Sina uhakika lakini sidhani kama mawaziri wanaweza kushitakiwa kwa makosa ya kiutendaji yaliyofanywa na watendaji katika wizara zao au taasis zilizoko chini ya wizara zao.
Upotevu wa fedha ulioko kwenye report ya CAG unahusu utendaji. Na nivyema mkatambua kuwa baadhi ya upotevu huo ni wa miaka 3 iliyopita wakati hata mawaziri husika walikya hawaja chaguliwa.
Pia ikumbukwe kuwa wengine kama Maige hawakutuhumiwa na CAG bali report za kamati za bunge.
Report hizi haziwezi kumpeleka mtu mahakamani hadi pale vyombo vinavyohusika vitafanya uchunguzi na kubaini kama tuhuma hizo ni za kweli au la.
Hapo ni kweli kwa sababu kulingana na sheria za Tanzania zipo Taasisi hususan polisi, Uhamiaji na Takukuru ambazo ndizo zenye mamlaka ya kufanya chunguzi za makosa ya kijinai na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa baada ya kujiridhisha kuwa upo ushahidi usio na mashaka unaowahusisha watuhumiwa, ripoti za CAG na Kamati za bunge zinaweza kusaidia katika uchunguzi wa tuhuma husika na haziwezi kutumika kwa asilimia 100 kama ushahidi. Aidha maofisa wa ofisi ya CAG na wajumbe wa kamati za Bunge wanaweza kuwa mashahidi wa Jamhuri lakini hawawezi kufungua kesi mahakamani. Ni muhimu wanaJF kulielewa hili!