Katiba mpya, Mbowe na Lissu ni wamoja? Wanazungumza lugha moja na kupaza sauti moja? Kwanini wanaonekana kama kila mtu na lake, kila mtu na lwake?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali la msingi, kisha majibu utayatoa wewe.

Swali la leo la bandiko hili ni kuhusu hoja ya kuipambania katiba mpya: Je, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe na Makamo Mwenyekiti wake, Mhe. Tundu Lissu ni Wamoja? Wanapambana pamoja, wanazungumza lugha moja na kupaza sauti moja? Je, ni mimi tu nawaona ni kama watu wawili tofauti, kila mtu na lake, na kila mtu na lwake?

Kwa kuanzia nijitambulishe ili kujenga uhalali wa kuzungumzia jambo lolote la CHADEMA.

CHADEMA, japo ni chama cha wanachama, ni chama cha umma, yaani it's a public party na sio a private party. Mimi ni Mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye mlipa kodi ya kuendeshea nchi.

Hivyo kila Mtanzania yoyote, anayelipa kodi kwa serikali ya JMT, ana haki ya kutoa mawazo yake yoyote kuhusu uendeshaji wa serikali ya JMT na kuhoji jambo lolote linalihusu matumizi ya fedha zake ambazo ni kodi yake.

CHADEMA kinaendeshwa kwa fedha za ruzuku ya vyama vya siasa, hivyo sisi walipa kodi, tuna haki kuzungumza na kuzungumzia jambo lolote kuhusu CHADEMA kwasababu ni fedha zetu zinazoendesha CHADEMA.

Nazifuatilia ziara za uhamasishaji wa katiba mpya na uimarishaji wa chama, zinazofanywa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, na Makamo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, naziona kama hazina coordination na haziko coordinated, japo zote zina lengo moja la amsha amsha na uhamasishaji wa katiba mpya na kuimarisha chama, mimi naziona kama Mbowe na Lissu, hawazungumzi lugha moja.

Mbowe anazungumza as a mature politicia, anazungumza kama a statesman in waiting kuja kuwa kiongozi mkubwa wa nchi kwa kuzungumza kwa upole, kwa heshima na lugha ya kistaarabu wakati Lissu anazungumza kama mwanaharakati anayepigania katiba mpya huku akizumza kwa ukali, na lugha kali, na sometimes hata kwa lugha ya machukizo!

Mbowe anazungumza kama a compromised leader aliyeko kwenye meza ya mazungumzo ya maridhiano na kuna mambo tayari wameisha kubaliana na kuridhiana japo bado hawajafikia muafaka na kuyatangaza wazi, wakati Lissu anazungumza as if CHADEMA bado iko kwenye Mapambano na yeye ni yuko vitani, yuko msituni kwenye fighting ya mapambano ya kupambania katiba mpya.

Jee haya anayoyazumza Lissu, Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? ametumwa na CHADEMA au ni yake? Kwa vile Mbowe anaonekana a compromised leader, kutokana na kuwa ni mtu wa shukrani kwa Mama kwa alomtendea, hivyo inambidi awe mpole tuu, hivyo ili Mbowe asionekane mbaya kwa Samia, haya mambo ambayo Lissu anazunguka kuyaongea, ni Mbowe amemtuma au amekubaliana nae. Kama ni hivyo, mbona mikutano ya Lissu haionekani kuwa na proper logistical support? Mfano ni huu, Lissu akiwa kwenye jukwaa la mabanzi (Kichanja) Huu kweli ni mkutano uliopangwa na Chadema kama chama au individual stand alone arrangements?.

Kama hayo Lissu anayozunguka kuyasema ni yake na hajatumwa na yeyote, then CHADEMA kina wajibu wa kumdhibiti, na wasipo mdhibiti now, huko mbele atakuja kuwagharimu very dearly!

Kwenye issue ya katiba mpya Rais Samia anaihandle vyema, ameunda kikosi kazi huku akifanya mazungumzo ya maridhiano na CHADEMA, kwa stage tuliofikia, ni nzuri na haihitaji mapambano na mapigano, sasa hizi lugha za kianaharakati za Lissu, anapambana na nani? Na Mama? na CCM au.

My Take
Ili Chadema ifanikiwe kwenye jambo lake lolote, viongozi wake wakuu, Chairman, VC na SG, lazima wazungumze pamoja, kwa lugha moja na sauti moja na sio kama hali ilivyo sasa kila mtu anazungumza lake, na kwa upande wa maandalizi ni kila mtu na lwake.

Viongozi wawili wakuu mnapo toa kauli zinazopishana pishana, mnawachanganya wafuasi wenu kujiuliza washike lipi?

