Mawaziri watakiwa kurudi Dar na Kurejesha magari Wizarani

Hivi ni nani staring wa filamu hili la kihindi?na mbona muziki umekua mwingi wakati ss tunataka kuona "mkono"?kha!!
 
Jamani tusubiri mambo yataiva hivi punde, ila swala la msingi je hata watakaochaguliwa watafanyafanyaje katika mfumo tuliopo ili kuwaridhisha wananchi? nilikuwa nafikili tuanzie ngazi za chini katika kufanya mabadiliko.
 
Hata kama wakishtakiwa na hata kupatikana na hatia, watakuwa ni kama "BANGUSILO" tuu. Hiyo ni kafara ya kiana maana wafujaji wa mali ya Uma ni wengi zaidi ya hawa jamaa nane. Ili kurudisha imani, ni vizuri kwanza wale waliochkua pesa za EPA na kufanya marejesho bila hata riba (Hata kwenye SACCOS hawafanyi hivyo) tukawajua kwa majina na kiasi walichorejesha. Pili, wote waliohusika kwenye EPA wafikishwe mahakamani na kesi zao zipewe kipa umbele ili zikamilike mapema. Vinginevyo hii itakuwa ni danganya toto ya mwaka!
 
Kama watendaji ni walewale huu utakuwa ni mvinyo uleule kwenye chupa ya konyagi!
 
Mkuu Ulukolokwitanga dalili zoooote zinaonyesha kwamba Mtoto wa Mkulima atarejea vinginevyo hakuna baraza jipya labda hadi wiki ijayo. Nasema hivyo kwa kuwa sijaona dalili zozote za kuitishwa kwa kikao cha dharura cha Bunge ili kupitisha jina la PM mpya.

kaka nashukuru sana kwa kutoa elimu,kwani kuna watu humu wapo ili mradi wapo

hawaelewi kuwa ili baraza livunjwe ni lazima waziri mkuu aondolewe ktk nafasi yake na kama haitatokea hivyo basi ni wazi kuwa hakuna baraza jipya ila kuna kuziba mapengo ama kubadirisha mawaziri nani aende wapi.
 
Gazeti lenyewe hili hapa

IMG-20120504-00306.jpg
 
Hathubutu kufanya hivyo, hao ni wabia wake katika mradi wao haramu wa kuifukarisha nchi yetu kwa kutumia madaraka yao.
 
Kwa kushtakiwa watakuwa wanaonewa my opinion, wachunguze wafujaji woote kwanza, imguse kilamtu inc mkulu
 
Kuna taarifa japo si rasmi kuwa mawaziri wote wamezuiwa kusafiri nje ya dar; je hi ni dalili ya kuvunjwa kwa baraza lao? jamani tetesi msiulize source
 
Back
Top Bottom