Taasisi,
Ndugu yetu karibu tena, karibu saaana na nadhani sasa hivi Augustine ataweza kurudi na mada mpya ya kutazama awamu ya JK kama vile tulivyofanya awamu ya Mkapa kule bcstimes...Ningeomba tu tuwe na mtu ambaye anaweza kuwa upande wa fence ya JK kama kiongozi nje ya CCM...
Tabasamu,
Ndugu yangu point yako hii:-
Majimbo yanajitokeza kama hoja mbadala kutokana na ukubwa wa nchi na hivyo uwezo wa serikali kuu kushughulikia maendeleo unapwaya.
Naikubali sana tu kwa mtazamo wa juuu juu bila kuzingatia madai yangu.
Ni hivi kama leo tukirudi nyuma na kuwauliza wazungu sababu za kuigawa Afrika watakupa jibu hilo hilo!.. Kwao kama vile viongozi wa Chadema hawakuona ubaya ya zoezi kama hili kiutawala na jinsi gani linaweza kutengua nguvu za wananchi bali walitanguliza interest zao.
Tofauti iliyopo kati ya Chadema na wazungu naweza kusema ni kwamba wazungu watasema hivyo kutuzuga hali walifahamu kabisa kuwa tutagawanyika na rahisi kwao kutu control baada ya kutuvunja nguvu ya UMOJA wetu hali Chadema hawafahamu matokeo zaidi ya dhana yenye malengo bora kwetu.
Problem kubwa ya mgao huu ni kwamba maamuzi ya uchumi yatafanywa na majimbo kwa hiyo hapa hatupunguzi ukubwa wa nchi ila tunaongeza idadi ya watawala -as a state and a nation, hali idadi ya wasomi wetu itabaki ileile na pengine kuanzisha hoja za ajira. Who will be first priority.. mkazi wa kanda ya ziwa ama mzaramo anayetaka kuhamia Mwanza!
Now, kabla Chadema hawajafanya makosa kama hayo ndio sababu nimetoa mawazo yangu mengi na mifano kibao nikitegemea kwamba Uongozi wa Chadema wanaweza kusita na kurudi kuutazama upya mpango wa majimbo na pengine kutunga plan inayoweza kutupa picha kamili na sio kutegemea wananchi kutunga plan ya majimbo ambayo wao hawakufikiria kabisa kuwepo kwake.
Mnapo buni jambo ni vizuri kuwepo na plan nzima ya uendeshaji wa hizo kanda kiasi kwamba kesho kanda ya ziwa wasianze kupiga mahesabu ya dhahabu zao against their population na kisha kuona Tanzania haina faida zaidi ya kuwa mzigo kwao.
Kumbukeni its a third gold reserve in the world na bado nyingine zinaendelea kuvumbuliwa! Now, tutaweza vipi kuwapa benefit hawa jamaa Kiuchumi?. Nafikiri mimi niliwahi kusema kuwa economic zones ndio suluhisho na nikaweka mifano ya China jinsi walivyoweza kufanikisha na utawala huohuo wa kikomunist...(Yaani wameweza kutenga mfumo wa Utawala na ule wa Kiuchumi)..
Kinacho nisikitisha ni kwamba hapa tunaendeleza mabishano bila kuwa na suluhisho ambalo sidhani kama kuna kosa Chadema mkisema tutalipitia upya swala hili kwa kuzingatia mawazo yako. Nina hakika, nyie nyote wasomi tena sii wadogo mmeweza kuona nachokisema isipokuwa mnafikiri hii itakuwa aibu.
lakini CCM wamefanya mangapi mabovu ambayo sera zake hazikufanya kazi tena basi bila kupitia kwa wananchi?...sera kibao wala hazina hesabu na leo hii wananchi wameweza kuwasamehe pamoja na kwamba tulihenya kwanza ndani ya sera hizo. Kama alivyosema mwanakijiji kwa ujenzi wa daraja tu watu wameisha samehe vifo zaidi ya mia vya wananchi waliokufa wakijaribu kuvuka mto huohuo kwa miaka 45 iliyopita.
Its no shame at all!.
Ni bora kufuta sera ama kuzirekebisha sera kabla hazijawekwa ktk matumizi kuliko sera za CCM ambazo zimekuwa forced kwa wananchi only to find too late kuwa haziwezi kufanya kazi. Mbali na hapo CCM never consult wananchi kutoa maoni yao kama mnavyofanya...
Tanzania haina ukubwa wowote ule wa kusema Utawala lazima ukatwekatwe vipande!..as a fact Tanzania nzima ina wasomi wachache sana ambao huwezi kuwagawa sawa ktk majimbo na hivi sasa wanalitumikia taifa letu kila kona. Tukiwajaza watawala ktk majimbo.. lets say kanda nne zitakuwa na bunge lao kila jimbo (kanda).. hapo kila kanda itakuwa na wabunge sii chini ya 50 kutengeneza wizara za majimbo..Kisha kutakuwepo na Wabunge wa kitaifa another 100+ kama sio 200.
Hapa hawa wote ni watawala na wote wataondoka na mashangingi, posho na fedha za kustaafu hali kinachotupa taabu sisi ni Ugawaji mzuri wa mapato ya taifa.
haya ni matatizo pia tuliyokuwa nayo ktk Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kiasi kwamba watu tumeshindwa kuelewa kuwa serikali zetu zinapoteza fedha nyingi kwa watawala na hawa hawa watawala ndio wanaozua mbinu za kutugawa zaidi kila siku.
Tumeweza kumkemea JK kwa baraza lake la mawaziri akisingizia vitu hivyo hivyo..but ukweli ni kwamba mbona wakati wa Nyerere wizara chache ziliweza kufanya kazi vizuri sana pamoja na kwamba hatukuwa na mfumo mzuri wa kiuchumi?
Trust me ndio maana kila siku husema kama Nyerere angekuwa na mawazo ya Mtei Kiuchumi (just open market) chini ya Uongozi wake...Naamini kabisa Tanzania tungekuwa mbali sanaaa!..