Mbeya: Ofisa Usalama auawa kinyama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbeya: Ofisa Usalama auawa kinyama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabato masalia, Dec 9, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. S

  Sabato masalia JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  MMOJA wa wasisi wa idara ya usalama wa taifa enzi za ukurugenzi wa hayati Emil Mzena, mzee Joseph Mwasokwa ameuawa kwa kuchinjwa usiku wa kuamkia leo jijini Mbeya.

  Chanzo hakijajulikana.

  Hayati mzee Mwasokwa atakumbukwa kwa uchapa kazi wake mahiri, wakati huo akiwa na akina mzee Kayugwa, mzee kiliwa mzee Adam Kilumbi, Mzee Shekalage, Mzee Lymo, Marehemu Amir Koyamba, Mzee Kashinde, Mzee Kisesa, Mzee Said Mawele, marehemu Mzee Mahmood Issa, marehemu mzee Ijagala, Mzee Bwimbo [upande wa PSU], mzee Kalumanga NA WENGINE WENGI.

  BWANA AMETOA BWANA AMETWAA

  *************
  More details:

  - Mwili wa marehemu ulikutwa getini kwake, maeneo ya Block T jijini Mbeya.
  - Marehemu alikuwa ameenda jirani kuangalia mechi ya mpira
  - Marehemu alikutwa na $200 na TShs 100,000 hivi na vitu kama saa, simu n.k ambavyo havikuchukuliwa
  - Hakuna uhakika kama aliuliwa palepale getini kwake au aliuawa mbali na mwili kutupwa getini kwake

  Habari imeandikwa kwa kirefu zaidi hapa - Ofisa Usalama wa Taifa auwawa kwa kuchinjwa kinyama Mbeya | Fikra Pevu
   
 2. zefounda

  zefounda Member

  #2
  Dec 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Rip joseph mwasokwa
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  RIP baba,Tulikupenda Mungu amekupenda zaidi.
  Huu pia ni msiba mkubwa kwa klabu ya Yanga,alikuwa ni mshauri mwema kwa wanajangwani.
   
 4. k

  kalanjadd Member

  #4
  Dec 9, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we Sabato kiboko!hiyo timu uliyoitaja ni kali haapo naona mzee Apson alikuwa hajaingia bado, nakumbuka Apson,RO walikuja wakati wa ukurugenzi wa mzee Gama, mzee huyo anajulikana kwa kazi alikuwa anaijua vyema, sijui tatizo walilomuulia ni nini? alale pema peponi
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,139
  Likes Received: 2,334
  Trophy Points: 280
  TISS Again @ Work......Umesahau Imrani Kombe alivyouawawa? Unganisha Dots.....
   
 6. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,791
  Likes Received: 637
  Trophy Points: 280
  kaka hapo kwa mzee Bwimbo unamaanisha yule Ndugu Kajanja? kama ni yeye ni PM mkuu.
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,002
  Likes Received: 2,620
  Trophy Points: 280
  kwa heri ya kuonana
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 22,511
  Likes Received: 18,466
  Trophy Points: 280
  Mungu kampenda zaidi ndio achinjwe?
   
 9. Moshe Dayan

  Moshe Dayan JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2012
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 811
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  rip...,

  As they say, there are no second chances!
   
 10. fyddell

  fyddell JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,922
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Dah Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.
   
 11. a

  adolay JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,116
  Likes Received: 2,270
  Trophy Points: 280
  Hili la kuwawa na usalama wa taifa wenzake kama litakuwa na ukweli, kwa kuisaidia CHADEMA ni kombora la kuendelea kuishindilia

  ccm shimoni wala hakuna kupumua. Itawaumiza sana wakaazi wa mbeya. Tusubili kama ni za uhakika habari hizi.

  Mwandosya

  Mwakyembe

  Mwangosi

  Mwasokwa

  Mwaikusa
  .
  .
  .
  Hapa kunakupona kweli ccm 2015
   
 12. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,854
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  R. I. P.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hakuna mtu baki mwenye kufanya hayo ila ni wenyewe kwa wenyewe. System imegawanyika na wanapomtuhumu mwenzao kuvujisha siri basi njia nyingine huwa nguvu kutumika kwa vile yupo kwenye system, kinachofanyika ni kikundi kidogo kinachoandaliwa kumaliza kwa njia za ujasusi wa kijambazi, ndivyo hawa jamaa walivyo.

  Angekuwa mtu wa kawaida propaganda zingetumika kumchafua hadi aharibikiwe mambo yake na inaposhindikana propaganda ni rushwa kutumika kwa kuhonga ili kukamilisha azima yao. Kwa huyo yote yameshindikana na kuamua kuchukua njia ya ujasusi wa kijambazi.
   
 14. t

  tenende JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Ulimboka,
  Mwaikambo,
  Juani Mwaikusa n.k.
  Hawa woote si bahati mbaya!
   
 15. a

  adolay JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,116
  Likes Received: 2,270
  Trophy Points: 280
  Mwandosya

  Mwakyembe

  Mwangosi

  Mwasokwa

  .
  Ulimboka,

  Mwaikambo,

  Juani Mwaikusa n.k.

  .
  .
  .
  .

  Kuna haja na kuangalia kwa makini hasa mikowa ya Arusha, mwanza, kilimanjro, Mara na mbeya yenyenye kunamdudu mtu nini?

  Au ni ajali za kijambazi za kawaida?
   
 16. W

  Waambi JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2012
  Joined: Dec 4, 2012
  Messages: 736
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari hizi zinanikumbusha kifo cha Prof. Jwani Mwaikusa mwezi Julai 2010. Ni huzuni
   
 17. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mkuu asante kwa taarifa. Hii habari ya kusikitisha. Alikuwa mzee poa sana na really easy goin. Tunaelekea mahala pabaya sana kama mtu anaweza chinjwa tena nyumbani kwake, Tanzania yenye amani inaelekea kuwa historia soon.

  R.I.P Mzee Mwasokwa. Ulikuwa moja ya wazee nawakubali sana kwa ucheshi na utashi wako.
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mungu alitoa na ametwaa tena, jina la Bwana lihimidiwe. Sote pamoja na wauaji lazima tuonje mauti.
   
 19. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,522
  Likes Received: 3,831
  Trophy Points: 280
  Heshima yako mkuu, hawa jamaa walikuwa moto wa kuotea mbali enzi zao - sina shaka waliacha wamewafundisha wenzao mbinu za kazi zao kabla hawaja staafu.

  Hila hili la mzee (R.I.P) wa watu kuuawawa kinyama nafikili ni mambo ya huko huko Mbeya, TISS haiwezi kuwa inahusika na kitu kama hicho.
   
 20. z

  zanzibar huru Senior Member

  #20
  Dec 9, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo aliyeanzisha TISS ni mtu wa Mbeya na Mnyakyusa

  na DG wa usalama aliyeondoka naye ni Mtu wa Mbeya na Mnyakyusa

  wote wanatoka sehemu moja, dini moja, kabila moja

  je tunaweza kujua TISS imegawanyinya namna hiyo? yaani dini moja, eneo moja? na hapa sizungumzii watu wa chini nazungumzia rank za juu.

  kama ni kweli bas itabidi wapelekewe somo la diversity.

  RIP
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...