singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,850
- 9,749
SIMULIZI HII NI YA KUTUNGA HAIUSIANI NA MTU YOYOTE WALA KIKUNDI CHOCHOTE , MAENEO , OFISI NA MAJINA YALIONDANI YA HII SIMULIZI NI YA KUBUNI
ENJOYSURA YA 01
Ilikuwa ni siku iliokuwa ikisubiriwa na kila mmoja ndani ya Taifa la Tanzania , kila mwananchi alionekana kufurahia lile jambo ambalo linakwenda kutokea muda mfupi ujao , nchi nzima ilionekana kuwa katika hali ya shangwe , huku kila mwananchi mmoja mmoja alikuwa akionesha kutoa maoni ya kufurahia jambo kubwa lililokuwa likienda kukamilika muda mfupi ujao.Lakini licha ya wengi wa wananchi wa taifa hili kuwa katika hali ya shangwe na furaha , upande mwingine hali ilikuwa mbaya na hii yote ilitokana na watu hao waliokuwa katika upande mwingine kutokuamini kile kilichotokea , hawakuamini kabisa.
Naam ilikuwa ni siku ya kuapishwa kwa raisi Awadhi Abdukarim Jembe raisi wa awamu ya kumi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na hii yote ni baada ya bwana Jembe kushinda kwa kishindo na kuweka historia ya chama pinzani kuchukua madaraka ndani ya Taifa la Tanzania huku chama Tawala na mgombea wake kushindwa vibaya sana , jambo ambalo liliushangaza ulimwengu , kwani hakuna alieamini kama kuna siku chama tawala ndani ya taifa hili kinaweza kuondolewa madarakani baada ya miongo yote hio ya kutawala taifa la Tanzania kwa kushinda kila chaguzi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini .
Mara baada ya raisi Jembe kumaliza kula kiapo uwanja wa Uhuru ulifurika kwa shangwe kubwa huku neno ‘Jembe ni jembe’ likiwa limetawala uwanja mzima , na yote hayo hayakuwa ndani ya uwanja huo tu bali kila kona ya Tanzania kwa wale waliokuwa wakifatilia kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya siku hio katika uwanja wa Uhuru walikuwa wakishangilia na kulitaja jina la Jembe ni Jembe.hakika bwana Jembe alikuwa akikubalika sana , jambo ambalo liliushangaza ulimwengu , kwani vyombo vingi vya habari Duniani kote vilikuwa vikionyesha yale yaliokuwa yakiendelea ndani ya taifa la Tanzania huku wakijaribu kuweka nakshi juu ya neno “Chama Pinzani cha weka rekodi ya kuchukua madaraka ya nchi baada ya kukishinda chama Tawala “,lakini pia kitendo cha Raisi wa China kuhudhuria uapisho huo ilikuwa ni historia nyingine .
Basi taratibu zote za Raisi jembe kuapishwa ziliendelea huku akibadilishana madaraka na mtangulizi wake , viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla hio ya kushuhudia bwana Jembe akipewa madaraka walimpongeza kila mtu kwa nafasi yake , huku wengi wao wakiahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia maendeleo ambayo wananchi wanatamani kuyaona chini ya utawala wa raisi Jembe.
Hata kwa raisi Jembe mwenyewe alikuwa na shauku kubwa ya kuwaongoza watanzania hususani katika kipindi hicho ambacho matukio ya kiuhalifu yalizidi kuongezeka ndani ya taifa la Tanzania, kwani ni wananchi wengi walikuwa na hofu na kile kinacho endelea ndani ya Taifa , kwani mtaani kulikithiri matukio mengi ya kikatili yaliokuwa yakifanyika huku serikali ikishindwa kutoa maelezo ya kueleweka kwa wananchi juu ya matukio hayo .
Na hio ikawa sababu kubwa kwa chama pinzani kuwashinda wagombea wa chama tawala kwa kishindo kikubwa , na hio yote ilitokana na wananchi kuchoshwa na hali ya hatari iliokuwa ikiendelea ndani ya Taifa la Tanzania .
Raisi jembe mwenyewe hakutegemea kama angeweza kushinda katika uchaguzi huo ,kwani alijua mambo ambayo yalikuwa yakifanywa na chama tawala katika kila uchaguzi , mambo ya kuiba kura za wananchi , lakini katika uchaguzi huu jambo hili lilimshangaza sana ,lakini pia lilimfurahisha sana , kwani lilijenga picha kamili kwenye kichwa chake kwamba wananchi wa Tanzania kwa awamu hio wameamua kuona mabadiliko yanatokea ndani ya nchi kupitia sanduku la kura.
Basi baada ya shughuli za uapisho kukamilika hatimae viongozi mbalimbali waalikwa walianza kuondoka ndani ya uwanja huo huku gari ya kwanza kuondoka ndani ya uwanja wa Uhuru ilikuwa ni gari iliombeba Raisi Jembe akiwa na msafara wa gari saba , gari ambazo zilikuwa zimejaa wanausalama kutoka kitengo cha usalama wa Taifa wa Tanzania na wale pia waliokuwa ndani ya Ikulu. .
Raisi mteule Jembe alikuwa kwenye wasiwasi mno , licha ya kuapishwa kuwa raisi lakini alionekana kuna jambo lililokuwa likimsumbua kichwa chake .
“Jiandae kuingia Ikulu muheshimiwa Jembe “ ni neno ambalo lilikuwa likijirudia mara kwa mara ndani ya kichwa chake , neno hili alipata kulisikia siku chache kabla ya siku mbili kuingia kwenye zoezi la kupiga kura , wakati akiwa anaingia nyumbani kwake akitokea kwenye hitimisho la kampeni iliofanyikia ndani ya viunga vya jiji la Dar es salaam katika kiwanja cha Tanganyika park Kawe.
Siku hio wakati anaingia nyumbani kwake Kigamboni ndipo alipoweza kupigiwa simu na mtu asiemfahamu na kumwambia hayo maneno ya kwamba ajiandae kuingia ikulu , mtu huyu hakuweza kujitambulisha kwake , kwani mara baada ya kuongea maneno hayo simu iliweza kukatwa hapo hapo na alijaribu kuipigia namba hio , lakini alijjikuta akishindwa kwani namba hio ilikuwa ni private.
Hata matokeo yalipotangazwa na kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mkubwa alijikuta akishangaa sana , lakini pia na kupatwa na hofu kubwa , jambo kubwa lililompa hofu licha ya kushinda kihalali ni juu ya mtu huyo aliempigia simu na kumwambia kwamba ajiandae kwenda Ikulu , aliamini kama mtu huyo alikuwa na nguvu ya kuutabiri uchaguzi na kweli yeye kushinda basi mtu huyo hakuwa peke yake , huenda ni kikundi cha watu ambacho kilikuwa kikifanya kazi nchini ambacho kilikuwa na malengo ambayo hakuyajua yeye na chenye nguvu sana , na aliogopa maelengo ya kikundi hicho yanaweza kuwa hatarishi kwa taifa lakini pia kukinzana na mtazamo wake juu ya maendeleo ambayo anatamani kuyaona yakitokea chini ya utawala wake .
Msafara uliokuwa umembeba raisi Jembe uliingia ndani ya barabara ya Nelsoni Mandela na kukunja kushoto na kuingia ndani ya barabara ya kilwa , wakati wa huu msafara unaendelea kusonga kwa mwendo wa taratibu sana huku Raisi akiwa amesimama kwenye gari maalumu akiwapungia wananchi waliosimama kando ya barabara,Upande mwingine mita miamoja ndani ya jengo la nyumba ya makazi (Apartment) lililokuwa likifahamika kwa jina la Sokoine House nyumba namba sabini na nane gorofa ya tano alionekana kijana mmoja alievalia kofia nyeusi ya kampuni ya Nike , akiwa na mavazi meusi kabisa huku mkononi akiwa amevalia gluvusi (Gloves) lakini kubwa Zaidi bwana huyu alionekana kushika mtutu(Sniper riffle gun 5 SAKO TRG 42 kutoka Finland) akiwa ameuelekezea barabarani huku sikioni akionekana kuvaa visikilizishi (Earpieces) vya rangi nyeusi vyenye mkanda ulioelekea shingoni vinavyofanana kabisa na vile wanavyovaa wanausalama , bwana huyu kwanza muonekano wake ulionesha kabisa sio mzawa wa Taifa la Tanzania na hii yote ni kutokana na Rangi yake nyeupe na nywele zake.
