Mbona Hassy Kitine hakualikwa/hakuhudhuria?

Mbona Hassy Kitine hakualikwa/hakuhudhuria?

Wazungu walifanya kusudi baada ya kumpika Mandela wakamtoa wakatuletea kama vile Sanamu

Sent using Jamii Forums mobile app

Mandela angefanya Kama Kagame kuwasaka Wahalifu wa Kimbari kupitia Mahakama za Gachacha Wazungu wasingempenda, Mandela aliwasamehe Makaburu kwa unyama wote walioufanya kupitia Tume ya Maridhiano ya Askof Desmund Tutu

Mandela angefanya Kama Kambarage kuwapora Wazungu Mali Basi Wazungu wasingemkubali

Mandela alikuwa Mbwa kibogoyo baada ya kutoka ndio sababu Wazungu walimpenda mpaka kumjengea Masanamu mpaka Uingereza
 
Wengi tu hawakuhudhuria kwa sababu kadhaa!

Hata Augustine Mahiga ( Waziri wetu wa Mambo ya Nje) kuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa lakin hakuhudhuria Mkutano huo!

Kwenye ile Kesi ya Uhaini ya 1983 Shahidi Muhimu aliekuwa anatambulika Kama Mr X alikuwa ni Balozi Augustine na ndie alietibua Mpango ule wa kumpiga Bomba Mwalimu Nyerere Kanisani St Peters Ostybay
Mkuu elezea kidogo basi hlo tukio la mwalimu kupgwa bomba maana wengine humu tulikuwa kwenye trouser enzi hzo.
 
Nimeshangaa Profesa Mbobezi wa Uchumi mwenye ofisi Buguruni kutokuwepo
 
Nafikiri ushujaa wao hao wazee wa zamani ulitokana na watu wa kipindi hicho na mazingira husika. Zamani watu wengi walikua mambumbumbu ndio maana hata ma Captain,Maluteni na hata other lanks wa majeshi mbalimbali Afrika walifanya mapinduzi kitu ambacho kwa sasa ni ngumu. Umahili wao nafikir kwa nyakati hizo sio zama za sasa za teknolojia nyakati zinebadilika sana na kwa nyakati hizi wapo wakali pia zaidi yao ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia.
 
Kizazi hiki nacho kinae Jack Zoka, Miaka ikipita itakuwa ruksa kuzungumza ya Nyuma ya Pazia kumhusu Jabali hili japo kwa sasa hivi haifai kuweka hadharani, Sie tunazungumza ya zamani kwa kuwa kwa kiwango Fulani degree yake ya confidentiality inakuwa imepungua!

Marekani Miaka kadhaa nadhan 30 ikishapita unaweza hata kutunga kitabu kuzungumza baadhi ya Mambo ya 'system'
Comrade upo wima.
Hivi vitu vinapatikana JF, embu tiririka kwa kizazi kijacho.
Andishi hili litadumu


aeiou
 
Tuwasamehe Vijana wetu!

Miaka ya Baadae wakiambiwa kwa Miaka kadhaa Meli za Iran zilikuwa zinapeperusha Bendera ya Tz ( bila ya Serikal ya Tz kujua) kukwepa Vikwazo vya kiuchumi mpaka ilipokuja kubumburuka Miaka ya hivi karibuni watabisha kuwa Hilo halikuwahi tokea
Hivi kwa nini walichagua Tanzania sio nchi nyingine? Nishawahi sikia hata trirand and Tobago nao wako poa kidiplomasia . Kiasi kwamba mtu hakiwa na pasipoti ya huko uwa hapati usumbufu. Kwa nini walichagua bendera ya Tanzania hapa kutakua na sababu tu?
 
