Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,467
- 7,258
Hakuna mtu baki mwenye kufanya hayo ila ni wenyewe kwa wenyewe. System imegawanyika na wanapomtuhumu mwenzao kuvujisha siri basi njia nyingine huwa nguvu kutumika kwa vile yupo kwenye system, kinachofanyika ni kikundi kidogo kinachoandaliwa kumaliza kwa njia za ujasusi wa kijambazi, ndivyo hawa jamaa walivyo.
Angekuwa mtu wa kawaida propaganda zingetumika kumchafua hadi aharibikiwe mambo yake na inaposhindikana propaganda ni rushwa kutumika kwa kuhonga ili kukamilisha azima yao. Kwa huyo yote yameshindikana na kuamua kuchukua njia ya ujasusi wa kijambazi.
Mambo haya sio madogo mkuu, hadi natetemeka....
"Wakiutenda mti mbichi namna hii je itakuwaje kwa mti mkavu?"
Nchi hii tulipofika!!!