Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Hivi ni mimi au magazeti? Noana kila habari ya Tanzania ninasoma habari za UCHAWI, watoto wanatumiwa kufanya mambo haya...hebu niambieni kuna nini kinaendelea?

Nimeambiwa kuwa watu wanataka utahjiri wa chap chap wanatumia watoto na maiti za watu..sasa hali ikiendelea kama hivi sijui kama atapona mtu. That said siyo kuwa mimi siamini kama haupo lakini hii stage ya kukata watoto vichwa na nadhani is abit far. Najuavyo mie kuwa zeu zeru wanafukiwa kule kwenye mchanga wa baharini nusu shingo na mechi ikiisha mnaenda kuwafukua lakini hii ya kuwaua is too much

Halafu ukitaka kujua kama uchawi tunauendekeza basi tazama ule MBUYU wa pale shule ya Mbuyuni hivi mnajua kwa nini hawakuukata wakati wanajenga ile bara bara?

Au kuna ule mbuyu kule nyuma kama unaenda Oysterbay ukitokea Salender Bridge...ule mbuyu una vimbwanga vya kila namna infact unachafua mandhari kabisa lakini hisikii city wakithubutu kuongoa


anyway point yangu ni kuwa whatever happened to simple ways kama kuvunja nazi?

Hii new breed of uchawi wa kukatana vichwa unanishinda kabisa. Nataka serikali ichukue hatua lakini sitopenda serikali kuwakataza watu wasifanye uchawi...hii itakuwa naviolate rights zao lakini nadhani inabidi tuwe na taratibu kufanya mambo haya

sijui wan JF mnasemaje?
 
Gembe wewe ni mchawi, inakuweje zeruzeru wafukiwe wakati mechi inachezwa? umewahi kushirikishwa ktk zoizi hilo mzee? Daa!!! ,

Hapa TZ haya si mapya hata kidogo, mara kichwa, mara maninihii!!! hapa kwetu si hatari, ila hilo la kuwafukia maaribino sikuwahi kusikia baba.
 
Mambo ya imani za kishirikina yana nguvu zaidi katika jamii isiyojiamini; inayoishi katika hofu; yenye matumaini katika nguvu zilizo "juu"; na jamii inayoishi kwenye ujima.

Ni psychological game inayotumiwa dhidi ya wajinga au mataahira.
 
Mambo ya imani za kishirikina yana nguvu zaidi katika jamii isiyojiamini; inayoishi katika hofu; yenye matumaini katika nguvu zilizo "juu"; na jamii inayoishi kwenye ujima.

Ni psychological game inayotumiwa dhidi ya wajinga au mataahira.

Sidhani kama uchawi ni mbaya..ila unakuwa ni mbaya pale watu wanapodhuriwa

sitaki kuamini mambo ya kizungu eti uchawi hauna nafasi and so on...hivi ndivyo walivyo tu enslave na kisha sisi tukajawa na slave mentality
 
Nilikuwa narejea hali ilivyo kwa waafrika wenzetu linapokuja suala la Albino na hali kadhalika hotuba JK ya Mwezi April ambayo ilileta matumaini mapya katika kupambana na wale wanaochangia mauaji ya albino.

Nikaona huko Malawi kuna mwanamuziki ambaye anahimiza Albino kujitetea wao wenyewe bnadala ya kutegemea mtu mwingine. Nako pia kuna unyanyapaa dhidi ya watu hawa.

Zimmbabwe nako, wanawake albino ndiyo wanma kazi kubwa, pengine kama ilivyo hapa, hawapati wachumba kirahisi, lakini baya zaidi wenye HIV wanaamini kuwa wakiwabaka kina mama hawa hawatapata Ukimwi.

Hapa kwetu ndiyo hivyo, Tangua JK atangaze vita dhidi ya wanaojihusisha na mauaji haya, wakiwemo waganga wanaoyachochea mwezi uliopita, hata sasa hakuna la maana, wanazidi kuawa, tumesikia majuzi huko mkoani Mara, na makaburi yao yanachimbuliwa na viungo vyao vinakatwa. Kati ya nchi hizi Watz tunaonekana kuwa wakatili zaidi kwa Albino.

Tunaendeleza usanii kwa kauli za kutia matumaini lakini hakuna kinachofanyika, nakumbuka ile enzi ya u play boy, kwamba NATO, no action talking only.

jamani ..... hiki ni kilio. Akifa balali tunasikitika, je albino hawa 20!
 
Sidhani kama uchawi ni mbaya..ila unakuwa ni mbaya pale watu wanapodhuriwa

sitaki kuamini mambo ya kizungu eti uchawi hauna nafasi and so on...hivi ndivyo walivyo tu enslave na kisha sisi tukajawa na slave mentality

GT, Uchawi utaonekana mbaya wakati wote, mpaka pale uchawi utakapo onekana na kuthibitika kuwa unakomboa jamii zetu.

Na hiyo primitive perception kuhusiana na uchawi haiondoki pale uchawi unapobakia kufundishwa gizani, na kuwa wa kurithishwa na usioandikika kwenye maandishi. Ili yoyote yule aaminiye na kutaka kujifunza aweze kuusoma.

Kuna post moja hapa ya Nikifufukammekwisha: https://www.jamiiforums.com/showpost.php?p=219663&postcount=127
Imenifurahisha jinsi ilivyotoa mfano, yakuwa kama uchawi ungelikuwa wa maana, basi mikataba yetu yote ingelikuwa ni yenye mafanikio kwetu!

SteveD.
 
WAPENDWA NIMEIPOST HII THREAD KWA MACHUNGU MAKUBWA.KILA MWENYE KUIPENDA TANZANIA NA AUCHUKIE UOVU!

Suala la maalbino kutekwa na kuuwawa limeendelea kujitokeza nchini na kwa staili tofauti kila uchwao.

Ndugu zangu ishu iliyotangazwa jana na kuandikwa magazetini leo kumhusu mtoto wa miezi saba, Albino huko shinyanga ambaye amekatwa mikono yake kuanzia kwenye mabega inazidi kutleta simanzi.

Chakusikitisha wauaji hao walivunja nyumba na kumchukua kunguvu akiwa na mama yake usiku.

Sielewi kilio hiki kama kina mwenyewe.Tangu maalbino walipoanza kuandamwa na kuuwawa serikali na polisi wamezungumza na kuweka mikakati lakini bado tatizo linaendelea tena kwa kutisha.

Watu wanadai ni masuala ya kishirikina ndiyo yanachangia kwa kuwa watu wanatafuta utajiri.

Utajiri utajiri utajiri! wa kazi gani? na ni nani huyu anayewatuma kuwaua maalbino? ni nani huyo anayetafuta utajiri? Hivi maswali haya nani wa kuyajibu?

Nasemaje,tukiwaachia polisi peke yao hawatafanikiwa.lazima vita hii wote tushiriki kikamilifu kwa sababu hao tunaotafuta utajiri na kuwatafutia watu utajiri ni sisi sisi.unajijua na kujuana fika.

Tusipobadili fikra potofu na kutubu uasi huu hakika tutamalizana taratibu.Baada ya maalbino tunaweza kusikia wanauwawa watu wenye vitambi kisha watafuata wenye ndevu, wembamba, wenye hips pana na mwishowe wataanza kuuwawa watu weusi.HATABAKI MTU!

"Kikulacho ki nguoni mwako"
 
Dakika chache zilizopita Shirika la Habari la Uingereza limetangaza katika matangazo yake ya habari kuwa kuna habari kwamba "some elements" za Jeshi la Polisi wao wenyewe wanahusika na mauaji ya Albino. Kama hili lina chembe ya ukweli basi kuna msingi wa kuwaogopa Polisi kutoa ulinzi kwa maalbino. Tukimbilie wapi sasa?
 
Dakika chache zilizopita Shirika la Habari la Uingereza limetangaza katika matangazo yake ya habari kuwa kuna habari kwamba "some elements" za Jeshi la Polisi wao wenyewe wanahusika na mauaji ya Albino. Kama hili lina chembe ya ukweli basi kuna msingi wa kuwaogopa Polisi kutoa ulinzi kwa maalbino. Tukimbilie wapi sasa?

mwnkjj na we sa nyingine bwana............... sasa hapa kweli tuseme kabsaaaaaaaaaaa unasubiri mapolisi watulinde wana nchi kweli??????
 
Dakika chache zilizopita Shirika la Habari la Uingereza limetangaza katika matangazo yake ya habari kuwa kuna habari kwamba "some elements" za Jeshi la Polisi wao wenyewe wanahusika na mauaji ya Albino. Kama hili lina chembe ya ukweli basi kuna msingi wa kuwaogopa Polisi kutoa ulinzi kwa maalbino. Tukimbilie wapi sasa?

Nafikiri sio kwa maalibino, tutalazimika kuwaogopa kutulinda kwa lolote! Usisahu pia kwamba huko nyuma polisi wetu wamewahi kuhusishwa na matukio ya ujambazi!!!

Sasa ukijumulisha na mambo ya ufisadi yanayoendelea, ambao kwa kweli umewezeshwa kwa kiasi kikubwa na wataalamu wetu katika sekta za fedha, hapa kuna picha kubwa, na inabidi tujiulize, what is wrong with professionalism in Tanzania? Yaani hawa maafisa wetu mbalimbali wanasomea wapi utaalamu wao na inakuwaje nyoyo zao zina utupwe kiasi hicho inapokuja maswala ya utu na maadili?
 
mwnkjj na we sa nyingine bwana............... sasa hapa kweli tuseme kabsaaaaaaaaaaa unasubiri mapolisi watulinde wana nchi kweli??????
Samahani Mkulu Tuandamane, analoliongelea Mzee Mwanakijiji ni jambo sensitive sana usilifanyie utani, kwako ni swala dogo sana maana wewe sio Albino. Sasa hivi wezi wakiona mambo magumu wanakimbilia vituo vya polisi, sasa je Albino akiona ngozi yake inawindwa naye akimbilie polisi ambao nao wanahitaji hiyo ngozi? Usifanye utani Mkulu, haya ni mambo magumu sana. Hapa zinatakiwa data, na kama ni jambo la kweli basi Serikali inatakiwa kujibu na wananchi waone majibu, vinginevyo huu ni wakati muafaka wa mawaziri husika kuendelea kujiuzulu wakiwajibika kwa makosa ya wizara zao, hii itawafanya watakaoingia madarakani wawe wakali sana kwa ngazi zilizoko chini yao. Hili litaletwa tu na wananchi wenye hasira wakiona wanachinjwa waziwazi.
 
The BBC has been investigating the unexplained murders of albinos in Tanzania and uncovered a gruesome trade in body parts. The evidence points to albinos being killed to order by witch doctors, who use their body parts for magic potions to make people rich.

There is a widely held belief in Tanzania and many parts of Africa that albinos have mystical powers. In Mali for example, albinos are seen as bearers of bad luck. Many are abandoned at birth or even slaughtered in ritual sacrifice.


Kwa style hii ninaweza amini kuwa Polisi wetu kweli wanahusika maana Linapokuja suala la Utajiri polisi wetu hupoteza maadili kabisa na wapo tayari kushirikiana hata na Majambazi, mafisadi ili mradi wapate utajiri, na haitakuwa ajabu kama wataambiwa watapewa mshiko wa maana ili wawapatie watu wanaotaka albino viungo au wawaruhusu wajichukulie badala ya wao kuwalinda.
 
Miezi kadhaa iliyopita niliwahi kuweka thread hapa jamvini kuzungumzia Tume ya Uchunguzi kuhusu pesa zilizoibiwa toka BOT. Katika ile thread nilishauri kuwa ulikuwa muda muafaka kwa serikali ya Tanzania kuacha kuombeleza fedha kutoka kwa nchi wafadhili esp. Europian countries. Nilisema vile kwa sababu ushahidi upo wazi kuwa Tanzania si maskini kabisa ila mafisadi ndio wanatumalizia fedha na raslimali zetu. Nikadokeza kuwa badala ya kuwa ombaomba wa fedha za bajeti, vizuri tukawa ombaomba wa misaada ya Uchunguzi wa Kimataifa kuchunguza UFISADI nchini. Sababu kuu ya kutafuta misaada ya uchunguzi toka ng'ambo ni kwamba Vyombo vya uchunguzi vinavyomilikiwa na serikali ya SISIEMU aidha havijui jinsi ya kufanya uchunguzi dhidi ya MAFISADI na wengineo ambao kwa njia moja au nyingine wana mahusiano na viongozi wa serikali ya SISIEMU.

