Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hii nayo kali sasa duh nashindwa kushangaa sasaaa!Hii nimeipata gazeti la Mwananchi:
Mtoto akamatwa na kichwa cha mtu, akitafuna mbele ya askari
Festo Polea na Kuruthum Ahmed
MTOTO Ramadhani Mussa (12) anashikiliwa na polisi Mkoa wa Ilala kwa kukutwa na kichwa cha mtoto mdogo Salome Yohana (3) alichokuwa amekibeba katika mfuko wa rambo.
Mtoto huyo alikutwa na kichwa hicho jana alfajiri baada ya kutiliwa mashaka na Fulgence Semfukwe ambaye ni mlinzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Muhimbili wakati akijaribu kuingia chuoni hapo akiwa na mfuko mkononi.
Baada ya askari hao kumuuliza mtoto huyo hakujibu kitu na badala yake akatoa kichwa cha mtoto kilichokuwa katika mfuko huo na kuanza kuking'ata na kutafuna nyama yake jambo ambalo liliwastua askari hao kumweka chini ya ulinzi huku wakiwasiliana na askari polisi kwa msaada zaidi.
Polisi walipomhoji mtoto huyo alisema anaishi Jeti Lumo na anaishi na bibi yake aliyemtaja kwa jina moja la Andenga na kuongeza kuwa mama yake mzazi anaitwa Khadija na ni mkazi wa Tabata kwa Bibi.
Mtoto huyo alijieleza zaidi kuwa yeye na bibi yake huwa wanaishi kwenye makaburi yaliyopo Jeti Lumo na kazi yao huwa ni kula nyama za watu.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Charles Mkumbo akizungumzia tukio hilo alisema linahusishwa na tukio lililotokea juzi saa 3.00 usiku ambapo mwili wa mtoto uliokotwa ukiwa umechinjwa kichwa eneo la Segerea.
Alisema katika tukio hilo, wakazi wa Kimara Baruti, Upendo Dastan (27) na mumewe Yohana Mussa Majani (26) aliyekuwa na mtoto wao Salome Yohana (3), juzi walikwenda kumtembelea bibi yao Furaha Majani anayeishi Segerea kwa Bibi kwa lengo la kulala huko.
Mkuu huyo wa upelelezi alisema walipofika kwa bibi yao mtoto wao alianza kucheza na ilipofika saa 3.00 usiku mtoto huyo akapotea katika mazingira ya kutatanisha.
Kamanda Mkombo aliongeza kuwa ilipofika juzi alfajiri, Lukas Kibaya (32) ambaye ni anafanya kazi ya kufyatua matofali katika eneo hilo alipokwenda kujisaidia chooni mita 800 kutoka kwa nyumba waliyofikia alikuta shimo la choo hicho limefunikwa na tofali huku likiwa limegandamizwa na nguo.
Alipolifunua akakuta kiwiliwili cha mtoto mdogo bila kichwa ndipo alipotoa taarifa polisi Sitakishari ambao walifika kuuchukua mwili huo hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda Mkumbo aliongeza kuwa baada ya kutukia tukio polisi iliwapeleka wazazi wa mtoto aliyepotea polisi kutambua kichwa cha mtoto kilichokamatwa na kuthibitisha kuwa ni cha mtoto wao.
�Tuliwasiliana na wazazi na wakathibitisha kuwa ndiye mtoto," alisema na kuongeza kuwa Ramadhani aliyekamatwa na kichwa hicho anashikiliwa na polisi SitakiShari kwa uchunguzi zaidi na kichwa hicho kimehifadhiwa katika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza na Mwananchi jana mama wa mtoto huyo, Upendo Dustani alisema mtoto wao Salome alishinda nyumbani kutwa nzima ilipofika saa 3:45 usiku baada ya kumlisha chakula cha usiku ndipo alipotoroka na kukutwa alfajiri akiwa amekufa.
Mama wa mtoto huyo alisema walikuja kwa ajili ya kumsalimia shangazi yake anayeishi Tabata Segerea ambaye hawakuonana kwa muda mrefu.
"Kifo cha mwanangu kimetokea katika mazingira ya kutatanisha na nina imani Mungu atatulipia kwa waliofanya kitendo hicho cha unyama", alisema mama huyo kwa uchungu.
Naye Mjumbe wa Shina wa eneo hilo, Salum Pembe alisema amepata taarifa hiyo alfajiri kutoka kwa majirani na kumueleza kuwa Salome alikutwa akiwa amekufa kwenye shimo la choo akiwa maiti yake ameviringishwa matambara na akiwa amekatwa kichwa.
' "hakuna dhambi kama kula nyama ya mtu, ukianza kula huachi"- JK Nyerere.'
(Sick)!!!!
sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu hili? huyu kijana anastahili kifungo cha maisha bila parole, iwe katika juvenile prisons, au jela za wagonjwa wa vichaa, kama sio Kunyongwa!, (kumradhi Human right activists!)
Mbaya zaidi sasa inaonekana yeye kama 'wenzake' wana prey on young victims, imagine kabinti ka miaka mitatu maskini!?,
Imefika wakati serikali ipitishe sheria ili makosa haya ya kishirikina vifungo viwe ni maisha, kwani hata watoto mazeruzeru nao mashakani siku hizi!
Mchongoma,
I get this feeling huyu mtoto alikua na wazimu na sio eti ni
ushirikina.He must have some psyche issues going on inside him!
Watoto wawili wanaojulikana kwa majina ya Yusufu na Ramadhani wamelidanganya kanisa la Mikocheni B la Assemblies Of God lililo chini ya Mchungaji Dk Getrude Rwakatare, wakijifanya wamedondoka kutoka angani walikokuwa wakiwanga baada ya kuchukuliwa na wachawi lakini kutokana na maombi ya waumini wa kanisa hilo ndiyo yaliyowaoko na ndizo sababu zilizowapelekea wao kuwasili kanisani hapo.
Habari kuhusiana na utapeli wa watoto hao uliwahi kutangazwa na kituo maarufu cha runinga hapa nchini cha ITV ambapo ulithibitishwa na kamanda wa polisi wilaya ya kinondoni bwana Jamal Rwambow na kudai kuwa kabla ya kujifanya wameangukia katika kanisa hilo, siku chache zilizopita wamewahi kufanya tukio kama hilo huko maeneo ya mbezi tangi bovu mnamo januari 6 mwaka huu.
"baada ya polisi kupokea taarifa hizo za watoto hao, vijana wangu walifika katika eneo la tukio huko mbezi na kuwachukua mpaka katika kituo kidogo kilichoko maeneo ya kawe na kuwahoji kasha kuwapeleka hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya zao ambapo wauguzi waliwacheki na kugundua hawana maradhi yoyote na baada ya muda tulipokea taarifa kutoka kwa raia wanaowafahamu vijana hao zikidai kuwa hawana lolote ni matapeli kwani mwanzoni mwa Februari waliwahi kujifanya wameangukia huko maeneo ya Manzese kwenye noja ya makanisa ya maeneo ambapo walichukuliwa na kupelekwa katika moja ya vituo vya kulelea watoto yatima huko maeneo ya kurasini" alisema Kamanda Rwambow.