Mauaji ya Albino: Kushindwa kwa serikali?

Nchi ikiongozwa na giza mambo hayo yatatokea. fikiria swala la albino!!!!!!!!!Tunahitai maombi ya kwelikweli.Siku hizi ma askofu namanabii na mitume kibao kama ni waukweli wakemee hayo mambo.
 
Hii ni hatari sana jamani na tena inatisha mno! Naomba waratibu muitoe hii mada kwenye siasa maana hii si siasa hata kidogo. Na tena heading ibadilishwe iendane na habari yenyewe. Weka kwenye "habari za kutisha" au kitu kama hicho!
 
Mods kwa maoni yangu naomba ibakie hapa lakini ipewe appropriate heading maana hiyo heading huwezi kujua kama ni kitu sensitive namna hiyo.
 
hii nayo kali sasa duh nashindwa kushangaa sasaaa!
 
maendeleo ya sakata hili ni kuwa kichwa cha huyo mtoto kimeshatambuliwa na kijana alokamatwa nacho ameshikwa yeye na mama yake
 
Huyu mtoto Ramadhani ni wa kwenda kumpima akili! Si uchawi, ni matatizo ya kisaikolojia. Hii inachangiwa kwa kiasi kikubwa na kukithiri kwa imani za ulozi katika jamii yetu. Watoto wanakuwa na kuamini kuwa kweli nao wanaweza kuingia huko. Hayo yote ya makaburini, kusafiri kwa ungo ni vitu alivyosikia na kuja kuamini ingawa sidhani kama kweli alikuwa akivitenda.

Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu Salome.
 
(Sick)!!!!

sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu hili? huyu kijana anastahili kifungo cha maisha bila parole, iwe katika juvenile prisons, au jela za wagonjwa wa vichaa, kama sio Kunyongwa!, (kumradhi Human right activists!)

' "hakuna dhambi kama kula nyama ya mtu, ukianza kula huachi"- JK Nyerere.'

Mbaya zaidi sasa inaonekana yeye kama 'wenzake' wana prey on young victims, imagine kabinti ka miaka mitatu maskini!?,

Imefika wakati serikali ipitishe sheria ili makosa haya ya kishirikina vifungo viwe ni maisha, kwani hata watoto mazeruzeru nao mashakani siku hizi!
 
Two Morogoro albino siblings under death threat

2008-04-27 10:57:00
By Peter Mwangu


The lives of Amina Abdul (11) and her brother Sadiki (13) are literally on the firing line. The youngsters, pupils at Mtibwa Primary School in Turiani, Morogoro, are being hunted by unknown people because they are albinos.

This has instilled fear and panic in the kids, as well as the school and Kidudwe village where they live.

This reporter has established that some strangers have been making enquiries on the siblings, who form part of the broader albino community in Tanzania who are targeted for murder, as a preamble for superstitious rituals linked to perceived fast wealth-generation.

Their schoolmate, Asteria Pascha, says: ``On Monday this week at around 4pm two short, tough-looking middle-aged men approached me while returning home after school. They asked me if I was studying alongside two albinos, to which I answered in the affirmative.

``I was very shocked when they offered to reward me handsomely with cash if I helped them get the pupils, who they said they wanted for a reason they did not disclose.

They explained that the exercise would be easy because they had established that the parents of the children had been away from the village on a paddy farming mission.``

Asteria said she was alarmed because she had heard news on the radio about albinos being kidnapped, killed, and some of their body parts being used for superstitious motives.

To play it safe, however, she faked co-operation by jotting down on a palm of her hand, a mobile phone number they gave her to facilitate follow-up contacts.

She explained, however, that the number was subsequently erased. She had not memorized it, and wasn`t keen to, because she wouldn`t contact them.

The girl reported the matter to the school administration which consolidated security around Amina and Sadiki, to protect them against abduction, particularly considering that they cover an eight-kilometre round trip to school and home, through a dense sugarcane plantation.

Sadiki was personally contacted by an unknown person who he feared was after him and her sister.

Sadiki said: ``One day two men (different from those who spoke to Asteria) came home with a box full of white garments like our school shirts and my sister Malizia Abdul was cooking in the house.

They told me that they had brought us some clothes but I declined the offer. They left, promising to bring more pleasant gifts on their return visit.``

Sadiki and his sister Amina have to walk the distance to and from school through the sugarcane plantations alone starting at 6am and late in the evening back home.

The school has reported the matter to respective authorities for further action on the security of the innocent kids. ``As teachers we are concerned.

We are taking necessary precautions to protect these kids and we have reported the issue to appropriate authorities,`` remarked a teacher who sought anonymity.

Abdul Said and Fatuma John, parents of the two albinos, have five children, Said, Idi and Malizia.

They lead a poor life and the health of Sadiki and Amina is not very good, due to their skins being too sensitive to ultra-violet radiation from the sun.

