Matukio ya kutengenezwa ya kujiteka

Matukio ya kutengenezwa ya kujiteka

Serikali isifanyie mzaha hawa watu wanaotafuta kiki kwa kuichafua serikali. Lazima uchunguzi wa ndani ufanyike kujua huyu anadai alitekwa kama maelezo yake ni ya kweli
Watu wengine ni mashabiki hadi kichefuchefu.
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Sasa wewe unataka tuyaamini maneno yako kwa kigezo kipi? maana ulichoandika hakina logic hata punje.
 
Hata Roma alijitekea kwa yule anayekupa msaada wa maisha.Acha upumbavu use your brain effectively.
 
Nimepata Taarifa ya mshangao mkubwa jioni ya leo punde tu nilivyowasili nyumbani kwangu Mafinga jioni ya leo baada ya kuona kwenye mitandao ya kijamii na kusikiliza kwenye vyombo vya Habari sasa nakaa natafakari ni aina gani ya vijana tuliokuwa nao

Mapema leo asubuhi muda wa saa 12:00 asubuhi nilipanda gari aina ya NEW FORCE yenye namba ya usajili ya T 226 DJQ nakukaa siti yenye namba G3 ambapo jirani wangu aliyekuwa amejivika shuka la kimasai alikuwa amekaa siti namba G4 ambaye alionekana kuwa na hofu wakati wote na kutumia simu yake kwa kutuma jumbe tofauti kila mara

Wakati tupo njiani kijana yule nilitaka kujenga urafiki walau Tupige hata stori mbili tatu lakini ilishindikana ila tulipofika Morogoro ndipo alianza kunisemesha kwa kuhitaji nimsaidie kununua maji kwa kuwa nilikuwa upande wa dirishani nikafanya hivyo nikiwa na dhamira ya kumsaidia ndipo tulipoanza kupiga stori mbili tatu

Lakini nilisikia tukiwa njiani anawasiliana na mtu mmoja mwenye sauti ya kike na kumtaka aandae mazingira ya hapo wanapokutani.

Wakati wote namuaangalia kijana huyu ambaye awali nilikuwa simfahamu vizuri nilimbaini kwa sura nikamjua na hakutaka kuongea na mimi zaidii ya kujifichaficha

Sasa nimefika nyumbani Naanda kusikiliza radio nasikia kuna kijana wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kutekwa nilipoingia Facebook ndo nikaona picha yake nikamwambia mke wangu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kuwa kijana huyu nimependa naye basi moja kutoka Dar es Salaam na mke wangu hakuamini

Nipende kuambia ndugu watanzania wenzangu kijana huyu HAJATEKWA WALA NINI MAANA NILIKUWA NAYE MWANZO WA SAFARI YOTE NA KAMA KATEKWA LABDA NI KWENYE NDOTO

HIVYO TAARIFA ZOTE ZA UTEKWAJI WAKE NI ZA KUPUUZWA MAANA ANATAKA KUTAFUTA UMAARUFU WA AJABU KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII

*JONATHANA KWEPE*

Umeenda Polisi kutoa ushahidi? au umekuja huku kusafisha hali ya hewa baada ya kuona wanafunzi wa vyuo wasingewaacha salama?

Walikuwa wanawafanyia kweli, Press ilishiba kuliko hata zile za Chadema....

Walikuwa wanafika na nyinyi hadi mwisho, Mnabahati mmemrudisha........

Kwa IQ ya Yule dogo unathani ni wa Kujiteka yule au kutengeneza Movie?
 
Kwanza mimi sitaki kabisa kuusikia huu ujinga wa huyu mtoto Abdul Nondo.Katekwa saa 6 usiku na wakati huohuo ameshatekwa anapata muda wa kuandika sms kwa rafiki yake tena kwa Kiingereza kibovu ambacho hata hakiendani hata na elimu yake ' I am at the high risk' kama ilivyoripotiwa na wasemaji wanafunzi wenzake.
Watekaji wanampa muda wa kuandika ujumbe.Na hata hayo mazingira ya kuonekana kwake yaani mtu wa kwanza kumuona ni ya utata mtupu.Ushauri wa bure tunampa tena huyu mtoto na kama wazazi wake wapo wamsisitizie kuwa bado kidogo tu amalize shule yake atafanya siasa mpaka atachoka na kama anayo hamu ya kupigwa kwa ajili ya vurugu na maandamano asubiri mpaka amalize shule kwanza, atapigwa sana akileta upuuzi mpaka atachoka mwenyewe ataacha.
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.

Wakimaliza upande huu watahamia huko huko kwenu, hiyo inaitwa mbwa kala mbwa.
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Hili nalo neno mtekaji anamruhusu mateka kutumia simu,mateka kapata hadi mda wa kuandika sms,mateka kajikuta yuko Mafinga sijuwi matekaji kachukuwa lain za simu tu inamaana mtekaji kamteka mateka kamsafirisha hadi mafinga sijuwi makambako kwa lengo la Kuchukuwa lain za simu tu mmmmmmmh na maswali mengi sana ya kujiuliza ila ngoja mateka aje atoe full story ya wezekana akawa na majibu yangu ndani yake
 
Mkuu Nyani Ngabu upo sahihi muda mwingine tu judge vitu kiuhalisia na si kika kitu alaumiwe mtawala... Mm pia nahisi hakutekwa huyo
 
Hawa watu wataendelea kucheza hii michezo ya kuigiza mpaka lini. Eti oh nimetekwa, huku bado unatumia simu. Kutekwa gani huko?
Sawa siku akipatwa maswahibu hayo ndugu yako ndio utajua uchungu nyie endeleeni tu si police wafanye uchunguzi ili tujue nyie ni polic
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom