Tanzania: Mauaji dhidi ya wanawake yaongezeka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu nchini Tanzania, LHRC, inayoonesha idadi ya wanawake wanaouwawa kila mwezi imeongezeka na kufikia 53 kutoka 43 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania pia imeonesha kuwa mauaji mengi ya wanawake hao yanafanywa na ndugu wa karibu, kwa imani za kishirikina na wivu wa kimapenzi.

Utafiti wa ripoti hiyo uliofanyika katika mikoa ya Geita, Shinyanga, Mwanza, Dar es Salaam na Kilimanjaro, pamoja na mambo mengine ulikuwa na lengo la kutathimini kwa ujumla hali ya mauaji ya wanawake katika mikoa iliyochaguliwa.

kadhalika ililenga kutathimini sera na mifumo ya kisheria ya sasa inayohusika kuwalinda wanawake pamoja na kutoa mapendekezo kwa serikali ya Tanzania juu ya kulishughulikia suala hilo.

Getrude Abene ni afisa mwandamizi wa masuala ya jinsia, wanawake, watoto pamoja na watu wenye ulemavu kutoka kituo cha LHRC, pamoja na kusisitiza kuwepo na sheria zinazowalinda wanawake ili kukomesha vitendo hivyo, lakini pia alitilia mkazo uwepo wa ushirikiano kutoka kwa mashirika yote yanayotetea haki za wanawake.

"kuunganisha nguvu za wadau kama mahakama, jeshi la polisi kuhakikisha kunapatikana taarifa hizi," alisema Abene.

Aliongeza kuwa kuna haja matukio haya kurekodiwa kama mauaji ya wenza na si kama mfumo wa sasa , ambo unarekodi kama mauaji mengine.

Ripoti hiyo inaonesha kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2018 hadi Septemba mwaka 2022, wanawake 2,438 waliuwawa ikiwa ni sawa na wastani wa wanawake 492 wanaouwawa kila mwaka na wastani wa wanawake 53 wanaouwawa kila mwezi.

LHRC inasema kuwa mauaji ya wanawake ni ukatili unaopaswa kukemewa na kipigwa vita kwa nguvu zote.
 
Back
Top Bottom