Chibati
Senior Member
- Jul 28, 2015
- 150
- 212
Wee utakuwa Chahali au umetumwa nae. Kuhoji Tundu Lisu kwa nini haongei,,,nyie ndio mliratibu mazungumzo yake kule Belgium!???Freeman Mbowe kwa sasa ni mtu huru kama ilivyo kwa jina lake, kesi yake ilifutwa na Mahakama Kuu, mmoja wa watu waliokuwa wakipiga kampeni ya kuhoji juu ya kesi aliyofunguliwa Mbowe na wenzake watatu ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Lissu alifikia hatua ya kuomba kuonana na Rais Samia Hassan Suluhu wakiwa huko Ubelgiji, mara baada ya mkutano wao, Lissu akajitokeza hadharani na kufafanua yale aliyozungumza na Rais Samia, moja ya hoja yake ni kuwa alimwambia kuhusu kesi ya Mbowe.
Kujitokeza kwa Lissu kuzungumza kile walichozungumza na Samia ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzi hayo iliwashangaa wengi lakini nilimuelewa kwa kuwa inawezekana alitaka kujisafisha, anajua CHADEMA wenzake wasingemuelewa kama angekaa kimya.
Sasa Mbowe ametoka gerezani, shangwe ni kubwa mitaani, mitandaoni nako kumechafuka kila mtu anazungumza lake kuhusu Mbowe kuachiwa, lakini ni tangu kesi hiyo ifutwe siku kadhaa zimepita sasa, Lissu yupo kimyaaaaaaa.
Kunani kwa Lissu kuhusu huu ukimya wake, mwenyekiti wake ametoka, yupo mtaani, lakini mbona hatuoni tamko lake wala reaction yake.
Wengi tunajua Lissu ni mmoj kati ya watu ambao akitaka kuzunguza kuhusu jambo lake huwa harudi nyuma, anazungumza hata kama jamii hasa wale wasiokubaliana na sera zake wataona kama anazingua, lakini kwa nini sasa yupo kimya.
Ampotea mitandaoni, hajaonyesha kama kilio chake kimesikika au hakijasikika, amefurahi au hajafurahi Mbowe kutoka gerezani? Cha kushangaza zaidi Mbowe mwenyewe hadi sasa hajataa jina la Lissu katika mahojiano yote aliyoyafanya hadi sasa tangu ametoka.
Keshamaliza kazi yake,Mbowe yuko uraiani.
So what?