Ofisa Usalama mstaafu afichua siri ya CCM kushindwa Mbeya

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Mbeya. Ofisa Usalama wa Taifa mstaafu, Said Salmin Said amefichua siri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kufanya vibaya katika uchaguzi.

Salmin aliyekuwa mgombea wa uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, amesema hayo leo Jumapili Desemba 3,2017 akiomba kura ukumbini kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa uchaguzi uliofanyikia jijini Mbeya.

Amesema CCM mkoani Mbeya imekuwa haisikilizi na kufanyia kazi ushauri wa kitaalamu inaopewa na ndiyo sababu ya kufanya vibaya kwenye uchaguzi.

Kauli hiyo aliitoa baada ya kuulizwa swali na mjumbe wa mkutano huo kwamba amekuwa kiongozi wa usalama wa Taifa mkoani Mbeya kwa miaka mingi, hivyo kutaka aeleze kwa nafasi yake alikisaidiaje chama hicho kupata maendeleo.

“Katika nafasi yangu nilikuwa mshauri kwa chama na nilitekeleza wajibu wangu kwa kukishauri, lakini tatizo likawa ni chama kutopokea na kupuuza ushauri na ndiyo sababu hakikufanikiwa,” amesema Salmin.

Amesema CCM mkoani Mbeya ina tatizo kubwa la makundi miongoni mwa wanachama, hali ambayo inasababisha kukosa umoja na mshikamano wa kuwakabili wapinzani wao.

Salmin amesema matatizo yote hayo anayatambua vizuri na kwamba endapo akichaguliwa kwa nafasi anayoomba, kazi yake kubwa ni kuyatatua.

Katika nafasi hiyo, Salmin alichuana na Dk Momole Kasambala, Jacob Mwakasole na Andilile Mwambalaswa.

Dk Kasambala amesema endapo atapata ridhaa ya kushika wadhifa huo atahakikisha anarejesha imani na kukusanya miradi ili kukuza uchumi wa chama hicho, lakini pia kuhakikisha kata zote zilizopo upinzani zinarejea CCM.

“Naomba mnipe ridhaa hii, nitahakikisha jimbo la Mbeya Mjini na kata zote ambazo zipo upinzani tunazirejesha mikononi mwa CCM,” amesema.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 CCM ilipoteza jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na Joseph Mbilinyi maarufu Sugu wa Chadema ambaye ameongoza kwa vipindi viwili mfululizo.

Pia, katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Ibighi wilayani Rungwe uliofanyika wiki iliyopita Lusubilo Simba wa Chadema alishinda kwa mara nyingine.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa mbeya mjini wasahau tu hili jimbo.

Mayb wakapambane huko rungwe na kyela
 
Kwa mbeya mjini wasahau tu hili jimbo.

Mayb wakapambane huko rungwe na kyela
Ni suala la kuamua wewe,wakilikunjia shati wanalipata kabla jogoo hajawika,Mzee wa pyupyu aende kuwa meneja Kule hotelini,ni suala la mda tu
 
Back
Top Bottom