Mbowe ashikiliwa Central Police

Mbowe ashikiliwa Central Police

Kufuatia mamuaji ya nyamongo hivi karibuni, mauaji ya Arusha na Tabora, kamatakamata za viongozi wa Upinzani, Mh.Mbowe, Zitto na kutekwa kwa viongozi wa BAVICHA ambao hawajulikani walipo ( Juliana ), nashawishika kusema JK ameamua kuwa Dikteta rasmi.
 
Nadhani unaota anyway sometimes its good to dream mimi nataka kiti kikubwa kuliko vyote pale bungeni lol. Lakini hivi mheshimiwa ange attend kwenye kesi kama sheria zinavyotaka tungekuwa tunalalamika na kumsimanga JK? Ina maana 2015 "tukichuku" JK akishitakiwa halafu asitie timu kwa pilato hatutamkamata? Basi tutakuwa na utawala wa ajabu sana na tutakuwa na haki kuomba kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia.

Anyway huwa sielewi kama unajua kuna kitu kinaitwa claw back clauses kwenye sheria yaan sheria moja inakupa haki na nyingine inakunyima haki hiyo,ndo matatizo ya sheria zetu,kama ni kweli aliombewa ruhusa ya kutokuwepo na wakili wake,na kama kweli walikubaliana hadi amalize vikao vya kamati za bunge,hakimu atakuwa alighafirika na kama si kweli basi ni kosa la mbowe na hasa mdhamini wake kutofika mahakamani kutoa taarifa.

Kwa upande mwingine,kama alivotuhabarisha mnadhimu wa kambi ya upinzani,na tena kwa vielelzo sahihi,mbunge hawezi kukamatwa hadi kibali kitoke kwa speaker,ni kwa nini polisi hawakuomba kibali toka kwa speaker,hata kama amri ya mahakama ya waranti ya kukamatwa ilitolewa? u have 2 think on that.
 
Nadhani unaota anyway sometimes its good to dream mimi nataka kiti kikubwa kuliko vyote pale bungeni lol. Lakini hivi mheshimiwa ange attend kwenye kesi kama sheria zinavyotaka tungekuwa tunalalamika na kumsimanga JK? Ina maana 2015 "tukichuku" JK akishitakiwa halafu asitie timu kwa pilato hatutamkamata? Basi tutakuwa na utawala wa ajabu sana na tutakuwa na haki kuomba kuingia kwenye kitabu cha rekodi za dunia.

wewe endelea kula tende huko ughaibuni, jua na njaa ya huku kwenu Tanga twaijua wenyewe....likely umeshavisahau!! acha tupambane na hawa wakoloni weusi, uhuru wa kweli ukishapatikana,"welcome back home,Muddy"
 

*Wafuasi waandamana, watawanywa, watatu mbaroni
*Dkt. Slaa asema 'ukondoo' wao umefika kikomo
*CUF waungana na CHADEMA, watangaza maandamano

Kauli ya Dkt. Slaa

CHADEMA kimesema kuwa 'ukondoo wao' na uvumilivu dhidi ya udhalilishaji na unyanyasaji unaofanywa na jeshi la polisi kwa viongozi na wabunge wake umefikia kikomo na sasa kitaanza kufanya maamuzi mazito muda wowote.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Willibrod Slaa alisemsa hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kulaani kitendo cha polisi kumshikilia Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe huku wakijua wazi ndiye Waziri Mkuu Kivuli na mwakilishi wa Kambi ya Upinzani kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge inayotrarajia kukutana leo Dodoma. Dkt. Slaa alisema kuwa uvumilivu wao umefikia mwisho wa kuona serikali kupitia Jeshi la Polisi ikiendelea na mkakati wa kuwadhalilisha na kuwadhoofisha wabunge na viongozi kwa kuwakamata bila kufuata taratibu husika, tofauti na wenzao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Alisema kutokana na hali hiyo CHADEMA kimetoa maazimio yao kwamba muda wowote kinaingia barabarani kuidhabu serikali kwa kutumia nguvu ya umma, ikiwa Bw. Mbowe ataendelea kushikiliwa na kushindwa kuhudhuria vikao vya bunge.

