Mbowe ashikiliwa Central Police

Mbowe ashikiliwa Central Police

Miezi mingapi mama, 5 au 8? Juzi ilikuwa issue hii mahakamani! Nakutahadharisha kutii mahakama, MBOWE hajaonewa kabisa, alikuwa anadhani sasa ameshakuwa above the law! Watamuachia J3, ila atakuwa amepata fundisho.

Hauko sahihi hata kidogo...Mbowe hajaonewa,Mbowe ameongezewa nguvu yeye na CHADEMA kwa ujumla...CCM inafanya upupu huu ikifikiri inamkomoa Mbowe na CHADEMA wakati ukweli ni wanajikomoa wao kwa kuendelea kudhihirisha kwa wananchi kwamba sasa wanaongoza nchi kibabe,Jeshi la Polisi ni la CCM..Wanapiga risasi kuwaua wananchi wanapojisikia tu,na waoga wote kama wewe endeleeni ku comment upuuzi hapa ila siku ikiwadia hata wale wenye kutetea upupu wa CCM tutawagonga nyundo..Mwanaume kamili hawezi kukubali kuonewa sababu anaogopa Keko au kufa,kuweni madume CCM wamefika mwisho na dawa inachemka jikoni na wakitaka tuanze leo wamjeruhi au wampe sumu Mbowe waone....ARRRRRRRRRRGHHHHHHHHHHHHHHHH
 
Nadhani mnachanganya mambo. Amri ya mahakama iliwahusu washitakiwa wote akiwemo Dr slaa.wenzake walijisalimisa. Mbowe alikataa kwa jeuri tu. Nchi yetu lazima itawaliwe kwa sheria siyo kwa jeuri ya mtu au watu. Nchi lazima ijiendeshe kwa sheria siyo kwa vitisho vya ccv.
 
Hapa nilipo vijana wanajiandaa na mapambano ya kesho. Wataandamana mpaka mahakamani kuishinikiza mahakama imuachie huru Mbowe lasinvo hapatatoha kesho.
 
Nadhani mnachanganya mambo. Amri ya mahakama iliwahusu washitakiwa wote akiwemo Dr slaa.wenzake walijisalimisa. Mbowe alikataa kwa jeuri tu. Nchi yetu lazima itawaliwe kwa sheria siyo kwa jeuri ya mtu au watu. Nchi lazima ijiendeshe kwa sheria siyo kwa vitisho vya ccv.

Acha kuongea bila kufikiri...kwa hiyo we unafikiri Mbowe hakutuma taarifa? si wanafanya kumkomoa na wakijua yeye ni mwenyekiti wa chama na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani..Mbona wakina Chenge walikuwa wanafanya mambo yao kitaa bila kutoa taarifa ya mahakama na hakimu hakuamuru wakamatwe wala nini..Acha kuongea pumba,waweza acha ku type kama unafikiri ki magamba magamba
YOTE HAYA NI MAANDALIZI YA MAGEUZI MAKUBWA YA KISIASA YAJAYO,CCM ITAMWAGA DAMU YA WATANZANIA LAKINI ITAKAA PEMBENI TUU...!!
 
Ni jukumu letu sisi kama watanzania kuona kuwa wakati umefika sasa kuawaaminisha waliomadarakani kuwa uwepo wao ni kwa sababu ya umma na kuna siku umma ukiamua kila mahali hapatakalika,hivyo chondechonde watanzania tuamke na kusema sasa ndio mwisho wa kuonewa na kunyanyaswa.SABABU TUNAYO,UWEZO TUNAO NA NIA TUNAYO.

tuanze na Arusha kesho j3.
 
Hapa nilipo vijana wanajiandaa na mapambano ya kesho. Wataandamana mpaka mahakamani kuishinikiza mahakama imuachie huru Mbowe lasinvo hapatatoha kesho.

Aisee.......Mi nilijua nawe ni mmoja wa hao vijana,ama ndio mambo ya kuwachoche halafu unakaa pembeni...

Kwa nini 'pasitohe' hiyo kesho?,kwani Polisi wamefanya kosa kumkamata Mhe.Freeman A. Mbowe MB/KUB?.....Ilikuwa sahihi kwa yeye na Mdhamini wake kudharau mahakama?,kwa nini yeye tu na si waheshimiwa Lema,Selasini,Ndesamburo ama Mwigamba?
 
