Matumizi ya CCTV camera Tanzania na uvunjifu wa haki ya faragha

Utakuja kupinga hata Camera za mtaani ni maendeleo hayo na kuwa na ulinzi kwa mfumo wa kisasa nimedokezwa pia ndege nyingi zimefungwa Camera kwenye vyoo ila abiria hawezi kuiona hiyo inatoka na mambo ya Ugaidi kuenea kwa kasi...
sipingi tunataka sheria ambayo itataja maeneo ambayo hizo camera zinatakiwa kufungwa siyo kila mtu anafunga anavyo jisikia.
 
Eneo la biahara langu, nina jukumu la kuweka ulinzi wa aina yoyote.
Serikali ipunguze kodi au ifute kodi kwenye uagizaji sawa hakuna sheria iliyo tungwa mfano kusema ukifunga camera kwenye duka lako mwisho lazima hiwe mita kama tano hivi hakuna.
 
sawa zimefungwa kwenye coridor unajua baada ya hizo kurekodiwa hakuna mtu anayejua hizo taarifa zinapelekwa wapi na zinahifadhiwa kwa mda gani Tunataka sheria ambayo itatupa muongozo.
watenda maovu mna shida. Kwani hizo taarifa zikihifadhiwa kuna shida gani.
 
lazima tujue zinahifadhiwa kwa njia ipi na mtu akiziitaji utaratibu gani aweze kufuaata ambao umewekwa kisheria.
 
Ukifika nyumba za wageni shusha mapazia zima taa ili pawe gizaa kabisa afu washa camera ya simu bila flash light anza kuzunguka chumba kama una shoot video kama kuna kamera imewekwa itaonekana kwa mbali kama mwale mwekundu kwenye kioo cha simu yako😁
 
Kumeibuka tabia ya kila mtu anafunga CCTV camera kwenye maeneo ya biashara au nyumba ya kuisha mfano mtu anafunga CCTV camera kwenye eneo la baa au nyumba ya kulala wageni na Hakuna sheria au muongozo ambao umewekwa na serikali kusimamia matumizi ya hizo camera mwisho siku unakuta haki za binadumu (haki ya faragha) inafunjwa kwani serikali imeshindwa kutunga sheria ambayo itaweza kutoa muongozo wa matumizi ya CCTV camera. Matokeo yake CCTV camera zinafungwa kwenye maeneo ambayo siyo sahii kufungwa.

kuna umuhimu wa kutunga sheria kuweka utaratibu kuakikisha kukua kwa TEHAMA hakufunji haki ya faragha kama ilivyotamkwa na Ibara 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Kama sio sheria lakini kanuni ipo nayo ni kuweka tangazo la kuonyesha kuwa eneo hilo lipo chini ya uangalizi wa CCTV camera.Bank wanaogopa wezi lakini bado wameweka matangazo hayo ambapo kwa akili ya kawaida unaweza waza "kwa nini wamstue mwizi?"
 
Ukifika nyumba za wageni shusha mapazia zima taa ili pawe gizaa kabisa afu washa camera ya simu bila flash light anza kuzunguka chumba kama una shoot video kama kuna kamera imewekwa itaonekana kwa mbali kama mwale mwekundu kwenye kioo cha simu yako😁
m'bongo mpe picha tu maelezo atatoa yeye,😂😂😂
 
CCTV zinasaidia Sana Kwenye ishu za ulinzi na usalama.
Ambapo Mara nyingi zinawekwa sehemu za wazi Kama magetini, mapokezi, counter, na Kwenye korido,Kwenye fensi za nyumba.
Ila tatizo siku hizi kuna watu wanaweka hidden camera maeneo ya hadi vyumbani
 
tunataka kuwepo na sheria ambayo itatoa taratibu na adhabu kwa mtu atakaye funga camera na kuzitumia kinyuma na matakwa ya sheria.
Kama kawaida. Watanzania ni wepesi wa kupinga bila kutafakari. Wengi hawaoni implication ya watu kujifungia kamera holela tu. Wanatoa majibu mepesi. Hii ni kwa sababu hawataki kutafakari. Nchi zilizoendelea zina kamera kibao lakini kuna sheria na kanuni zinasimamia ufungaji na kuhifadhi na kuangalia kilichorikodiwa. Wengi wanadhani umetaka serikali ipige marufuku.
 
Back
Top Bottom