Nadhani usiende huko utaharibu Uzi
Kama unamzungumzia Mohamed Said hata Yeye huwa Anakiri kuwa Mwl alikuwa na akili nzuri sana na Mjengaji Mzuri wa hoja, hoja yake ni kwny Mengine ambayo si sehemu ya Mjadala wetu
Kwa Mfano Mimi namkubali sana Mwl kwny Masuala ya Security, ujasusi, Uafrica, Uzalendo , kutojilimbukizia Mali n.k lakin kwny Uchumi wake wa Kijamaa simkubali japo Wapo wanaomkubali kwny Uchumi wa Kijamaa ni tofauti ya kutafakari jambo Moja kwa perspective tofauti

usiogope kuongea ukwel kisa mohamed said hatapenda!
uchumi wa kijamaa ndo suluhisho pekee lakini maliberali na mabwenyenye wenye mtazamo kama wako lazima waukosoe!
 
Mkuu nasikitika sifa mnazowapa hawa waliopaswa kuwa mashujaa wetu.Sio sifa zingine ila ni zile za kuweza kutupa kisago raia wasio na directions wala nini .Yaani sisi raia tuliopo ktk ulabu wa mbege ndio specimen zenu.Km vile mnawashusha saaaana.Ila sio vita za uchumi duniani,sio vita za kiteknologia au hata vita ya kulinda nchi toka kwa mafisadi,au wahindi wanoahamisha dollar zetu na kununua uraia ktk mataifa mengine. Nina mashaka sana km hata kitabu cha huyu mzee kinaweza vutia watu kukinunua kihivyo.Interview yake ipo wazi sana.

Balozi Mahiga kaiingiza Tanzania katika United Nations Security council hapo Turtle Bay New York City.

Watanzania wengi hata hawajui UN Security Council ni kitu gani.

Wakati George Bush anakwenda gung-ho kwenye "War on Terror" akitaka dunia nzima iweke macho kwenye ugaidi, Mahiga ndiye aliyesimama na kusema jamani eeh, tunajua ugaidi mbaya, hata sisi wamelipua watu wetu walipolipua ubalozi wa Marekani Laibon St hapo Oysterbay. Lakini, huko kwetu kuna gaidi mwingine mkubwa zaidi anaogopwa kuliko Osama.

Anaitwa njaa.

Dr. Mahiga alipigana sana UN Security Council kuwezesha suala la food security liwekwe kuongelewa kama a security issue, sio ugaidi tu.

Huo ni mfano mmoja tu ninaoujua mimi, lakini ipo mifano mingi sana ya kazi za hawa watu zinazogusa maisha ya mtu wa kawaida wa kila siku.



Sent from my Kimulimuli
 
Hivi Mandela anasifika kwa sababu ipi? Maana niliulizwa swali nikashindwa ni jambo gani Mandela amefanya kuliko Nyerere kuliko Kaunda

Sent using Jamii Forums mobile app
Mandela amekaa jela sana mpaka watu wanakuwa hawajui au wanasahau historia yake kabla ya jela.

Mandela miaka ya sitini kabla ya kufungwa alikuwa namba chafu sana katika ku organize resistance ya ANC. Ndiyo maana wakamfunga kama kinara. Alikuwa anataka kupindua nchi kwa armed struggle.

Mandela kaanzisha "Umkotho we Sizwe" (Spear of the Nation) baada ya Sharpeville massacre. Hiki ni kikosi cha umoja wa vijana cha ANC kilichokuwa machachari sana.

Mandela alikuwa bonge la "jasusi" akizunguka Africa nzima, Dar esalaam mpaka Algiers mpaka Accra etc (kwa passport ya Tanzania aliyopewa na Nyerere, makaburu hapo walikuwa wanamtafuta) akisuka mipango ya kusaidia uhuru wa Afrika Kusini.

Mandela katika The Rivonia Trials aliwahi kusema yuko tayari kufa kwa ajili ya anachoamini.

Hata mimi nilikuwa naangalia historia ya Mandela ya baafa ya kufunguliwa nikawa nafikiri anapaishwa kwa ku reconcile na wazungu tu, nilivyosoma "Long Walk to Freedom" na kuangalia historia yake kabla hajafungwa, nikaona hii ni namba chafu.