Itata, itata ndwalila i ngwegho jangu ngaghoghe i ngebhe isi! Naomba muongozo jamani,tunaanzia wapi? leteni humuhumu hata kama wamo HATUWAOGOPI!
 
Heche unampa nani masaa 48 mahakama au JK? Bahati mbaya mahakama haina siasa! Kwanza mahakam haijui hata Bavicha ni sehemu gani!?
 
Ccm hamna pa kutokea juu ya hili.Ni wabunge wangapi wa ccm walishakamatwa na polisi hovyohovyo?Yule mgombea ubunge kupitia ccm alienkata OCD mitama hadharani mbona hakuna kilichofanyika?Kila siku ni uonevu kwa Chadema tu hamchoki?Kama mnafikiri wananchi tutawaogopa polisi hiyo mmekosea.Mtatuua mtumalize,tutaanza na wabunge wa ccm kula nao sahani moja
 
Hapa nilipo vijana wanajiandaa na mapambano ya kesho. Wataandamana mpaka mahakamani kuishinikiza mahakama imuachie huru Mbowe lasinvo hapatatoha kesho.

Mkuu fanyeni maandamano atolewe leo, hiyo ya kesho mbona ata ungelikuwa wewe ungetolewa tu..
 
Kukamatwa kwa Mbowe na wabunge wengine wa Chadema, ni matunda ya semina elekezi iliyofanyika Dodoma wiki mbili zilizopita ambapo Jaji Mkuu Chande alihudhuria. Kwanza, ni mkakati wa kuidhoofisha Chadema ili kumpa unafuu ****** ambaye anatuhumiwa na wenzake kuvuruga chama.

Pili, kumelenga kumsaidia Othumani Rashid ndugu wa Kilaza wa umri -Jaji Chande ili angalau aonekane anamsaidia Kikwete. Gazeti la kila wiki la MwanaHALISI liliandika makala hii wiki iliyopita, kujadili hatua ya Jaji Chabde kuhudhuria semina elekezi na kile kinachotokea sasa, bila shaka ni matunda ya semina hiyo.

Jaji mkuu ni sehemu ya serikali?
Na Isaack Kimweri
SEMINA elekezi iliyoandaliwa kwa ajili ya watendaji serikalini wiki tatu zilizopita mjini Dodoma imeibua jambo zito.
Jambo hilo ni ushiriki wa mihimili mingine miwili ya dola Bunge na Mahakama katika semina hiyo ambayo ililenga mhimili wa tatu – watendaji wakuu serikalini.
Katika hali ya kawaida, mihimili hii haitakiwi kuingiliana katika utendaji wake wa kila siku.
Kwa bahati mbaya na kwa kweli kwa utashi wa kiitikadi, katiba ya Jamhuri imempa ruhusa rais kuteua wabunge kuwa mawaziri na hivyo kulifanya bunge kuwa sehemu ya serikali. Kelele nyingi zimepigwa juu ya kasoro hii na naamini kuwa katiba mpya itashughulikia kasoro hii ili mihimili hii itenganishwe.
Wengi tunaamini mahakama haipokei amri wala maelekezo kutoka serikali wala bunge. Ni matumaini ya wengi kuwa mihimili hii itaendelea kutenganishwa kwa ajili ya kuboresha utawala bora katika taifa letu.
Kilichoshangaza katika semina elekezi ile ni uwepo, siku ya ufunguzi, wa Jaji Mkuu Othman Chande. Baadaye nilidokezwa kuwa alikuwa mmoja wa watoa mada (mwezeshaji).
Uhusika wa Jaji mkuu katika semina elekezi ya viongozi wa serikali unatia shaka na kuna kila sababu ya kuhoji utaratibu huu mpya wa utendaji kazi wa serikali ya awamu ya nne.
Jamhuri yetu si ya muungano wa mihimili ya dola kiasi cha kumfanya Jaji Mkuu kuwa sehemu ya serikali. Ili kumwepusha na majaribu yanayoweza kutia dosari maamuzi yake na uendeshaji wa mhimili wa mahakama, Jaji mkuu anapaswa kuwa mbali na maelekezo ya serikali – asiyasikie wala kuhusika kama chombo cha kuyatoa kwa watendaji wa serikali.
Hii ni kwa sababu, baadhi ya watendaji wa serikali wanaweza kujikuta wakitenda kazi zao kwa kuongozwa na jinsi jaji mkuu alivyosema au kujikuta wanamtumia kama shahidi wao ili kuwatisha waathirika wa maamuzi yao.
Jaji mkuu, kama mwanadamu, ana utashi binafsi na vionjo vya kiitikadi. Unapomhusisha katika semina elekezi ya watendaji wa serikali, unachokoza vionjo vyake na matamshi yake kiitikadi yanayoweza kuamsha na kuingilia maamuzi yake ya baadaye anaporejea katika wajibu wake wa kazi zake.
Ikumbukwe kuwa serikali iliyo madarakani ina sera maalum na ilani yake ya uchaguzi ambayo ni tofauti na vyama vingine ambavyo havijazuiwa kuchukua madaraka ya nchi wakati jaji mkuu akiwa bado madarakani. Hali hiyo ikitokea, jaji mkuu huyo atapokea au kushiriki semina elekezi ngapi?
Jaji mkuu ni kiongozi mkuu wa mhimili wa mahakama lakini si kiranja mkuu mwenye wajibu wa kuhakikisha majaji na mahakimu wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata maelekezo yake katika jukumu la utoaji haki.
Majaji na mahakimu wana uhuru kamili wa kuendesha na kutoa maamuzi juu ya kesi mbalimbali na kwa hiyo ili kuutunza uhuru huo, jaji mkuu anapaswa ajiepushe na mazingira yoyote yanayoweza kumfanya kuingilia uhuru wa majaji na mahakimu.
Uhuru walionao majaji na mahakimu, anao pia Jaji mkuu. Lakini kwa kitendo cha kuhusishwa katika maelekezo maalum ya serikali kwa watendaji wake, amejifanya kuwa mtendaji kama wao na hivyo kupokea maelekezo ya mkuu wa serikali. Athari za kitendo hiki zitaonekana hivi punde katika utendaji wake.
Nasema haya kwa sababu uhuru wa mahakama umekuwa ukilalamikiwa na wengi. Uteuzi wa Jaji mkuu na majaji unaoacha maswali mengi, pamoja na mbinyo wa bajeti ya mahakama unaosababisha mahakama iwe ombaomba kwa serikali, vinaufanya uhuru wa mhimili huu uwe wa kinadharia zaidi.
Kuna mambo mengi ya kuhoji. Mathalani wakati wakuu wa mihimili ya serikali na bunge wana uhuru wa kuteua au hata kuongoza michakato ya kuchagua watendaji fulani katika mihimili yao, mhimili wa mahakama, jaji mkuu anateuliwa na rais na anapokea pia majaji atakaowaongoza kutoka kwa rais.
Hata kama rais anaweza kumshirikisha wakati wa uteuzi, bado hana mamlaka itoshayo juu ya majaji wengine kwa sababu aliyemteua yeye, ndiye aliyewateua wao. Utaratibu huu unaufanya mhimili wa mahakama kuwa sehemu ya mhimili wa serikali.
Matokeo ya mchakato huu wa kisiasa unaolazimishwa kuingia mahakamani, haki za watu zinacheleweshwa na hivi sasa bila fedha au kujuana na mtu mkubwa katika mahakama zetu ni ndoto mtu kupata haki yake kwa wakati.
Madhambi yaliyozagaa katika vyombo vingine vya dola na ndani ya serikali, yamezagaa pia katika mhimili wa mahakama kiasi cha kutishia amani ya taifa letu.
Imani ya maskini katika mahakama zetu imetoweka na kwa hiyo badala ya jaji mkuu kuhudhuria semina elekezi za serikali angeendesha za kwake ili kutafuta suluhu ya matatizo ya ndani ya mahakama.
Baba wa Taifa aliwahi kusema wakati akiwahutubia majaji kuwa, uhuru wa mahakama ni dhana kwanza kabla haijawa vitendo. Dhana hii inatakiwa ionekane uhalisi wake katika mwenendo wa majaji wenyewe na jinsi wanavyohusiana na viongozi wa serikali.
Mwenendo na maisha binafsi ya majaji vinahitaji visiache maswali juu ya uhuru wao katika kutoa maamuzi ya haki kwa Watanzania. Hivi sasa kuna wakuu wa mikoa (RC) na wilaya (DC) wanadiriki kuandika barua za maelekezo kwa mahakimu au kutoa maelekezo kwa watendaji wa chini yao kisha kuwapa nakala mahakimu kana kwamba wanataka barua hizo zitumike kama ushahidi dhidi ya watakaokiuka maelekezo hayo na kufikishwa mahakamani.
Imetokea hadharani mahakimu kuagizwa na ma-DC na ma-RC kujificha ili kuwakwepa wanasiasa wa vyama vya upinzani ili kutosaini viapo vyao nyakati za uchaguzi. Siyo siri tena kuwa majaji kupitia jaji mkuu wanapokea maelekezo ya nini kifanyike katika kesi nyeti zinazogusa maslahi ya kisiasa ya chama fulani au wanasiasa fulani.
Tumeshuhudia mahakimu wakipokea maelekezo maalum kutoka kwa wakuu wao juu nini kifanyike katika kesi fulani zenye mvuto wa kipekee. Tumeshuhudia masharti ya dhamana za washtakiwa fulani zikifanywa kuwa ngumu ili kuwaridhisha wakubwa fulani.
Vitendo vya namna hii vinaiondolea mahakama heshima na hadhi yake mbele ya jamii. Hata kukithiri kwa rushwa katika chombo hiki nyeti ni dalili tosha kuwa hakina uhuru wowote juu ya maamuzi na uendeshaji wake.
Uhuru kamili wa mahakama ni tishio kwa watawala dhalimu kuliko ulivyo tishio kwa wahalifu wa kawaida wa sheria. Kwa mantiki hiyo, kuongezeka udhalimu katika utawala wa nchi ni dalili kuwa uhuru wa mahakama unapungua.
Uwiano huu wa ongezeko la udhalimu wa watawala na kupungua kwa uhuru wa mahakama, ndicho kiini cha mwaliko wa jaji mkuu Othman Chande katika semina elekezi ya watendaji wa serikali kule Dodoma.
Tujiulize, siku serikali hii ikishtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma kupitia semina elekezi, Jaji Mkuu atakuwa mshatkiwa au shahidi?
 
