MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

Hiyo adhabu haifai kabisa , Je ? mtoto wake anaweza akamfanyia hivyo, inauma , inaumiza sana , fikilia kama mdogo wako au mwanao anafanyiwa hivyo, bora waniue kuliko kunifanyia hivyo, nawageuza paka kabisaaa.
Mbona mnachapwa sana na polisi.
 
*****, kama huyo mtoto angekuwa wakwangu saivi walikuwa wanachangishana pesa za kununua majeneza
 
Nimetambua sababu mojawapo ya sirikali kuwanyima hawa kizazi cha mitandao ajira ya ualimu maana hawa hawana tofauti na huyu mpofua macho scorpion!! Tena hawa ndo wanawaharibu watoto wetu wa kike mashuleni,MAJAMBAZI KABISA HAWA!!!
 
Dada mchawi balaa nisieleweke vibaya kama nawatetea wale walimu ila nahis hakujua madhara kama yatakuwa makubwa hivyo kwa video aliyorekod
Sio kwamba mchawi ni wewe usiyetaka yale ya gizani yajulikane?
 
Vile vibao ni vibaya sana huwa kuna mwingine vinapelekea kuwa kiziwi nakumbuka zamani kuna mwanafunz alipigwa vibao kama vile vilipelekea sikio kutoa usaha kwa kuwa tulikuwa kijijini noma iliisha tu ila jamaa alipona na mwalimu hakuwa na amani kamwe
nawashangaa sana hawa wanao justify unyama kama huu tena kwa mtoto
 
Wadau,

Clip hii sijui ni shule gani lakini yaonekana ni hapa nchini kutokana na sauti ya dada inayosikika kwenye background.

Hata kama huyo kijana amekosa vipi si angepelekwa vyombo vya sheria?

Wana tofauti gani na wale wanakijiji walioua watafiti?

Sheria ifuate mkondo wake, inaumiza sana.

=======

UPDATE:

Mkuu wa shule ya Mbeya Day pamoja na baadhi ya walimu wamechukuliwa na jeshi la polis kwa mahojiano zaidi. Tukio hilo lilitokea 28. September.

Jumanne tarehe 24 mwalimu wa vitendo alitoa homework kwa kidato cha 3 A, kwa bahati mbaya mwanafunzi huyo hakuwepo, Jumatano wakati mwalimu anakusanya homework yule mwanafunzi alimwambia mwalimu kuwa jana yake hakuwepo alikuwa anaumwa.

Mwalimu alianza kumpiga makofi darasani lakini akaondoka naye hadi ofisini na kuwaambia walimu wenzake kwamba mwanafunzi huyo hakufanya homework ndiyo walimu wakamchangia kumpiga.

Hali ya mwanafunzi bado siyo nzuri kwani aliumia sana sehemu ya kichwa na machoni. Tayari Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza walimu hao kuchukuliwa hatua za kisheria.

========

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A Mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.


Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video.

Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali. Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.

MWIGULU Nchemba, W MNN




MKUU WA MKOA WA MBEYA AZUNGUMZIA TUKIO HILO

​

mbona inasemekana huyo dgo si mwanafunzi,alivaa uniform ili apate chance ya kuwadanganya watoto wakike kimapenzi
 
No no no.

That is unacceptable.

Hiyo ni jinai.

Hao walimu, hususan huyo anayempiga huyo dogo usoni ni wa kufungwa jela kabisa.

Na wana bahati huyo dogo si ndugu yangu la sivyo street justice ingewahusu.
Hata kama sio ndugu yako! Kama upo kwenye nafasi ya kuchukua hatua go on!
 
Asee hivi walimu wote wangekua hivi na kueajenga watoto tangu wakiwa chekechea.. wakakua wakiwa na walimu design hii unadhani ayo ya namna iyo tunayoyaona yangetokea..!? Big up sana mkubwa.. you deserve kuitwa MWALIMU MWEMA.... na Mungu ndio anawalipa walimu kama nyie...
Asante mkuu.
 
watanyea debe wote si alikuwepo eneo la tukio.na hakureport wala nini? anareport whatsup ili iweje?
yule nafikri alifanya kwa lengo la kuonyesha tu rafiki zake sasa km alituma kwa group ndo mambo yameharibika hivi!!

Soo sad!
 
Hata kama sio ndugu yako! Kama upo kwenye nafasi ya kuchukua hatua go on!
I actually would if I could.

But I believe their comeuppance is coming.

What a bunch of heartless and rotten scoundrels!
 
Hapo jela inawahusu. Tatizo wanasahau majukumu yao. Uongozi huu sijui kama hao walimu watasalimika?
 
Hawa ualimu sio wito wao...wameamua tu kuingia kwenye fani hii kutokana wamekosa nafas za kazi za ndoto zao ili kujikimu na maisha wameamua kuvamia fani hii ..naagiza watapopatikana na kuhojiwa wauulizwe kwanza walipenda kufanya kazi gani katika maisha yao,hawa na scorpion mtoboa macho hawana utofauti...sometime natamani ningekuwa afisa usalama kesi kama hizi ningependa nipangiwe mimi hawa wahuni wangekuwa mfano wa kuigwa n.a. wajinga wengine wote wanaokiuka maadili ya fani zao.mwalimu alorekodi hili tukio asije ukataa ushahidi wake pia kama yule mlinzi wa kule hospital maana tz ina mambo sheria ifate mkondo wake mishahara ya miezi 3 ya wote walompiga ifidie matibabu ya huyo denti.mwanangu akifika umri wa kuanza shule kayumba ataisikia kwenye bomba kwa stlye kama hizi ntakuja nijikoki kama Rambo mwanangu akisoma kayumba akija na taarifa eti walimu wamemgeuza mpira wa kona kuepusha haya yote shule za mboga saba zitamuhusu japo elimu bure her I nigharamie kuliko kuja kutinga shule n.a. panga,jembe,sululu,fyekeo,rungu,nondo,Manati,viwembe v yote nikiwa nimevibeba kwa pamoja kama baba ubaya
 
Back
Top Bottom