Sasa aibu ni hii hapa: Shirika la Habari la Uingereza (BBC) lilimtuma mfanyakazi wake kwenda Jijini Mwanza kutafuta ukweli juu ya mauaji ya Albino. Huyu mfanyakazi alikwenda (As Undercover) si kama mwandishi bali kama mtu anayetafuta utajiri wa haraka haraka. Kwa hiyo yeye alikuwa na mandate ya kupata ukweli juu ya mauaji ya Albinos. Kwa wale ambao mlisikiliza BBC World Service leo tarehe 21/07/08, kwa kweli ilikuwa inauma sana na inatia aibu machoni mwa watu pamoja na Mungu. Mimi nilikuwa drive gari huku nasikiliza BBC, naamini kuna wengine ambao waliona kwenye TV maana walikuwa wanafanya mahojiano na waathirika PAMOJA na MGANGA wa KIENYEJI ambaye alikuwa anawapa mbinu ya kufanya jinsi ya kupata huo utajiri. Huyo Mganga alisikika akisema kuwa viungo vya Albinos vinatumika katika biashara na MADINI. Na alidai kumsaidia huyo mwandishi kuweza kufanikiwa HAJA yake.

Sasa kama huyu mwandishi wa BBC ambaye hana dola lakini yeye aliamua kutafuta ukweli juu ya mauaji haya lakini JK, Manumba, Mwema wamekalisha makengere yao huko maofisini. Wana dola inakuwaje AlbInos wanazidi kuuawa? Cha kusikitisha zaidi ni pale Dada mmoja ambaye ni Albino alipokuwa anahojiwa, kweli machozi yalinitoka. Alidai kuwa Kaka yake ambaye naye alikuwa albino ndiye alikuwa PROTECTOR wake, lakini na yeye alikumbwa na mauti ya kusikitisha baada ya kuuawa na wafanyabiashara wa Madini. Sasa kama Protector aliuawa, na yeye alikuwa mbioni kuuawa.

JK aliwahi kutoa tamko kuwa hawa watu walindwe, Siku hizi kauli za Prezidaa haina UZITO wowote na wala aheshimiwi. Sasa ni Rais gani ambaye aheshimiki hata kwa juniors wake???. Fisadi atamuheshimu vipi fisadi mwenzake? Wenyewe wamekalia kujisafisha na UFISADI. Mnakimbilia kwenye Ofisi za MwanaHalisi kama hamna akili nzuri. Mara tayari mmeshakutana na waandishi wa habari kuelezea sakata hilo. Lakini wananchi pamoja na waandishi wakiuliza mambo ya Meremeta, EPA, Tangold, Dowans mnakuwa BUBU na mnazima simu zenu, au u-busy ndo unaongezeka.

Sasa hamuoni kama hii ni aibu kwa Taifa mwandishi eti toka nje ya nchi ambaye hana dola, anafanya uchunguzi wake mpaka anafika kwa huyo mganga wa kienyeji anayetoa instructions ya kutumia viungo vya Albino na kufanya nae mahojiano. NANI anaweza kuwajibika within JK's circle kuhusu hili sakata. Mh. JK na wenzako, mna dola kweli mnashindwa kukamata wale wanao-advocate mauaji ya wenzetu Albino. Kama hamuwezi kuwalinda kwa nini msiwatafutie hifadhi katika nchi nyingine.

Namalizia kwa kusema: NI AIBU KWA SERIKALI YA JK KUENDELEA KUFANYA MZAHA NA HII MISIBA. SASA BBC KAWAUMBUA ESP. JK MAANA WAMEKUPONDA KUHUSU KAULI YAKO JUU YA USALAMA WA ALBINO. LABDA SASA MTAZINDUKA, JF WALIPIGA SANA KELELE KUHUSU HILI NA NINAAMINI HATA HAO BBC WALIANZA KUPATA INSIGHTS THRU JF. JK SASA KAZI KWAKO.
 
Indume yene ndani ya dakika kumi zijazo nitarusha onesho hilo unalolizungumzia.. na ikiwezekana nitaweka link hapa hapa kwenye hii post. Kwa hiyo ambaye amemiss anaweza kusikiliza kupitia KLHN..
 
Nimeisikia pia jana mtangazaji alikuwa ni vicky mtetema...huyu dada anakwenda mahala pengi sana tanzania na sehemu nyingi dunia....kuna wakati alikuwa amekwenda israel.

Jana jioni ndio alikuwa mpakani mwa mwanza na shinyanga....kwa huyo mganga.
mwanakijiji...no link mpaka sasa...wapi?
 
salva alisema tusizungumzie mambo ya ushirikina wala mauaji ya albino kwa sababu yatakimbiza wawekezaji!

bbc inatangaza, wao wanasema tusilizungumzie......yaani serikali ya JK haikubali ukweli wa matatizo yaliyopo na ina hiari iishi kwenye ndoto ya kuwa tanzania ni safi haina matatizo
 
Back
Top Bottom