zinakatisha tamaa kabisa.
 
Mkandara,
Great debate I see. umenifumbua macho kwa hiyo analogy ya cancer,dawa na side effect. Unajua mafumbo mengine bila mifano yakwama kooni! Kwa sasa nachekicheki tu kwa pembeni maana nafasi inagomba kiasi kutokana na majukumu. Ila natumia nami nitashuka na uchambuzi wangu baadae kidogo. Great discussion wazee Mkandara, Eric na Kichwamaji. Yaani ndo mnagonga ikulu kwenyewe.FD bado tunakungoja
 
Mkandara upo sawa, CHADEMA inasema ikishika madaraka itabadilisha kwanza katiba kabla ya kupendekeza sera ya majimbo kwa wanachi.

Kimsingi naamini unakubaliana na mantiki ya sera ya majimbo kinachogomba kwako ni taathira/athari zitakazo jitokeza baada ya kuanza kwa kutekelezwa kwa sera ya majimbo.

Kwa mujibu wa maelezo yako athari ambazo unahisi zitajitokeza ni:

1. Ukabila
2. Kuongezeka kwa Gharama

Kwa kweli, hapa ndipo tunashindwa kuelewana sioni ni kwa jinsi gani sera ya majimbo itachochea ukabila Tanzania suala la gharama linahitaji tafakari.
 
Eric Ongara,
ndugu yangu basi yaonyesha ulikuwa ukisoma vipande vipande hoja zangu maanake kila napoandika hutoa sababu, mifano na hata dhana ya jinsi kitu hicho kitakavyoweza kujitokeza.

1.UKABILA...
Nilisema hii dose ni kubwa sana, kwa sababu kwanza Gavana atakayechaguliwa mara nyingi atatoka kabila ambalo lina Population kubwa. Sijui kama unakumbuka mfano wa Wahaya na Wasukuma. Na nikaitosheleza hoja nzima kwa kukupa mfano kuwa leo hii na toka miaka ya nyuma Wabunge wengi wameshinda toka sehemu za makabila yao ama kule waliko Oa/Olewa...
Baadaye nikakupa tafsiri nyingi za makabila ktk Ulimwengu huu kuwa sii lazima kabila iwe ni asili na nasaba ya mtu siku hizi, kuna Ukabila wa Uzawa. Yaani Wazanzibar wanajiita wao Wazanzibar hali asili yao wengi ni nje ya visiwa hivyo wengi ni toka Oman, Bara na Komoro lakini identity yao imebadilika kutokana na Uzawa wao. Nikaendelea kukupa mifano ya majimbo ya nje kama vile Quebec na kadhalika.
Kwa mtazamo wangu, hivi sasa tulivyogawanywa kwa wilaya zetu tosha kabisa hata kama wabunge wana/tachaguliwa kwa misingi ya Ukabila hakuna shida kwani huyo mbunge anawakilisha watu wake. Pia wale wote wanaogombea sehemu zisizo na Ukabila kabisa kama vile mkoa wa Dar wataendelea ku enjoy nafasi hiyo. Hii system ya wabunge tulikuwa nayo inafanya kazi vizuri kutokana na kuwa ile cancer ya Ukabila Kitaifa haipo tena. Nachoogopa mimi ni kwamba nguvu za hawa wabunge badala ya kwenda moja kwa moja bunge kuu itakwenda kwa rais mdogo wa jimbo ambaye ni mfumo mpya kabisa!.
Jimbo litakuwa ni mikapa mipya na kuijenga jumuiya yake kama jimbo ni kazi moja mpya kabisa. Tutaweka mikapa lakini tukumbuke tu watu wataanza kuji-identify kwa hayo majimbo kulingana na Katiba. Nani mwenye haki zaidi ya mwingine na kadhalika hali wenzetu wote wenye majimbo (nchi nyinginezo) walianza kuwa na majimbo kabla ya hata kuunda Taifa!..Sisi tunatoka kule walikojenga wenzetu na kuanza kuigawa nchi. Mfumo huu hauna mfano kabisa wa kulinganisha pia ni zoezi ambalo sii lazima. Wakati wa kujaribu sio huu tukiwa wagonjwa..hii ni dose kubwa sana! haijawahi kufanyiwa utafiti na vibaya kuianza kwa binadamu mgonjwa. Marekebisho ya Katiba yana ml za kutosha kabisa kuponya maradhi ya madaraka na Utawala! na ikiwa tunataka kutazama uchumi basi kama alivyofanya Nyerere na intro ya Ujamaa - ndio hapo mnapokuja na sera za Ki - Conservative. Tena basi hao CCM, CUF na wengine wote inabidi wajieleze vizuri wamesimama wapi, sio kila chama kina mlengo sawa isipokuwa sura za viongozi ndio tofauti ktk uchaguzi.

