Miss Halima
Senior Member
- Aug 4, 2026
- 170
- 374
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, amethibitisha kifo cha mwanafunzi Peter Maira, aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Makongoro, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Kamanda Lutumo amesema mwanafunzi huyo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, baada ya kudaiwa kuzimia wakati akipewa adhabu shuleni.
Kwa mujibu wa Kamanda Lutumo, hadi sasa walimu sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi, huku uchunguzi wa kitabibu ukisubiriwa ili kubaini chanzo halisi cha kifo cha mwanafunzi huyo.
Kamanda Lutumo ameeleza kuwa wakati mwanafunzi huyo akipewa adhabu, alizirai na kukimbizwa hospitalini kwa ajili ya matibabu, lakini baadaye alipoteza maisha.