Kwa wanasheria hili la mtu kutohudhuria mahakamani hadi akamatwe na polisi haliwezi likasababisha hakimu kumnyima dhamana mtuhumiwa kwa kutokuwa muaminifu kwa mahakama
 
Hakuna aliye juu ya mahakama. Tusiwe vipofu wa sheria. Mbowe ni mtanzania kama wengine wote,, anapokiuka amri ya mahakama, sheria inachukua mkondo kama kawaida. Yeye ni nani aidharau mahakama? Mbowe yuko salama, na kila kitu kitafanyika kufuata sheria, wewe unayewashauri wenzako, utajikuta peke yako mahakamani. Watanzania si mbumbumbu wa sheria siku hizi.
si ni mahakama hizi ya Tanzania ilishindwa kutoa maamuzi mgombea binafsi, ikasema ni mambo ya kisiasa? mbona leo mbowe ana kinga ya kisiasa mnasema tuheshemu mahakama tena?
 
peoplezzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz! waendelee kutupa umaarufu tu.. ha ha ha ha ha ha ha!
 
Huyo Heche mjinga tu kama kióngoz wa Taifa anashabikia uvunjwaji wa sheria_mahakama zipo kwa ajili ya mama yake na baba yake tu? Tuache ujinga kwa kutaka kutekezwa kwa maslah binafsi_ya msing tuyape nafasi yake
 
heche usitudanganye, utafanya kitu gani ikiwa masaa hayo yataisha hajaachiwa? hadi j3 ndio siku ya kazi yatakuwa yamepita masaa zidi ya 48, acha usanii, piga hesabu zako vizuri ww

Usanii ni upi lofa..wewe unaona ni sawa kiongozi wa Upinzani kukamatwa bila sababu kwani katoroka ama alikua na majukumu mengine ya kitaifa?!! hujaona ocd anapigwa na mgombea wa ccm halafu polisi wanasema hayo ni mambo binafsi!! ingekua cdm ingekuaje?!! tumia kichwa kufikiria
 
Back
Top Bottom