Mbona Hassy Kitine hakualikwa/hakuhudhuria?

Mbona Hassy Kitine hakualikwa/hakuhudhuria?

..Orengo ni mwanaharakati.

..ukisoma historia yake anasema ameanza harakati tangu yuko shule ya msingi.
Ok nahisi sio mtu wa vyombo vya habari sana maana miaka yote nimekuja kumsikia kwenye hii kesi ya uchaguzi. Uyu yupo tofauti na wajaluo wengine wapenda sifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok nahisi sio mtu wa vyombo vya habari sana maana miaka yote nimekuja kumsikia kwenye hii kesi ya uchaguzi. Uyu yupo tofauti na wajaluo wengine wapenda sifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Humjui Orengo vizuri asee. Ni mwanaharakati wa toka enzi za Moi na mwanasheria Nguli Kenya. Aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi enzi za serikali ya mseto.
 
Kuna mengi sana yalio jiri kwa mujibu wa maandiko mbalimbali, lakini kwa leo naomba nianzie kwanye HUKUMU YA WALIOTAKA KUMUUA NYERERE 1983

Walioshitakiwa kwa uhaini mwaka 1983 walikuwa wengi.
Ilielezwa mbele ya jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Nassor Mzavas kwamba washitakiwa walikuwa 19.
Miongoni mwao alikuwepo Thomas Lugangira au ‘Uncle Tom’ au ‘Uncle Check bob.’

Wenzake walikuwa ni Hatibu Gandi au ‘Hatty Mac Ghee’, Kapteni Mohammed Tamim, Kapteni Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege, Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Mapunda.

Wengine walikuwa ni Banyikwa na mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Hans Pope , Kapteni Rodrick Rosham Robert na wengine kibao ambao jumla yao walikuwa 19.

Wakati kesi inaendelea Lugangira na Hatty Mc Ghee walipanga njama na kufanikiwa kutoroka kutoka katika Gereza la Keko, Dar.
Ilidaiwa kuwa walitorokea nchini Kenya. Baada ya kufika Kenya, Lugangira akatorokea Uingereza. Hatty Mc Ghee alikamatwa na kurudishwa Tanzania kwa kubadilishana na mtu mmoja aliyekuwa akitakiwa Kenya aliyetajwa kwa jina la Private Hezekiah Ochuka ilidaiwa kuwa alifanya ‘madudu’ huko Kenya.

Mc Ghee aliporejeshwa nchini aliunganishwa na wenzake na kesi ikapamba moto.
Komandoo Tamim aliuawa wakati wa kurupushani za kumkamata pale Kinondoni Mkwajuni.

Lakini hata mahakamani wakati wa kutoa ushahidi juu ya komandoo huyo mwana usalama mmoja aliyekuwa akiitwa Mr X alisema walijaribu kumkamata lakini akawatoroka kwa kuruka ukuta wa nyumba aliyokuwa akiishi.

Akasema wakati wakimkimbiza Komandoo Tamim alidandia gari moja pick up iliyokuwa imebeba masanduku ya bia na kuanza kuwarushia wana usalama waliokuwa wakimkimbiza, hivyo akapigwa risasi na kufa.

Kesi hiyo ya uhaini ilikuwa inasisimua sana haswa maswali ya wakili wa utetezi aliyekuwa akiitwa Murtaza Lakha. Mawakili wengine wa utetezi ninaowakumbuka kwa jina moja moja ni Mucadam, Jadeja na Tarimo.
Upande wa serikali ulikuwa unaongozwa na Wakili William Sekule, pia alikuwepo Johnson Mwanyika.

Wakili Sekule alileta mashahidi kadhaa ambao walisumbuliwa sana na mawakili wa utetezi haswa Murtaza Lakha.
Jaji Mnzavas alitoa hukumu Desemba 28, 1985 ambapo washitakiwa wengine aliwafunga kifungo cha maisha na wengine walifungwa miaka kadhaa lakini Banyikwa na Ngaiza waliachiwa huru.
Mwanyika uyu uyu alikuwa AG?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahiga ukimuona juuu juu unaweza kumchukulia kama wanasiasa wengine ila ukifuatilia historia yake unachoka tu. Mzee katulia sana huyu.

Lile tukio la mkewe lilipotokea, alitulia tu. Wangekuwa wanasiasa wengine wa kisasa, wangeanza kutweet mipasho. Vijana tujifunze kwa hawa wazee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee Mahiga ni kati ya watu ninaowakubali sana katika utulivu. Halafu ukimkuta anapiga story na vijana enzi zake balozi, utafikiri mtu wa kawaida tu.

Namuonea huruma sana kufanya kazi serikali hii ingawa najua anafanya kwa uzalendo sana tu.
 
Ni Long story Ndugu yangu lakin kwa ufupi baada ya jaribio la Mapinduzi kushindwa 1983 Baadhi ya Watuhumiwa walitoroshwa Gerezani Ukonga na kupelekwa Kenya Kupitia Mpaka wa Horohoro na lilitumika Gari la Kubebea Mkaa kuwabeba kina Kapten Maganga

Mwl Baada ya kugundua Mpango huo ndipo akatengeneza Revenge

Baada ya Arap Moi kutikiswa ikabidi wafanye Mazungumzo na Mwl Nyerere na wakakubaliana wabadilishane Wale Wahaini ndipo kina Maganga wakadanganywa na Utawala wa Kenya kuwa wanawapeleka kuwaficha Ethiopia kwa kuwa kuna Vijana wa Nyerere Wapo mitaa ya Nairobi wanaweza kuwadaka Kumbe ni Mpango wa kwenda kuwakabidhi Dodoma si Dsm
Nyerere nae aka swap kwa kukabidhi Wahaini feki kwa Moi wakat huo tayari kina Odinga ( Wahaini halisi ) wameenda kufichwa Canada Kama wakimbiziwa Kisiasa kishawasafirisha, Moi baada ya kugundua alipoteza kabisa Interest na Tanzania na Mwl kabisa kwa kuingizwa Chaka

Tanzania haitokuja kupata Rais Mwenye akili Nyingi sana Kama Julius Kambarage Nyerere never never!
halafu akija mtu km mudi analeta dharau na kejeli na kama watu wake wa vijiwe vya kahawa
 
Hawa Wazee kwny ujana wao walikuwa sio Watu wa Mchezo ni Watu Hatari sana sema utu uzima unawafanya tuwaone Kama Simba Wazee
Mkuu nasikitika sifa mnazowapa hawa waliopaswa kuwa mashujaa wetu.Sio sifa zingine ila ni zile za kuweza kutupa kisago raia wasio na directions wala nini .Yaani sisi raia tuliopo ktk ulabu wa mbege ndio specimen zenu.Km vile mnawashusha saaaana.Ila sio vita za uchumi duniani,sio vita za kiteknologia au hata vita ya kulinda nchi toka kwa mafisadi,au wahindi wanoahamisha dollar zetu na kununua uraia ktk mataifa mengine. Nina mashaka sana km hata kitabu cha huyu mzee kinaweza vutia watu kukinunua kihivyo.Interview yake ipo wazi sana.
 
Sana kabisa mkuu Mandela asingejulikana bila ya kambarage.

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh, mkuu sometimes life siyo hivyo? Shujaa yoyote njiani alisaidiwa na wengi ambao walitimiza wajibu wao.Si vyema sana kusema bila fulani fulani asingekuwepo hapo.Inawezekana huyo fulani akawa kampunguzia kimo ambacho angefikia.Tujiepushe sana kuongea kwa jinsi hii.Inawezekana Mwalimu akawa anashukuru kwa kuwa sehemu ya historia ya jamaa.Ndio maana mwalimu alikuwa kiongozi mkubwa,alipunguza sana kujidanganya na kujikweza km wengine. Ujamaa tuu ndio mwl alijidanganya na ujamaa ukamsaliti.
 
Hivi Mandela anasifika kwa sababu ipi? Maana niliulizwa swali nikashindwa ni jambo gani Mandela amefanya kuliko Nyerere kuliko Kaunda

Sent using Jamii Forums mobile app

Nyerere na Kaunda hawatendewi haki na Africa kwa kuwalinganisha na kina Mandela

Wahenga Kama kina Robert Mugabe wanajua role ya Kambarage kuliko sisi wa Tz!
 
halafu akija mtu km mudi analeta dharau na kejeli na kama watu wake wa vijiwe vya kahawa

Nadhani usiende huko utaharibu Uzi
Kama unamzungumzia Mohamed Said hata Yeye huwa Anakiri kuwa Mwl alikuwa na akili nzuri sana na Mjengaji Mzuri wa hoja, hoja yake ni kwny Mengine ambayo si sehemu ya Mjadala wetu
Kwa Mfano Mimi namkubali sana Mwl kwny Masuala ya Security, ujasusi, Uafrica, Uzalendo , kutojilimbukizia Mali n.k lakin kwny Uchumi wake wa Kijamaa simkubali japo Wapo wanaomkubali kwny Uchumi wa Kijamaa ni tofauti ya kutafakari jambo Moja kwa perspective tofauti
 
Back
Top Bottom