Pia alisema kuwa wabunge wote wa CHADEMA hawatashiriki katika bunge lijalo na hata vikao vinavyoanza leo mkoani Dodoma. Dkt. Slaa alisema chama hicho kisitupiwe lawama ikiwa machafuko yatatokea nchini bali lawama zielekezwe kwa Rais Jakaya Kikwete pamoja na jeshi lake la polisi na taarifa tayari zimefikishwa sehemu zote husika ndani na nje ya nchi. Alisema kuwa kitendo cha serikali kudai kwamba CHADEMA inaendesha uchochezi unaohatarisha amani nchini katika mikutano yao si kweli, bali imeona chama hicho kinatoa elimu kwa wananchi ili kujua haki zao ndio maana imeanzisha mkakati wa 'kamata kamata na dhalilisha'.

Dkt. Slaa alisema hivi sasa anaendelea na mawasiliano na viongozi wa Chadema katika mikoa yote nchini ili kujipanga kuiadhibu serikali kwa kuwa tangu matukio yatokee hakuna kauli yoyote ilitolewa na Rais Kikwete au Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda kuomba radhi au kutoa pole kwa mauaji yalitokea mkoani Mara.

Wakati mkutano huo ukiendelea tayari mamia ya vijana walikuwa wamejikusanya makao makuu ya chama hicho wakisubiri kupewa amri ya kuingia barabarani lakini Dkt. Slaa aliwaomba kuwa na subira ili kuimarisha mawasiliano sehemu zote za nchi. "Napigiwa simu na RCO kila mara akinitaka kuwatuliza vijana wangu ambao wengine tayari wamefika kituoni lakini ninachomueleza na kumsisitizia ni kwamba ninaendelea kuwasiliana na wengine nchi nzima ili kuongeza nguvu... na hili tusilaumiwe kamwe," alisisitiza na kushangaliwa na vijana wakitaka kupewa ruksa muda huo. Baadhi ya viongozi wa chama hicho na upinzani walifika katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam anakoshikiliwa Bw. Mbowe ili kujua hatma yake na kufanya kikao na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Bw. Suleiman Kova.

Waliofika hapo ni Mbunge wa Ubungo, Bw. John Mnyika, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wengine ambao walitoa mapendekezo yao. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka kwenye kikao hicho, Profesa Lipumba alisema kuwa lengo la kufika hapo ni kutaka kumwekea dhamana Bw. Mbowe kwa kuwa ni tegemeo lao katika Kambi ya Upinzania na hasa bunge lijalo. "Nimestushwa sana na kitendo cha Mbowe kukamatwa kipindi hiki wakati akiwa katika maandalizi ya hoja za Bunge la bajeti, na hii ni kuminya demokrasia, na kitendo cha kuendelea kumshikilia kinaongeza hasira ukizingatia hivi sasa hakuna heshima tena kwa wabunge wa upinzani, isitoshe spika yupo kimya, hatukubaliani na hili," alisema.

Alisema kuwa wapinzani watakutana muda wowote ili kutoa tamko la pamoja kwa kuwa tayari imeonesha wazi sheria hazifuatwi katika kesi hii badala yake siasa zimechukua nafasi kubwa. "Kuna wezi wa mabilioni wanatembea barabarani hadi sasa na hawakamatwi na polisi, lakini jeshi la polisi limeonekana kufanya oporesheni ya kuwamakata wabunge, sasa tunaondoa tofauti zetu na sasa tunaungana kupinga vitendo hivi," alisema.

Naye Bw. Mnyika alisema katika kikao hicho walimuomba Bw. Kova kuwa hakuna sababu ya kumpeleka Bw. Mbowe Arusha, aachiwe huru ili ahudhuria bungeni, na kama anapelekwa asipelekwe chini ya ulinzi kwa kuwa wananchi wanaweza kusababisha machafuko. Hata hivyo, alisema licha ya mazungumzo yao ya muda mrefu na Bw. Kova, afande huyo alisisitiza kwamba polisi kama chombo cha ulinzi kinatekeleza amri iliyolewa na mahakama.

Bw. Kova alilieleza majira kuwa jeshi la polisi limejiandaa kumpeleka Bw. Mbowe mkoani Arusha muda wowote ili kufikishwa mahakamani leo. Alisema kuwa taratibu za kumsafirisha zimekamilika na kutoa mwito kwa wananchi kuwa watulivu na kuiachia mahakama ifanya kazi zake. Bw. Kova alisema kuwa jeshi la polisi halina nafasi ya kujadilia amri ya mahakama, hivyo lazima Bw. Mbowe afikishwe mahakamani na tayari ulinzi umeimarishwa hapo Arusha.