Sent from my Kimulimuli
 
Balozi Mahiga kaiingiza Tanzania katika United Nations Security council hapo Turtle Bay New York City.

Watanzania wengi hata hawajui UN Security Council ni kitu gani.

Wakati George Bush anakwenda gung-ho kwenye "War on Terror" akitaka dunia nzima iweke macho kwenye ugaidi, Mahiga ndiye aliyesimama na kusema jamani eeh, tunajua ugaidi mbaya, hata sisi wamelipua watu wetu walipolipua ubalozi wa Marekani Laibon St hapo Oysterbay. Lakini, huko kwetu kuna gaidi mwingine mkubwa zaidi anaogopwa kuliko Osama.

Anaitwa njaa.

Dr. Mahiga alipigana sana UN Security Council kuwezesha suala la food security liwekwe kuongelewa kama a security issue, sio ugaidi tu.

Huo ni mfano mmoja tu ninaoujua mimi, lakini ipo mifano mingi sana ya kazi za hawa watu zinazogusa maisha ya mtu wa kawaida wa kila siku.



Sent from my Kimulimuli
Shukran sana kwa ushuhuda wako!

Huyu die Balozi Augustine Mahiga Nguli wa Diplomasia na Ujasusi na Ukachero wa kiwango kisichomithilika!

Siasa bana, Huyu Jamaa utakuta kwny Masuala ya Protocal za Kisiasa anatakiwa Paper zake za Kazi za Kidiplomasia anatakiwa kuzipeleka kwa John Magufuli ili azi approve na hata kupunguza au kuongeza kitu!
 
Alipofuatwa na kuulizwa na waandishi wa habari kama tayari wamesha mpandisha cheo askari yule kama rais alivyo agiza, aliyekua mkuu wa jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu alisema jeshi la Polisi lina utaratibu wake wa kupandisha askari wake vyeo, na moja wapo anapaswa aombe kwenda kusomea hiyo ngazi ya cheo na maombi yake yatapitiwa kama ana kidhi vigezo.
Mangu alikumbana na mambo magumu hadi kufika hapo alipo sasa
 
Alifukuzwa na Mwalimu Nyerere kwenye Ukurugenzi wa Usalama wa Taifa kwa kosa la Kununua Mercedez Benz bila ya kumjulisha Mwalimu

Akaja Tena kupoteza Uwaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala bora wa Mzee Benjamin Mkapa kwa kosa la kughushi Malipo ya Matibabu ya Mkewe Nchini Marekani

Alipoongea na Media nyumban kwake Upanga alikanusha tuhuma za kughushi akamtaja PM wa wakati huo ambae kwa sasa ni Mwenyekt wa Chama Fulani kanda ya Pwani kuwa ndie anamchafua kwa kuwa wote wanautaka Urais japo mwishowe wote wakaukosa


kwa jinsi nilivyosoma yale mahojiano huyu mzee ni mpigaji mzur tu mwishoni anahamasisha watu wachukue pesa za rushwa kwa viongozi wanaotoa akumbuke vya watu haviliwagi hovyo kuna muda utatakiwa kurudisha kimya kimya kama huna ndo pa kuonja umauti mwalimu alitumia akili tu kumtupa shule kutokana na nyazifa alizokwisha kuzikamata kubwa kubwa ni rahisi hawa kukuzunguka.
 
Shukran sana kwa ushuhuda wako!

Huyu die Balozi Augustine Mahiga Nguli wa Diplomasia na Ujasusi na Ukachero wa kiwango kisichomithilika!

Siasa bana, Huyu Jamaa utakuta kwny Masuala ya Protocal za Kisiasa anatakiwa Paper zake za Kazi za Kidiplomasia anatakiwa kuzipeleka kwa John Magufuli ili azi approve na hata kupunguza au kuongeza kitu!
Umenifanya nicheke sana. Nilikuwa nasoma btn the lines, ukweli ni kwamba huyu mzee anajua mengi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom