Mbowe ashikiliwa Central Police

Mbowe ashikiliwa Central Police

Viva MBOWE wewe na Watanzania duni kama alivyokuwa MANDELA na SouthAfrica na wabaguzi.
 
Saizi wana muona huyo hakimu aliyetoa amri ya kukamatwa Mh. Mbowe ni wa maana sana lakini mambo yakiharibika watamuona nyoka aliyekuwa hatumii akili na kueandeshwa na ushabiki na kuacha kabisa kutumia weledi wake!. We ngojeni tu, namsubiri wamlete Arusha kisha gereza la mahabusu Arusha tuone kama patatosha.
 
Vijana mko tayari ? Andaeni zana zenu ukombozi umikoni mwenu. . !
 
Wanajamvi, kiukweli nimesikitishwa sana na kukamatwa kwa Mh. Mbowe na polisi tena kibabe bila kujali protocol za kukamata mbunge au mtu mwenye wadhifa unaofanana na yeye kama kiongozi wa kambi ya upinzani, waziri mkuu kivuli. Katika tafakari yangu nimeona tunalaumu sana jeshi la polisi ambalo kiukweli haliwezi kukosa kulaumiwa kutokana na kutumika vibaya na utawala LAKINI MIMI SHUTMA ZANGU ZOTE NAZIELEKEZA KWA MDHAMINI AU MWANASHERIA WA MBOWE AMBAYE AMESHINDWA KUHUDHURIA KARIBU MARA MBILI HADI KUPELEKEA Mh. Mbowe kukamatwa.

  • Mara ya kwanza inasemekana alichelewa kufika mahakamani na kukutwa kesi imeshatajwa.
  • Mara ya pili alikuwa anaumwa tumbo la kuhara. Hoja za namana hii zinatilisha mashaka umakini wa mtu, hivi kweli tumbo la kuhara linakuzuia mtu hata kufika na kutoa taarifa ya ugonjwa au kutumua mbadala ambao ungelea matokeo chanya?
Angalizo katika hili la kukamatwa Mh. Mbowe inaweza kutokea vurugu na hata vifo kutokana na washabiki na wafuasi wa CDM kuona wamechoka kuonewa kwa viongozi wao kukamatwa ovyo ovyo na jeshi la polisi, ambapo ukichunguza kwa undani hoja hii ina mashiko lakini kwa hili la Mbowe naomba nae mdhamini wake asichekewe kwa uzumbe wake ulioleteleza kukamatwa kwa Mbowe.

Ni hilo tu, naomba kuwakilisha.
 
uko sahihi, nami nijiuliza pamoja na kinga anazotajwa kuwa nazo mbunge, lkn kesi ilishakuwa mahakamani, mdhamini kwann hakuwa anafika mahakani siku ya kesi kutajwa? pamoja na udhuru ambao folio D aliutoa mahakamani kwamba anahudhuria vikao vya kamati za bunge, mdhamini c angeendelea kuhudhuria? hii ni fedheha kwa mbunge mwenyewe na cdm kwa ujumla. Napenda mabadiliko,lkn mwendo huu hauwezi kutuharakisha
 
Nasikitika kuona kwamba mfumo wetu wa sheria haujakomaa kiasi cha kuweza kutoa haki sawa kwa wote. Ukiangalia mwenendo wa utekekelezaji wa sheria utona tofauti Kati ya Mtu mmoja na mwingine mfano amri Kama hii ilipotolewa ili Chenge akamatwe hakimu alirudishwa mahakamani ili aifute. Mbowe na viongozi wengine wajarubu kwa kadri inavyowezekana kutoujaribu mfumo wa sheria kwa namna hii. Ingawa umma uko upande wao wajue makali ya kisu yapo upande wao pia. Ningekua mimi ni Mbowe ningepanda helkopta kwenda mahakamani na kurudi kuendelea na vikao vya Kamati za bunge.
 
Kila siku zinavyokwenda wanachi wanaamka kisiasa,na kila siku zinavyokwenda wananchi wanaondokwa na woga woga,itafika time watu hawaogopi tena bunduki kama wanzanzibari,hapo ndipo itakuwa worste.