Kauli ya Chadema Mara
Mwandishi wetu Hellena Magabe anaripoti kutoka Musoma kuwa Chadema mkoani Mara imesema kufikia leo saa nne asubuhi inataka kumwona Bw. Mbowe ameachiwa huru bila masharti yoyote. Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara, Bw. Charles Kayere alisema wanamtaka Spika wa Bunge atoe tamko juu ya kinga ya wabunge kukamatwa ovyo ovyo na kudhalilishwa, hasa wale wa upinzani.

Alilaani kitendo cha polisi kumkamata kiongozi huyo siku ambazo si za kazi ili asote mahabusu, akisema ni cha kinyama na kitasababisha uzalendo uwashinde. Aliongeza kuwa mahakama imekuwa ikitaja kesi hiyo ovyo kabla ya upelelezi kukamilika, jambo ambalo linawatia mashaka kuwa hujuma inafanyika ili kuwadhalilisha wabunge hao wa Chadema.


CUF kupinga kwa maandamano
Chama cha Wananchi (CUF), kimetangaza kufanya maandamano ya amani kupinga udhalilishwaji wanaofanyiwa wabunge kwa kukamatwa wakiwa katika majukumu yao na mauaji ya raia wasiokuwa na hatia unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini.

Kaimu Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa mipango, uchaguzi na Bunge, Shaweji Mketo, alisema jana kuwa chama hicho kitafanya maandamano Juni 12, mwaka huu yakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba. Alisema maandamano hayo yatakayoanzia Ubungo Mataa na kuishia katika viwanja vya Manzese Bakharesa kwa mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya taifa.

Mketo, alisema Jeshi la Polisi hivi sasa limekuwa likiwadhalilisha wabunge na kuwaua wananchi wasio na hatia hasa pindi wanapokuwa wanadai haki zao za kimsingi kwa mujibu wa katiba ya nchi. “Sote tumekuwa mashahidi kwa hili raia wanauawa na polisi bila hatia, lakini bado kumekuwa na tabia iliyojengeka ya kuwadhalilisha wabunge hasa kutoka vyama vya upinzani. Huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na tunawaomba wanaharakati na wananachi wote kwa ujumla watuunge mkono kwa hili,” alisema Mketo.

Aidha CUF imelaani kitendo cha polisi kuwakamata waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao ya kazi katika Kijiji cha Nyamongo, wilayani Tarime kwani si kitendo cha kiungwana na kinakwenda kinyume cha katiba na tamko la haki za binadamu ambalo Tanzania imeridhia.

Alisema kitendo cha kuwakamata wabunge hao ni udhalilishaji wa wazi na kutoheshimu hadhi ya mbunge na madaraka ya bunge. Wabunge waliokamatwa ni pamoja , Bi Magdalena Sakayana (Viti Maalumu-CUF_, Bw. Tundu Lissu (Singida Mashariki-CHADEMA), Bi. Ester Matiko (Viti Maalumu-CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe-CHADEMA.

Pamoja na hatu hiyo alisema CUF inalaani kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwanyima dhamana wajumbe wake wa Baraza Kuu akiwemo Zainabu Nyumba, ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino). Alisema mbali na kuwanyima dhamana viongozi hao, Jeshi la Polisi limeendelea kuwakatama wananchi katika Jimbo la Urambo Magharibi na kufikia 30 hadi kufikia juzi.

Majira
 
Kinachotia moyo sasa upinzani kuanza kukomaa na kuwa na mshikamanao tofauti na awali, huku CUF kama chama kikuu cha pili cha upinzani Tanzania kuwaunga mkono Chadema kudai haki ya ubakwaji demokrasia nchini, Nampongeza Lipumba, bora tofauti zetu kuweka kando kwanza na kuanza kutetea maslahi ya msingi.
 
Wana JF nimeshindwa kupata jibu Kukamatwa kwa Mbowe Serikali imeshindwa kulala, Je angekuwa Rais wa Watu Dr.Slaa ingekuwaje? Je hiko Kituo kingelindwaje?

Naona CCM walikuwa wanajaribu zali kuona kama Nguvu ya Umma ipo au imelala sasa wameamni kuwa Chadema ni moto wa kuotea mbali. Kwani hata Jeshi la CCM linaloongozwa na Saidi Mwema limeonja nguvu ya umma.

Mahakama iliamuru kuwa Fisadi Chenge akamatwe mwaka jana lakini hakuna hata aliyetii amri ya Mahakama katika Jeshi la CCM kwenda kumkamata Fisadi Chenge iweje Jeshi hilo hilo likimbilie kumkamata Mbowe? Kikwete kama ulikuwa unasikilizia Upepo basi nadhani salamu ulizipata jana la leo Kwa hiyo ukae kichugachuga ukileta ujinga tu wa kumkamata Rais wa watu Dr.Slaa ujue ndio utakuwa mwisho wako wa kukaa Magogoni
 
Ha ha ha haaaa kweli umepitwa na matukio, kwenye hili la kesi ya arusha mbona alikamatwa ? na Rais ni mmoja tu kwa mujibu wa katiba na yeye ndio amiri jeshi mkuu, si umeona mbowe alivyokuwa mdogo. Usicheze na dola wewe !
 
Kiukweli polisi wanajitafutia ubusy usio wa lazima kabisa, hivi kumkamta Mbowe kwa mbwembwe kiasi kile na kusafirisha kisha anafika anapewa dhamana mimi naona ni kumpa umaarufu usio na maana.
 
Hakimu wa willaya anatafuta umaarufu kupitia kwa mbowe, ujinga mtupu.
 
Tufikie mahala tuache kulaani,tuingie kazini.Kutoa matamko ni jadi ya CCM inayoambatana na ukada...Wakati wa mapambano tuwe mstari wa mbele.Tusipiganie kukamatwa kwa mtu mmoja mmoja,tupiganie ukandamizaji wa Demokrasia,tupinge matumizi mabaya ya mahakama kisiasa.
 
Kufuatia mamuaji ya nyamongo hivi karibuni, mauaji ya Arusha na Tabora, kamatakamata za viongozi wa Upinzani, Mh.Mbowe, Zitto na kutekwa kwa viongozi wa BAVICHA ambao hawajulikani walipo ( Juliana ), nashawishika kusema JK ameamua kuwa Dikteta rasmi.

Juliana Shonza yupo mahabusu,jana tulikuwa tunafanya mipango ya dhamana.Delay tactics zilitumika leo watatoka
 
Mahakama iko kwa ajiri ya nani?Wapinzani na walalahoi?Mifisadi iliojaa CCM pamoja na JK mwenyewe imefuja na inaendelea kufuja rasilimali zetu inaendelea kudunda na kutanua na hata huku ndani ya chama inafahamiana badala ya kuchuliwa hatua za kisheria inaendelea kutuimbia nyimbo za kujivua magamba huu ni wakati muafaka kwa nguvu ya umma kuchukua mkondo wake.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Na uwe wa kwanza i.e front line si kwenye key board hapo!
 
Duh! Ubabe wa dola unaonekana kwa kuwakandamiza Chadema. Hii ni hatari. Chuki ya wananchi kwa CCM itaongezeka mara dufu.

Sijakuelewa mkuu, wewe ulitegemea mahakama ichukuwe hatua gani kwa mtuhumiwa ambaye yuko nje kwa dhamana na hataki kuheshimu masharti ya dhamana kwa kuhudhuria mahakamani au kama ana udhuru kuitaarifu mahakama. Ni watu wangapi wanaodharau amri ya mahakama na kufutiwa dhamana zao. Mh Mbowe ana tofauti gani na watu hao?

Kwani tunapoongolea watu wote tuko sawa mbele ya sheria, kiongozi wa upinzani anakuwa sio mtu? Raisi anaingiaje katika hili? Raisi alijua kama Mh Mbowe angedhalau amri ya Mahakama?

Mbona Mh Slaa aliyerekebisha dosari na kujusalimisha mahakamni hakukumbana na madhara yoyote? Mbone hata Mh. Mbowe alisalimishwa mahakamani ametendewa haki na kuendelea kuwa katika dhamana?

Kwa nini watanzania hatujiamini na kuongozwa na hisia? Mh Mbowe wakati anaongea na wandishi wa habari baada ya kuachiwa huru alikiri kwamba hakufanyiwa uonevu wowote. Sasa wewe unayesema ameonewa na tena kuna mkono wa viongozi wa juu wa dola unajua kuliko mhusika mwenyewe?
 
Magamba Typical!
Hapa wewe unaona ni sheria inafuatwa au ni udharirishaji tu wa wa wapinzani ? UNA AKILI AU MATOPE? Kwa akili yako fupi na wenzako Mbowe anaweza kutofika mahakamani kwa makusidi, mbona amekuwa ikihudhuria toka kesi ianze na kuahirishwa kila mara ili kuwapotezea muda tu?

kwa akili yako fupi unadhani kesi hii ni ya kweli au ni kujaribu kuficha makosa ya uuaji ya polisi.
Damu ya mtu haipotei hivi hivi, polisi waliua na wataendelea kuua maana damu ya watu wale inaendelea kuwasumbua mpaka watakapokili makosa yao na kutubu mbele ya wafiwa.

Nani asiyejua kuwa kesi zote tunazoziona ni politically motivated?
Kuna sheria gani inavunjwa kama watanzania wote wako salama hata kama chadema wakifanya maandamano kila siku na kila mahali?

Endeleeni kuwanyanyasa Chadema lakini mateso yenu yatakuwa makubwa kuliko mnayowafanyia wenzenu maana mnapanda kisasi.

Walikuwepo akina mbaraka,waliokuwa na utawala imara na hata nchi ilikuwa imetulia, leo wako wapi bwana?

kama wananchi wamewachoka ni better ukakubali ukakaa pemebeni wengine wakajaribu kuliko kung'ang'ania wakati nchi imewashinda!

Mtalazimisha kuitawala Tanzania lakini hamwezi kuwatawala watanzania!

Mungu ibariki Chadema
Mungu wabariki viongozi wa chadema
Mungu wabariki watanzania wenye uchungu na nchi yetu

Amen.


Kwa matusi mimi nakupa ushindi japo kutokana na taratibu zetu za Jamii Forum haturuhusiwa kutumia lugha za matusi. Kwa hilo mhariri kama yupo atanikosoa.

Nikirudi katika hoja zako unaonekana kuchukua nafasi ya msemaji wa Mh. Mbowe. Hamna anakataa kwamba Mh. Mbowe alikuwa na sababu za kushindwa kwenda mahakamani. Suala lilopo hapa ni kwamba mahakama ingejuwaje kisheria kama Mbowe hakuja mahakamani kwa sababu halali au la? Ki kawaida unapopewa dhamana kunakuwa na mdhamini ambaye ndiye anapaswa kuja mahakamani kukuwakilisha kama una udhuru na kuitaarifu mahakama juu ya hilo.

Mh Mbowe hakufanya hivyo wala mdhamini wake. Mahakama si Mungu wala malaika kuweza kujua kwamba Mbowe hayuko mahakamani kwa sababu inayokubalika na Matonya hayupo mahakamani kwa kudhalau mahakama. Kinachofanyika ni kutoa amri ya kukamatwa na kuletwa mahakamani atowe sababu ya kutokuwepo mahakamani.

Amri ya kukamatwa kwa Mbowe ilitolewa siku kadhaa kabla ya kukamatwa. Kwa hali ya kawaida angeweza kutumia mda huo kujisalimisha mahakamani na kutoa sababu zilizomfanya kutokuwepo. Badala yake yeye alianza kulumbana na mahakama kupitia vyombo vya habari akiigeuza mahakama kama chombo cha siasa. Hilo ni kosa hata mh. Mbowe hakulikanusha mahakamani.

Lazima tukubaliane kwamba mh Mbowe ni binaadamu kama mimi na wewe. Anaweza kukosea kama mimi na wewe. Hayuko juu ua sherai kama mimi na wewe. Akikosea na sheria ikachukua mkondo wake tusione kama amedhalilishwa maana Mbowe sio bora kuliko mamia ya watu waliopo magerezani.

Ndugu yangu hata kama nimekosea katika hoja, hamna sababu ya kunijibu kwa lugha ya matusi. Heshima ni kitu cha maana sana. Tofauti za kisiasa na mitizamo ni sehemu ya maisha wa wanaadamu. Hatuwezi kukubalina siku zote. Ndio maana kuna Chadema,CCM, CUF na kadhalika. Sasa kama kila tukitofautiana tunaitana hatuna akili au tuna akili fupi, kama wote tukilipiza kama wewe kutakuwa na Jamii Forum kweli? Wananchi wataelimika kweli? Amani itakuwepo kweli ndani ya Jamii Forum?
 
Back
Top Bottom