Labda nirudie tena kwa nini Nyerere aliweka mikoa na wilaya kuondoa majimbo toka mwanzo isije kuwa ukaanza kuuliza mbona Nyerere alifanya hivyo?..
Kumbuka swala lilikuwa kuondoa UKABILA... na dawa yake ilikuwa kuigawa mikoa kwa makabila yake makubwa kisha wilaya na kata kwa makabila madogo...Tanzania tuna makabila zaidi ya 120 na pengine machief walifika hata 100. sasa dose ya Nyerere kuondoa Ukabila alihakikisha kila kabila linapata kiongozi nje ya chief wao ndio hao ma DC kushika hizo wilaya. Hawa walizima kabisa nguvu za kina Mirambo, Marealle kiutawala na kweli JKN akaweza kufuta kabisa Ukabila hii cancer.
Sasa tunaporudisha majimbo kuna hizi side effect ambazo nashindwa kuamini kama mzaramo anaweza kuchaguliwa kanda ya ziwa ama mgombea toka kabila dogo sana kushinda kanda ya juu kama Gavana. Hapa wananchi wana choice tofauti na wakati wa Nyerere (RC na DC) .. na tunapowapa watu choice - rangi za kabila na dini hucheza game kubwa...Hii ni hulka ya binadamu wote haiwezi kuepukwa kirahisi. Kati ya watu kumi ni wachache sana ambao hawatazami rangi hata ukitazama uchaguzi wa mke/mume utagundua kuwa rangi (kabila/dini) hutangulia tabia na uwezo wa mhusika.

Hizo Gharama tutazungumza baadaye, tumalize hili kwanza.
 
Ndugu Mkandara,

Si kwamba sisomi vizuri michango yako, naisoma sana. Ninachojaribu kusema ni kuwa watanzania sia wakabila, ukabila ni hulka ambpo wakati mwingine uanachochewa na makovu ya kihistora na si suala la kimfumo. Tukirejea kwenye enzi za Nyerere, maana umesema Nyerere alifuta uchifu kuondoa ukabila? Ulikuwepo? Ikiwa kila chifu alikuwa anaongoza kabila lake kulikuwa na ukabila kati ya nani na nani? Kabila gani lilikuwa linakandamiza jingine?

Pili, ikiwa kulikuwa na ukabila kwa nini hakukuwa na "resistance" wilayani, ya kwamba watu wenye msukumo mkubwa wa ukabila wangechachamaa kupinga watawala wapya MaDC dhidi ya machifu, ilikuaaje wakakubali kirahisi hivyo? Hii haisharii kuwa hawa watu hakuwa na hulka ya ukabila hata kabla?

Tatu, baada ya kuwa tumepata uhuru, kama ukabila ungekuwepo tungekuwa na kinyang'anyiro kikubwa sana cha watu kugombea uraisi kwa msukumo wa ukabila,kwenye ule uchaguzi uliowashindanisha Nyerere na Mtemvu kwanini makabila makubwa hayakusimamisha wagombea?

Maana kama dawa ya ukabila ni mfumo wa kiutawala mfumo tunaotumia unatofautiana vipi na wa Kenya? Mbona kenya haujakoma? Ndio hapo nasema kama suluhisho la kuondoa ukabila ni mfumo wa utawala kwanini ina
kuwa ngumu kuondoa ukabila katika nchi za Rwanda,Burundi na Kenya? Si ni suala la kumcahagua Rc mtusi katika wilaya inayokaliwa na watusi? wajaribu waone baruti itakayolipuka!!

