Sifahamu kabila lake Ila Historia yake inanivutia sana!
Alianza kwa kuwa Mwalimu wa Secondari kule Bukoba baada ya kumaliza Chuo Kikuu
Baadae ikaamriwa wote ambao hawakupita JKT waende Hata Kama Wapo kazini
Hassy akajaribu na wenzie kukwepa Mafunzo ikashindikana mwishowe wakasalim Amri wakaenda na Yeye akapangwa Songea
Baada ya kumaliza Mafunzo ambayo walikuwa hawayapendi kuanzia wanatoka Makazini mpaka wakat wa Mafunzo Hassy akajikuta Miongoni Mwa wanaochaguliwa kubaki kuendelea na JKT rasmi wakat tayari akili yake ilianza kufurahia kurudi kazini na kuanzia hapo ndipo akaanza kuandaliwa na mpaka kufikia Cheo hicho kikubwa cha Ukuu wa Usalama wa Taifa
Mwalimu Nyerere kwny Masuala ya Usalama wa Taifa alikuwa sio Mtu wa Mchezo Mchezo
Aliwahi kupeleka Maafisa 15 Nchini Israel depo la Kina Bregadier Muhidin Kimario kujifunza Mambo ya Usalama bila ya wao wenyewe kujuana kwa kuwa walionekana wana tokea Mataifa ya Nje kwa kuwa Uhusiano wa Isarel na Tanzania haukuwa Mzuri, alitumia hati za kusafiri a za Mataifa Rafiki yenye uhusiano Mzuri na Isarel