Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

...Speculations (?),

Huyu mtoto ndiyo yule aliyeanguka na mwenzie pale kanisani mikocheni b kwa mama rwakatare, kwa wale waliomuona siku ile watamtambua, ni yule yule.

...mnh,
...Kamtu, unauhakika alianguka, au 'alianguka'?

Pia kuna habari zinazagaa mtaani kuwa hii ni system at work kuhamisha fikra za wananchi kwenye discussion ya ufisadi????????????????

...systen at work 'kuhamisha fikra za wananchi' kwenye discussion ya mafisadi (?) kwa faida ya nani?

This is MURDER!!! wala sio manslaughter, mtoto kachinjwa,

Exhibit A (kichwa) kimepatikana
Exhibit B (Kiwiliwili)kimepatikana
1st Suspect (Ramadhan) kakamatwa
Witnesses (Walinzi wa Muhimbili) wapo,

Jeshi la polisi na serikali isilikalie kimya eti 'tuhuma' za uchawi hazina nguvu! actions speaks better than words, ilianzia kwa watoto maalbino, sasa 'wanakula' vichwa hadharani,

hatari!!!!!!!!!!!!
 
Mimi sielewi nini kilitokea kati ya kushuka na ungo hadi hii itokee. Kuna kitu hakijakaa sawa.

Halafu kuna kitu sielewi, naona blog zetu zina uhuru sana wakuweka graphic pics, sana sana mambo ya ajali za gari etc, na hii ya leo. Mtu uki-hit tu page, unakutana na picha. Bora hizo picha ziwe zinawekwa kama link, mtu akitaka anabonyeza mwenyewe.

Nilipoisoma mara ya kwanza sikumaliza hata para ya kwanza ikabidi nikimbie kwenye thread nyingine haraka sana. Duh!....:(
 
nijuavyo huyu kijana kawahi kudondoka ktk 5different churchies akidai alikuwa anaenda kuwanga peke yake kadondoka likiwemo tabata caholic.kote alikodondokea aliomba alelewe hapo apate kusoma insteady alikuwa akiiba na kutoroka.mara ya mwisho alitokea kwa lwakatare na kujiita misukule na siyo wachawi polisi wakaona na kwenda kuwakamata due 2mashtaka yaliyokuwepo b4.mama yao alihojiwa pia na kusema wanawe wamekataa shule huwa wanapotea 4 2-4 wks hivyo kubuni utapeli wapate mlo.kwa issue ya juzi it seems kuna a big hidden information kwani i believe peke yake hawezi kufanya hilo huenda kashirikiana na mama yake ambaye b4 alikiri anaihi nao but this time kasema ametokea mtwara huwa hakai naye.Mungu na atuepushe na balaa hili.AMEN!
 
Aliyekutwa akitafuna kichwa cha mtoto atoa madai mazito

2008-04-29 10:13:52
Na Simon Mhina

Kijana Ramadhani Seleman Mussa (18), anayedaiwa kukutwa akitafuna kichwa cha mtoto Salome Yohana (3), amedai kumiliki vichwa vingine 50.

Mbali ya kumiliki vichwa hivyo, pia kijana huyo amedai kwamba, amekuwa `akitengeneza` ajali barabarani kwa njia za kishirikina kwa lengo la kujipatia damu ya kunywa.

Alitoa madai hayo jana katika kituo kidogo cha polisi cha Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salaam ambako anashikiliwa pamoja na mama yake mzazi, Khadija Ally na baba yake wa kufikia, Lucas Kibaya.

Akiwa kituoni hapo, kijana huyo alionekana akitoa maelezo hayo kwa ujasiri na pasipo wasiwasi wowote.

Hata hivyo, kutokana na maneno mazito na yakutisha aliyokuwa akiyatoa, polisi walilazimika kuwaondoa baadhi ya watu katika chumba cha mahojiano.

Watu walioshuhudia mahojiano hayo , waliiambia Nipashe kuwa, Ramadhani aliwaeleza polisi kwamba, anamiliki vichwa hivyo 50 kwenye maeneo tofauti hapa jijini Dar es Salaam na mkoani Mtwara alikodai alikuwa akiishi na baba yake mzazi.

Aidha, alidai kuwa ametega`kombora` la kichawi la kusababisha ajali katika barabara ya Morogoro pembezoni mwa daraja la Manzese ambalo hutumiwa na watembea kwa miguu.

Madai hayo yaliungwa mkono na majirani wa sehemu aliyokuwa akiishi kijana huyo, eneo la Segerea kwa Bibi.

Mmoja wa majirani hao, Bw. Sadi Marando, alidai kuwa, kijana huyo alimweleza kwamba, kila baada ya miezi mitatu, hupata kiu ya kunywa damu ya mtu.

Bw. Marando, amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kumshikilia mama wa kijana huyo kwa madai kwamba, Ramadhani alikuwa akisema siku zote kwamba, kazi zote za ushirikina hushirikiana na mama yake Khadija Ally.

``Kijana yule ni hatari ukisikiliza masimulizi yake unaweza kukimbia, hapa mtaani alikuwa na maisha ambayo kwa kweli yalikuwa ya kutisha, si mtu wa kawaida,`` alidai Bw. Marando.

Bw. Marando, alisema kutokana na kijana huyo kutoonekana kama binadamu wa kawaida, majirani walikuwa wakimhoji kila mara na kuna siku alisema kwamba wanacho kikundi chao chenye watu 10 akiwemo mama yake na kwamba yeye ndiye kiongozi.

Alisema katika mfululizo wa vituko vya kijana huyo, Alhamis iliyopita alitaka kumchinja mdogo wake, Pascal Lucas.

``Alikuwa ameshamkanyaga chini kama kuku na kuanza kumchinja, bahati nzuri majirani wakafanikiwa kumkamata, nadhani kiu ya damu iliendelea ndiyo maana alimteka na baadaye kumuua Salome,`` alisema Bw. Marando.

Ramadhani amenukuliwa akisema kwamba `makao makuu` ya kundi hilo yako mkoani Mtwara na wameweka `matawi` maeneo ya Manzese Darajani na Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Polisi mmoja wa kituo cha Stakishari aliyeomba jina lake lisitajwe, alisema Ramadhani bila woga amesisitiza kwamba, si mara yake ya kwanza kula nyama ya mtu na kwamba ataendelea kwa vile nyama za watu ndizo humpa nguvu katika mambo ya kishirikina.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Bw. Charles Mkumbo, alisema upelelezi na maneno yaliyozungumzwa na kijana huyo ni siri yao kwa ajili ya kutengeneza kesi.

Alisema hata kama kijana huyo anadaiwa kutoa maneno hayo, polisi hawatishiki na watamfungulia kesi kama muuaji wa kawaida.

``Tunachopeleleza sasa ni siri yetu, tunatafuta ushahidi na kujua mazingira ya tukio hilo na sisi tutamshughulikia kama muuaji mwingine yeyote na kamwe suala la uchawi kwetu halipo,`` alisema Kamanda Mkumbo.

Alipoulizwa kwamba kama polisi hawasadiki taarifa za uchawi ni kwanini wanawashikilia wazazi wa kijana huyo, Kamanda Mkumbo alijibu kwamba, wanawashikilia kwa kutambua kuwa, huenda wanajua mengi juu ya mtoto wao kutokana na kuishi naye kwa muda wote.

Kuhusu mazishi ya marehemu mtoto Salome, Kamanda huyo alisema polisi haina neno juu ya hilo bali inasubiri taratibu za maziko zitangazwe na familia.

Hata hivyo, alisisitiza kwamba, kabla ya maziko, lazima mwili wa marehemu ufanyiwe uchunguzi ambapo polisi wameomba ndugu wapeleke mwakilishi atakeyeshuhudia.

``Ndugu wakiwa tayari, muda wowote waje tuwakabidhi mwili, lakini kwaza tutaufanyia auchunguzi,`` alisisitiza Kamanda.

Nipashe ilitembelea familia ya marehemu huyo huku mama na baba wa mtoto aliyeuawa kwa kuchinjwa, wakiwa wamegubikwa kwa majonzi.

Mama wa mtoto huyo, Bi. Pendo Dunstan, alisema majonzi aliyo nayo hawezi kuyaelezea.

``Ni Mungu tu anayejua moyo wangu unaugua kwa jinsi gani,`` alisema kwa masitiko makubwa.

Naye baba wa marehemu, Bw. Yohane Majana, aliwataka polisi wamuachie huru kijana huyo anayedai kuwa ni mchawi ili na yeye amwonyeshe uchawi wa kisayansi.

``Wamwachie! Mimi naomba aachiwe huru ili nikutane naye ana kwa ana tuone,`` alisema.

Kuhusu mazishi, Bw. Majana alisema bado wanajikusanya ili kupata fedha hasa ikizingatiwa kwamba familia yao ni maskini.

Alisema ndugu na jamaa walitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya michango na kwamba wanatarajia mazishi yafanyike leo eneo la Segerea.

Wakati huo huo, Godfrey Monyo na Karama Kenyunko wanaripoti kuwa, polisi jijini Dar es Salaam, inawashikilia wazazi wa mtoto aliyekutwa na kichwa cha mtoto katika mfuko wa rambo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Bw. Charles Mkumbo, alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na kwa kuanzia wameanza kwa kuwashikilia wazazi wa mtoto huyo.

``Tumewashikilia wazazi wa mtoto aliyesababisha mauaji hayo na mtoto mwenyewe pia tunaye kwa hiyo tunaangalia nini kifanyike ili kubaini chanzo cha tatizo hilo,`` alisema.

Kamanda Mkumbo alisemapolisi hawaamini kama suala hilo ni la uchawi bali ni tukio la uhalifu kama mengine na kuwataka wananchi kuwapa muda ili kulifanyia uchunguzi kwa kina.

Alisema uchunguzi utakapokamilika, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara moja kujibu tuhuma hizo.

Jumamosi ya wiki iliyopita, kijana Mussa (18) anayedaiwa kuingia jijini Dar es Salaam akitokea Mtwara, alinaswa akiwa na kichwa cha mtoto.

Mtoto huyo wa kike, Salome Yohana, alipotea nyumbani kwao Tabata Segerea, wiki iliyopita na baadaye kiwiliwili chake kilikutwa katika choo cha nyumba ya jirani kabla ya kupata taarifa za kuonekana kwa kichwa chake hospitali ya Taifa Muhimbili.

SOURCE: Nipashe
 
Mmoja wa majirani hao, Bw. Sadi Marando, alidai kuwa, kijana huyo alimweleza kwamba, kila baada ya miezi mitatu, hupata kiu ya kunywa damu ya mtu.

Bw. Marando, amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kumshikilia mama wa kijana huyo kwa madai kwamba, Ramadhani alikuwa akisema siku zote kwamba, kazi zote za ushirikina hushirikiana na mama yake Khadija Ally.

``Kijana yule ni hatari ukisikiliza masimulizi yake unaweza kukimbia, hapa mtaani alikuwa na maisha ambayo kwa kweli yalikuwa ya kutisha, si mtu wa kawaida,`` alidai Bw. Marando.

Bw. Marando, alisema kutokana na kijana huyo kutoonekana kama binadamu wa kawaida, majirani walikuwa wakimhoji kila mara na kuna siku alisema kwamba wanacho kikundi chao chenye watu 10 akiwemo mama yake na kwamba yeye ndiye kiongozi.

Alisema katika mfululizo wa vituko vya kijana huyo, Alhamis iliyopita alitaka kumchinja mdogo wake, Pascal Lucas.

``Alikuwa ameshamkanyaga chini kama kuku na kuanza kumchinja, bahati nzuri majirani wakafanikiwa kumkamata, nadhani kiu ya damu iliendelea ndiyo maana alimteka na baadaye kumuua Salome,`` alisema Bw. Marando.

Huyu Bwana marando baada ya kuambiwa hivyo na mtoto Ramadhani alichukua hatua gani? Pale alipotaka kumchinja mdogo wake napo walichukua hatua gani? Huyu mtoto angepelekwa hospitali mapema Salome angekuwa hai mpaka leo. Ni hizi imani zetu za ushirikina ndizo zilizotufikisha hapa. Ukisikia hayo maelezo ya huyo mtoto utajua tu kuwa ana matatizo ya akili. Itakuwaje achinje watu hamsini bila jamii kustuka hasa ukiangalia uchache wa watu huko Mtwara? na kweli tunaamini kuwa ameweka mtego wa ajali za barabarani?

Huyu si wa kumfungulia mashtaka bali ni kumpeleka kwa wataalamu wa mambo ya akili.

Wakati huo huo, Godfrey Monyo na Karama Kenyunko wanaripoti kuwa, polisi jijini Dar es Salaam, inawashikilia wazazi wa mtoto aliyekutwa na kichwa cha mtoto katika mfuko wa rambo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Bw. Charles Mkumbo, alisema polisi wanaendelea na uchunguzi wa sakata hilo na kwa kuanzia wameanza kwa kuwashikilia wazazi wa mtoto huyo.

``Tumewashikilia wazazi wa mtoto aliyesababisha mauaji hayo na mtoto mwenyewe pia tunaye kwa hiyo tunaangalia nini kifanyike ili kubaini chanzo cha tatizo hilo,`` alisema.

Kamanda Mkumbo alisemapolisi hawaamini kama suala hilo ni la uchawi bali ni tukio la uhalifu kama mengine na kuwataka wananchi kuwapa muda ili kulifanyia uchunguzi kwa kina.

Wazazi wahausika vipi kama sio hizo imani zetu tena? Ukimsikiliza huyo msemaji wa polisi utahisi kuwa nae anajibharagua tu bali nae anaamini kabisa kuwa yule mtoto ni mwanga! Namuonea huruma mama wa huyu mtoto maana jamii imeisha mhukumu!
 
Huyu si wa kumfungulia mashtaka bali ni kumpeleka kwa wataalamu wa mambo ya akili.[/FONT]

Alikuwa amelazwa Psychiatric ward pale Muhimbili tangu alipopatikana kanisani pale Mikocheni, na inasemekana alitoroka siku chache zilizopita na ndio alikuwa anarudi wodini kabeba kichwa cha mtoto! Hatujui alipotoka kama taratibu zilifuatwa inapotokea mgonjwa kutoroka wodini na kama waliohusika waliwajibishwa
 
Hapa kuna utata,Kama huyu mtoto anatumia nguvu za giza then asingekamatwa pale Muhimbili,na pia inakuwaje mpaka anamchinja asionwe na mtu hata mmoja na kule Tabata nyumba ziko karibu,jamani nomba Mungu jibu lipatikane na kuwe na solution as soon as possible.
 
Mimi naona kuna mtu mwingine nyuma ya hawa watoto wanaofanya haya mambo.... mara ya kwanza walishuka na ungo.... mara ya pili mmoja kati ya wale walioshuka na ungo amemchinja mtoto wa watu....

Huyu mtoto akibanwa vizuri na hizi imani za kishirikina zikawekwa pembeni najua atasema ukweli nani yupo nyuma yake.... mimi naimani kuna mtu anamtumia huyu mtoto. mwenye masikio haambiwa sikia
 
Domo na Wengine!

Miye nadhani wote kama mnafungia macho hili swala na linazungumzwa hapa na kwengineko kama (samahania kwa hili neno linalofata kama lita watanza) KINAFIKI NAFIKI.
Wote tunajua na wale ambao hawajuu ni kwamba ,kama a month a go Huyu mtoto aliyechinja mwenzie na mdogo wake walisadikika walidondosha kwa kutoka kwenye ungo (wakiwa safarini,Mungu anajua from where to where) kwa MAOMBI makari yaliyo kua yakifanywa kwenye kanisa la MUHESHIMIWA MBUNGE WA VITI MAALUM CCM , Mama, DK,Mushemiwa GETRUDE LWAKATALE (MBUNGE).
Baadaye tukasikia matangazo kwenye Radio hasa Clauds FM kwamba '"NJOONI KWENYE MKUTANO MKUBWA WA INJIRI AMAKO WALE WATOTO WALIO DONDOKA NA UNGO BAADA YA MAOOMBI WATAONESHWA HAZARANI" na Mama,Mushimiwa,Mbunge,Dk. tukamuona akielezea jinsi mambo hayo yallivyo tokea tena kwenye TV.
A week baadae tulisikia Dakitari wa magonjwa ya akiri akisema watoto hao niwazima na watoto walipoojiwa (CHINI YA KIBANO CHA POLISI) walisema kutokana na maisha kua magumu walijingiza kwenye DEAL hizi ili Kupata pesa za chakula.
Tena wiki jana,tunasikia mtoto yul;e yule amekamatwa akiwa na kichwa cha mtoto mwenzie kwenye mfuko na baada ya hapo akaanza kunyonya damu na mengine mengi yamesemwa.
Sasa lakujiuliza hapa ni,KWELI MAMBO HAYA YANAWEZEKANA!?
AU MTU FULANI (MAMA,MH,DK,MB) ANAJARIBU KUTAKA KUJISAFISHA NA KUSISITIZA KWAMBA WATOTO HAO NA WAZAI WAO NI WACHAWI!
MTUMISHI WA MUNGU KAMA YEYE KUFANYA MABO KAMA HAYO NISAWA KWELI JAMANI?AU HIZI IMANI NYINGINE NI DEAL ZETU WENYEWE
Tafadhani jamaani tunapo liaangalia hili jamabo tusifumbie macho watu fulani fulani huyu mama ndio mtu wakwanza wa kuisaidia polisi asitake kuleta mambo ya ajabu hapa,HUU MPANGO WAKE HAUKUA KABAMBE UNA MAKOSA KIBAO!NA TENA YA KITOTO NA HAWA WASAIDIZI WAKE(WAPAMBE WAKE)WAMESHINDWA KUPANGA MPANGO HUU)
 
Kumuhusisha Lwakatare na haya mauaji ni kwenda kwenye another extreme.
Huyu kijana miaka 14,au 18, alianza tabia mbaya tangu hata hajadondoka kanisani kwake, amedondoka makanisa mengi tu, kwa hiyo kwa argument ya kuhusisha makanisa, ni kuwa wameshirikiana kusafisha jina, hiyo ni ngumu zaidi kukubali, bora hata uchawi.
Pia kuhusisha siasa za mafisadi pia naona ni out of place.
mimi naona labda sanasana ni ujambazi, ukichaa au sijui nini.
naomba kusahihishwa.
 
Nionavyo mimi huyu mtoto ni mgonjwa wa akili. Tatizo letu tunaendekeza sana ushirikina na ndo maana haya mauaji yanozungumziwa ki namna namna. Na mambo yote ambayo amefanya au anafanya ni kama kilio ili aonekane katika hii jamii anayoishi. Ugonjwa wa akili unawaadhiri wengi, na kutokana na serikali kutokuwa na ufuatiliaji mzuri na wataalamu ambao wangeweza kuchunguza vizuri ugonjwa wa huyu mtoto (kijana?) ndo maana amefikia hatua ya kuchinja mtoto. Hii ingeweza kuzuilika angekuwa kuna system nzuri ha social services/ health care. Inasikitisha.
 
Sawa kabisa Choveki, ila mimi natofautiana nawe kwa machace ulomalizia nayo;

kwanza,Huyu KIJANA (maana kumbe ana miaka 18 sasa, sio ile 12/14 walosema awali) Daktari wa magonjwa ya akili amethibitisha ana akili zake sawa sawa!,

pili, huyu KIJANA (na mwenzake/wenzake) inasemekana weshajaribu utapeli huko makanisani

Tatu, huyu KIJANA amekutwa na kichwa cha mtoto Salome, anajulikana mpaka wazazi wake na wapi alipopotelea mpaka kuchinjwa,

Nne, huyu KIJANA amekiri kwamba amemchinja Salome,

Tano, kuna shahidi anasema nusura amchinje mdogo wake wiki moja ilopita,

ushahidi gani tena unatakiwa hapa ASINYONGWE mpaka afe???

for the sake of sanity ya watanzania wenzetu, mtu kama huyu adhabu inayomfaa ni KIFO! Hakuna kumtetea ooh, imani za kishirikina, oooh, anaumwa akili, oooh atatuloga, mara anapotea kimiujiza...
Damn,...

keshasema ana kiu ya damu za watu, hatufai, ANYONGWE!!!!

mwishowe tutaanza ujinga wa kusema vitu ooh, anasumbuliwa na Attention Deficit Disoder nk...

Muuaji kwa makusudi hukumu yake ni nini?

tunaendekeza sana ushirikina jamani,...duh, hata ukweli mna u deviate?
 
Mtu mwenye akili timamu anamchinja mwenzake, anatia kichwa kwenye mfuko wa rambo halafu anampelekea shangazi yake aliyelazwa wodini? huko wodini angemkabidhi vipi ukiangalia wodi zetu jinsi zilivyo? huyo daktari nina wasiwasi nae. Huyu ni mgonjwa na kumnyonga hakutasaidia kitu bali kutosheleza kiu yetu ya visasi. Choveki yuko sahihi kabisa. Katika jamii inayojali watu wake haya yote yasingetokea maana dalili za matatizo yake ziliisha onekana mapema. Cha kujiuliza, ni kwa nini tuliziachia zitufikishe hapa? Ni yale yale ya kuwatuhumu vibibi vizee vyenye Alzheimer vikikutwa viko uchi kuwa ni wanga! Imani kama hizi hazitufikishi mbali.
 
kwa nn mwaka huu?

mbona huu mwaka unavituko kwa tanzania?

mnajumi wetu sheikh yahya anasemaje?

kila nikikumbuka maandishi ya shetani ktk mwaka huu
 
Huyu si wa kumfungulia mashtaka bali ni kumpeleka kwa wataalamu wa mambo ya akili.[/FONT]

Alikuwa amelazwa Psychiatric ward pale Muhimbili tangu alipopatikana kanisani pale Mikocheni, na inasemekana alitoroka siku chache zilizopita na ndio alikuwa anarudi wodini kabeba kichwa cha mtoto! Hatujui alipotoka kama taratibu zilifuatwa inapotokea mgonjwa kutoroka wodini na kama waliohusika waliwajibishwa

Nafikiri hata hawa madaktari nao yawezekana kabisa wana matatizo, mi sishangai kama mtu anapelekwa wodini akiwa na matatizo ya akili na asionekane kuwa na matatizo hayo!!!
So far katika hospitali zetu anayegundulika ana matatizo ni yule tu anaebeba makopo na kutembea uchi...
On the other hand bado hatuwezi kumuachia huyu kijana japo ana matatizo ya akili. Kwa kuwa anaonyesha wazi yeye anakijua vizuri anachokifanya ni lazima pia apate hukumu yake!!! Sidhani kwamba huyu kijana hajui kwamba sheria inakemea vibaya kitendo cha kuondoa uhai wa binadamu mwingine na kuna adhabu kali zinazoambatana na hii sheria...!!!

Lakini pia mi naona kuna matatizo mengi sana haswa kutokea kwa majirani na wazazi. Hivi inawezakanaje mtu akafanya attempt ya kumchinja binadamu mwenzake na akaachwa tu kimya kimya??? Does it mean aliwapumbaza na "ushirikina wake" au ndio walisubiri iwe too late ndo watoe maelezo??
 
Wana JF, baada ya kusoma habari hii ya kutisha nimekuwa najiuliza, lakini nimeshindwa kupata jibu, labda mnaweza kunisaidia kuelewa kidogo. Kama kweli uchawi upo, KWANINI HAWA WACHAWI WANAKUWA MASKINI?
WHAT IS THE BENEFIT OF BEING WITCH,
Ningekuwa mchawi ningependa sana niingine BOT nikiwa invisible na kuwa bilionea, na mimi niwe kama Chenge!
Anyone who can help me understand!
 
Nafikiri hata hawa madaktari nao yawezekana kabisa wana matatizo, mi sishangai kama mtu anapelekwa wodini akiwa na matatizo ya akili na asionekane kuwa na matatizo hayo!!!
So far katika hospitali zetu anayegundulika ana matatizo ni yule tu anaebeba makopo na kutembea uchi...
On the other hand bado hatuwezi kumuachia huyu kijana japo ana matatizo ya akili. Kwa kuwa anaonyesha wazi yeye anakijua vizuri anachokifanya ni lazima pia apate hukumu yake!!! Sidhani kwamba huyu kijana hajui kwamba sheria inakemea vibaya kitendo cha kuondoa uhai wa binadamu mwingine na kuna adhabu kali zinazoambatana na hii sheria...!!!

Lakini pia mi naona kuna matatizo mengi sana haswa kutokea kwa majirani na wazazi. Hivi inawezakanaje mtu akafanya attempt ya kumchinja binadamu mwenzake na akaachwa tu kimya kimya??? Does it mean aliwapumbaza na "ushirikina wake" au ndio walisubiri iwe too late ndo watoe maelezo??

Watu kama hawa huwa wanatengwa na jamii katika hospitali maalum ambako anapatiwa tiba mpaka hapo atakapoonekana anaweza kurudi katika jamii. Hauwezi kumfananisha na mtu mwenye akili zake anayeenda kumchinja albino ili apate utajiri!
 
Sawa kabisa Choveki, ila mimi natofautiana nawe kwa machace ulomalizia nayo......

mimi ningependa niongee na huyo daktari na nisikie sababu zake za kusema ati huyu kijana siyo mgonjwa wa akili. Kwani ukisoma habari nyingi utagundua kuwa huyu ni mgonjwa wa akili bila hata ya kuwa daktari.
 
Ahsanteni kwa maoni yenu nyote.

Kwa maoni yangu; RAMADHAN is guilty until proven Innocent!

Kids who kill fall into different categories, according to their traits, situations, and motivations. Some kills are accidental, such as those involving kids who find their parents' guns, but many occur within a specific type of context and have motives. Most of the experts categorize these killings;

3. Cult killings: ...A lot of kids identify themselves as Satanists because it gives them the feeling of power over others and the mystique of having secret associations with another world. It also gives them license to do things like rob, damage property, and kill. Sometimes they decide that human sacrifice is necessary to increase their powers, so they kill...

source; http://www.crimelibrary.com/serial_killers/weird/kids2/killers_2.html
 
Mtoto mtafuna vichwa... mengi zaidi yaibuka

2008-05-01 11:45:48
Na Moshi Lusonzo

Kijana Ramadhani Mussa (18), ambaye anadaiwa kumchinja mtoto Salome Yohana (3), imeelezwa kuwa aliwahi kulazwa katika wodi ya vichaa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, imedaiwa kuwa, kabla ya kufanya mauaji ya mtoto huyo, pia aliwahi kuvamia wodi moja ya hospitali ya Taifa Muhimbili na kudai ametumwa kuchukua vichwa na damu za watu waliokuwa wamelazwa hapo.

Kwa mujibu wa mfanyakazi mmoja wa hospitali hiyo ambaye hakutaka jina lake litajwe, Mussa alifika katika wodi ya wagonjwa wa akili hospitali hapo na kumueleza mhudumu wa zamu azma yake hiyo.

Hata hivyo, alisema mhudumu huyo alimfukuza na kumtoa nje.

Kuhusu kupata tiba katika wodi hiyo ya wagonjwa wa akili, alisema Mussa alifikishwa hapo akiwa na mtoto mwenzake ambapo baada ya kutibiwa, kwa takriban mwezi mmoja, waliruhusiwa kurudi nyumbani.

``Huyu kijana alikuwa hapa baada ya kuletwa ili apatiwe tiba ya maradhi ya akili kutokana na maneno ya kutisha aliyokuwa akiyatoa, kwa kweli hata sisi alikuwa akituogopesha pale alipokuwa akisema lakini tulimchukulia kama mgonjwa,`` alisema mfanyakazi huyo.

Alisema siku ya Ijumaa walipokuwa wakifanya shughuli zao, ghafla alitokea kijana huyo na kumueleza mhudumu mmoja kuwa amerudi tena wodini humo kwa kuwa ametumwa vichwa vya watu pamoja na damu.

Wakiwa katika hali hiyo kushangaa, Mussa aliwaeleza wahudumu hao kuwa, kama hawataki kumruhusu kuchukua vitu hivyo, basi atakwenda katika wodi ya watoto kuchukua kama anavyofanya usiku akiwa na kundi lake.

``Pale tuliamua kumtoa nje ili kutowasumbua wagonjwa tuliokuwa tukiwahudumia, hatukuweza kujua maneno yale alikuwa akisema kweli na hata kama tungemuacha, angefanya maafa makubwa kwa wagonjwa wenzake wodini,`` alisema.

Alisema, siku iliyofuata, walipata taarifa kuwa, kijana huyo alikamatwa katika lango la hospitali ya Muhimbili akiwa na kichwa cha mtoto na kwamba hali hiyo iliwashtua mno.

Katika kipindi cha wiki moja sasa, jiji la Dar es Salaam limezizima kwa tukio hilo la aina yake linalohusishwa na ushirikina.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom