Mbowe ashikiliwa Central Police | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe ashikiliwa Central Police

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MJIMPYA, Jun 4, 2011.

 1. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  HATMA ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, itajulikana Jumatatu ya wiki ijayo kwa kuwa mdhamini wake amejisalimisha mahakamani jana.

  Mdhamini huyo, Julius Magwe alijisalimisha katika mahakama hiyo saa 5.15 huku akiambatana na wafuasi mbalimbali wa chama hicho na wakili wa upande wa utetezi, Method Kimomogoro.


  Wakili Kimomogoro alidai kuwa, mdhamini huyo alikuwa akihudhuria mahakamani siku zote lakini isipokuwa juzi kwa kuwa alikuwa mgonjwa.


  Ili kuongeza nguvu katika utetezi wake, Magwe aliwasilisha vielelezo mahakamani hapo ikiwemo cheti cha daktari aliyemruhusu kupumzika.


  Wakati mdhamini huyo akijisalimisha mahakamani mkoani Arusha, jijini Dar es Salaam Mbowe aliitisha mkutano na waandishi akidai kuwa alikuwa sahihi kutokwenda mahakamani kama alivyopaswa.


  Katika mkutano huo, Mbowe alisema atasimamia haki yake kwa gharama yoyote iwapo Polisi watatekeleza agizo la kumkamata kwa madai ya kudharau Mahakama.


  "Ni bora ufe umesimama kuliko kuishi umepiga magoti," alisema Mbowe na kusisitiza "huu ni uonevu wa polisi, tutaupinga kwa nguvu zote," alisema Mbowe wakati akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Bunge kupinga madai kuwa ameidharau Mahakama.


  Juzi Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Charles Magesa alitoa amri ya kukamatwa kwa Mbowe na mdhamini wake kwa kutofika mahakamani siku hiyo, kitendo kinachotafasiriwa kuwa ni kuidharau Mahakama.


  Wakati Mbowe akijitetea kuwa alikuwa sahihi, Mbunge mwenzake Godbless Lema (Arusha) alifika mahakamani na Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini) alituma mdhamini jambo lililotafsiriwa kuwa waliheshimu Mahakama.


  Wakati huo huo Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu alisema Mbowe hakuhudhuria mahakamani katika tarehe zote mbili kwa kuwa amekuwa akihudhuria vikao vyote vya kamati mbalimbali za Bunge.


  Lissu ambaye pia ni mwanasheria, alisema mila na desturi za kibunge za Jumuia ya Madola zinataka kinga ya wabunge dhidi ya kukamatwa iwe na nguvu wakati wa mkutano wa Bunge pamoja na muda muafaka wa kutosha kabla na baada ya mkutano wa Bunge.


  "Hivyo Mbowe akiwa ndani ya gari lake la ofisi, haruhusiwi kukamatwa, akiwa nyumbani kwake, akiwa humu ndani na hata akiwa barabarani ni eneo la Bunge kwani yuko hapa kuhudhuria vikao vya Bunge," alisema Lissu.


  Alidai kuwa mila hizo zinataka muda muafaka na wa kutosha kuwa siku arobaini kabla na baada ya mkutano wa Bunge "Kwa mantiki hiyo wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha inatoa amri dhidi yake, Mbowe alikuwa analindwa na kinga ya Bunge."


  Source; Habari Leo
   
 2. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #2
  Jun 4, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania Daima linasema, 'Mbowe agoma kuipigia magoti mahakama'

  WENYEKITI wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amekataa kujisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyoamuru akamatwe kwa kosa la kutotii amri ya kufika mahakamani hapo. Bila kumung'unya maneno, Mbowe alisisitiza kutojisalimisha akisema, "Ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nikiwa nimepiga magoti!"

  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, alisema walishatoa ombi mbele ya Hakimu Mkazi Charles Magesa la kuruhusiwa kushiriki vikao vya kamati ya Bunge kwa mujibu wa nafasi zao, ambalo lilikubaliwa na mahakama hiyo.

  Alisema katika ombi hilo, waliomba dhamana yao iendelee wakiwa nje jambo ambalo pia mahakama hiyo ililiridhia, hivyo kuwa na uhuru wa kushiriki vikao vya kamati ya Bunge la bajeti litakaloanza Juni 7, mwaka huu.

  Alisema kutokana na maombi hayo, mahakama iliamuru wabunge wote waendelee na majukumu yao ikiwemo kushiriki vikao vya kamati za Bunge lakini baada ya siku chache alishangaa kusikia anatakiwa kukamatwa.

  "Siwezi kuzuia hali hii, najua kuna jambo vyombo vya usalama vinataka kufanya ikiwemo kuwadhoofisha wabunge wa vyama vya upinzani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea bajeti ya nchi.

  "Kwa nafasi yangu ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni ni mjumbe wa Kamati ya Fedha ya Bunge, na ninasimamia serikali kivuli katika kuandaa maoni ya kambi ya upinzani, sasa kama wao wanaona wana haki ya kunikamata wafanye hivyo, lakini ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nikiwa nimepiga magoti… sitafanya hivyo kama wanavyotaka hata kidogo," alisisitiza Mbowe.

  Alisema yeye na chama chake hawawezi kukaidi amri ya mahakama ila kinachotakiwa ni mahakama yenyewe kutanguliza busara kuliko kutanguliza utashi na shinikizo la kisiasa kutoka kwa watawala.

  Hivyo, alisema kilichofanyika dhidi yake na watu waliomdhamini ni udhalilishaji hasa kwa nafasi yake kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
  Kwa upande wake Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Tundu Lissu, alisema kambi yao imepokea kwa mshtuko, masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha kutoa amri ya kumkamata Mbowe.

  Alisema kiongozi wao hakuhudhuria mahakamani mara mbili kwa kuwa alikuwa akihudhuria vikao vya kamati mbalimbali za Bunge vilivyoanza Mei 23 mwaka huu.

  "Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na amri ya kumkamata Mheshimiwa Mbowe kwa vile inakiuka moja kwa moja sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na mamlaka ya Bunge na ambazo ni msingi mkuu wa demokrasia yetu ya kibunge.

  "Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua na kulinda uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

  "Uhuru huu wa Kikatiba umetiliwa mkazo katika vifungu vya 5, 6 na 11 vya Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988 vinavyokataza mbunge kukamatwa au kupewa amri ya kuhudhuria mahakamani wakati akiwa ndani ya eneo la Bunge au wakati Bunge limekutana bila kuwepo kwa kibali cha Spika," alisema Lissu ambaye ni mwanasheria kitaaluma.

  Alisema maneno ‘eneo la Bunge' yametafsiriwa na kifungu cha pili cha sheria hiyo kumaanisha "ukumbi ambao hutumiwa kwa vikao vya Bunge, pamoja na ofisi, vyumba, vibambaza, maeneo ya wageni, bustani na maeneo mengine yaliyowekwa kwa ajili ya matumizi au malazi ya wajumbe, maafisa au wageni wa Bunge pamoja na njia zinazounganisha maeneo hayo na maeneo mengine yanayoweza kutangazwa na Spika kuwa ndani ya maeneo ya Bunge.

  Alisema kwa maana hiyo, mbunge anapokuwa anahudhuria vikao vya Bunge au kamati zake au anapokuwa mahali pengine popote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria vikao hivyo vya Bunge hawezi akakamatwa ili kutekeleza amri ya mahakama au ya chombo kingine chochote nje ya Bunge.

  Akigusia kile alichokiita ‘upendeleo', Lissu alisema inashangaza kuona wabunge wa upinzani wakikamatwa na polisi bila kuomba kibali kwa Spika, lakini wanapotaka kuwakamata wabunge wa CCM hufanya hivyo.

  Alisema wabunge wa kambi ya upinzani waliokamatwa kinyume cha sheria ni Freeman Mbowe (Hai), Godbless Lema (Arusha Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Meshack Opulukwa (Meatu), Ester Matiko (Viti Maalum CHADEMA) Felimon Ndesamburo (Moshi Mjini), Joseph Selasini (Rombo) na Madgalena Sakaya (Viti Maalum CUF).

  Akitoa ushahidi wa vibali vinavyoombwa pindi polisi inapotaka kuwakamata wabunge wa CCM, alionyesha barua ya mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Mwanza SP B.M. Wakulyamba kwenda kwa Katibu wa Bunge, ambayo ilimwomba ruksa ya kumhoji Mbunge Dk. Titus Kamani (Busega, CCM) kuhusiana na njama za kutaka kumuua aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk. Raphael Chegeni.

  Kutokana na hali hiyo alisema hakuna mbunge hata mmoja wa CHADEMA au chama kingine cha upinzani ambaye kwa taarifa zao amewahi kuombewa kibali cha kukamatwa na polisi kama inavyoonekana kwa wabunge wa CCM.

  Alisisitiza kuwa hali hiyo inadhihirihisha upendeleo wa wazi wa Jeshi la Polisi kwa wabunge wa CCM na uonevu kwa wapinzani.

  "Tutapinga kwa nguvu zetu zote kitendo chochote cha kumtishia au kumkamata kiongozi wa kambi ya upinzani," alisema.

  Alisema wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha inatoa amri ya kumkamata Mbowe, kiongozi huyo tayari analindwa na kinga ya Bunge.

  "Mbowe ataendelea kulindwa na kinga hiyo kwa kipindi chote cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na muda muafaka na wa kutosha kama unavyotambuliwa katika mila na desturi za Mabunge ya Jumuiya ya Madola hadi baada ya kwisha mkutano huo," alisema mnadhimu huyo.
   
 3. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hayam ngoja tuone nini kitatokea siku za usoni maana wenye kutafsiri hizo sheria si ndio hao Mahakimu?
  Tutamsikia nae akijibu thuhuma hizo nzito.... Tusishangae kuona Mbowe anafutiwa dhamana na kuwekwa rumande kwa shinikizo hilo hilo la watawala wa kisiasa!!
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hii ndiyo raha ya kujua unacho kifanya..serikali ilijichanganya yenye tarehe 29.4 utata huu ulijitokeza kuwa tehehe ilikuwa imepangwa ni kwamba wabunge watakuwa kwenye shughuli za kibunge, wakili wa serikali akaahidi huwaombea ruhusa wabunge wote kitu ambacho hakikufanyika, hivyo utata wote ulitokana mkanganyiko huu, je kwa kuwa serikali iliahidi kuwaombea ruhusa hivyo iliimanisha kama ingefanya kinyumechake washitakiwa wasingetakiwa kufika mahakani..na ikumbukwe kesi hii iliiendelee washitakiwa wote wata
   
 5. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #5
  Jun 4, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kama ulivyosema , lakini kumbuka kesi hii inapressure ya dola, excutive anasukuma muhimili huu kisiasa. Namhurumia hakimu yule, yupo ktk mtatiziko wa kitaaluma dhidi ya watawala walevi , mafisadi na hayawani.
   
 6. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bwana Mheshimiwa, toka nje ujisalimishe unahitajika kituoni kwa kosa la kuidharau mahakama! Nyumba yako sio jengo la bunge wala ofisi ya bunge hivyo haina kinga - toka nje ujisalimishe kwa mujibu wa amri ya mahakama!
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Nyie polisi kwanza nendeni mkaombe kibali kwa Spika -- kama mlivyofanya kwa Mbunge wa Busega -- kwa nini mnabagua namna hii?' Inashangaza sana mnavyofanya kazi nyie polisi -- yaani kumhoji tu Mbunge wa CCM hadi kibali kutoka kwa Spika -- lakini kwa Mbunge wa CDM hakuna haja ya kibali hata kama ni kosa katenda (na siyo kuhojiwa tu).
   
 8. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  'Kibali' kimeshatoka ndo maana polisi wako kifua mbele kuizingira rezidensi ya bwana mheshimiwa. Atoke nje fasta ajisalimishe, wakihesabu ...tatu, yatakujatokea mengine halafu polisi walaumiwe bure na wananchi!
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama 'kibali' kimetoka, basi sasa itakuwa ni halali kwa Mbowe kukamatwa. Ni lesson nzuri kwa polisi katika kufuata sheria kanuni na utaratibu, kama vile wao wanavukuwa wakisisitiza kwa wananchi.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hapana, asitoke, inawezekana kibali ni feki, au hakuna kibali kabisa. Ampigie simu lawyer Lissu afike ili akikague kibali. hawa polisi ni majambazi -- hawaaminiki kabisa.

  Watu wanaouwa na baadaye kuleta visingizio siyo watu wa kuaminika.

  Hata hivyo asante CDM kwa kuamsha jamii katika kuelewa haki zao.
   
 11. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Waheshimiwa wazoefu wa enzi hizo (ex. MP wa rombo, etc) hawakuwahi kuidharau mahakama japo walisota keko wakisubiri dhamana. Bwana mheshimiwa jisalimishe upesi, polisi wako kwa ajili ya kulinda raia (wema?) na mali zao, unaogopa nini? Jisalimishe sasa kwa usalama wako, ohoooo...usiwachoshe polisi wana kazi kibao za kufanya, sio kukusaka wewe tu kwa wiki nzima, alaaa!
   
 12. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 4, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Utani wa kuvuka mpaka. Lakini ndiyo Bongo nothing serious like JK like sons like raia wa chama cha magamba.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni taarifa za kutatanisha kidogo...

  Baadhi ya viongozi wa Chadema wamedokeza kuwa mwenyekiti wao yu central Police akiwa chini ya ulinzi. Lakini wengine wanakanusha kuwa hajakamatwa.

  Atashikiliwa mpaka Jumatatu? Patatosha?
   
 14. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  we chukulia utani, polisi wako siriaz na makini kwa sana tu, hawana utani na Bwana mheshimiwa, salama yake akimbilie ukumbi wa Bunge lakini atapita wapi, ndege yuko tunduni keshanasa na akikurukupuka kutoka tu kakamatwa! Tafadhali jisalimishe uende kituoni kwa usalama wako na wa familia yako, giza likiingia hujatoka itakuwa balaa Bwana mheshimiwa.
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  MJ hembu tuhabarishe ni central police ya mkoa gani twende tukamwekee dhamana!
   
 16. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magamba at work
   
 17. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli wakuu,Dkt Slaa tupo naye hapa Skanska Kwenye uzinduzi wa Chaso Ardhi ametupa hiyo taarifa na mipango mbalimbali inafanyika kuweka hali ya mambo sawa ingawa dhamana mpaka jumatatu.
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ni kweli
   
 19. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  He is where he should have been a looooong time ago
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Itakuwa Dar...habari mbaya sana hii
   
Loading...