Naamini kuna mapitio ya kihistoria ambayo nchi hizo zimeyapitia tofauti na Tanzania.

Nakubali wako watanzania wachache wenye chembechembe za ukabila, wapo na wanaonekana hata sasa tukiwa tungali tuna mfumo huu ulioshindwa.

Nyerere alibadilisha tu jina ya maeneo ya kiutawala na sio mfumo, na hata baada ya uhuru tulikuwa na mikoa tisa, ikaawa inaendelea siku hadi siku,na mmoja tumeongeza juzi(Manyara) na tunaendelea kubuni mikoa mingine.Nyerere aliongeza mikoa na wilaya si kwa minajili ya kuondoa ukabila, kwa maana hutajawahi kuwa na Tatizo hilo, yeye aliamini kwa kuweka viongozi wengi wangeweza kuchochea maendeleo na kusogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi, hoja hizi zinaendelea kutumiwa na serekali ya CCM kila wanapobuni wilaya mpya.

Nyerere alikaribia kutekeleza sera ya majimbo miaka ya sabibi walipo anzisha madaraka mikoani. Lengo la madaraka ya mikoani ilikuwa kuongeza nguvu ya kimadaraka katika mikoa na mikoa husika kuweza kutumia vizuri rasilimali zake kujiletea maendeleo(sehemu ya sera ya majimbo),hapa kama wangefanikiwa tungekuwa na majimbo 21(mikoa ya sasa).Hapa walikuwa wanataka kuondokana na utegemezi wa kimamuzi toka Dar-es-salaam.

Walikuja kuanguka kwa sababu ya walishindwa kuanisha vizuri majukumu ya serekali kuu na serekali za mikoa hivyo kukawa na muingiliano mkubwa wa kimajukumu, pili viongozi wa mikoa na wilaya waliendea kuawajibika kwa rais badala ya kwa wanachi wa maeneo usiku na tatu hakukuwa na ushiriki mzuri wa wananchi, nguvu ya umma haikuthaminiwa.

Historia ni mwalimu mzuri, baada ya madaraka mikoani kushindikana wakachanganyikwa, hawakufanya utafiti wa kina kubaini sababu za mfumo ule kushindikana matokeo yake wakaendelea na mfumo mbovu, ambao walishabaini ndio maana wakabuni madaraka mikoani.

Sera murua ya majimbo ya CHADEMA inaziba mapungufu ya madaraka mikoani, Ingekuwa tumeaanza na mguu mzuri wakati ule wa madaraka mikoani sasa hivi Tz Ingekuwa chini ya sera ya majimbo kama ambavyo inapendekezwa na CHADEMA.

Halafu umenifurahisha sana uliposema maeneo yasio na ukabila kama Dar-es-salaam. Kwanini hakuna ukabila Dar? Kwa sababu ndipo kwenye rasilimali zote za nchi kila mtu anakimbilia Dar,hali hii impelekea mchanganyiko mkubwa, ni kwa mtririko huhuo tukiwa na sera ya majimbo, amabapo kutakuwa na mgawanyo mzuri wa rasilimali tutetengeneza "Dar" nyingi mno, tutakuwa nazo maeneo kama geita, kahama, mikumi,kiwila,serengeti,pangani,dodoma............ Dar hizi mpa nazo zitakuwa ma mchanganyiko mkubwa wa makabila malimbali.
 
Eric,

Naona sasa umetoka kabisa ktk swala zima la Majimbo na kuanza ku-question Ukabila nchini. Na sielewi imefika vipi hadi uniulize kama nilikuwepo!..
Haya ndio maneno ya Mwanasiasa kuwa CCM hawasikii sauti za watu wengine isipokuwa zao wenyewe!... dhahiri unaanza kuwa mstari huo.

Inaonyesha wazi unaanza kujadili kama kweli Nyerere aliweza kuondoa Ukabila bila kufahamu tofauti zilizopo kati ya watu waliokuwa HURU na wale walio - TAWALIWA.
sasa nikuulize wewe unaepinga ama ku-question Ukabila!
Chini ya Utawala wa Mkoloni (Muingereza) uliwahi kusikia Wajaluo wakipigana na Wakikuyu? na unaweza kunipa historia ya resistance yoyote kati ya makabila ya Kenya wakati wa Mkoloni?...Na tuache kenya twende rwanda uliwahi kusikia resistance kati ya Tutsi na hao wahutu chini ya Mjarumani ama M-Belgiji..! Wasomali -unajua nao baada ya kuvunjika utawala wa central Government ndipo kulipo zuka hizi clan! leo hii wasomali wana kaskazini Djibout, Mogadishu na Kismayu na wanachuki ya ajabu hali watu hawa wanazungumza lugha moja. nachokuuliza mimi ni kwamba ikiwa haya maswala yanaweza kutokea Chadema mnazo mbinu gani kuhakikisha hayawezi kutokea kabisa! wewe unataka tufumbe macho na kuomba Mungu tu hali dalili na uwezekano upo!

Hii ndio tofauti kubwa kati yangu na wewe kwa sababu wewe mshikaji unatazama yale yaliyopo usoni pako hujaribu kutazama mbali, na ndio maana nimekwambia kuwa Majimbo ni dose kubwa ambayo inaweza kuwa na side effect. Sasa ikiwa wewe unaelewa jinsi dawa zinavyofanya kazi utanielewa vizuri zaidi. Medical ingredients zote za dawa yenu kanipa Mwanansiasa kwa kirefu - nikasema ni bomba, safi kabisa ktk kuondoa dosari za Kiutawala na hizi mbinu zinaweza kutumika bila kuwepo kwa majimbo. majimbo ni capsule kubwa yenye dosage (ml) kubwa sana kuliko matakwa ya tiba ya mgonjwa Tanzania Kiuatawala. na iwapo haya majimbo ni ktk kufanikisha Utendaji kazi KIUCHUMI basi zipo mifumo mingine bora zaidi ikiwa ni pamoja na economic zones.

Haya maswala ya kusema baada ya uhuru tulikuwa na mikoa TISA sijui tumeongeza hivi majuzi ni habari za kusimuliwa na watu huna hakika kabisa kwani nimesoma wakati huo - 60's, na kwa taarifa yako sisi tumekaa mtihani wa mwisho wa east Afrika shule za msingi -hivyo piga hesabu utajua unazungumza na umri gani hapa.
 
Mjadala umekolea sana.
Chinga rudi tukupe tuzo kwani thread yako inatamba hadi leo na umevunja rekodi watu wanakimbilia 13,000.
tuwe na utaratibu wa kuwatunza wana forum wenye vitu kama Chinga na Es.
 
Ukiwa na akili ya kitumwa utazaa watoto watakuwa watumwa pia .
 
Lunyungu,

Ndugu yangu una machungu sana na Mswahili, mwache aseme kutuliza roho yake unajua tena babu ubishi hapa nimesha kolea na hoja!...

Eric,
Usiingie mitini hii mada muhimu sana hivi tunavuta subra kumsubiri J.J Mnyika maanake anajua hii ngoma nzito sana.. inabidi waipitie upya kuhakikisha capsule ni tosha kwa kipimo cha dawa.

Sote hapa tunaelewa vizuri kuwa kasha la dawa hii ya uongozi lebel ya CCM ni nzuri sana kuitazama tena zinashindana na hiyo ya Chadema na pengine kuishinda Chadema kwa umbo la capsule zake (ndogo ndogo -Mikoa na wilaya) lakini kibaya, tumekuja gundua kuwa kilichowekwa ndani ya capsule hizo ni uchafu mtupu (dawa fake)- made in India.. hakuna dawa ni maandishi matupu. Tumefungiwa kanyaboya.
Gonjwa letu haliwezi kupona hata siku moja kwa dawa za Uongo na Chadema dawa mnayo tena nzuri sana lakini mshikaji hili la majimbo kuna mshiker, na amini maneno yangu nauona kama vile nimewekewa maji mezani... kidonge hakipiti kooni!
Kuna msemo mmoja ngoja nikupe hapa:-
Watoto wa mjini huwa tunasema unapoandaa chakula mara nyingi tazama kwanza akina nani umewaandalia chakula hicho. Harusi ya O'bay sii sawa kabisa na harusi ya Tandale, Uwanja wa fisi. Unaweza kabisa kuandaa sahani moja kubwa la ubwabwa (Buffet) O'bay watu wakala na kusaza lakini huwezi kufanya hivyo Uwanja wa fisi.. watu NJAA kali, sahani litakwisha kabla hata halijagusa ardhi na mara nyingi chakula kingi kumwagika! wanyonge hukung'utwa viganja vya mkono kabla chakula hakijafika kinywani.. mtu ngangari hutangaza ushindi kirahisi. Sasa mshikaji unataka kuifanya harusi yako Tandale na inatakiwa ifane, iwe yenye kheri na kila mtu aridhike na shibe..
Je, mbinu ipi utaitumia kuhakikisha harusi hii imefana?

