
An albino spokesman said there was a belief that the condition was the result of a curse put on the family.
Some witch-doctors also say they can use albino body parts in a potion to make people rich.
A teacher in the northern town of Arusha has been arrested for killing his own child, who was albino.
As well as the four killings, the body of an albino has also been exhumed. It was found with its limbs cut off.
The BBC's Vicky Ntetma in Dar es Salaam says there is now fear in the albino community there.
Christopher Dadenekeye from the TAS said the witch-doctors must also be arrested.
Some people in Tanzania think albinos are a kind of ghost-like creature.
"We need to clear out all these beliefs," Mr Dadenekeye said.
There are some 270,000 albinos among Tanzania's population of some 35 million.
Old women with red eyes have been killed in parts of Tanzania in the past, after being accused of witchcraft but our correspondent says this is the first time that albinos have been targeted in ritual killings.
TAS also wants more help for albinos and says the condition should be treated as a disability.
Source: BBC
Takwimu za mauaji ya Albino Mpaka Septemba, 2014
Mkurugenzi wa Shirika la Under The Same Sun, Vicky Ntetema
Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata), limeitaka serikali kupitisha adhabu ya kunyongwa kwa wale wanaohusika na mauaji ya Albino.
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Amani Kimataifa ya Albino jana jijini Dar es Salaam, Rais wa Chama cha Albino Tanzania (Tas), Joseph Tona, alisema kauli hiyo imetokana na ongezeko la idadi ya mauaji dhidi yao.
Kadhalika, takwimu za kutoka mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wameongezewa ulemavu mwingine wa kudumu.
"Tunaadhimisha siku ya amani Tanzania, lakini hatuna amani kabisa, wenzenu tunakatwa viungo na kuuawa kama kuku bila huruma, kingine cha ajabu makaburi 18 ya albino wenzetu yamefukuliwa na miili yao imetolewa, picha hii inaashiria nini?" alihoji Tona.
Alisema hofu hiyo imesababisha maziko yao kutokuwa na heshima kama wengine kutokana na baadhi ya familia kuwazika wapendwa wao kwa siri na wengine ndani ya nyumba, au kuweka zege nzito katika makaburi kuzuia ufukuaji wa miili yao.
Alisema licha ya serikali kuweka vikosi kazi katika kudhibiti mauaji hayo, bado haisaidii kitu kutokana na baadhi ya polisi na maofisa kuwa miongoni mwa vinara wa kupokea rushwa.
Kwa mujibu wa Tona, matukio zaidi ya 120 ni kesi za mauji ya albino, kati yake 11 ndiyo yaliyofikishwa Mahakama, ambapo kati ya hizo kesi tano tu zimeweza kutolewa hukumu hadi sasa.
Akitoa ushuhuda mmoja kati ya waathirika ambaye mikono yake miwili imekatwa, Mariam Stanford, mkazi wa Ngara, mkoani Kagera, aliwataka wauaji wa albino wanyongwe hadharani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizo.
"Japokuwa Tanzania inasifika ndani na nje kama kisiwa cha amani, tafsiri hiyo ni kinyume kwani ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mauaji ya kikatili, hivyo mwito wangu kwa viongozi wa dini tumieni midomo yenu kupinga hali hii kwa sababu na sisi tumeumbwa na Mungu na tunastahili kuisha kama wengine," alisema Miriam.
Mkurugenzi wa Shirika la Under The Same Sun, Vicky Ntetema, aliishauri serikali kupitia vikosi kazi vilivyochukua jukumu la kuchunguza mauaji na ukatwaji wa viungo kwa albino, kutangaza matokeo kwa umma ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Pia, iuelezee umma matokeo ya kura za siri zilizopigwa katika mikoa tangu mwaka 2009 hadi sasa zibainishwe wazi kwani nyingi zimeonyesha waganga wa jadi kutumiwa na na viongozi wa kubwa katika kuwania nyadhfa mbalimbali serikalini.
Kutokana na hofu hiyo, ameitaka serikali kurejea mkakati wa mwaka 2009 uliotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ili kupiga marufuku leseni za waganga wa kienyeji na wale wa jadi.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, alizitaka taasisi zilizopewa jukumu la kusimamia vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya walemavu hususani albino kutekeleza majukumu waliyopewa kisheria kwa uadilifu mkubwa jamii ya Watanzania ione haki inatendeka ili kudumisha amani ya nchi.
CHANZO: NIPASHE
Waziri mkuu mstaafu, Sumaye alaani mauaji ya Albino
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye (pichani), amesema serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kudhibiti na kupambana na vitendo vya mauaji vinavyofanywa dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na hivyo kusababisha kukithiri.
Akizungumza jijini Mwanza juzi wakati wa uzinduzi wa albamu ya watoto ya Kanisa la EAGT Lumala mpya, Sumaye alisema vitendo vya baadhi ya watu kuwanyakua watoto wenye ulemavu wa ngozi na kuwaua, vinasikitisha, kwani vinakiuka haki za binadamu.
Alisema serikali kutochukua hatua mwafaka dhidi ya vitendo hivyo, kunalisababishia taifa aibu, hasa pale inapoonekana baadhi ya wahusika kutumia viungo vya albino kutafuta madaraka au utajiri.
Hivyo, aliishauri serikali na vyombo vya usalama kuchukua hatua zaidi ili kukabiliana na vitendo hivyo.
"Haiwezi kuingia akilini eti viungo vya binadamu, hasa albino vinasaidia kupata umaarufu wa uongozi ama madaraka. Kama ni hivyo, kwanini usitumie kiungo chako ili ufaidike na utajiri huo," alisema Sumaye.
Alisema fedha zinazotolewa na baadhi ya watu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu zinatokana na ubadhirifu wa mali za umma na kuwatahadharisha viongozi wanaosimamia michakato ya uchaguzi kutenda haki kwa wagombea na wapigakura ili kuepukana na machafuko kama yanavyotokea kwa baadhi ya nchi barani Afrika
Awali, Mchungaji wa Kanisa hilo, Daniel Kulola, alisema wamekuwa wakiwalea watoto katika matunzo ya kumtukuza Mungu ili kupeukana na matendo maovu.
Chanzo:Nipashe
Dr. Bilal kuwachukulia hatua kali Wauaji wa ALBINO
Mhe. Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametoa tamko kali la kulaani mauaji ya Albino na amesema atawachukulia hatua kali sana hao Wauaji wa ALBINO.
SOURCE: ITV Habari saa 2 usiku, Tarehe 21 Februari, 2015
Wabunge watoa kauli zao kuhusu mauaji ya albino
![]()
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
Serikali yakiri ni jambo la aibu, Wabunge waitaka ichukue hatua za dhati kuzuia mauaji kwa wenye ulemavu.
Dodoma. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema kuwa suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hapa ni aibu kubwa kwa nchi hivyo jamii nzima iangalie jinsi gani watu hao wanalindwa.
Pinda alisema hayo juzi Dodoma alipokuwa akifungua semina iliyoandaliwa na UNDP kwa wabunge kuhusu watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.
Alisema mfumo wa watu wenye ulemavu wa ngozi katika elimu ni tofauti na watu wanavyofikiri kwa kuwa kama wakifundishwa kama wengine hawawezi kufika popote.
"Wana tatizo la kuona ukiancha tatizo la ngozi, hivyo ni muhimu wakaangaliwa vizuri," alisema Pinda.
Kwa upande wake Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema ni muhimu wabunge wakaelewa tatizo la watu hao ili waweze kuwaangalia katika majimbo yao na hata kuwafikiria katika bajeti wanazozipitisha.
"Ni muhimu utaratibu wetu wa bajeti tukawafikiria hawa kwa kuwa mimi binafsi kuna mambo wamenieleza ambayo mnapaswa kuyajua," alisema Makinda.
Alisema ni muhimu wakafikiria kutunga sheria za kuwalinda watu wenye ulemavu huo ili waweze kulindwa na sheria hiyo.
Akijadili suala hilo, Mbunge wa Kisarawe (CCM), Selemani Jafo alisema ni muhimu Bunge likapitisha sheria ya kuondoa kodi kwenye vifaa na dawa za kuwakinga walemavu wote.
"Pia Hospitali ya Ocean Road isaidiwe ili iweze kuwasaidia hawa walemavu," alisema Jafo.
Mbunge wa Busega (CCM), Dk Titus Kamani alishauri halmashauri zote nchini kuweka mazingira maalumu kwa ajili ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu huo na kuwapa dawa.
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy alisema kuwa Serikali ndiyo inachangia watu wenye ulemavu wa ngozi kuuawa kwa kuwa inawalinda waganga wa jadi.
Mbunge wa Mpanda Mjini(Chadema), Said Arfi aliitaka Serikali iwawekee utaratibu maalumu wa kuwafikisha hospitalini na kuwapatia matibabu watu hao.
Chanzo: mwananchi.co.tz
Last edited by a moderator: