Matukio ya kutengenezwa ya kujiteka

Matukio ya kutengenezwa ya kujiteka

We gonna clarify it soon if he knows.....just chill out.
cc: NN
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Yaani we ndio unalingundua leo,kwani ile crip ya mwanausalama wao wanapanga mikakati hiyo umesahau,hawa jamaa wanaamini katika siasa za kueneza hofu na wasiwasi.
 
.Nimepata Taarifa ya mshangao mkubwa jioni ya leo punde tu nilivyowasili nyumbani kwangu Mafinga jioni ya leo baada ya kuona kwenye mitandao ya kijamii na kusikiliza kwenye vyombo vya Habari sasa nakaa natafakari ni aina gani ya vijana tuliokuwa nao

Mapema leo asubuhi muda wa saa 12:00 asubuhi nilipanda gari aina ya NEW FORCE yenye namba ya usajili ya T 226 DJQ nakukaa siti yenye namba G3 ambapo jirani wangu aliyekuwa amejivika shuka la kimasai alikuwa amekaa siti namba G4 ambaye alionekana kuwa na hofu wakati wote na kutumia simu yake kwa kutuma jumbe tofauti kila mara

Wakati tupo njiani kijana yule nilitaka kujenga urafiki walau Tupige hata stori mbili tatu lakini ilishindikana ila tulipofika Morogoro ndipo alianza kunisemesha kwa kuhitaji nimsaidie kununua maji kwa kuwa nilikuwa upande wa dirishani nikafanya hivyo nikiwa na dhamira ya kumsaidia ndipo tulipoanza kupiga stori mbili tatu

Lakini nilisikia tukiwa njiani anawasiliana na mtu mmoja mwenye sauti ya kike na kumtaka aandae mazingira ya hapo wanapokutani.

Wakati wote namuaangalia kijana huyu ambaye awali nilikuwa simfahamu vizuri nilimbaini kwa sura nikamjua na hakutaka kuongea na mimi zaidii ya kujifichaficha

Sasa nimefika nyumbani Naanda kusikiliza radio nasikia kuna kijana wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kutekwa nilipoingia Facebook ndo nikaona picha yake nikamwambia mke wangu ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kuwa kijana huyu nimependa naye basi moja kutoka Dar es Salaam na mke wangu hakuamini

Nipende kuambia ndugu watanzania wenzangu kijana huyu HAJATEKWA WALA NINI MAANA NILIKUWA NAYE MWANZO WA SAFARI YOTE NA KAMA KATEKWA LABDA NI KWENYE NDOTO

HIVYO TAARIFA ZOTE ZA UTEKWAJI WAKE NI ZA KUPUUZWA MAANA ANATAKA KUTAFUTA UMAARUFU WA AJABU KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII

*JONATHANA KWEPE*
Kazi kweli kweli....!
 
Tumuombee daima raisi wetu apate ujasiri kuyakabili haya maovu.
 
Maeneo mengi sana watu wameripotiwa kutekwa na kupigwa,
Huo ni uharifu kama uharifu mwingine tu!
Usalama hawawezi kufanya kazi kishamba namna ambavyo inaripotiwa; inawezekana kuna magenge ya chama yamejivika majukumu!
Kuweni makini na kauli zenu Kwa wapinzani wenu huko makwenu.
 
Binafsi tangu yule dereva wa rip Chacha Wangwe aliyejulikana kwa jina la Malya alipoonekana akiwa katika msafara fulani akielekea Libya nimekuwa siwaamini kabisa baadhi ya vijana wa Chadema. Hapa najiuliza tu Nyani Ngabu alijuaje kuwa Nondo hajatekwa bali kajiteka?!!....Ngabu nijibu tafadhali maana haya mambo yanatuchanganya sana!
Huyo ni lumumba mwenzako
 
Maeneo mengi sana watu wameripotiwa kutekwa na kupigwa,
Huo ni uharifu kama uharifu mwingine tu!
Usalama hawawezi kufanya kazi kishamba namna ambavyo inaripotiwa; inawezekana kuna magenge ya chama yamejivika majukumu!
Kuweni makini na kauli zenu Kwa wapinzani wenu huko makwenu.
Kuna chembe ya ukweli lakini kwann hilo genge halikamatiki?
 
Kwa hiyo mkubwa ikikaguliwa orodha ya wasafiri wa hilo basi tajwa na hicho kiti litakutwa jina la kijana anaesemekana alipotea? Hizi ni tuhuma nzito, na kama ikithibitika ni kweli, natoa wito adhabu kali zichukuliwe dhidi yake.
Atakuwa amekatiwa tiket na mtu hakutumia jina lake
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Huenda ukawa sahihi, mbona ni rahisi tu kugundua, tumia sim ya aliedai kutekwa na ukiangalia mchoro wa mawasiliano, unajua tu anadanganya au hyu kwel katekwa...

Bado usalama wa nchi upo sawa, ila huenda kunawatu wanapima kina cha maji, cha mhimu, tusiruhusu haya mambo yakawa ndyo ajenda...
 
Nyani amevurugwa, juzi kanitukuna mbaya sana hapa.
 
Haya mambo ya kukuzwa kwamba na kulazimisha kwamba tuna udikteta, hakuna uhuru wa habari, kutekwa, mauaji ya wanasiasa, kuponda juhudi za Dola katika kulinda rasilimali na maliasili ya nchi, vyeti feki, rushwa, ujangili, [HASHTAG]#hapakazitu[/HASHTAG], kumshambulia na kumuonea wivu Mh. Lukuvi na Kigwangalla na hata kuchonga barua za kufukuzwa kazi kwa kutumia nembo za Ikulu na wahusika wake n.k. n.k. Ni dalili tosha sana kwamba raia wake (ambao ni wachache) ni watu wa kizushi sana, wamechoka na amani, wanataka kuwe na vurumai na machafuko ya nchi ili sijuwi wafaidike na nini hasa?! INASIKITISHA SANA SANA...
Kwani yakitokea haya machafuko hawa wazushi wanajiona watapona?! Ni uzuzu usio na kifani kwa kweli...
 
Mapema leo asubuhi muda wa saa 12:00 asubuhi nilipanda gari aina ya NEW FORCE yenye namba ya usajili ya T 226 DJQ

*JONATHANA KWEPE*
Uongo mwingine Bwana,hilo Bus aina ya "NEW FORCE" linatengenenezwa Nchi gani?
 
Naanza kupatwa na mashaka kuwa huenda kuna watu wanaunda matukio flani flani ili kutimiza azma zao za kisiasa dhidi ya rais Magufuli.

Mtu anaenda kujificha kwa mjomba wake huko halafu wenzake wanasema kapotea au katekwa halafu lawama anaanza kupewa rais Magufuli.

Haya matukio ya kupotea potea watu inabidi tuyaangalie kwa jicho la tatu na si kumeza kila kitu tukisikiacho.

Msidanganyike kirahisi. Stukeni.
Mtu wa kwanza kushtukiwa inatakiwa uwe wewe. Mpaka sasa hakuna mtu aliyepotea na alipoonekana alidai alikuwa kwa mjomba wake, bali kuna watu wamepotea mazima na hawajaonekana, na wala serikali haiyapi uzito tena matukio hayo, na watu wanaoumizwa na mambo hayo (sio wewe mvizia makombo) wakipaza sauti uwepo uchunguzi huru, mawakala (wewe ukiwemo) yanapiga kelele kuwa polisi wetu hawajashindwa. Hatumwoni Saanane, hatumwoni mwandishi wa Mwananchi. Roma Mkatoliki ambaye nyie mawakala mliungana na Bashite kuwa angepatikana "Jumapili" , simulizi yake haionyeshi kuwa alikuwa kwa mjomba wake. "Asingeenda Zimbabwe." Kwa kuwa umeleta ngonjera hizi wakati kutoweka kwa Nondo ndio stori, bila shaka unataka kushirikiana na mawakala wenzake kufifisha hili. Umewahi sana, tusubiri Nondo aongee, kama ataweza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom