..nina maswali mengi kuliko majibu, kuhusu madai kwamba Tz ilipeleka maofisa wake wa jeshi Israel huku wakidanganya kuwa wametokea nchi nyingine, mfano Ghana.
..kabla askari hao hawajapelekwa inabidi kuwe na mawasiliano baina ya serikali/wizara/majeshi ya nchi mbili husika.
..sasa katika mazingira kama hayo utampeleka vipi askari ng'ambo kwa kutumia njia za ujanja-ujanja?
..kwa mfano, tukubaliane kwamba askari walipelekwa kwa kutumia pasi za Ghana. Je, hilo linawezekana vipi bila kuishirikisha Ghana!
..Zaidi, askari wetu walipofika Israel, vipi kama wangekutana na askari kutoka Ghana. Je, askari wetu walifundishwa lugha au tamaduni zozote za Ghana ili wasiwezi kugundulika na wakufunzi wao kuwa wanadanganya?