Mbowe, Lissu: Rais Samia amegawa Maliasili za Taifa bila Bunge kushirikishwa

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
- Baada ya Bandari, sasa atuhumiwa kugawa raslimali nyingine kwa Wageni

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAKATI sakata la "Mkataba wa Bandari" likizidi kupamba moto, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kimemtumbukiza rasmi Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye kashifa nyingine kubwa, kikidai amevunja sheria za nchi na kugawa kimya kimya maliasili za misitu, maeneo ya hifadhi za taifa na mbuga kwa wawekezaji wa kigeni, bila Bunge kushirikishwa wala kuridhia mikataba ya uwekezaji huo.

Rais Samia anatuhumiwa kugawa kiholela jumla ya hekta milioni nane za misitu ya Tanzania kwa wawekezaji wa Kiarabu kutoka Dubai kwa mkataba ambao umesainiwa bila kuwekwa wazi na kupata ridhaa ya Bunge.

Anatuhumiwa pia kuhamisha wananchi wa jamii ya Kimasai na kugawa maeneo ya hifadhi za Ngorongoro na Loliondo kwa wawekezaji wa Kiarabu, kinyume cha sheria kwani mikataba hiyo haijapata ridhaa ya Bunge.

Aidha, anahusishwa pia na ugawaji wa ekari milioni sita za mbuga ya wanyama kwa kampuni ya Mwiba Holdings inayodaiwa kumilikiwa na Bilionea wa Kimarekani, Dan Friedkin, bila bunge kushirikishwa kwenye kupitia na kuridhia mkataba wa uwekezaji huo.

Kutokana na kile alichokiita "kukithiri kwa ugawaji na uuzaji wa maliasili na raslimali za nchi", Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amewaomba Watanzania kote nchini kuzidi kuamka na kujiunga kwa wingi na chama hicho ili kuokoa urithi wa raslimali za watoto wa Kitanzania, alizodai zimezidi kugawiwa kiholela kwa wageni, hata chini ya serikali ya sasa ya rais Samia Suluhu Hassan.

Mbowe ameyasema hayo leo mjini Shinyanga wakati akifunga mkutano wa uzinduzi wa Operesheni +255 kwenye kanda ya kichama ya Serengeti inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.

Operesheni hiyo yenye ujumbe wa "Katiba Mpya:Okoa Bandari Zetu", inalenga kuibua kero na matatizo ya wananchi, ikinadi sera za Chadema na kujenga mtandao imara wa chama hicho nchi nzima.

Akiwasili dakika za mwisho na kuzungumza kwa ufupi, baada ya kuchelewa kwenye mkutano huo kwasababu za kiufundi, Mbowe alisema:

"Miaka 62 ya uhuru, serikali za CCM wamethibitisha kwamba hawana uwezo hata kidogo wa kuwaondoa Watanzania kwenye umaskini mkubwa unaowakabili. Uwezo pekee waliobakia nao ni wa kugawa na kuuza raslimali zetu

Nawaomba Watanzania wote, kote nchini tuzidi kuamka na kukipokea Chama hiki, tukikumbatie chama hiki, mjiunge kwa wingi, kwa pamoja tupiganie na kuokoa urithi wa raslimali za nchi yetu ambazo zimezidi kugawiwa na kuuzwa kiholela", alisema Mbowe.

Kwamba, kwa mwenendo huo, Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake, wamekuwa si viongozi wa nchi, bali ni kikundi tu cha madalali tu kinachofanya kazi ya kunadi, kugawa na kuuza kila raslimali za nchi kiholela, kwa maslahi yao binafsi.

Awali, akichambua tuhuma hizo za ugawaji wa maliasili za nchi, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, alisema, rais Samia amevunja Sheria ya Enzi kuu ya Nchi inayoipa nchi Mamlaka ya Kulinda Umiliki wa Maliasili, "The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignity) Act", ya mwaka 2017, iliyopitishwa wakati wa utawala wa hayati rais John Pombe Magufuli.

Kwamba, wakati Sheria hiyo inataka mikataba yote ya uwekezaji katika maliasili kuidhinishwa na Bunge, rais Samia, ameingia mikataba yote hiyo ya uwekezaji bila Bunge kushirikishwa katika kupitia au kuridhia mikataba hiyo kama sheria inavyotaka.

Lissu, ambaye pia ni Wakili, aliongeza kuwa sheria nyingine iliyovunjwa na rais Samia ni Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Mikataba ya Maliasili za Nchi, "The Natural Wealth and Resorces Contracts (Review and Re-negotiations of Unconscionable Terms) Act", nayo ya mwaka 2017.

Kwamba, wakati Sheria hiyo inalipa Bunge nguvu ya kupitia upya mikataba yote inayokwishaingiwa na serikali kuhusiana na maliasili za Tanzania, rais Samia hajalipa Bunge haki na wajibu wa kupitia mikataba hiyo ya uwekezaji iliyoingiwa na serikali yake mpaka sasa, hali inayoibua shaka kuhusu maslahi ya Taifa kuhatarishwa ndani ya mikataba hiyo.

Huyu anayesambaza mabango ya picha zake nchi nzima, akijiita ni Mnyenyekevu, ni Mzalendo, sijui nini....kama kweli yeye ni Mzalendo basi tunataka aoneshe uzalendo wake kwa kuweka wazi mikataba yote ya uwekezaji waliyosaini na kuwagawia wawekezaji maliasili zetu", alisema Lissu.

Aliongeza kuwa haya Rais Benjamin Mkapa alibinafsisha kiholela mashirika ya umma 450, pamoja na migodi yote ya madini, kisha akafuatiwa na rais Kikwete aliyedai kuwa yeye aliwapa wageni vitalu vya gesi asilia na mafuta na kwamba sasa ugawaji na uuzaji holela wa raslimali za nchi unaendelezwa kwa kasi kubwa zaidi na rais Samia.

Magufuli, yeye alijaribu kurejesha raslimali za nchi, lakini alikwama kwasababu alifanya kama mtu ambaye hakwenda darasani, hakuwa na uelewa wala maarifa ya kushughulika na mikataba ya uwekezaji, akaishia kuitia nchi hasara kubwa kwa kushitakiwa na wawekezaji"*, alisema Lissu, na kuongeza

Sasa amekuja huyu anayeitwa "Nani kama Mama". Ndani ya mwaka mmoja tu, tayari keshagawa bandari zetu zote kwa Waarabu, kahamisha wananchi kule kwenye hifadhi za Ngorongoro na Loliondo kwaajili ya kuwapa Waarabu, kagawa hekta milioni 6 za maliasili za misitu kwa Waarabu hao hao wa Dubai. Na kuna taarifa kuwa wamegawa ekari milioni 6 za mbuga ya wanyama kule Meatu kwa bilionea wa Kimarekani anayeitwa Dan Friedkin.

Tuna kazi moja tu ya kufanya, nayo ni kuungana Watanzania wote ili tupiganie urithi huu wa watoto zetu unaogawiwa kwa wageni",

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mji wa Shinyanga, aliyekuwa diwani wa CCM, Thomas Maganga Chuma, pamoja na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM, Joseph Sura Masanja, walitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga rasmi na Chadema.
IMG_20230825_201302_207.jpg
 
- Baada ya Bandari, sasa atuhumiwa kugawa raslimali nyingine kwa Wageni

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAKATI sakata la "Mkataba wa Bandari" likizidi kupamba moto, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo zi wa CCM, Joseph Sura Masanja, walitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga rasmi na Chadema.View attachment 2728770
Mungu ibariki CHADEMA
869bd07e67e29c35d24b6d4892fd3015.jpg
 
- Baada ya Bandari, sasa atuhumiwa kugawa raslimali nyingine kwa Wageni

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAKATI sakata la "Mkataba wa Bandari" likizidi kupamba moto, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo
Ni kweli tupu!
Na sio siri....
Na ilianzia hapa!
JamiiForums-1957254544.jpg
JamiiForums1210543597.jpg
JamiiForums1574589568.jpg

Na baada ya DP-WORLD kuna "ENOC"inakuja!

Ilianzia kwenye picha ya mama kubandikwa Burj El khalifa
Jengo refu kuliko yote Dubai pale..
kisha vikao vikafuatia huko Dubai na hapahapa Dodoma.
Kisha ndio ikazaliwa hii inaitwa DP-WORLD. (Deep-world).

Sasa mnaposhangaa mama kukaa kimya muelewe hili.

Nukuu ya mama kanisani KKKT-Arusha.
"Kwa hilo baba askofu,nimechagua kukaa kimya na nitaendelea kukaa kimya"

Eeh Mola Inusuru Tanzania
Pia unaweza Soma hii kwa kina!

"Samia’s administration has made the UAE a top target of its international economic diplomacy agenda.
During an official visit to Dubai in February 2022, she made a personal appearance at the Expo Dubai festival.36 bilateral MoUs were signed between Tanzania and UAE authorities for total investments of $7.49 billion.The deals involved energy, agriculture, tourism, infrastructure and transport technology sectors."
Mwisho wa kunukuu!!
 
- Baada ya Bandari, sasa atuhumiwa kugawa raslimali nyingine kwa Wageni

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAKATI sakata la "Mkataba wa Bandari" likizidi kupamba moto, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo /ATTACH]
Duh
 
- Baada ya Bandari, sasa atuhumiwa kugawa raslimali nyingine kwa Wageni

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
WAKATI sakata la "Mkataba wa Bandari" likizidi kupamba moto, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kimemtumbukiza rasmi Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye kashifa nyingine kubwa, kikidai amevunja sheria za nchi na [/ATTACH]
Mungu Ibariki TZ
 
Back
Top Bottom