Haikueleweka moja kwa moja ni kwa namna gani bwana huyu aliingia ndani ya jengo hilo na kuweka makazi yake hapo akiwa na mtutu akiulekezea barabarani kwani njia hio ilikuwa imekaguliwa na wanausalama , kwani ndio njia ambayo ilikusudiwa kwa raisi mteule Jembe kupitia mara baada ya uapisho akiwa anaelekea Ikulu magogoni .
Zilikuwa ni dakika kadhaa wananchi walio jipanga katika barabara ya Sokoine kushangilia na kumfanya bwana huyu alieshikilia mtutu kuongeza umakini kuelekea barabarani , na umakini wake ulimfanya kutabasamu na hilo ni mara baada ya kuona kile alichokuwa akikisubiria.
“Target is at 12 O`clock and clear Need permission”(Mhusika yuko kwenye shabaha mbele yangu naomba ruhusa “) Bwana huyu alionekana kuongea maneno hayo na hii ni mara baada ya kumuwekea shabaha raisi mteule yaani Mheshimiwa Jembe ambaye alionekana kutokuwa na habari na kinachoendelea upande wa pili , kwani sura ya furaha iliokuwa imeupamba uso wake iliwafanya wananchi wazidi kushangilia .
“I need permission”.(Nataka ruhusa )
“Umeruhusiwa “Ilisikika sauti nzito upande wa pili na baada ya bwana huyu kupata ruhusa aliseti vizuri kioo chake cha lenzi na kisha alivuta triga akimlenga raisi jembe , alionekana kuwa makini kweli na mbobezi katika kazi yake , kwani alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa na kile alichokuwa akikifanya .
Kilichosikika ni mlio uliokatika hali ya utulivu kabisa na hio ni mara baada ya bwana huyu kuachia Triga na kuruhusu risasi iliokuwa katika shabaha , huku akiamini risasi hio isingemkosa bwana jembo kwa namna yoyote ile .
Kitendo cha kumaliza kuachia risasi hio hapo hapo alijikuta akipigwa na kitu kizito kwenye shingo na kudondokea pembeni kwenye mlango wa kwenda jikoni huku akijihisi maumivu makali mno , lakini licha ya maumivu hayo hakutaka kuzubaa kwani pale pale alinyanyuka kwa kasi na kusimama na hapo ndipo alipo jikuta akishangaa kwani mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni mwanamke tena akiwa katika hali ya urembo kabisa , jambo lililomfanya bwana huyo aangalie mara moja bunduki lake lililodondokea pembeni ikifuka moshi kama mtu aliekuwa akihakikisha kwamba risasi ilitoka vyema kwenye bunduki hilo na kisha kumwangalia mwanadada huyu huku akijipanga kimapigano .
Lakini katika hali ya kushangaa alijjikuta akifikiwa na mwanadada huyo na mapigo ya haraka sana staili ya Krav Maga , roundhouse kick iliompata kisawa sawa na ile anajiweka vizuri kupangua pigo la pili alijikuta akishindwa kwani mwanadada huyu alievalia suti nyeusi alionekana kujua anachokifanya kwani ndani ya sekunde tano tu bwana huyo alikuwa amedhibitiwa vyema .
*****
SIKU TATU NYUMA KABLA YA UAPISHO
Licha ya kwamba chama tawala kilishindwa uchaguzi , lakini hakikiwa katika hali ya kukata tamaa kabisa ya kuachia nchi kwenda chama pinzani, kitendo cha wao kushindwa katika boksi la kura ilikuwa ni jambo baya sana kwao kuruhusu kutokea , hawakuelewa mara moja ni nini kilitokea mpaka swala la wao kishindwa likatokea , kwani kila kiongozi aliekuwa amewekwa kwa ajili ya kusimamia kura , walikuwa ni mtu wao , lakini bado walikuwa wameshindwa , jithada zote walizofanya katika kuhakikisha kwamba wanashinda uchaguzi huo licha ya kujua mwaka huo uungwaji mkono wao na wananchi ulikuwa mdogo sana lakini waliamini kwa kutumia nguvu yao kama serikali basi kusingekuwa na shida ,, lakini jambo la kushangaza ni pale walivyoona anaetangaza matokeo kwenda kinyume na matakwa yao na kumtangaza mheshimiwa Jumbe kuwa raisi mteule , jambo hilo kwa kila mwanachama kuanzia kwenye jeshi , viongozi na usalama wa Taifa kwa ujumla walifedheheshwa na jambo hilo kwa ujumla , hakuna aliekuwa akiamini kwamba jambo hilo limetokea la chama tawala kukosa kura za kushinda na kuwapeleka ikulu na kuendelea kuingoza nchi kama ilivyokuwa kawaida kwa miongo yote tokea kwa kuanzishwa kwa vyama vingi .
Hali sasa ilikuwa hali kwao , kwani waliamini yale maslahi yao waliokuwa wamejiwekea ndani ya serikali wanakwenda kuyakosa kama tu hawatafanya kitu kuokoa hali hio iliowakumba.
Viongozi wakubwa wote wa chama akiwemo raisi anaekwenda kuachia madaraka bwaba Mathayo kilubwa , mkuu wa majeshi ya nchi ambae na yeye alikuwa ni mwanachama kindakindani wa chama tawala , mkuu wa usalama wa taifa , na baadhi ya maraisi wastaafu walionekana kuwa katika meza ndani ya jengo la usalama wa Taifa Osterbay jijini Dar es salaam .
“Hatuwezi kuruhusu Jembe kuapishwa kwa namna yoyote ile “ Aliongea raisi anaekwenda kuachia madaraka au alieyamaliza muda wake huku akionekana kumaanisha kile anachokiongea kwa haiba ya sura yake
“Kila mtu ni tamanio lake hilo muheshimiwa , hatuwezi kuruhusu hilo litokee , na nadhani siku ya leo baada ya kikao hiki kumalizika tutakuwa na muafaka juu ya hili , sisi wote tulio hapa ni viongozii wakubwa wa nchi hii , naweza kusema kwamba sisi ndio serikali yenyewe hatuwezi kukosa muafaka” Alizungumza Nassoro kinga mkuu wa usalama wa Taifa.
“Naunga mkono hoja , Nadhani ni swala la sisi kuangalia ni namna gani tunaweza kulifanikisha hili…”Aliongezea mkuu wa majeshi ,Lakini wakati akiendelea kuongea mara mlango ulifunguliwa na aliingia mwanadada mmoja aliekuwa amevalia suti afahamikae kwa jina la Lucy , huyu alikuwa ni moja ya Special agent aliekuwa akimlinda raisi .
Basi baada ya Lucy kuingia alimsogelea moja kwa moja mheshimiwa Mathayo raisi anaemaliza muda wake madarakani na kisha alimwambia jambo kwa namna ya chini kabisa , na kumfanya bwana huyu kutabasamu na kisha alimruhusu Lucy kuondoka lakini pia aliongea na kumpa maelekezo mengine , na ilichukuwa takribani dakika moja tu alionekana mwanaume mwingine wa kizungu kuingia ndani ya ofisi hio iliokuwa ikifanyika kikao .
Bwana huyu alikuwa mzee kiasi makadirio ya umri wake si chini ya miaka sitini , akiwa na mwili wenye afya , alikuwa amevalia suti ya rangi ya bahari(bluu ambayo haijakolea ) , shati jeupe na tai ya kahawia huku nywele zake zilizoacha nafasi ya uwararaza zikiwa zimechanwa vyema alionekana ni wale wazee wanaojipenda sana kwa muonekano wake. . “Karibu sana mheshimiwa Kent nilifikiri utachelewa kufika “Aliongea raisi Mathayo akimkaribisha bwana Kent .
“Nisingeweza kuchelewa kutokana na jambo hili kugusa moja kwa moja Umoja wetu , na naweza kusema ni jambo ambalo linauhusu umoja kwa asilimia mia moja , kwa hio nadhani na mimi ni sahihi kabisa kuwepo mahali hapa kuliongelea “.
Baada ya makaribisho mheshimiwa raisi Mathayo aliitoa kwa ufupi kile walichokuwa wakieongelea katika kikao hicho na kisha baada ya kumaliza alimkaribisha bwana Kent kwa mchango wake .
“Nimekuja hapa nikiwa na madaraka kamili kutoka U-97, na maagizo niliopewa ni kuhakikisha Jembe anakufa kabla ya kuapishwa “Aliongea Kent na kufanya hali ya chumba hiko kuwa kimya kila mtu akitafakari jambo alilokuwa akiongea kwa kina .
“Inawezekana vipi , kwani mpaka sasa Jembe hajulikani alipo , mimi nadhani kwa sasa atakuwa amechuku a Tahadhari za kutosha mara baada ya kutangazwa kuwa Raisi hivyo itakuwa ngumu kwa sasa kumpata “
“ Ni kweli mpaka sasa hatujui Jembe alipo , mimi nadhani tusubiri siku ya kuapishwa kwake” “Lakini hili lazima lifanyike kabla ya yeye kuapishwa , kwani kama atapishwa kuwa Raisi hata tumuue haitokuwa na maana kwani mtu atakae mrithi atakuwa ni makamu wake kikatiba, hivyo tutakuwa tumefeli”Aliongea raisi .
“Umoja ulikuwa na tahadhari na kila kilichokuwa kikiendelea nchini , kwani umoja ulitambua hali ya kushinda kwenye boksi la kura ilikuwa ni nusu kwa nusu , hivyo tulichukuwa tahadhari mapema”Aliongea Kent
“Tahadhari gani hizo wakubwa wamezichukua?”
“Mgombea mwenza wa Jembe ni mfuasi wetu “.Aliongea Kent na kuwafanya watu waliokuwa ndani ya chumba hiko kupigwa na mshangao .
“Kwa muda gani alikuwa moja ya wanachama wa U-97?”
“Miaka kumi “Alijibu Kent na kuwafanya kila mtu hapo ndani ashangae .
“Hivyo misheni yetu ni kumuua Jembe , jembe akishaondoka duniani basi naamini hakuna mtu hata mmoja hapa ndani atapaswa kuwa na wasiwasi , kwani sisi wote ni wanachama na wanachama tunalindana kimaslahi “Aliongea Kent na kuwafanya kila mtu hapo ndani apumue . “Basi mpaka hapo naona jambo rahisi la kutimiza azima yetu ni siku ambayo Jembe atakuwa ashaapishwa litakuwa jambo jepesi sana kukamilisha misheni hio , kwani wanausalama wetu ndio watakuwa wanamlinda “Aliongea Kinga na kila mtu aliunga mkono hoja yake .
Walikubaliana siku ya kuapishwa kwa Jembe kabla ya kufika Ikulu basi awe ni mfu , lakini licha ya kupanga jambo hilo walitafakari nini ataenda kutimiza azma hio ya kumuua Raisi mteule Jembe, na wanajumuia hao waliokuwa na mipango yao inayokiuka katiba ya Jamhuri walimgeukia tena Kent kuona ni mtu gani anaweza kumuua raisi mteule Jembe.
“Mtu wa kukamilisha zoezi hilo tayari yupo “Aliongea bwana Kent na kisha alitoa simu yake na kumpatia Kinga na kisha alianza kusoma taarifa ya mtu ambae ndie atakaekwenda kukamilisha jambo hilo .
Peskorov Sunik special agent kutoka kitengo cha walenga shabaha kutoka nchini Ukraine ndie mtu ambae alitakiwa kukamilisha jambo hilo .
Kinga aliridhika na sifa za bwana Peskorov na kuwaangalia wenzake wote hapo ndani , na kuwaashiria kuwa jambo hilo ni jema likafanywa na bwana Peskorov .
“Mnachotakiwa ni kuhakikisha siku ya uapisho kila kitu kinakuwa chini ya TISS , kwanzia ukaguzi wa usalama na kila kitu , ili kumuwezesha bwana Peskorov kufanya kazi yake kiufanisi “Aliongea Kent na Mkuu wa majeshi na wengine wote walikubaliana .
SURA YA 02
Swala la kumruhusu Peskorov kufanya mauaji ya Raisi mteule Jembe lilikuwa limefanikiwa kwa asilimia mia moja ,kwani alipatiwa chumba mahususi kabisa ndani ya jengo la Sokoine , kwa ajili ya kukamilisha mauaji hayo, huku waliokuwa wakiratibu shughuli nzima ya mauaji hayo ni wakuu kabisa wa usalama wa Taifa la Tanzania , yaani kuanzia kwa mkuu wa majeshi, mkuu wa usalama wa Taifa na viongozi wengine waandamizi wa maswala ya kiusalama wa Nchi.
Hata pale bwana Peskorov alipo omba ruhusa ya kuruhusu risasi baada ya kumuweka raisi Jembe kwenye shabaha , alietoa ruhusa hio alikuwa ni mkuu wa majeshi akiwakilishwa na msaidizi wake , kwani yeye kwa wakati huo alikuwa uwanjani kwa ajili ya kuhakikisha shughuli za uapisho zikienda vyema kabisa .
Lakini wakati mpango huo ukiendelea upande mwingine alionekana mwanadada mrembo sana akiwa anapita mbele kabisa ya jengo la mtaa wa Nyerere square , Mwanadada huyu aliekuwa amevalia suti yake nyeusi , alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa , hata pale alipokuwa akikaribia kutoka kabisa nje ya barabara ya mwendo kasi , hakuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi , mwanadada huyu alitembea kwa haraka kabisa mpaka kufika ndani ya jengo la Sokoine House na baada ya kufika katika lango la kuingilia , alisimamishwa na wanaume wawili ambao walikuwa wamevalia kiraia , baada ya mwanadada huyu kusimamishwa , alijjikuta akigeuza shingo yake kama mtu ambae alikuwa akikagua uwepo wa watu ndani ya eneo hilo , na ile baada ya kuridhishwa kwa kuona kwamba eneo hilo hakukuwa na watu wengi , aliwaangalia wale mabwana na kisha alitoa kitambulisho na kuwakabidhi , na kisha aliruhusiwa kuingia .
Baada ya kuingia ndani ya Lift alijigusa eneo la shingoni kama mtu anaejifinya na kisha alitamka maneno kadhaa ambayo hayakusikika , na wakati huo ndipo lift ile ilifunguka , lakini ni kama alikuwa anasubiriwa kwani ile lift inafunguka wanaume wawili waliovalia mavazi ya kiraia walionekana kusimama katika korido iliokuwa ikitenganisha nyumba ya namba 77 na 79 watu hawa ni kama walikuwa wakimsubiria katika eneo hilo , kwani kitendo cha yeye kutokea tu walimnyooshea bastora .
“Nyoosha mikono yako juu ,ukileta ubishi hii itakuhusu “Aliongea mwanaume huuyo mmoja kati ya wale wawili kwa sauti nzito kabisa ambayo haikuwa na mzaha , lakini licha ya hayo mwanadada yule mrembo hakuonesha hata sura ya wasiwasi Zaidi ya kufanya kile alichokuwa ameambiwa , lakini wakati wote huo alionekana kupanga yake kichwani , kwani alimwangalia yule mwanaume wa pili yake ambaye alionekana kuwa bize kumkagua na jambo hilo lilimfanya kufurahia moyoni.
Ilikuwa ni kitendo cha kushitukiza tu cha mwanadada huyu kupiga bastora ya mwanume aliekuwa amemlenga na kwenda pembeni , na hii ni baada ya mwanaume huyu kumwangalia mwenzake wakati wa kumsachi na hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa sana kwake , kwani mwadada huyu kwa ustadi wa hali ya juu kabisa alitumia nafasi hio na kisha aliipangua ile bastora na kudondokea mbali , lakini hakuishia hapo tu kwani alikuwa tayari ashaachia pigo lililomyumbisha mwanaume yule aliekuwa akimkagua na kumtegua taya , lakini kwa wakati mmoja akijiandaa kupambana na mwanume ambaye alikuwa amepiga kerebu na bastora kwenda pembeni .
Jambo lililomfurahisha mwanadada huyu ni pale alipoona adui yake hakuwa na mafunzo ya kimapigano kama alivyokuwa ametegemea na aligundua adui yake siraha yake kubwa ilikuwa ni ile bastora kwani baada ya kudondoka pembeni aliikimbilia pasipo kuchukua tahadhari na hilo ndilo lilimfanya mwanadada huyu ampige teke la shingo na kumzimisha kabisa na baada ya kuona zoezi lake lilimalizika alimgeukia yule mwingine ambae alikuwa akihaha na kisha na yeye alimpiga shingoni na kuzima huku akiacha mdomo wazi kwani alikuuwa ameteguliwa taya lake.
Kitendo cha kufungua mlango wa nyumba na sabini na nane ndipo alipoweza kumshuhudia mwanume wa kizungu akiwa amelenga shabaha kuelekea barabarani , lakini ni kama alichelewa kwani ile anamfikia tayari mwanaume yule alikuwa alisharuhusu risasi kutoka katika bunduki lake hilo refu la kudungulia .
“Mhalifu yuko chini” Alitamka mwanadada huyu kwa sauti ya kikamavu .
“ Vizuri sana ajenti Linda , hakikisha unatoweka kwenye eneo kabla ya wanausalama kufika hapo “
“Copied” Umeeleweka “
Mwanadada yule mara baada ya kumaliza kazi yake aliacha alama ya utambulisho katika paji la uso la bwana Peskorov na kisha akatoweka ndani ya eneo hilo huku mdunguaji akiwa hajitambui .
Huku upande wa nje baada ya bwana Peskorov kuachia Risasi ile moja kwa moja ilimpiga Raisi Jembe kifuani na akadodoka chini , huku taharuki ndani ya eneo hilo ikizuka , wanausalama waliokuwa wakitoa ulinzi walijikuta wakianza kuimarisha ulinzi wa eneo hilo huku wengine wakitawanyika kufuatia upande ambao waliamini ndiko Risasi ilitokea .
Dakika chache gari ilioonekana kumbeba mheshimiwa ilitoka ndani ya eneo hilo kwa haraka sana ikielekea upande wa hospitali ya Muhimbili .
Hakuna alieweza kuamini jambo kama hilo lingeweza kutokea , sio wananchi sio wanausalama waliokuwa wakitoa ulinzi.
Dakika chache mbele baada ya Raisi Jembe kuwahishwa hospitalini , hatimae bwana peskorov alitolewa kwenye jengo hilo la Sokoine na wakati huo akiwa anajitambua , lakini akiwa chini ya ulinzi wa wanausalama wa Taifa.
Vyombo mbalimbali vilianza kutangaza habari ya raisi Jembe kupigwa risasi akiwa njiani kuelekea ikulu mara baada ya kuapishwa , Jambo hilo lilikuwa ni jambo ambalo halijawahi kutegemewa kutokea ndani ya Taifa la Tanzania , kila mwanahabari aliongea lake , huku sintofahamu ikiendelea kuibuka juu ya hali ya mheshimiwa.
****
BAADA YA MASAA MAWILI
Baada ya masaa mawili ya kutokea kwa tukio la kushitusha sana ndani ya Taifa la Tanzania katika lango la kuingilia ndani ya hospitali ya taifa ya Muhimbili zilionekana gari nne aina ya V8 zikiingia hospitalini hapo na kwenda kwenye maegesho ya muda mfupi pembeni kabisa ya jingo la magonjwa ya moyo .
Baada ya gari hizi kusimama walionekana watu watatu wakiwa wameingia ndani ya hospitali hio , mtu wa kwanza kabisa kuonekana alikuwa ni mkuu wa majeshi bwana Nduli Semongo , mtu wa pili alikuwa ni raisi mstaafu alieachia madaraka masaa mawili yaliopita bwana Mathayo Kilubwa , mtu wa tatu alikuwa ni Nassoro Kinga huyu akiuwa ni mkuu wa usalama wa
Taifa .
Mara baada ya watu hawa kwa jumla yao waliongozana na wanausalama wengine na kuelekea ofisi za mganga mkuu wa Hospitali hio na mara baada ya kukaribishwa na mganga mkuu afahamikae kwa jina la Magreth Singano , walienda moja kwa moja katika kutaka kujua hali aliokuwa nayo mheshimiwa Jembe , lakini jibu lililotoka kwa mwanamama huyu mwenye umri usiopungua miaka arobaini liliwaacha hoi na katika tafakuri nzito.
“Raisi jembe licha ya mimi kusikia Taaifa zake , sikuweza kumpkea hospitali hii mpaka wakati huu “
“Unamaanisha Raisi Jembe hakueletwa hapa”
“Ndio muheshimiwa , mimi ndio mganga mkuu hapa na taarifa ya mgonjwa mwenye mamlaka makubwa kama hayo akifika hapa lazima nijulishwe kuandaa utaratibu wa kiulinzi na matibabu “Aliongea mwanamama huyu na kuwafanya wazee hawa ambao kila mmoja alioneesha umri kwenda , walionekana kusawajika nyuso zao mara baada ya jibu hilo , kila mtu alijiuliza swali linalofanana na mwenzake .
“Kama Jembe hakuletwa hapa , kapelekwa hospitali gani ?“ Hilo ndio swali la kwanza lililoibuka katika vichwa vya watu hawa , kwani ujio wao ndani ya hospitali hio ilikuwa ni kuja kuthibitisha kifo cha Jembe tu , ili wakitangaze rasmi , lakini kitendo cha kufika mahali hapo na kukuta taarifa ambazo zilikuwa nje ya mategemeo yao walishangaa na kupatwa na mshituko kwa wakati mmoja.
Waliamua kuondoka mara baada ya kupata taarifa hizo ,huku wakimwamrisha mganga huyo kutotoa kauli yoyote kuhusiana na kile kinacho endelea juu ya raisi mteule Jembe.
Taarifa ziliwafikiwa wakuu wa nchi ambao ndio waliandaa na kuidhinisha mpango mzima wa mauaji ya Jembe ,taairfa hizo ziliambatana na kikao cha dharula na hii ni baada ya msako kwa kila hospitali ya kujua mahali ambapo raisi mteule alikuwa akipatiwa matibabu au maiti yake ilipokuwepo , mpaka masaa mawili kupita ya msako huo hakukuwa na majawabu yaliokatika uhakika juu ya maswali mawili :
Swali la kwanza kwa wapangaji hawa wa tukio lilikuwa ni ‘Maiti ya jembe iko wapi’ na swali la pili ‘Ni nani alifanikisha kuificha maiti ya Jembe’.
Walikuwa wanayo kila sababu ya kujiuliza maswali hayo kwani waliamiani mpango wa ulikuwa umefanikiwa kwa asilimia mia moja , na jambo lililowafanya waamini hivyo ni kutokana na sehemu ambayo Risasi ilioruhusiwa na bwana Peskorov ilipompata raisi , kwani kwa kutumia mtaalamu wao wa ‘Anatomy’ Professa Shukuru Omari waliweza kujua kwamba risasi ile ililenga katika eneo la moyo na kwa mantiki hio ni kwamba asilimia za raisi Jembe kupona risasi hio ni asilimia moja tu .
Walifanya tafiti zote za kuhakikisha Risasi ile ilimpata Jembe , mpaka kupima vinasaba vya damu iliomwagika katika eneo alilodondokea Raisi jembe na vikathibitisha damu hio kuwa yake , kupitita CCTV kamera waliweza pia kuona Risasi hio ilimpata Raisi Jembe hivyo uhakika wao wa kwamba Raisi Jembe kusalimiana na Kuzimu ilikuwa ni asilimia tisini na tisa .
“Jamani mpaka sasa hatujui Maiti ya Raisi mteule Jembe iko wapi.Na wanausalama waliohusika katika kumpeleka Raisi jembe hospitalini pia hawaonekani walipo , jambo ambalo linatuacha katika maswali “ Aliongea Mheshimiwa Raisi Mstaafu bwana Mathayo Kilubwa.
“Nadhani kwa taairfa tulizonazo mpaka sasa zintupa maswali mawili ambayo yanawakilisha asiliama za ushindi kwa kile tulichopanga“Aliongea Nassoro .
“Naunga mkono hoja mpaka sasa Tuna asilimia moja tu ya kusema Raisi jembo yupo hai , nadhani maswali yetu yajikite kutafuta mwili wa Jembe ili akaiage ikulu kabla ya kwenda kusalimiana na kaburi “Aliongea Mkuu wa majeshi bwana Nduli .
“Ninaunga mkono hoja ya kila lililoongelewa katika kikao hichi , lakini bado swala la upotevu wa mwili wa Jembe ni swala ambalo tunatakiwa kulifikiria kwa kina na kujua ni wapi mwili wake ulipo na ni nani walihusika katika kuuchukua mwili hio , na ni kwa madhumuni gani“ Aliongea bwana |Kent na kufanya wenzake wote waliokuwepo hapo ndani kuunga mkono hoja.
“Lakini mpaka sasa ni Zaidi ya masaa manne hatujapata kujua ni wapi Raisi jembe alipo na wananchi wanataka kufahamu raisi wao alipo“.
“Mheshimiwa makamu nadhani kauli yako uirekebishe kidogo ni vizuri ukisema ni wapi maiti ya jembe Ipo wapi kuliko kusema ni wapi Jembe alipo“Aliongea Raisi akimrekebisha makamu wake ambaye pia alikuwa yupo ndani ya mpango huo , makamu huyu alikuwa akifahamika kwa jina la Anandumi Kiwia .
Masaa yalizidi kusonga , wanausalama waliokuwa wamepewa jukumu la kufatilia ni wapi maiti ya jembe ilipo mapaka wakati huo hawajapata mwanga, wananchi nao walitaka kujua ni nini kinaendelea juu ya raisi wao mpendwa Jembe , waandishi nao walikuwa na maswali ambayo hayakuwa yamepata majibu mpaka kwa wakati hio,kila taasisi ya habari ilitaka kujua na kuripoti ni hali gani aliokuwa nayo Jembe, walichoweza kujua ni taarifa za kwamba raisi mteule huyo alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili , jambo ambalo liliwafanya wananchi wengi waliokuwa na hasira kali juu ya kile kilichomtokea raisi wao kufurika katika hospitali hio huku kila mmoja akiwa na bango lake , wengine walikuwa wakimuombea raisi hiyo aweze kupona , wengine walikuwa wakihitaji muhusika wa shambulio hilo , hakukuwa na gari iliokuwa ikiingia wala kutoka ndani ya hospitali , hakuna kiongozi wa hospitali wala wa taifa aliejitokeza kuongea na waandishi , jambo ambalo liliibua taharuki ndani ya Taifa la Tanzania na nje ya Mipaka yake.
Upande wa jengo la umoja wa usalama wa Taifa viongozi wa juu wa taifa walionekana wakiwa katika sehemu zao kwa masaa kadhaa huku wakijadiliana juu ya maamuzi ya kuchukua , jambo kubwa liliowafanya kubaki hapo ni kutaka kupata ripoti ya ufatiliaji wa wapi alipokwepo Raisi jembe , baada ya kama nusu saa ya kusubiri hatimae taarifa ya kipelelezi iliowakilishwa na jasusi wa kimataifa bwana Bakari Nyuu au Mister white kama walivyojuwa wakipenda kumuita akiwa kazini , ripoti hio ilisomwa .
Ripoti hio ilikuwa ikieleza tukio zima mara baada ya mheshimiwa Jumbe kutolewa eneo la tukio na gari la wangonjwa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili THB 1011 gari ilnayomilikiwa na hospitali ya Muhimbili , Ripoti iliendelea na kusema gari hio ilionekana ikiptia baadhi ya maeneo , ambayo kamera ziliweza kuinasa , na katika ufuatiliaji hio waliweza kugundua kwamba gari hio iliingia ndani ya hospitali ya Muhimbili ikiwa na mgonjwa Mahututi aliekuwa akifahamika kwa jina la Semeni yahaya akiwa ametolewa hospitali ya Amana , akaendelea na kusoma kwa mpangilio wa ufatiliaji wa gari hio waliweza kukisia huenda kulikuwa na gari aina hio hio lenye namba za usajili hizo hizo ambazo ndio ziliweza kumbeba raisi Jembe .
Taairfa hio ilionekana kuwachosha tu waheshimiwa hao , kwani haikuwa na mwanga wowote huo hivyo mpaka kwa wakti huo waliona jambo la busara ni kufanya maamuzi .
Na maamuzi walioyaona yanafaa ni kutangaza kifo cha Raisi jembe na kuandaa utaratiubu wa kumuapisha makamu wa raisi wa jembe yaani mheshimiwa Madiru Seba kuwa Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,lakini licha ya kufanya maamuzi hayo walipanga kuchukua tahadhari zote juu ya asilimia moja ambayo walikuwa wakiamini kwamba huenda mheshimiwa Jembe angekuwa hai , hivyo mpango wa kiusalama ulikuwa ni kuhakikisha siku ya kumuapisha makamu wa Raisi bwana Madiru kuwa Raisi , walidhamiria kuhakikisha hakuna kitu chochote cha kuingilia zoezi hilo hata kama ingekuwa mzimu wa Jembe walidhamiria kuuzuia kutokuharibu uapisho huo .
Hivyo Muafaka ulikuwa ushaamuliwa na vyombo vya habari vilikuwa vishapewa taarifa ya kufika ndani ya ukumbi wa serikali kwa ajili ya kujua kile kilichokuwa kikiendelea . ambapo mkuu wamajeshi akiambatana na makamu wa wa Raisi ndio watu ambao walikusudiwa kutangaza .
Wakati watu hao wanajiandaa kwenda kutangaza kifo cha raisi mteule Jembe , wengine walibaki wakiendelea kujadiliana maswala mbali mbali ya kiuongozi katika taifa hilo huku kubwa Zaidi likiwa ni juu ya kuimarisha nguvu ya Umoja namba tisini na saba ndani ya Taifa la Tanzania .
Baada ya masaa mawili kupita , ndani ya ukumbi wa kitaifa unaomilikuwa na Serikali walionekana waandishi wengi wakiwa wamefurika ndani ya eneo hilo wakitaka kujua kile kinachoendelea juu ya sintofahamu juu ya shambulio la raisi mteule Jembe .
Havikuwa vyombo vya habari vya ndani ya nchi tu bali kulikuwa na vyombo vikubw Duniani ambvyo vyenyewe vilikuwa msitari wa mbele kutaka kuripoti kile kinacho endelea ndani ya Taifa la Tanzania , wananchi nao hawakua mbali n a Runinga zao ,kwani walikuwa wakifahamu fika mkutano wa waandishi wa habari huo unaokwenda kufanyika muda huo
Makamu wa Raisi , akiambatana na wakuu wa chama , pamojana mkuu wamajeshi , walikuwa mbele ya maiki zilizokuwa zimepangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu ili kunasa sauti .
Makamu wa raisi alianza kujitambulisha pia na kutoa pole kwa watanzania kwa hali inayo endelea nchini huku akitoa wito kwa watanzania kuwa watulivyo kwa kipindi hicho …. Wananchi waliokuwa wakifatilia matangazo hayo yaliokuwa yakirushwa moja kwa moja ni kama walimuona makamu huyo kuwachelewesha kwani walichokuwa wakitaka kwa wakati hio ni kujua jibu moja katika mawili yaliokuwa yakiwasumbua yaani raisi wao kuwa hai ama kafariki .
“Nasikitika kutangaza ki…..”Wakati akikaribia kutangaza alijikuta akishituliwa na mguso na kusita kutangaza na kisha akageuka nyuma na kukutanisha sura ya mkuu wa majeshi ambae ndie aliekuwa anamwangalia , jambo ambalo pia liliwashangaza waandishi wa habari pamoja na wote waliokuwa wakifatiliwa matangazo hayo .
Baada ya kugeuka nyumba mkuu wa majeshi alimkabidhi karatasi nyingine na kuchukua ile aliokuwa ameshikilia makamu wa raisi na kisha alimwambia anapaswa kutangaza kilicho andikwa humo . Kitendo kile kiliwachanganya sana waandihi na watu wengine waliokuwa wakishudia tukio hilo .
Baada ya makamu wa raisi kupewa karatasi ile alijikuta akipitia haraka haraka na kujikuta macho yakimtoka , lakini alijitahidi kuficha mshituko wake .
“Nasikitika kutangaza hali ya kiafya ya mheshimiwa Jembe sio nzuri sana na mpaka wasaa huu bado anaendelea na matibabu , kutokana na hali ya kiusalama nasita kutangaza hospitali ambayo anapatiwa matibabu kwani tukio la leo linaonekana sio la kawaida , na wahusika wote ambao wamehusika na shambulio hilo tunaendelea kufanya uchunguzi na tunawahakikishia wananchi watu waliohusika watapatikana na watafikishwa mbele ya sheria ,.hivyo wananchi tunaomba muwe na watulivu na tuzidi kumuombea raisi Jembe kupona haraka ili kuendelea na majukumu yake ya kuliongoza Taifa ”Yalikuwa ni maneno machache sana yaliokuwa kwenye karatasi hio tofauti na ile ya mwanzo ambayo ilionekana kuwa Zaidi ya kurasa mbili..
SURA YA 03
“Mpaka kufikia hatua hii ni dhahiri Damiani ushafanikiwa kumpata mwanangu na pia umefanikiwa kupata kidani , lakini pia umefanikwa kunisaidia kulipiza kisasi kwa walioimaliza familia yangu , lakini pia kuangalia vidio hii inamaanisha Bendera kafanikiwa kunizuia kutimiza malengo yangu hivyo misheni naweza kusema kwamba imefeli .Nina sikitika kukuambia kwamba mimi ndio mtu niliehusika kumuua mama yako Damiani na si mtu mwingine , na yote ililikuwa kwenye mpango wangu ambao nimeupa jina la mpango x .
mmi nipo hai ni mzima wa afya na sikufa kama dunia inavyo fahamu pamoja na wewe pia , mtu aliekufa siku ya tukio sio mimi bruno lamberk bali ni clone yangu .
Mimi bruno lamberk halisi sijawahi kuonana na wewe ana kwa ana zaidi ya kukupa maagizo ya kila hatua unayopita kwa msaada wa Nara .
Hivyo kutokana na kifo cha mama yako ambae mhusika mkuu ni mimi nakuomba msamaha , lakini pia natengua kauli yangu ya kukumilikisha mali zangu zote kwanzia sasa na mmiliki halali atakuwa ni mtoto wangu .
Mwisho mama yako hakufa bure ila kafa kwa ajli ya watanzania wote hivyo ahadI niliowekeana na bendera ni kukuambia siri ya MPANGO ZERO , na hii ni kama zawadi kwa Bendera baada ya kunishinda na kuzuia mpango wangu wa kuwaangamiza maadui tisini katika karatasi niliokupatia .
MPANGO ZERO ni mpango ambao unahistoria ndefu hivyo kuujua kwa undani mpango huu nenda kasome kitabu cha ‘BOOK OF ALL NAMES ‘.”
Huwa kila ninapoangalia hii video Napata uchungu mwingi , nashindwa hata kuelezea kile ninchojiskia nikiangalia video hii , kwani uchungu ninaoupata huwa ni mkali sana , na unaweza ukashangaa kwanini napenda kuangalia video hii mara kwa mara japo inanifanya kuwa na uchungu mwingi sana , jibu ni kwamba huwa nafanya hivi makusudi kabisa , maumivu ambayo niliyapata siku ya mama yangu kupoteza maisha na siku ambayo mwanamke ambae nilikuwa nimetokea kumpenda kufa mbele yangu ni jambo ambalo mtu aliezoea kuliona hili neno ‘maumivu’ pasipo kupata udhoefu wa maana halisi ya neno lenyewe hawezi kuelewa kile ninachomaanisha na naangalia video hii mara kwamara ili kutozisahau siku ambayo Bruno alinisababishia maumivu katika maisha yangu
Bruno Lamberk ni mtu ambae nilikuwa nikimfikiria usiku na mchana, ni Zaidi ya miaka kumi sasa sijawahi kulisahau jina hili , ni adui yangu namba moja duniani ambae nilikuwa nikiamini siku ambayo nitamtia mikononi mwangu sijui hata ni kipi nitakifanya ili kuridhika juu ya maumivu alionisababishia katika maisha yangu .
Katika miaka yangu yote kumi ya mafunzo ya kijasusi na kikomandoo jina moja ambalo lilikuwa likinifanya nipambane Zaidi ili kujiweka sawa ni juu ya huyu mtu anaefahakika kwa jina la Bruno Lamberk na umoja wake unaofahamika kwa jina la U-97.
Kila siku nilikuwa nikirudia rudia video hii mara kwa mara hii yote ni kutotaka kusahau hata mara moja uchungu niliokuwa nao moyoni , wanawake wangu wawili niliotokea kuwapenda ndani ya dunia hii kufa na msababishaji mkuu akiwa ni U-97 huku umoja huu ukiongozwa na Bruno , swala hili lilinifanya niweke kisasi ambacho niliamini kwa kukitimiza hiko ndani ya maisha yangu nitaweza kuishi huru japo si kama zamani .
Nipo nchini kwa miezi kadhaa tokea nitoke kwenye mafunzo yangu Cuba ambako nilikaa kwa miaka mitano nikisomea maswala ya kimapigano na kipelelezi baada ya kutokea nchini Urusi nikijiimarisha Zaidi katika maswala ya kimapigano , naweza kusema mpaka sasa mimi ni mtu hatari sana kutokea ndani ya taifa la Tanzania tokea kuanzishwa kwake , kwani uwezo wangu niliokuwa nao ni mkubwa sana na mimi ndio mwanajeshi pekee mabae nimepata mafunzo kwa
miaka mingi sana na kufanya operesheni nyingi sana za hatari nikiwa mafunzoni na kuzifanikisha kwa asilimia mia moja .
Jambo moja lililonirudisha nchini ni juu ya uchaguzi mkuu ndani ya taifa la Tanzania , nilidhamiria ndani ya uchaguzi huu raisi atakae ingia madarakani lazimia awe mwanachama katika kitengo chetu cha siri ambacho viongozi wengi wa kiserikali wanaamini kwamba walikikomesha ndani ya utawala wa raisi Mathayo Kilubwa lakini jambo ambalo walikuwa hawalifahamu ni kwamba kitengo hichi hakikutokomezwa nchini bali kilikuwa kikifanya kazi zake kwa kutokuonekana huku ma ajenti wengi wa kikundi hiki wakiwa mafunzoni wakiongozwa na mimi mwenyewe .
Kati ya wanafunzi tuliokuwa katika mafunzo nchini Urusi na Cuba tulikuwa jumla ya wanafunzi nane ambao tulikuwa chini ya kitengo chetu cha siri ambacho kilipata kuvumbuliwa na Raisi John Bendera na kukipa jina la Mzalendo .
Basi ni asubuhi ya leo nikiwa ndani ya barabara ya Bagamoyo nikiwa eneo la Mbezi beach nikitokea nyumbani kwangu Makongo Juu , foleni siku hii ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba sisi wenye magari tulikaa barabarani kwa muda mrefu sana , licha ya foleni hio kubwa , kwangu haikunikera kabisa kwani niliweza kupata wasaa wa kuangalia video aliaoniachia Bwana Bruno Lamberk .
Siku hii ya leo kulikuwa na Shamra shamra nyingi sana kwani ilikuwa ni siku ambayo mheshimiwa Jembe raisi mteule alikuwa akiapishwa na ndio kitu ambacho kilisababisha foleni kubwa sana kwa siku hii , kwangu nilijikuta nikiwa na furaha sana na pia kujiona nimepiga hatua kubwa sana ya kuhakikisha mheshimiwa Jembe anashinda uchaguzi na hatimae kuapishwa , kwangu hio ilikuwa ni hatua ya kwanza katika mipango yangu zidi ya U-97 ,umoja ambao ulikuwa ukiongozwa na Bruno lakini pia umoja ambao ulimfanya raisi Bendera kuunda kitengo cha Mzalendo, kikundi ambacho lengo lake kuu ni kuutokomeza umoja huu ndani ya taifa laTanzania
Siku ya leo siku panga kwenda kushuhudia uapisho wa Raisi Jembe .licha ya Mzalendo na mimi nikiwa kama mkuu wa kitengo hichi kuhusika na kushinda kwake ,kwani kama isingekuwa sisi licha ya Jembe kuungwa mkono na wananchi wengi , lakini kwa serikali ya chama tawala asingefua dafu kwani kulikuwa na tabia ya wizi wa kura .
Nilikuwa nimepanga niende moja kwa moja mpaka kwenye kambi yetu ya siri ya Mzalendo kwa ajili ya kushugulikia misheni ambayo tulikuwa tukidhamiria kuifanya kwa siku hio , na muda huo ambao nilikuwa kwenye gari ni kwamba ajenti wa Mzalendo walikuwa kwenye majukumu yao kama kawaida.
Baada ya masaa mawili niliweza kufika ndani ya kiwanda changu cha maswala ya Tehama kilichokuwa maeneo ya Kurasini , mara baada ya kuingia zangu ofisini na kusalimiana na wafanya kazi ,moja kwamoja nilielekea ndani ya ofisi yangu , na mara baada ya kuingia ndani ya ofisi hii na kuweka mambo sawa , nilitoka na kuingia kwenye lift tena na kisha nilibonyeza vitufe kwa mfumo wa ‘commbination button’ na lift moja kwamoja ilinipeleka mpaka kwenye
‘basement’ Vyumba chini ya ardhi , ambako ndio sehemu chimbo letu la wanaMzalendo tilikuwa tukifanya kazi humo na kuandaa operesheni mbalimbali ambazo zinalenga moja kwa moja katika kuuuondoa U-97 nchini.
Baada tu ya kuingia ndani ya ‘basement’ hii ambayo ilikuwa na ulinzi wa hali ya juu sana , kiasi kwamba kwa mtu ambae sio muhusika wa kitengo hichi akijaribu kuingia kwenye kambi hii ni Dhahiri kabisa ataishia kwenye kizuizi namba moja , kwani hii sehemu licha ya teknolojia yake kuwa kubwa , lakini pia ilikuwa ikilindwa na mionzi mikali ambayo kama ikikunasa inabadilisha kabisa mfumo wako wa akili .
Basi baada ya kuingia ndani ya hii ‘basement’ mtu wa kwanza kuonana nae alikuwa ni Janeth , kwa wasiomjua huyu mwanadada kifupi ni kwamba ni moja ya watoto wa mzee Bendera warembo sana , yaani ana umbo flani hivi ukiliangalia lazima umeze mate , huyu bibie kuwaweka wazi tu ni kwamba huwaga najipigia tu na ninachofahamu ni kwamba ananipenda sana na anatamani siku moja tuyajenge maisha tukiwa pamoja , lakini kutokana na majukumu yetu ambayo tunayafanya , jambo hilo kwangu na kwake pia linaonekana gumu , Huyu bibie japo ya kuwa mrembo lakini pia ni moja ya wanawake wenye akili nyingi sana ndani ya taifa hili na kuthibitisha akili yake ni kwamba aliweza kupata PhD yake akiwa na umri wa miaka ishirini tu , Ni mtu ambae namkubali sana katika maswala ya teknolojia , na ndio mtu pekee ambae anafanya kitengo chetu kuwa ‘invicible’(kutokuonekana ).
“Babe!!!” Mara baada tu ya Janeth kunitegemea wakati nikiingia ndani ya kambi hio alinikimbilia na kunihug , kanapenda kujibebisha sana haka katoto yaani naweza kusema katika videmu vyangu ambavyo nimeweza kutembea navyo , hakuna anaemshinda Janeth kwa kuwa ‘Romantic’.
“Nataka kujua maendeleo ya operesheni”
“Mpaka sasa naweza kusema mipango yetu ipo kwa asilimia moja , kila ajenti yupo kwenye mkao kuendana na operesheni”
“Safi , inatakiwa kuhakikisha hakuna kosa linaloteokea kwani tukizembea kidogo tu tunaweza kumpoteza Raisi jembe “Niliongea nikiweka msisitizo , kwani mpaka wakati huo tulikuwa tuna taarifa zote za mpango ambao umeandaliwa juu ya kumuua raisi jembe kabla ya kuingia ikulu na taarifa hio tulikuwa tumeipata kutoka kwa moja ya wanamipango hio ambae ni shushu wetu .
Mpango wenyewe uko hivi : baada ya kutangazwa kwa raisi Jembe kuwa raisi tuliamini kwamba chama tawala kisingemruhusu kuchukua madaraka , kwani siasa ilikuwa imesambaa mpaka kwenye vyombo vya usalama wa nchi jambo ambalo lilikuwa likimuweka Jembe katika hali hatarishi Zaidi .
Hivyo baada ya Jembe kutangazwa kushinda, tulimpa maelekezo kwa njia ya simu kwa kwenda sehemu ambayo tulikuwa tumeandaa sisi , ambayo tulikuwa tukiamini ni sehemu salama ambayo mtu yoyote hawezi kuifikia , unaweza kudhani ni kwa namna gani Jembe aliweza kutumaini , ukweli ni kwamba kabla ya kuingia kwenye zoezi la kupiga kura tulimtaarifu raisi Jembe kwamba lazima atashinda na sisi ndio tutafanikisha hilo hivyo yeye ajiandae kwenda ikulu .
Na baada ya yeye kushinda alituamiani kwani hata yeye mwenyewe alikuwa akijua kuwa asingeweza kuwashinda chama tawala katika sanduku la kura , labda tu kungekuwa na Tume huru jambo ambalo hata jembe mwenyewe katika maisha yake ya siasa alikuwa akilipigia Debe kila siku lakini halikuweza kusikilizwa na watu wa chama tawala .hivyo alikuwa ni kama anachangamsha uchaguzi tu kwani alikuwa anaamini yeye kushinda ilikuwa ni kwa asilimia ndogo sana .
Basi baada ya kuhakikisha Raisi mteule yupo sehemu salama mpaka siku ya uapisho wake , tuliendelea kufatilia mienendo ya watu kutoka chama tawala , kwani tuliamini kwa namna yoyote ile ni lazima wangepanga jambo ambalo lingepelekea raisi Jembe asiingie Ikulu na hapo ndipo kwa kutumia shushu wetu tulipoweza kupata taarifa kamili za mpango huo , tuliweza kumjua Peskorov kama moja ya wadunguaji hatari sana kuwahi kuwepo katika uso wa dunia kutumika katika mpango huo , na kwanzia siku ambayo bwana huyu wa kizungu anaingia nchini kila hatua aliokuwa akipiga , alikuwa akifatiliwa na Ajenti Linda moja ya wanachama wa kitengo cha Mzalendo na huyu Linda na yeye alikuwa ni moja ya wanafunzi ambao tulikuwa wote mafunzoni Nchini urusi kabla ya mimi kuelekea Cuba , na niseme tu huyu ajenti na yeye ni hatari Zaidi , kwani licha ya Urembo wake wa kikabila la Kirangi , lakini alikuwa ni mwepesi sana likija swala la mapigano na kwa sifa alizokuwa nazo Peskorov basi tuliona Linda anaweza kummudu vyema .
Kwakua mpango wote tulikuwa nao basi jambo hili tuliweza kulipangilia kwa akili sana , kwanza tulihakikisha kuwa na gari ya wagonjwa katika msafara wa raisi kuelekea ikulu na ndio maana mara baada ya raisi kupigwa risasi ya kifua na bwana Peskorov ambae nilimkubali sana kwa ulengaji wake , kwani sehemu ambayo alikuwa amekusudia kulenga ndio hapo hapo risasi ya mheshimiwa Jembe ilipotua.
Baada ya Risasi ile kumpiga mheshimiwa Jembe , wanausalama ambao walikuwa chini ya mpango wa Mzalendo ambao walikuwa wamejichanganya na kundi la wanausalma kutoka kitengo cha usalama wa Taifa , waliupakia mwili wa mheshimiwa katika Ambulance ,baada ya kufika mbele kidogo ya ukumbi wa aghakani mjini Posta mbele kidogo tuliweza kufanya mabadilishano ya kimagari , yaani gari ambalo lilikuwa likitoka Amana hospital lilikuwa likifanana na la kwetu ambalo tulikuwa tumelipandikiza na kuendeshwa na wanasalama wa kitengo chetu , hivyo gari ile ya kubebea wagonjwa iliokuwa ikitokea Amana iliendelea na safari ya kuelekea Muhimbili na gari ya kwetu ilisogea mpaka mkabala wa njia inayoingia mtaa wa Mindu na baada ya kufika hapo tulikuwa tunamawasiliano na watu wa Temple ya wachina na gari yetu ile iliingia hapo na baada tu ya kuingia hapo , raisi tulimtoa katika ile gari na kumuigiza katika V8 na kumleta kambini huku tukihakikisha hakuna namna yoyote ile tunaacha hatua nyuma, kwani mara baada ya kutoka kwenye hio Temple gari ile ilifanyiwa kazi na mafundi kubadilishwa rangi , na tulihakikisha kamera zote tunazipa taarifa tunazotaka sisi zionekane na wanausalama wa kitengo cha Taifa .
Naam mpango ukawa umekamilishwa na ajenti Elvice , ajenti Linda .Ajenti Karim , Ajent Patrick, ajenti Janeth , Ajent Nasra mrembo sana huyu ila ananikazia ila aataingia kwenye kumi na nane zangu , Ajenti Zakayo Na mimi mwenyewe Damiani Rabani mkuu wa kitengo cha Mzalendo Sisi wote ni special ajenti na kupambana na sisi inahitaji akili ,ujuzi na maarifa , tupo ndani ya Taifa hili kwa ajili ya kupambana na U-97.
*****
Mheshimiwa Jembe alijikuta akishituka na kukutana na nyuso ambazo zilikuwa zikimuangalia , zilikuwa ni nyuso za watu kumi jumla waliokuwa wakimwangalia wakiwa wamevalia mavazi ya aina moja , yaani rangi nyeupe , kitendo kilicho mfanya ajifikiche macho , kwani aliamini wakati huo ni lazima watu waliokuwa mbele yake walikuwa ni malaika , lakini akili yake iligoma kukubali kuwa watu hao ni malaika , kwani alikuwa ni moja ya watu waliopata kusikia habari mbali mbali zilizokuwa zikihusiana na malaika , kuwa wengi wao ni wazuri na hawana makunyanzi na sio weusi , lakini kwake kitendo cha kuona baadhi ya watu hao kuwa na sura mbaya baadhi yao na ndevu zisizokuwa katika mpangilio , aliamini bado hakufa , aliamini bado huenda hayo ndio mavazi ya watu wa Ikulu wanayovaa wakati wakiwa wanamhudumia Raisi , na hapo yupo kwenye chumba maalumu ambacho anasubiriwa aamke ili ahudumiwe .
“Karibu duniani mheshimiwa “Aliongea Damiani na kumfanya Jembe anyanyuke , lakini wakati anajilazimisha kunyanyuka alijihisi maumivu kwenye kifua na hapo ndipo alipokumbuka kwamba alipigwa Risasi kwani akili zake mpaka wakati huo hazikuwa sawa bado , lakini jambo la kushangaza alijihisi maumivu ya kawaida sana jambo ambalo lilikuwa mshangao kwake , kwani katika maisha yake alipata kuambia kwamba risasi ikikupata lazima itoboe nyama , lakini kwake hakuwa hata na tundu la risasi Zaidi ya maumivu .
“Hapa ni wapi ?”
“Upo ndani ya kambi ya Mzalendo “
“Kambi ya Mzalendo!, Nchi gani ?”
“Upo ndani ya Nchi yako Muheshimiwa , chini ya Kambi ya kitengo cha siri cha Mzalendo na sisi unaotuona hapa ndio ajenti kumi wa kitengo hichi “Aliongea Damiani kwa Urefu jambo ambalo lilimfanya Jembe ashangae , kwani hakuwahi kusikia juu ya kitengo cha Siri , lakini alivyokumbuka kwamba yeye ni raisi , na huo ni mwanzo wa kujua siri za nchi aliona jambo hilo ni la kawaida na kwa muda huo anachohitaji yeye ni maelezo ya kina .
“Sisi ndio tuliokupigia simu na kukueleza juu ya safari yako kuelekea Ikulu, sisi ndio tuliokupigia simu na kukupa ulinzi mpaka siku ya kuapishwa kwako , sisi ndio tuliokuokoa katika kifo”Maneno hayo ndio yaliomfanya sasa mheshimiwa Jembe kujua anazungumza na watu gani, wale watu ambao walikuwa wakimuumiza akili yake sasa wapo mbele yake , hakika alistaajabu , hakuweza kuamini watu hao kumi ndio walioweza kuudhibiti uchaguzi na kushinda kihalali .
“Nahitaji kuwajua Zaidi , na tukio zima la mimi kupigwa risasi “Aliongea mheshimiwa Jembe na kuwafanya wanamzalendo kutabasamu .
Mheshimiwa mara baada ya kuomba kuwajua Zaidi , wanamzalendo , aliombwa kunyanyuka na kuendelea chumba ambacho ndio shughuli zote za kitengo hichi cha siri zilikuwa zikifanyika , alijikuta akishangaa mno , kwani kwa kila chumba alichokuwa akipitishwa ndani ya ‘basement’ hii alijikuta akihusudu muundo na mpangilio wa eneo hilo .
“Sijawahi kupata kuingia sehemu kama hii kwenye maisha yangu” aliongea mheshimiwa Jembe mara baada ya kufikiwa eneo maalumu ambalo lilikjuwa na mitambo mikubwa ya kisasa , huku tarakishi kubwa zilizokuwa zimefungwa zikionyesha eneo zima la jiji la Dar es salaam .
Damiani hakutaka kumueleza mheshimiwa Jembe kwa njia ya mdomo bali alivuta faili kweye tarakishi na kumruhusu mheshimiwa aanze kusoma , na mheshimiwa hakutaka kuchelewa alianza kusoma faili hilo , na kadri alivyokuwa akiendelea kusoma mwili ulikuwa ukimsisimka , alitumia madakika kadhaa kumaliza kusoma ripoti hio ya mzalendo mpaka kuimaliza , katika mambo yote aliosoma alielewa kasoro jambo moja tu ambalo kwake hakuliewa kabisa , na alihitaji ufumbuzi Zaidi .
“UMOJA NAMBA TISINI NA SABA nataka kujua Zaidi kuhusu huu umoja “ Aliongea na
Janeth hakukawia alimvutia faili linguine na kumpatia Mheshimiwa na , alianza kupitia tena na faili hilo , na hapa ndipo mwili ulipozidi kumsisimka , kwani kwa mambo alioyasoma alikiri kwamba kiti cha uraisi kilikuwa cha moto , hakuamini kama ndani ya taifa la Tanzania kulikuwa na Nguvu ambayo ilikuwa ikiliendesha Taifa kwa namna ya siri kabisa , huku viongozi wakiwa kama masanamui tu Pale Ikulu , lakini Zaidi ya yote alijikuta akimhusudu sana mheshimiwa John Bendera , alikiri kwamba huyo bwana alikuwa ni shujaa wa nchi.
“Ni hali ya kutisha kwelikweli , sikupata kujua kwamba taifa lipo kwenye mikono ya watu kama hawa”Aliongea mheshimiwa Jembe huku akijifuta jasho .
“Ni kweli uyasemayo mheshimiwa na nadhani mpaka sasa umepata kuelewa nini maana ya Mzalendo”
“Kwanza niwape pongezi kubwa sana , kwa jambo ambalo mnalifanya kwa taifa hili , hii ni historia ambayo mnaandika , ambayo itakumbukwa na vizazi vingi , ni ushujaa wa hali ya juu sana mnaoufanya , na nadhani itakuwa vyema kwa mimi kuwafahamu kwa kila mmoja , japo baadhi yenu nawafahamu , akiwepo Profesa hapa”Aliongea mheshimiwa huku akimwangalia ?Janeth na kumfanya atabasamu
Damiani aliwatambulisha ajenti wote wa Mzalendo , pamoja na kuelezea historia yake yote ya mambo ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia wakati huo (Hakikisha umesoma U-97WARAKA WA RAISI ), aliamweleza mheshimiwa juu ya mambo yote ambayo yalikuwa yamefanywa na wanamzalendo kwanzia kuundwa kwake , mafanikio yote .
“Nataka kujua kabla ya yote imewezakana vipi mimi kupona ile risasi “
“Mheshimiwa suti uliovaa siku ile ilikuwa imeundwa kwa muundo wa Bullet proof kwa teknolojia ya hali ya juu ambayo kwa sasa watengenezaji wa suti hizo ni Z-Styllish wear inayomilikuwa na moja ya familia ya wanamzalendo”
“Inamaana kuna wanafamilia wengine ambao wapo chini ya mzalendo ?”
“Ndio mheshimiwa kuna wengi ambao wapo undercover”.
“Nimefanikiwa kusoma maelengo yenu ya kitengo hichi cha siri , lakini sijapata kujua ni kwa namna gani mtaweza kuondoa umoja huu ndani ya Taifa hili , kwani kwa kile ninacho ona ni kwamba umoja huu ni wenye nguvu sana Duniani”.
“Ni kweli kabisa mheshimiwa , umoja huu ni wenye Nguvu kubwa Duniania na kila siku unaendelea kujipanua katika Nyanja zote ,lakini sisi kama wazalendo tunaamini kwamba hakuna jambo ambalo halina udhaifu”
“Unamaanisha nini bwana Damiani?”
“Kila jambo ndani ya dunia hii lina udhaifu wake Mheshimiwa , na hicho ndio kitu ambacho kitengo hichi tunafanyia kazi , na swala hili tunampa pongezi sana mheshimiwa bendera kwani kabla ya kifo chake aliacha waraka”
“Unahusu nini huo waraka ?”
“Damiani hakutaka kuongea sana , alivuta kitabu kimoja kilichoandikwa na mwandishi nguli kabisa SinganoJr na kisha akamkabidhi , kitabu hicho juu kabisa kinasomeka kwa jina la
UMOJA NAMBA TISINI NA SABA –WARAKA WA RAISI KABLA YA KIFO.