Mbeya: Ofisa Usalama auawa kinyama!

Status
Not open for further replies.
Hakuna mtu baki mwenye kufanya hayo ila ni wenyewe kwa wenyewe. System imegawanyika na wanapomtuhumu mwenzao kuvujisha siri basi njia nyingine huwa nguvu kutumika kwa vile yupo kwenye system, kinachofanyika ni kikundi kidogo kinachoandaliwa kumaliza kwa njia za ujasusi wa kijambazi, ndivyo hawa jamaa walivyo.

Angekuwa mtu wa kawaida propaganda zingetumika kumchafua hadi aharibikiwe mambo yake na inaposhindikana propaganda ni rushwa kutumika kwa kuhonga ili kukamilisha azima yao. Kwa huyo yote yameshindikana na kuamua kuchukua njia ya ujasusi wa kijambazi.


Matukio kama haya si lazima yawe yanahusu saisa: Vipo pia visasi vya kibiashara na mambo ya mapenzi. Kwa umri wake Kisasi cha mapenzi sidhani kama yeweza kuwa sababu. Kwa hiyo tukio linaacha mambo mawili yanayoweza kuwa sababu: Kisasi cha Kibiashara na Siasa.

RIP Mzee Mwasokwa.
 
Watanzania,mbona utu umepotea tumeuvaa unyama jamani? MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
 
Mtu anauwawa kinyama kama kweli kwa namna uliyosema, kisha unamalizia kwa kusema eti Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Bwana yupi? Mnafanya utani na Mwenyezi Mungu.

R.I.P Mzee wetu. Poleni wafiwa wote. Mungu awatie nguvu wakati huu wa majonzi mazito kwa mpendwa wenu kukatiliwa uhai wake.
 
Confirmation ya hali mbaya ya usalama nchi hii ni pale RPC wa Mwanza alipouliwa kinyama. Huko mbele ni giza tupu na cha kushangaza wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama bado wapo ofisini, huku wengine wakiendelea kuchangisha harambee za makanisa!

RIP Mzee Mwasokwa, poleni sana wafiwa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
huyu mzee atakuwa alikuwa anawafanyia watu wa mbeya ujeuri wa kiu TISS sasa wasafwa wakamfanyia unyama
 
Tatizo wanataka kuendesha operation ya kukusanya silaha zisizo na kibali itakayoanza mwakani,wamehisi upepo wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe unanukia.
 
Matukio kama haya si lazima yawe yanahusu saisa: Vipo pia visasi vya kibiashara na mambo ya mapenzi. Kwa umri wake Kisasi cha mapenzi sidhani kama yeweza kuwa sababu. Kwa hiyo tukio linaacha mambo mawili yanayoweza kuwa sababu: Kisasi cha Kibiashara na Siasa.

RIP Mzee Mwasokwa.

Kama kawaida zitakuja propaganda nyingi katika hili kwa kauli hii sishangai.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema Mzee Mwasokwa.Inasikitisha kuona kuwa watu wameanza kwa kasi ya ajabu kujichukulia sheria mikononi.Hii ni hatari kubwa........inabidi vyombo vya sheria na usalama vijipange upya kukabiliana na uvunjifu huu mkubwa wa Utawala wa sheria.
 
I speak peace for each and every common citizen...I throw a word of confusion to the camp of organized criminals..May they start fighting each other to the point of exposing their hidden evils...In the might name of Jesus the name above all I decree and declare this; Amen!

R.I.P mzee wetu damu yako haijamwagika bure....Itatuletea kila lililo jema katika Taifa letu!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom