Mbona Hassy Kitine hakualikwa/hakuhudhuria?

Mbona Hassy Kitine hakualikwa/hakuhudhuria?

M
Emilio Mzena ambaye nae aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS bado yupo hai? Sijamsikia siku nyingi? Huyu ndio aliyeratibu kumtorosha Mwalimu Nyerere na Kawawa Ikulu na kwenda kuwaficha Kigamboni mwaka 1964 wakati Jeshi lilipoasi.

Kwa mchango wake mkubwa ndani ya Idara, Hospitali ya wanakitengo pale Makumbusho imepewa jina lake.
Mzee Mzena alishafariki, sikumbuki vizuri mwaka ila ni miaka hii ya 2000's
 
Ni Long story Ndugu yangu lakin kwa ufupi baada ya jaribio la Mapinduzi kushindwa 1983 Baadhi ya Watuhumiwa walitoroshwa Gerezani Ukonga na kupelekwa Kenya Kupitia Mpaka wa Horohoro na lilitumika Gari la Kubebea Mkaa kuwabeba kina Kapten Maganga

Mwl Baada ya kugundua Mpango huo ndipo akatengeneza Revenge

Baada ya Arap Moi kutikiswa ikabidi wafanye Mazungumzo na Mwl Nyerere na wakakubaliana wabadilishane Wale Wahaini ndipo kina Maganga wakadanganywa na Utawala wa Kenya kuwa wanawapeleka kuwaficha Ethiopia kwa kuwa kuna Vijana wa Nyerere Wapo mitaa ya Nairobi wanaweza kuwadaka Kumbe ni Mpango wa kwenda kuwakabidhi Dodoma si Dsm
Nyerere nae aka swap kwa kukabidhi Wahaini feki kwa Moi wakat huo tayari kina Odinga ( Wahaini halisi ) wameenda kufichwa Canada Kama wakimbiziwa Kisiasa kishawasafirisha, Moi baada ya kugundua alipoteza kabisa Interest na Tanzania na Mwl kabisa kwa kuingizwa Chaka

Tanzania haitokuja kupata Rais Mwenye akili Nyingi sana Kama Julius Kambarage Nyerere never never!
Kwani huyu wa sasa hafanani na Nyerere? Mbona naona ana AKILI sana?

-Domhome-
 
Kitenge mbona hawamdhibiti asee. Siku ile alitaka kudhalilisha taaluma. Mchana peupe
 
Mkuu, heshima Kwako...
Nilisoma Habari hizi za uhaini 1983 nikiwa std 7 nazikumbuka kidogo sana na hasa huyuTamim(rip)....tena hii ilitokea mwaka mmoja baada ya1982 ndege ya ATC, kutekwa na kupelekwa hadi London, Uingereza na kufanikiwa kurudishwa na Rubani DEO MAZULA..

Mkuu,
Tungumbushe kidogo Habari za Uhaini ule....

-Domhome-
Kuna mengi sana yalio jiri kwa mujibu wa maandiko mbalimbali, lakini kwa leo naomba nianzie kwanye HUKUMU YA WALIOTAKA KUMUUA NYERERE 1983

Walioshitakiwa kwa uhaini mwaka 1983 walikuwa wengi.
Ilielezwa mbele ya jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Nassor Mzavas kwamba washitakiwa walikuwa 19.
Miongoni mwao alikuwepo Thomas Lugangira au ‘Uncle Tom’ au ‘Uncle Check bob.’

Wenzake walikuwa ni Hatibu Gandi au ‘Hatty Mac Ghee’, Kapteni Mohammed Tamim, Kapteni Mbogoro, Kapteni Christopher Kadege, Luteni Badru Rwechungura Kajaja na Kapteni Mapunda.

Wengine walikuwa ni Banyikwa na mkewe, Christopher Ngaiza, Zacharia Hans Pope , Kapteni Rodrick Rosham Robert na wengine kibao ambao jumla yao walikuwa 19.

Wakati kesi inaendelea Lugangira na Hatty Mc Ghee walipanga njama na kufanikiwa kutoroka kutoka katika Gereza la Keko, Dar.
Ilidaiwa kuwa walitorokea nchini Kenya. Baada ya kufika Kenya, Lugangira akatorokea Uingereza. Hatty Mc Ghee alikamatwa na kurudishwa Tanzania kwa kubadilishana na mtu mmoja aliyekuwa akitakiwa Kenya aliyetajwa kwa jina la Private Hezekiah Ochuka ilidaiwa kuwa alifanya ‘madudu’ huko Kenya.

Mc Ghee aliporejeshwa nchini aliunganishwa na wenzake na kesi ikapamba moto.
Komandoo Tamim aliuawa wakati wa kurupushani za kumkamata pale Kinondoni Mkwajuni.

Lakini hata mahakamani wakati wa kutoa ushahidi juu ya komandoo huyo mwana usalama mmoja aliyekuwa akiitwa Mr X alisema walijaribu kumkamata lakini akawatoroka kwa kuruka ukuta wa nyumba aliyokuwa akiishi.

Akasema wakati wakimkimbiza Komandoo Tamim alidandia gari moja pick up iliyokuwa imebeba masanduku ya bia na kuanza kuwarushia wana usalama waliokuwa wakimkimbiza, hivyo akapigwa risasi na kufa.

Kesi hiyo ya uhaini ilikuwa inasisimua sana haswa maswali ya wakili wa utetezi aliyekuwa akiitwa Murtaza Lakha. Mawakili wengine wa utetezi ninaowakumbuka kwa jina moja moja ni Mucadam, Jadeja na Tarimo.
Upande wa serikali ulikuwa unaongozwa na Wakili William Sekule, pia alikuwepo Johnson Mwanyika.

Wakili Sekule alileta mashahidi kadhaa ambao walisumbuliwa sana na mawakili wa utetezi haswa Murtaza Lakha.
Jaji Mnzavas alitoa hukumu Desemba 28, 1985 ambapo washitakiwa wengine aliwafunga kifungo cha maisha na wengine walifungwa miaka kadhaa lakini Banyikwa na Ngaiza waliachiwa huru.
 
Alipofuatwa na kuulizwa na waandishi wa habari kama tayari wamesha mpandisha cheo askari yule kama rais alivyo agiza, aliyekua mkuu wa jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu alisema jeshi la Polisi lina utaratibu wake wa kupandisha askari wake vyeo, na moja wapo anapaswa aombe kwenda kusomea hiyo ngazi ya cheo na maombi yake yatapitiwa kama ana kidhi vigezo.
Hapa ndipo safari ya Mangu kuelekea chumba cha magazeti ilipoanzia!
 
Kuna vitu mnashindwa kuelewa! Kama watanzania walienda Israel kama wamalawi (mfano) na kutokea malawi, nani ataanza kuhangaika nao kujua kama ni wamalawi au sio!!

Tuwasamehe Vijana wetu!

Miaka ya Baadae wakiambiwa kwa Miaka kadhaa Meli za Iran zilikuwa zinapeperusha Bendera ya Tz ( bila ya Serikal ya Tz kujua) kukwepa Vikwazo vya kiuchumi mpaka ilipokuja kubumburuka Miaka ya hivi karibuni watabisha kuwa Hilo halikuwahi tokea
 
Back
Top Bottom