Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 59,525
- 104,226
Ebu Soma vizuri, hakuna binadamu anaweza kukaa zaidi ya siku Saba bila kula. Sasa unasema wamekaa bila kula miezi mitano ??
Elewa ni siku za mahakamani ndo wanakosa chakula Cha mchana ingawa siyo haki kumnyima mtuhumiwa chakula Cha mchana.
Maagizo ni wao kukomolewa
tatizo hilo liko kwa kina Mbowe pekee wanapokuja mahakamani au ni kwa wafungwa wote?.
Kama Bwana jela ametoa option yakubeba take away wanapokuja mahakamani, shida iko wapi?,
Kwa wazoefu, mtuhumiwa anapokuwa mahakamani wakati wa break haruhusiwi kupewa chakula kutoka nje?...
Kwanini imepita miezi mitano linasemwa leo?
nakipindi chote cha kesi huwa tunaona watu wanabreak kwenda kula, Jaji na mawakili pande zote...
Nimeuliza maswali hayo kwa nia njema, tujadili bila siasa kwenye jambo hili..
Kama Mbowe na umaarufu wake wote anafanyiwa hivyo, itakuwa hao watuhumiwa wengine? Kimsingi mifumo karibia yote ya kutoa haki inafanya kazi kikatili sana, na ni mambo yanafahamika kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu.