MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

MBEYA: Walimu warekodiwa Video, wakimfanyia unyama Mwanafunzi

Unaandika kama jinga fulani hivi wewe si mwalimu wewe upo hapo kwa sababu ya UKALI wa life na si vinginevyo. Mwanafunzi mtovu wa nidhamu ANASIMAMISHWA MASOMO sio kumpiga kama MUHALIFU unasikia wewe mwalimu kila.za? Hao walimu wangemuua huyo mwanafunzi ingekuwaje? Hili tutapinga na kukumbusha kwamba nchi hii inafuata taratibu si kupiga wengine kwasababu tu unaona inafaa. Kaa kimya wewe ndugu mwenye chuki kwa wanafunzi/vijana
Mshamba ww unamsimamisha masomo ili iweje na akajifunze nn ukishamsimamisha..apigwe ili keshi ajue walimu hawataki ujinga


Taarifa rasmi za tukio la kupigwa Mwanafunzi

Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo. Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo. MWIGULU Nchemba, W MNN
 
Haya ndio madhara ya mtu kusomea fani......baada ya mambo yote kugoma....

Vijana wa siku hizi wanasoma ualimu kwa kuwa tu wasikae nyumbani lakini hawana pasion nao kabisa....
 
Sidhani km alikuwa na lengo la kuifikisha kwenye mamlaka husika..nahisi ni baada ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii (walimu wanalindana na kusaidiana wana umoja) usikute saa hizi huko alipo anajuta kurekodi hiyo video
Off course anajuta na atajuta maisha yake yote!!

Yaani huyo Dada huko aliko analia tu!
 
Huyu Mwalimu aliyetajwa na Mwigulu sijui itakuwaje!!Maana sasa kaonekana kuwa ndio "mnoko" wa wenzake.Halafu hao jamaa Walimu ni walimu wa Field,masharudi vyuoni kwao.Mwalimu Mkuu ndio katiwa ndani
 
Tayari Mh. Waziri Mwigulu kwa kukurupuka kwake kamtaja Mwalimu huyo kwa jina kuwa ni Mwl xxxxxxxxxxxx wa Iringa University nadhan baada ya wadau kumkosoa ndio kafuta jina na kuweka initials za Mwalimu wakat tayari post yake ya awali ishasambaa!
Halafu Mwigulu yy ni waziri wa elimu?

Waziri wa tamisemi,DEO,REO?amkurupuka mpk nimeshangaa sana

Mbona hawafati utaratibu hata km tukio la kihalifu!
 
Inadaiwa huyo dogo sio Mwanafunzi bali aliingia hapo kumlaghai mtoto mmoja wa kike aliva sale kama student also na wanafunzi nao shida maana Kuna dogo kamkung'uta headmaster mbele ya wanafunzi wenzake je unafanyaje
 
Kule kwetu miaka ya 2000 mwanzoni kuna Mwalimu alimchapa mwanafunzi mpaka fimbo ikamtoboa jicho, yule Mwalimu akalogwa mikono yake ikawa haina nguvu kabisa, alianza kushindwa kuandika ubaoni, baadae akapewa somo la stadi za kazi ili awe anafundisha kwa mdomo tu, mpaka leo hawezi kunyanyua mkono kumsalimia mtu maana ni kama mikono haina mfupa au msuli wowote.
Alishastaafu siku hizi anakaa tu nyumbani kwake maana hawezi kufanya kazi yeyote.
Huwa kuna story kuwa huko miaka ya nyuma alikuwa mbabe sana alishawahi kumchapa mwanafunzi huyo mwanafunzi akaenda kumleta mzazi wake mzazi wake naye akachapwa vilevile.
 
Nafikir alirekodi tu akijua atamuonyesha huyu na yule then yameisha kwa maana na yeye kukaa anarekodi bila kwenda kuingilia ule ugomv ni kama anasuport
Amefanya watu wapoteze kazi!!

I heard kua walimu wote wa pale wamefukuzwa!
Sina hakika lakini
 
Huyu Mwalimu aliyetajwa na Mwigulu sijui itakuwaje!!Maana sasa kaonekana kuwa ndio "mnoko" wa wenzake.Halafu hao jamaa Walimu ni walimu wa Field,masharudi vyuoni kwao.Mwalimu Mkuu ndio katiwa ndani
Hadi picha zake zimeanza kuenea,ss sijui za nn?
 
Ajabu sana mkuu!Wanaume wa shoka wanakusanyana kukapiga kavulana kadogo hivyo?Hawa wana bahati,wangeweza kumuua huyo mtoto na kesi ikawa mbaya zaidi.Wachunguzwe hao huenda kuna la zaidi.Mwigulu hebu fuatilia hawa vijana.
Nimeshikwa na hasira kweli,natamani nionyeshwe hao vijana halafu niwaombe wanipige mimi hayo makofi ili niwafundishe matumizi sahihi ya "nguvu za kiume".
Yaani inashangaza kweli mkuu tena wanajirekodi kabisa
 
Wote wana makosa kuanzia huyo mwl. aliyerecord video kwanza amekosa ethics za ualimu, pia nadhani hakusoma na kuelewa baadhi ya kozi akiwa chuoni.
Kuna kozi ya "Classroom Interaction" ambayo kwa 90% mwl mtoa adhabu hakuiapply vema kuanzia darasani.

Pia mrecord video hana maadili ya kazi kwani yeye kama sehemu ya teaching staff alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na kamati husika za shule. School administration and management ya chuon kwake itakuwa alifeli kabisa ama hajaielewa.

Pia punishment & reward ni part and parcel of learning and teaching processes.
Mwalimu anaonya kitu kibaya na kutoa zawadi kwa jambo zuri. Hili lipo kwenye Educational Psychology, Education measurement & evaluation, na baadhi ya ma philosopher wanakubaliana na adhabu, haya ameyakuta chuoni kwake kwenye somo la Philosophy of Education. Kama hamtaki adhabu hao watoto wenu muwafundishe wenyewe majumbani mwenu.
Kama huwezi kazi ya ualimu nenda kuwa Tyson , corporal pursnishment inatakiwa kutekeleza na Mwl mkuu au wa nidhamu kwa kibali maalumu. Sio kumchangia mtoto Kama unapiga mwizi. Hao waalimu hawana maadili Kama wale vijana walio mbaka Yule dada kule mikumi nakuji record
Ushahidi ni kitu muhimu Kama video ingekosekana itakuwa taabu kiwatia hatiani wahusika. Pongezi kwa Mwl aliye record .
Na je unajua hali ya mtoto ilivyo sasa hivi , yaani hawa waalimu hawana tofauti na scorpion
 
Back
Top Bottom