Shura ya Maimamu Tanzania tuwapongeza Afrika Kusini na Wadau wa Haki za Binadamu Tanzania

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
304
518
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
S.L.B.2055, DAR ES SALAAM.
SIMU: 0656654546. 24/01/2024.

KONGOLE AFRIKA KUSINI, KONGOLE WADAU WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA

Katika itifaki za ushirikiano na Afrika Kusini jana tarehe 24.1.2024, wadau kadhaa wa haki za binadamu Tanzania wamefanya mazungumzo na balozi wa taifa hilo, jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalihusu hatua ya Afrika Kusini ya kufungua kesi Mahakama ya Kimataifa (International Court of Justice ICJ), dhidi ya Israel kwa vitendo vyao vya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina.

Katika mazungumzo hayo, waraka wa pongezi kwa taifa hilo, uliotumwa kwa Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, ulisomwa kwa msisitizo mkubwa na hatimaye kukabidhiwa kwa kwa balozi huyo.

Shura ya Maimamu Tanzania nasi tunatumia fursa hii kuwapongeza Afrika Kusini lakini pia kuwapongeza wa Wadau wa Haki za Binadamu Tanzania, kwa kutuwakilisha vema Watanzania katika tukio hili kubwa duniani.

Aidha, baada ya kuupata waraka huo ulioandikwa kwa lugha ya kingereza, na kutafsiriwa kwa kiswahilli, tumeona kwetu itakuwa ni jambo la fahari kubwa kuambatanisha na pongezi zetu. Waraka huo uliosainiwa na Watanzania wenye makaliba mbalimba zaidi ya 120, una maudhui mazuri na ya kijasiri:

“Mhe. Waziri Grace Naledi Mandisha Pandor, Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, 460 Barabara ya Soutpansberg, Rietondale, PRETORIA, Afrika Kusini.
Sisi Watanzania na wanamajumui kindakindaki wa Afrika tuliotia saini zetu mwishoni mwa waraka huu, kwa unyenyekevu lakini pia kwa fahari kubwa, tunatoa kongole kwa Serikali ya Afrika Kusini na kwako binafsi kwa kuchukua msimamo madhubuti dhidi ya mauji ya kimbari yanayofanywa na Israel kwa Wapalestina.

Kwa kulifikisha suala hili katika Mahakama ya Kimataifa, mmetufanya sisi Waafrika tujifaharishe, kwani mmeipatia Afrika heshima kubwa katika kipindi hiki ambacho propaganda za kikatili na uzushi zinasambazwa duniani na vyombo vya habari vya mabeberu na Wazayuni.

Serikali yako imesimama imara kwenye misingi ya heshima ambayo ilifundishwa na waasisi wa mataifa yetu ambao ni Komredi Mzee Mandela na Mwalimu Julius K. Nyerere.

Kwetu sisi Waafrika, suala la ubaguzi wa kikaburu sio jambo la kusimuliwa. Waafrika tumepitia katika madhila ya namna hiyo ya kidhalimu na bado tunateseka kwa athari na taathira za udhalimu huo.

Hivyo, sisi tuna uzoefu wa kutosha na tunaujua uchungu wa udhalilishaji wa binadamu na mashaka yatokanayo kwa watu kufanywa kama si binadamu, hali ambayo ndugu zetu Wapalestina wamegubikwa nayo hivi sasa na ambayo wamedumu nayo kuanzia miaka 75 iliyopita.

Nyoyo zetu zinatoa machozi ya damu tunaposhuhudia maelfu ya watu wasio na hatia wakiuwawa na wengine kuzikwa wakiwa hai chini ya mabaki ya vifusi vya nyumba zao, hospitali, shule pamoja na miundombinu mingine ya taasisi mbalimbali.

Ninyi ndugu zetu viongozi wa Afrika Kusini, mliokomazwa katika tanuri la kupambana na ubaguzi wa kikaburu, mkaona kwamba kulia peke yake hakutoshi. Mkaamua kuchukua hatua zaidi kwa kupaza sauti kuungana na maelfu kwa maelfu ya raia wa Afrika Kusini na raia wa nchi nyingine duniani kupinga mauaji ya kimbari ya Israel.

Kitendo chenu hicho kimerejesha imani kuwa, ubinadamu bado upo. Mmetuongezea imani kuwa ubinadamu haujafa na hivyo kuchochea ari yetu ya kupigania haki.

Kwa kupitia waraka huu, tunakupongeza kwa ujasiri wako na serikali ya watu wa Afrika Kusini kwa kutoogopa. Pia tunatumia fursa hii kusisitiza juu ya kutokutetereka kwa mshikamano wetu na watu wa Palestina.

Tumejizatiti kutoa ushirikiano madhubuti kwa watu wa Afrika Kusini kwa kuunga mkono juhudi zao katika jitihada na harakati wanazozifanya dhidi ya Uzayuni na ubeberu katika majukwaa ya kidunia, wanaojaribu kuwatisha watu wa Afrika Kusini na serikali yao.

Ingawa hukumu ya Mahakama ya Kimataifa bado haijatoka lakini tayari mmekwishashinda kesi hiyo katika Mahakama ya Ubinadamu na katika Mahakama ya Kimataifa ya maoni ya watu, kwani kitendo chenu kimezigusa nyoyo na akili za mamilioni ya watu dunia nzima.

Tunakutafadhalisha uridhie kupokea salamu zetu za kindugu. 22 Januari 2024”.

WALIOTIA SAINI:

1. Issa Shivji (Professor Emeritus, University of Dar es Salaam).
2. Walter Bgoya (Independent).
3. Sheikh Ponda Issa Ponda (Katibu Mkuu, Shura ya Maimamu Tanzania).
4. Ikaweba Bunting (Tanzania Global Pan-African Movement).
5. Diana Kamara (Makerere Institute of Social Research).
6. Abdullah M. Othman (Chairman, Tanzania Palestinian Solidarity Committee).

7. Hamza Mustafa Njozi (Professor, Muslim University of Morogoro).
8. Kulikoyela Kahigi (Professor, St. Augustine University, Tanzania).
9. Karim F Hirji (Professor of Medical Statistics, retired).
10. Amil Shivji (Director – Kijiweni Productions).

11. Chris Maina Peter (Professor Emeritus, University of Dar es Salaam)
12. Joseph Chiombola (Land Rights Research and Resources Institute).
13. Saida Yahya-Othman (Professor, University of Dar es Salaam, retired)
14. Inessa Hadjivyanis (Legal Advisor & PhD Candidate, SOAS, University of London).
15. Wilbert Kapinga (Managing Partner, Bowmans Tanzania).
16. Bahame To Nyandunga (Advocate, Former Human Rights Commissioner, African Commission).
17. Ng ’wanza Kamata (Senior Lecturer, Dept Of Political Science, University of Dar es Salaam).
18. Salvatory S. Nyanto (Lecturer, Dept of History, university of Dar es Salaam).
19. Chambi Chachage (Independent).
20. Theodora Pius (MVIWATA).
21. Sabatho Nyamsenda (Asst. Lecturer, Dept of Political Science, University of Dar es Salaam).
22. Christina Mfanga (Tanzania Socialist Forum).
23. Richard Mabala (Researcher & Educationist).
24. Salha Hamdani (Retired UN WFP Staff).
25. Capt. Ibrahim Mbiu Bendera (Executive Partner, Bendera & Co, Advocates).
26. Nahida Esmail (Author).
27. Ian Bryceson (Professor, retired).
28. Ramesh Chauhan (Retired).

29. Bernard Baha (Tanzania Land Alliance).
30. Natasha Shivji (Lecturer, Dept of Historical Studies, University of Cape Town).
31. Stephen Ruvuga (MVIWATA).
32. Marjorie Mbilinyi (Professor, University of Dar es Salaam, retired).
33. Penina Mlama (Professor Emiritus, University of Dar es Salaam).

34. Demere Kitunga (Transformative Feminist Movement Building).
35. Ado Shaibu (Secretary General, ACT Wazalendo).
36. Ahmed Rajab (Gazeti la Dunia).

37. Emma Lwaitama Nyerere (Pan African Women Organisation, AU Agency).
38. Abdul Sheriff, Zanzibar (Professor, University of Dar es Salaam, retired).
39. Deus Valentine Rweyemamu (Chief Executive Officer, Centre for Strategic Litigation).
40. Juma Mwapachu (Ambassador of Tanzania).
41. Mona Mwakilinga (University of Dar es Salaam).
42. Navaya Ndaskoi (Human Rights Activist).

43. Adolfo Mascarenhas (Professor, University of Dar es Salaam, retired).
44. Hamudi Ismail Majamba (Professor of Law, University of Dar es Salaam).
45. Kajubi Mukajanga (Journalist, former Executive Secretary of Media Council of Tanzania).
46. F. E. M. K. Senkoro (Professor, University of Dar es Salaam, retired).
47. Ida Hadjivyanis (Senior Lecturer, SOAS University of London).
48. Nassoro Kitunda (Asst. Lecturer, Sociology Dept, University of Dar es Salaam).
49. Nizar K Visram (Tanzania Palestine Solidarity Committee).
50. George Hadjivyanis (Retired University Professor).
51. Boniface Kamara (Tutorial Assistant, University of Dar es Salaam).

52. Theresa Kaijage (Herbert Kairuki Medical University).
53. Onesmo Olengurumwa (Tanzania Human Rights Defenders Coalition).
54. Mussa J Assad (Vice Chancellor Muslim University of Morogoro).
55. Paschal Mihyo (Retired Professor).
56. Aldin Mutembei (Professor, Institute of Kiswahili Studies, University of Dar es Salaam).
57. Cathbert Tomitho (HAKIARDHI).
58. Irene Mgonja (Advocate).
59. Aysha Mbarak Meghji (Independent).
60. Ismat Sheriff (Teacher, Secondary School).

61. Hasnain Khimji (Tanzania Palestine Solidarity Committee).
62. Mneke Jafari (Deputy Director of Foreign Relations, Civic United Front, CUF).
63. Abdul Wakati (Imam Mkuu Masjid Taqwa Ilala Bungoni).
64. Sheikh Ibrahim Ghulaam (Katibu Mtendaji, Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania)

Wajumbe sita Profesa Issa Shivji, Bw. Walter Bgoya, Bw. Abdul Miraji, Bi. Christina Mfinanga, Bw. Sabatho Nyamsenda na Sheikh Ponda Issa Ponda, jana walikutana na Balozi wa Afrika Kusini kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya raia wa Tsnzania na Afrika Kusini.
 
Attachments

  • Letter to South African Foreign Minister final with names.pdf
    107.1 KB · Views: 2
1706216042644.png
 
Wazuru hawana akili hata moja
Kwanza walishindwa kuwafukuza wakoloni hadi leo mzungu yupo nchini

Pili kila mwaka watu 20,000 hufariki kwa mauaji ya uhalifu

Afu waenda kushtaki israel??? Yaan watu wanaokufa SA kwa kuuawa na risasi ni hawafikii hata robo ya watu wanaliokufa palestina tangu vita iianze
 
Ni Sawa na kupiga ngumi ukuta! Kipigo dhidi ya magaidi kiko pale pale.

Myahudi hana muda wa kusikiliza porojo kwenye mambo yanayohusu usalama wa nchi yake.
 
Hii nchi ina maajabu yake, ni ngumu sana watu kuona changamoto zinazotukabili ila wapo bize na yasiyotuhusu.....Huo mgogoro hautakaaa uishe
 
ni wapuuzi kujipendekeza na udini/uanaharakati wa kipuuzi, kwani hawakuona shambulizi la oktoba 7 lililoanzisha hiyo vita? Kwa hiyo israel ndio ishambuliwe na ikose mtetetezi/kujitetea? Hiyo kesi iliyofunguliwa na afrika kusini ni abrakadabra tu, israeli itashinda na afrika kusini itaaibika pamoja na hawa mazumbukuku waliotia saini kuunga mkono
 
Hamna ambae hajui uhalisia wa haya yanayoendelea ila kujifariji tu subir Gaza ifanyiwe restructuring kwanza wabaki na west bank
 
Back
Top Bottom