Sijui kama umenipata?
 
Mkandara, Tupo pamoja siwezi kukimbia mjadala hata siku moja hasa ukiwa ni mjadala chanya kama huu.

Sijafanya suala la ukabila kuwa ajenda, nimejaribu kukuonyesha kuwa tatizo la ukabila Tanzania ni suala la kubuni, sio kubwa kama ambavyo unataka kuonyesha. Na pia nimejaribu kukuonyesja kuwa ukabila si suala la kimfumo ni suala la hulka na wakati mwingine linachochewa na historia.

Rwanda, Mkoloni alimtumia mtusi kuwatawala wahutu, kisha akaja kuiacha nchi mikononi mwa wahutu na huo ndio ukawa mwanzo wa utungu.

Ukabila ni ubinafsi, na ubinafsi unajitokeza kwa njia nyingi, kama uchama(watu kuweka maslahi ya chama mbele dhidi ya taifa), udini,rushwa na kadhalika.TZ kwa kiasi kikubwa tunaliwa na rushwa ambayo inachangiwa na kutokuwepo kwa mfumo wa kuwajibisha viongozi ambapo sera ya majimbo ni suluhisho.

Nimezungumzia ukabila kwa kuwa hoja yako ya kupinga sera ya majimbo imejikita katika hoja ya ukabila, kwamba sera itachochea ukabila, nimejenga hoja kuwa sera ya majimbo itachochea muingiliano mkubwa wa baina ya makabila na pili Tz haina historia au makovu ya kikabila,pengine hii ni hoja ya kubuni inayoletwa na watu wanahofia mabadiliko.

Mimi si bishi kama CCM, sijashawishika na hoja ya ukabila Tz, sera ya majimbo italeta vipi suala ambalo halipo? Je ukabila unaoendelea katika nchi za jirani ni tokeo kimfumo? Ikiwa ni hapana, iweje sera murua ya majimbo ilete Tatizo hilo?

Nimejaribu kuonyesha kuwa, wakati tunapata uhuru, kungeweza kutokea mlipuko wa makabila, tungeweza kuwa na uchaguzi wenye mgongano wa makabila lakini halikutokea kwa nini? Kwa sababu hakukuwepo na ukabila. Na kama una hofu na ukabila kiwango hicho, ulipaswa kuogopa mfumo wa sasa wa kugawa wilaya kwa misingi ya kikabila kuliko hata sera ya majimbo.

Nakuabali zipo changamoto zitakazo jitokeza katika sera ya majimbo, ndio maana kwenye sehemu nyingine nimesema tutafakari kwa kina changamato kama gharama na mgawanyo wa kimajukumu baina ya serekali kuu na serekali za majimbo na zile za wilaya.
 
Eric,

Labda sasa tuzungumzie swala la Ukabila kwa picha kubwa zaidi maanake nilikuwa nakupa picha ya Tanzania na sikupenda kuzihusisha nchi nyingine isipokuwa pale ulipotumia mifano ya Kenya na Rwanda.
Sii kweli kuwa Ukabila wa Rwanda umetokana na ati Mkoloni kumwachia madaraka Mtusi ila hilo limechangia kutokea kwa vita kati yao baada ya mikapa kuanza kuwa issue -ARDHI.
Ukabila bado unasimama palepale. Mbona sisi wakoloni waliwapendelea Wanyakyusa, Wahaya na Wachagga na bado tuliweza kutoweka ukabila mbele?.. naweza hata kudiriki kusema waislaam wa tanzania walitengwa sawa kabisa na hao wahutu, yet matokeo hayakuwa sawa baada ya uhuru!.. Ni kitu gani kilichopoza ubaguzi nchini?..
Sii kweli kuwa Ukabila sio swala la mfumo... Mimi naamini kabisa kuwa mfumo ndio kichochezi kikubwa cha Ukabila ambao mara nyingi huwa ni sawa na Volcano iliyolala. Je, Unataka kunambia mfumo wa Utawala wa South Afrika na Rhodesia haukuwa sababu ya ubaguzi wa rangi ktk nchi hizo?..and wht's is the reason behind... utakuta ni KIUCHUMI zaidi kuliko hulka ama chuki baina ya watu.
Ndugu Eric, hata Wahutu na Watusi swala kubwa lilikuwa Kiuchumi na sio hulka yao. ndio maana nikasema wakati wakitawaliwa Mhutu na Mtusi waliishi pamoja... mfumo wa kuwapendelea Watusi ndicho chanzo cha uadui wao na hasa pale kabila moja liliweza kufaidika zaidi kiuchumi kuliko jingine. hayo hayo yametokea Kenya, Uganda na hata nchi nyinginezo.
mafanikio hutazamwa kwa rangi zake iwe Ukabila ama dini na ndipo chuki baridi huanza kinachotakiwa ni cheche tu kuanzisha moto mkubwa wa ubaguzi.
mara nyingi humu umetumia sana nchi zenye mfumo kama wa tanzania kutofanikiwa kiutawala lakini umesahau kabisa kuwa zile zenye majimbo ndizo zina matatizo makubwa zaidi kuliko zile ambazo zipo chini ya central government. Hawa wanapigana vita kabisa na kuna makundi hata ya kijeshi kwa makabila yake lakini ukitazama Kenya ni Ukabila ambao unatumika hali nchi yao bado ina amani. Kwa ujumla matokeo ya Ukabila yana tofauti kati ya nchi na nchi lakini mfumo wa kiutawala ndio kiberiti cha mpasuko wa Ukabila.
tazama Somalia na Iraq leo hii..ni nchi zenye historia tofauti kabisa lakini mfumo pekee ndio umezua matokeo yaleyale. Iraq walikuwa wakitawaliwa kimabavu lakini Saadam alishindwa kuyaunganisha makabila yake kama alivyofanya Nyerere. Kurdish walibaki wakitumia lugha yao, identity yao, na kibaya zaidi mikapa yao - pia Waarabu wenyewe waligawanyika kwa dini zao chini ya Utawala ambao ulisistiza Umoja wao kwa mabavu bila mfumo bora wa kujenga umoja huo.
Matokeo yake leo hii zile tofauti zao ndizo zimekuwa cheche ya mgogoro mkubwa uliopo leo.
Hizi ni baadhi ya mifano michache ambayo imekuwepo kutokana na mifumo ya kisiasa na sio kweli ati Ubaguzi wa kikabila hutokana na Hulka... laaa binadamu wote tunayo pride ya who we are, where we came from na hii ni nature kuwa na uchungu na kile kinachokufanya wewe nani!..
Cheche moja tu ikiwashwa kwa kutumia tofauti hizo ndugu yangu hakuna cha kusema Wachagga hawawezi kujiona wao bora kuliko Msukuma na msukuma akajenga uhasama na kusema I never liked you in the first place!.. Hii haina maana ni hulka ya msukuma kumchukia Mchagga.

tazama leo hii wapo watu wanaodai kuwa Chadema ni chama cha Wachagga ktk nchi ambayo wote tunadai hakuna Ukabila. Just to think that Wachagga wanaweza kufanya hivyo ni dalili tosha ya kukuonyesha kuwa sub consiously, people are aware of that na ndio sababu wapo wanaosita kuwakubali kutokana na cheche iliyokwisha washwa. CUF wameshindwa kabisa kujitangaza vizuri kwa sababu hiyohiyo hali tunazidi kudai kuwa Tanzania hakuna Udini...
haya ni mambo ambayo mnatakiwa kuwa makini sana hasa mnapojenga mfumo uliokuwa wazi kwa mtu yeyote yule kuwasha cheche hizi. Zinatakiwa mbinu za kufunga kabisa uwezekano wa hili kutokea hasa mnapotaka kuondoa kile kilichojenga Umoja wetu kwa kuanzisha mikapa mipya.
 
Mkandara,

Mfano wa Afrika kusini ni tofauti kabisa na ukabila.Noamba ufafanuwe namna wakoloni walivyopendelea Wahaya, Wachaga na Wanyakyusa dhidi ya makabila mengine

Upo sawa, ukabila ni njia mojawapo ya ubinafisi kama ilivyo rushwa na udini.

CCM ni wadini na wakabila ndio maana wamekuwa wepesi kurusha propaganda kwa vyama vingine kwa maana fikra zao ziko karibu mno na ukabila na udini, na hata mfumo wanaoutumia unakazia ukabila, rejea mgawanyo wa wilaya, ndio maana naendea kukushangaa kwa hofu ulionayo juu ya ukabila, kwanini haupingi mfumo wa sasa ambao ndio unajenga na kuimarisha ukabila.

Kwenye mchango wako mmoja umesema kuwa Dar ni mmoja ya maeneo ambayo hakuna "ukabila", hii ni kwa sababu Dar ndipo rasilimaliu zote za nchi zinapelekwa, ndipo tunasema kwa mgawanyo muafaka wa mapato ya rasilamali yatakayotokana na majimbo, "Dar" nyingi zitazaliwa zenye mchamgonyiko mkubwa wa makabila na kufuta kabisa chembechembe ndogo za ukabila ziliopo miongoni mwa watanzania wachache.

Naiona sera ya majimbo kama suluhisho badala ya tatizo, kama ukabila ndio kizingiti kikuu kwa mtazamo wako dhidi ya sera murua ya majimbo.

kuna wakati ulipendekeza kuwa tuchukue hoja ya sera ya majimbo tuweke kwenye mfumo wa sasa, kama kweli ukabila upo TZ pendekezo lako ndio hatari zaidi, maana tutakuwa na serekali za mikoa zilizo huru zenye makabila machache, hivi ukichukua kanda ya ziwa kabila gani litamnyanyasa mwingine na kivipi? au kanda ya kusini?

Ndugu Mkandara, umoja wa taifa unamomonyolewa kila siku na ufisadi. Tusijidanganye kwamba umoja wa watanzania uko imara sasa, wakati ambapo watanzania maskini wanalazimika kuishi kwenye ufukara mkubwa kwa sababu ya ubinafsi wa viongozi na mfumo unaominya haki za wananchi.Hasira zinazidi kuchemka miongoni mwa watanzania, chukulia bei ya umeme inavozidi kupanda, ambao maana yake watanzania wanalazimika kugharamia maisha ya anasa ya wezi wa IPTL!! Mambo yakiharabika itakuwa ni ukabila?

Taifa tunaligawa kila siku kati ya matajiri na mafukara. Ufisadi na watu wa CCM kujioni wenye haki zaidi ya wengine Unachochea ufa miongoni mwa wanachi.Naamini umoja wa watanzania uko katika hatari katika mfumo wa kinyonyaji unaofukarisha wengi na kuwaneemesha wachache, mfumo unaodhibiti ushiriki wa wanachi kuamua hatma yao, mfumo unaotengeneza miungu watu, naona sera ya majimbo inayaondoa yote haya.

Ukabila utazuka vipi ikiwa watu wananufaika vizuri na raislimali zao? Ikiwa kuna muingiliano mkubwa wa watu? na tishio pekea la umoja wa watanzania ni ukabila? Tangu lini umoja ukashamiri kwenye ufisadi na pasipo na haki.

Je ukitafakari, kati ya sera ya majimbo na mfumo wa sasa, ni mfupo upi unatetea haki zaidi? Ni mfumo upi utakaowezesha wanachi kufaidika na rasilimali zaidi? Ni mfumo upi utakaochochea muingiliaono wa watu?
 
Eric Ongara,

Heshima yako mkuu..kumbe bado upo? .. sawa mzee, sasa nitajibu hoja zako kwa kituo. Moja baada ya nyingine.