Kwe haya Mapambano ya katiba mpya, jee Mbowe na Lissu ni pamoja?

Paskali.
 
Chadema kinaendeshwa kwa fedha za ruzuku ya vyama vya siasa, hivyo sisi walipa kodi, tuna haki kuzungumza na kuzungumzia jambo lolote kuhusu Chadema kwasababu ni fedha zetu zinazoendesha Chadema.
Bila ya kujibu swali, naweka msisitizo wa hoja iliyopo juu sambamba na kusema niliibua hoja ifananayo na hiyo.....

CHADEMA haiwezi kuja kuwahadaa Wananchi kuwa wanataka kupunguza matumizi ya walipa kodi huku wao wakiendekeza utumiaji wa Kodi, tena kupitia ruzuku kwa kukodisha helikopta, kukodisha dereva(ana vibali huyo?) wake, kupaka rangi, yaani hiyo nizaidi ya V8 tatu kimatumizi na kifedha....
....waache hadaa, wanaziba ziba na kukandamiza hoja za Kunani nyuma ya pazia ya Maridhiano. Its a Distraction. Hatahivyo, kama ulivyoelezea
mnawachanganya wafuasi wenu kujiuliza washike lipi?
Wanachagulika?
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali la msingi, kisha majibu utayatoa wewe.

Swali la leo la bandiko hili ni kuhusu hoja ya kuipambania katiba mpya: Je, Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman

Paskali.
Mbowe na Lisu ni wamoja .

Strategy wanayoitumia ni njema sababu CCCM Si chama kinachoheshimu makubaliano bila shinikizo, SUK ni mfano mzuri.

Katika Mapambano lazima tuwe na Alternative zaidi ya moja.

Na nionavyo, Lissu atasaidia sana maridhiano yaheshimiwe na kutekelezwa, maana mtaani tupo tayari kuidai Katiba mpya Kwa MAANDAMANO ikiwa CCCM wataendelea na chenga zao kupoteza muda.
 
Wakibanwa hapo wanapaita hiyo ndio "game plan" kwamba kwa sasa plan yao ni kiongozi mmoja wa chama aelekee Kaskazini akiongea yake, huku mwingine akielekea Kusini kujisemea yake!.

Kwangu sioni kama kuna plan yoyote pale, kinachotokea kwa sasa ndani ya Chadema ni uendawazimu tu, wale watu sio wamoja, inawezekana kabisa wamevurugana wenyewe ndani kwa ndani kwa muda wakifanya siri, sasa naona imefikia wakati mmoja kazidiwa kaona bora akaropoke nje.
 
Mbowe na Lisu ni wamoja .

Strategy wanayoitumia ni njema sababu CCCM Si chama kinachoheshimu makubaliano bila shinikizo, SUK ni mfano mzuri.

Katika Mapambano lazima tuwe na Alternative zaidi ya moja.

Na nionavyo, Lissu atasaidia sana maridhiano yaheshimiwe na kutekelezwa, maana mtaani tupo tayari kuidai Katiba mpya Kwa MAANDAMANO ikiwa CCCM wataendelea na chenga zao kupoteza muda.
Maridhiano gani bwashee? 😃😃
 
Tundu Lissu always ni project ya nchi za magharibi katika kuleta machafuko hapa Tanzania. Ni wakati muhimu kwa Serikali kumdhibiti tusije kuwa Sudan nyingine
Wakati hayati Magufuli yupo madarakani mlikuwa pamoja na Lissu, Samia kaingia mnamkana kwa kua mnalamba asali,acheni ujinga Mbowe kanunuliwa na CCM,
Lissu yuko sawa kabisa na aendelee kuanika janja ya CCM na mnaojiita wapinzani wakati ni CCM B
 
Ma CCM hayataki mtu awe mpole saana (Mbowe) huwa ni maongo, so Lisu staili yake ya mapambano ni plan b ambayo ni muhimu sana kwa kuzingatia ulaghai huo wa ma ccm!.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zenye swali la msingi, kisha majibu utayatoa wewe.

Swali la leo la bandiko hili ni kuhusu hoja ya kuipambania katiba mpya: Je, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe na Makamo Mwenyekiti wake, Mhe. Tundu Lissu ni Wamoja? Wanapambana pamoja, wanazungumza lugha moja na kupaza sauti moja? Je, ni mimi tu nawaona ni kama watu wawili tofauti, kila mtu na lake, na kila mtu na lwake?

Kwa kuanzia nijitambulishe ili kujenga uhalali wa kuzungumzia jambo lolote la CHADEMA.

CHADEMA, japo ni chama cha wanachama, ni chama cha umma, yaani it's a public party na sio a private party. Mimi ni Mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye mlipa kodi ya kuendeshea nchi.

Hivyo kila Mtanzania yoyote, anayelipa kodi kwa serikali ya JMT, ana haki ya kutoa mawazo yake yoyote kuhusu uendeshaji wa serikali ya JMT na kuhoji jambo lolote linalihusu matumizi ya fedha zake ambazo ni kodi yake.

CHADEMA kinaendeshwa kwa fedha za ruzuku ya vyama vya siasa, hivyo sisi walipa kodi, tuna haki kuzungumza na kuzungumzia jambo lolote kuhusu CHADEMA kwasababu ni fedha zetu zinazoendesha CHADEMA.

Nazifuatilia ziara za uhamasishaji wa katiba mpya na uimarishaji wa chama, zinazofanywa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, na Makamo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, naziona kama hazina coordination na haziko coordinated, japo zote zina lengo moja la amsha amsha na uhamasishaji wa katiba mpya na kuimarisha chama, mimi naziona kama Mbowe na Lissu, hawazungumzi lugha moja.

Mbowe anazungumza as a mature politicia, anazungumza kama a statesman in waiting kuja kuwa kiongozi mkubwa wa nchi kwa kuzungumza kwa upole, kwa heshima na lugha ya kistaarabu wakati Lissu anazungumza kama mwanaharakati anayepigania katiba mpya huku akizumza kwa ukali, na lugha kali, na sometimes hata kwa lugha ya machukizo!

Mbowe anazungumza kama a compromised leader aliyeko kwenye meza ya mazungumzo ya maridhiano na kuna mambo tayari wameisha kubaliana na kuridhiana japo bado hawajafikia muafaka na kuyatangaza wazi, wakati Lissu anazungumza as if CHADEMA bado iko kwenye Mapambano na yeye ni yuko vitani, yuko msituni kwenye fighting ya mapambano ya kupambania katiba mpya.

Jee haya anayoyazumza Lissu, Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability? ametumwa na CHADEMA au ni yake? Kwa vile Mbowe anaonekana a compromised leader, kutokana na kuwa ni mtu wa shukrani kwa Mama kwa alomtendea, hivyo inambidi awe mpole tuu, hivyo ili Mbowe asionekane mbaya kwa Samia, haya mambo ambayo Lissu anazunguka kuyaongea, ni Mbowe amemtuma au amekubaliana nae. Kama ni hivyo, mbona mikutano ya Lissu haionekani kuwa na proper logistical support? Mfano ni huu, Lissu akiwa kwenye jukwaa la mabanzi (Kichanja) Huu kweli ni mkutano uliopangwa na Chadema kama chama au individual stand alone arrangements?.

Kama hayo Lissu anayozunguka kuyasema ni yake na hajatumwa na yeyote, then CHADEMA kina wajibu wa kumdhibiti, na wasipo mdhibiti now, huko mbele atakuja kuwagharimu very dearly!

Kwenye issue ya katiba mpya Rais Samia anaihandle vyema, ameunda kikosi kazi huku akifanya mazungumzo ya maridhiano na CHADEMA, kwa stage tuliofikia, ni nzuri na haihitaji mapambano na mapigano, sasa hizi lugha za kianaharakati za Lissu, anapambana na nani? Na Mama? na CCM au.

My Take
Ili Chadema ifanikiwe kwenye jambo lake lolote, viongozi wake wakuu, Chairman, VC na SG, lazima wazungumze pamoja, kwa lugha moja na sauti moja na sio kama hali ilivyo sasa kila mtu anazungumza lake, na kwa upande wa maandalizi ni kila mtu na lwake.

Viongozi wawili wakuu mnapo toa kauli zinazopishana pishana, mnawachanganya wafuasi wenu kujiuliza washike lipi?

Kwe haya Mapambano ya katiba mpya, jee Mbowe na Lissu ni pamoja?

Paskali.
For reasons best known to yourself , you are over- obsessed with Chadema issues!!!!!!!!
 
Tundu Lissu always ni project ya nchi za magharibi katika kuleta machafuko hapa Tanzania. Ni wakati muhimu kwa Serikali kumdhibiti tusije kuwa Sudan nyingine
Bila machafuko tutaendelea kutawaliwa kwa shuruti na CCM. Maana CCM inakaa madarakani kwa project za nchi za Asia, na lengo ni kuhakikisha CCM haitoki madarakani ili nchi za Asia hasa China iendelee kufaidika na rasilimali za nchi hii. Na CCM wanafanya lolote ikiwemo kupora chaguzi za nchi hii, maana wanajua wanabackup ya China.
 
Back
Top Bottom