Tunaweza kuweka kambi katika ikulu zote za tanganyika na zanzibar viongozi wote wang'oke,naamini tunaweza ,waliwezaje TUNIA NA Egypt sisi tusiweze ? Tuwache ushabiki tufanye action.
 
Nimeamini kweli wanasiasa wanafiki!, hawa kila siku wanalalamika sheria inatekelezwa kwa walala hoi wakubwa wanaachwa.
Leo amekamatwa kiongozi wa kisiasa kelele nyingi, walalahoi wangapi wako rumande tena wengine bila kosa hamtetei?, Sheria ni smumeno
 
Hakuna aliye juu ya mahakama. Tusiwe vipofu wa sheria. Mbowe ni mtanzania kama wengine wote,, anapokiuka amri ya mahakama, sheria inachukua mkondo kama kawaida. Yeye ni nani aidharau mahakama? Mbowe yuko salama, na kila kitu kitafanyika kufuata sheria, wewe unayewashauri wenzako, utajikuta peke yako mahakamani. Watanzania si mbumbumbu wa sheria siku hizi.

Nikweli bwana sio mambumbu maana hata wezi wa EPA hawakukamatwa ila tu walibebembelezwa warudishe! hatujui kama walirudisha du! kumbe kunawengine wanaiba mambilioni ya pesa lakini wao wanasamehewa na kuombwa kurudisha! Hongereni sana Wazanzibar mulioamua kujianzishia nchi yenu kama zamani kabla ya muungano maana haya magumu hata kuyameza, sisi bado tuna meza meza bado lakini karibu wengine tutaamua kujitangazia uhuru kama ilivyo kuwa kule chechenia maana ndiyo matokeo ya ugandamizaji!

Dawa ndiyo hiyo tu kujitangazia uhuru maana kila kitu tunaibiwa na akitokea mwanaharakati wakututetea anafanyiwa unyama na wakoloni weusi.
 
Mh Freeman Aikael Mbowe Mbunge wa Hai,Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni(KUB)Mimi binafsi ninakuhakikishia chochote kitakachokupata Ccm na Serikali yake na familia zao watabeba na kamwe hawatakwepa lawama kabisa,Ninapenda kuweka wazi tena wazi sana kuwa Mungu akufanya makosa kumleta dunia Freeman na Jina lake litakamilisha uhuru wa kweli.Mungu mmbariki Freeman Mungu ibariki Tanzania Mungu tupe moyo wa Ujasiri kupigania ukombozi wetu hatimaye tuwe huru.
 
mimi nilishawai kusema jambo hapa jf kuwa Mungu anapotaka kufanya jambo fulani juu ya kuwakomboa watu wake kama haya lazima yatokee na mimi nakuhakikishia mbowe Mungu atakusimamia mpaka mwisho kwa sababu ni yeye ameruhusu haya yatokee hapa duniani ameona watu wake wanavyo nyanyasika
 
Mh Freeman Aikael Mbowe Mbunge wa Hai,Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni(KUB)Mimi binafsi ninakuhakikishia chochote kitakachokupata Ccm na Serikali yake na familia zao watabeba na kamwe hawatakwepa lawama kabisa,Ninapenda kuweka wazi tena wazi sana kuwa Mungu akufanya makosa kumleta dunia Freeman na Jina lake litakamilisha uhuru wa kweli.Mungu mmbariki Freeman Mungu ibariki Tanzania Mungu tupe moyo wa Ujasiri kupigania ukombozi wetu hatimaye tuwe huru.

Binadamu wote dunia wameletwa na Mungu, kwa hiyo Mbowe sio Mtume ni binadamu kama sisi inabidi afate sheria za nchi,kama wakili wake angefika mahakamani yote haya yasingekuepo
 
Binadamu wote dunia wameletwa na Mungu, kwa hiyo Mbowe sio Mtume ni binadamu kama sisi inabidi afate sheria za nchi,kama wakili wake angefika mahakamani yote haya yasinegkuepo

Kwanza hongera kwa kubadirisha Avatar. Pili hatujadili Mambo ya Mungu. Hoja mezani ni kumtia moyo Mbowe. Badiri basi na fikra
 
Back
Top Bottom