Nitarudia kusema kuwa mfano wa South ulikuwa kujibu hoja yako uliyodai kuwa Ukabila hutokana na HULKA sio MFUMO. Ilikuwa kukuonyesha kuwa source ya ubaguzi ni mfumo mbaya, na sidhani kama kuna tofauti ya source za ubaguzi wa rangi, kabila ama dini. Kifupi cheche hizi huwashwa na mifumo iliyopo sehemu husika na sio hulka.

Ukabila sio sawa kabisa na RUSHWA kwa sababu rushwa sio moja ya ubaguzi.

Umesema CCM ndio wakabila kwa kuweka wilaya.... hapa umeshindwa kuangalia matokeo. Kama kweli maneno yako mbona Tanzania hadi leo hii baada ya miaka 40 haina Ukabila?..ni kipi kilichozuia hata baada ya wakoloni kuwapendelea baadhi ya makabila.
Hapa unapotazama wilaya zetu unazitazama kama mgao wa ardhi vile vile kwa makabila yake hali umeshindwa kuona kuwa target ya Nyerere kwanza ni UKABILA sio UCHUMI. Kuwaondoa Machief kuweza kuwa- replace na ma DC otherwise nambie wewe ungeweza vipi kuwakata nguvu machief ktk maamuzi ya serikali. Hili ni jambo ambalo halikufanyika nchi nyingi zenye Ukabila. Nyerere alifahamu kuwa cheche za Ukabila huanza toka juu kwa viongozi na ndiko alikoanzia. Hivyo basi Ukabila ulikuwa ni main reason ya mfumo mzima wa wilaya. Nyie Chadema, Ukabila sio sababu ya kuwepo kwa majimbo yaani mna li-over look swala hili kwa sababu za kiuchumi. Mpango wa majimbo unatazama sehemu moja tu - kwenda mbele yaani Offensive force ya kiuchumi hali hakuna Defence ya swala la Ukabila.
Now, ndugu Eric nimesema sana hili na nitazidi kurudia kusema kuwa Nyerere aliweza kufanikisha kuondoa Ukabila kwa mfumo wake lakini hakuweza kutujenga kiuchumi why? - kwa sababu sio mipaka inayojenga uchumi wa nchi ila ni mfumo wa kiuchumi. Sasa ikiwa wewe unaamini mfumo wa mipaka ni kichombezo bora ktk uchumi sawa kabisa lakini kuna mfumo upi kudefend Ukabila. isije kuwa kama Nyerere kaweza Ukabila kaja shindwa ktk uchumi.

Mfano wa mkoa wa Dar ni kuchanganya kati ya Ukabila na Uchumi... mkoa wa Dar una wilaya kama mikoa mingineyo yote.. na sababu za kuwepo RC na DC ni zile zile ambazo zilikuwepo mikoa na wilaya nyinginezo. Dar ni matokeo ya mfumo wa Nyerere ktk kuzuia cheche za Ukabila na hakika hata miji mingi mikoani imesha anza kuwa kama Dar ktk ukabila lakini sivyo kiuchumi. Kufanikiwa kwa Dar kiuchumi ni matokeo ya miji yote mikuu duniani - Central of business na hii haina Lagos, Mumbai, Nairobi wala NewYork, kifupi haihusiani kabisa na mipaka pia hakuna kati yetu anayeweza kusema Dar ingekuwa tofauti ktk ukabila chini ya majimbo.
Tena basi ukitazama Tanzania na mikoa yake nina hakika imejijenga vizuri sana per mile kuliko nchi maskini zenye majimbo. Kuwepo kwa majimbo inabidi pia tukumbuke kuwa miji kama Bukoba na Musoma inaweza kudondoka zaidi kwa sababu makao makuu yatahamia mji fulani.. Hivyo kweli tunaweza kuwa na Dar nyingi yaani 4 (pia urbanization!) lakini wakati huohuo tumeuwa miji mingine 14 ambayo ina kila uwezo wa kuwahudumia watu wasiopungua millioni 2.
Kwa hiyo ni bora tuziendeleze miji yetu kwa mikoa na wilaya zake kuboresha wananchi wa sehemu hizo kuliko kuboresha mji mmoja ktk eneo kubwa, jambo ambalo linaweza kabisa kuanzisha cheche mpya!..
WHY them not us,... mjomba bado haija sink in!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom