Wewe unaona hiki ni kitu chepesi?!! Unajua wanafunzi wangapi wanafanyiwa unyama kama huu? Achilia mbali wanafunzi,watoto wangapi wanafanyiwa unyama kama huu? Unajua athari yake kwenye makuzi?watanzania mnapenda sana vitu vyepesi
Wadau,
Clip hii sijui ni shule gani lakini yaonekana ni hapa nchini kutokana na sauti ya dada inayosikika kwenye background.
Hata kama huyo kijana amekosa vipi si angepelekwa vyombo vya sheria?
Wana tofauti gani na wale wanakijiji walioua watafiti?
Sheria ifuate mkondo wake, inaumiza sana.
=======
UPDATE:
Mkuu wa shule ya Mbeya Day pamoja na baadhi ya walimu wamechukuliwa na jeshi la polis kwa mahojiano zaidi. Tukio hilo lilitokea 28. September.
Jumanne tarehe 24 mwalimu wa vitendo alitoa homework kwa kidato cha 3 A, kwa bahati mbaya mwanafunzi huyo hakuwepo, Jumatano wakati mwalimu anakusanya homework yule mwanafunzi alimwambia mwalimu kuwa jana yake hakuwepo alikuwa anaumwa.
Mwalimu alianza kumpiga makofi darasani lakini akaondoka naye hadi ofisini na kuwaambia walimu wenzake kwamba mwanafunzi huyo hakufanya homework ndiyo walimu wakamchangia kumpiga.
Hali ya mwanafunzi bado siyo nzuri kwani aliumia sana sehemu ya kichwa na machoni. Tayari Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza walimu hao kuchukuliwa hatua za kisheria.
========
Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A Mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo.
Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video.
Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali. Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo.
MWIGULU Nchemba, W MNN
Wameshadakwa. Hasira hasara. Na inabidi wakae ndani kwa muda wa kutosha bila dhamana ''kwa usalama wao'' maana raia wenye hasira kali wanaweza kufanya yao huko mtaani.
Usinitafutie ban we jambazi uchwara,nitakuteka nikulete chuga.We jamaa mama yangu anaingia vipi hapo? unavuja nini
Safi maana kila nikiikumbuka ile video moyo unauma, hii muifuatilie hadi jamaa watakapopewa adhabu ndipo nitaridhika, yaweza kua maneno tu kupunguza kelele za wananchi. Walimu wa design ya wale jamaa ni wengi sana Tanzania ila wangechukua muda kufanya research kama kumpiga mwanafunzi heavy inamsaidia wangejua kua wanapoteza muda tu, mtu mtukutu ni mtukutu tu hata umchape viboko vingapi akitoka shuleni ni yule yule a better treatment ni psychological na hii inafanywa kistaarabu.[/QUUnaongea kama vile unaishi nchi isiyo Tz
Soma hapo chini halafu useme ni vitu vyepesi.watanzania mnapenda sana vitu vyepesi
....na macho yamepoteza uwezo wa kuona.
Madaktari wanasema yamevilia damu na la kushoto mshipa umekatika
So sad kwa kweli!Tunaelekea wapi jamani?!Where is love?Homework tu ndio kumpondaponda mtoto hivyo?!Hakuna jingine kweli?Jamani hali ya mwanafunzi ni mbaya...kaumia sana kichwani
umenfurahisha sana na comment yako mkuuDaah huyo mwalimu aliyerekodi video hii sijui ana hali gani
Ila jamaa mwenye sarawili ya khaki anatembeza slap za adabu utadhani anampiga mgoni aliyemfumania
kumbe sio mwanafunzi yule?
Ww ni teacher unaonekana tena ulitefeli channe na ukaunga kama hujanunua chetiAfu aliyewarekodi wenzia n msengerema mkubwa kabsa,yaan mim ndo ningekuwa miongoni mwa walimu hao huyo alierekodi angenitambua
ni ujuha tu ! mbona miaka ya nyuma jkt ilikuepo na walikua na maadili yaliyotukuka!hawa waalimu ndio wale wanaopitishwa kwanza JKT wanapewa matizi mpaka wanazimia na wanagalagazwa kwenye maji?baada ya hapo ndipo wanaruhusiwa kuomba chuo?
anyway hawakufanya jambo jema,viroba,ugoro,kuvaa milegezo,ujana