They have wounds almost all over their bodies due to poor shelter and medication.

More than 20 albinos have been killed in several parts of the country for purposes of getting rich.

SOURCE: Sunday Observer

Comment on this article
 


Mchongoma,

I get this feeling huyu mtoto alikua na wazimu na sio eti ni
ushirikina.He must have some psyche issues going on inside him!
 
Well mi nafikiri hapa pia chanzo ni lazima kijulikane maana hata akifungwa maisha huyu dogo, the person behind all this bado ataendelea kufanya mambo haya!!!
Huyo anayewatumia ni lazima awe tracked down na apewe adhabu kali... afungwe maisha na viboko 20kila siku!!!!
 
Huyu mtoto ni kioo cha jamii yetu. Imani za ushirikina zikishikamana si ajabu watoto nao wakiona wachangamkie dili! Ikiwa kila siku anawasikia wale anaowaheshimu wakizungumzia kwa imani masuala ya usafiri wa ungo, wanga, kuchuna ngozi na upuuzi mwingine kama huo ataacha kuamini? Ni sisi tuliowafikisha wote wawili, Salome na Ramadhani, hapo walipo. Sitashangaa kama sasa watashikwa wazazi wake, shangazi zake na bibi zake kwa tuhuma kama hizi ingawa pengine hawana hata hatia!
 
Kwa aibu nakumbuka wakati nikiwa mdogo nilifundishwa kutema mate kifuani nikikutana na albino (unaona sijui hata wenyewe wangependa kuitwa vipi!)ama sivyo balaa gani sijui itanikumba. Na sidhani kuwa ni peke yangu niliyefundishwa hivi. Ni hatua ndogo kutoka hapo hadi kujenga dharau ambayo nayo itafuatwa na kuwaona kuwa ni expendables! Kwenye hili la hawa ndugu zetu, wote tumo kama jamii. Ni wajibu wetu kama jamii kupiga vita imani na vitendo vyote viovu dhidi yao. Inabidi viongozi wetu wa imani zetu nao wainue sauti zao. Inabidi mashuleni watoto wote wafundishwe athari za aina yeyote ya discrimination. Serikali peke yake haitaweza ingawa hii isiwe kisingizio cha kutokufanya kitu. Bado wanawajibika kuwalinda kwa kadri ya uwezo wao na kuwasaka wale wote wanaowatendea maovu.
 
Mchongoma,

I get this feeling huyu mtoto alikua na wazimu na sio eti ni
ushirikina.He must have some psyche issues going on inside him!

...kuna mtoa mada mmoja hapo nyuma aligusia huyu mtoto 'Ramadhan', anahusiana na article iliyotoka kabla ya 31st March 2008 kwenye www.freemedia.co.tz na www.bongo5.com watoto wamtia 'changa la macho' Dr Rwakatare,
ni kweli???
au mkanganyiko wa majina tu?


...haya basi, kama ni wazimu, je wale wanaoua watoto maalbino?
 
Mchongoma,

Asante kwa kunipa taarifa.
Hao wanaoua mazeruzeru ni wahuni tu.
Wanalao jambo!
 
Huyu mtoto ndiyo yule aliyeanguka na mwenzie pale kanisani mikocheni b kwa mama rwakatare, kwa wale waliomuona siku ile watamtambua, ni yule yule. Pia kuna habari zinazagaa mtaani kuwa hii ni system at work kuhamisha fikra za wananchi kwenye discussion ya ufisadi????????????????
 
Ebwana hiyo inatisha inabidi sasa serikali iandae sheria mahsusi ya kudhibiti hivi vitu. Nadhani serikali imelifumbia macho limekuwa ni kama wimbo wa bongo flava utapigwa wee mwishowe watu wanachoka na kusahau. Haitofautiani sana na mauaji ya albino na uchunaji wa ngozi.
 
Asalamu alaykum.

Kama hana wazimu hupo na akili timamu basi ana udogo wa kufanya jambo bila ya kujua lazima anafahamu vyema kutokana na umri wake na kama anafahamu lazima angekataa kutumwa mambo mabaya kama hayo lakini amefanya kwa kujua kabisa.

lakini mimi nahisi wapo wakubwa wanaomtuma kufnaya vitendo hivyo na hao ndio wa kukamatwa kwa sababu wanaweza kusababisha watoto wnegi kuingia katika mchezo huo mbaya ambapo hivi sasa jamii yetu imekosa maadili mema vijana wengi wamekuwa na tamaa ya maisha na kukosa mafunzo mema kw ahivyo ni rahisi sana kuingia katika michezo michafu ya aina hiyo wakiwa na lengo la kupata fedha za kukimu maisha yao tu.
Mungu atusaidie lakini ni balaa kubwa sana ikiwa imani inamfanya mtu athubutu kumkata kichwa mwenzake? ni hatari kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…