Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Matokeo ya Uchaguzi mdogo Igunga (matokeo ya awali)

Status
Not open for further replies.
Zitto katika twitter amekiri CDM kushindwa, tuache ushabiki lets face the facts magamba kwa hapa wamesha shinda CDM ijipange upya

Mwenye mamlaka ya kutangaza mshindi ni NEC.

Hata msemaji wenu Nape alitangaza mmeshinda lakini baada ya watu kusoma takwimu zake kwa macho angavu wakagundua amechakachua. Mara tunamsikia TBC1 anakanusha kwamba siye aliyepost hayo matokeo.

Kwa dalili hizi za kuchelewesha kutangaza matokeo na polisi kupiga mabomu mjini igunga, naanza kumuamini wa jikoni kwamba chadema wameshinda uchaguzi ila ccm wanatafuta mbinu ya kuchakachua kwahiyo wameizuia tume ya uchaguzi kutangaza matokeo hadi wafanikishe mpango wao wa kuchakachua mahesabu.
 
Najua hatimaye magamba watatangazwa washindi, sio kwa sababu wameshinda isipokuwa kwa kuwa ni lazima washinde. Vyovyote itakavyokuwa CDM wajue kuwa ndio washindi kwani walikuwa wanapambana na maadui wanne:

1. CCM
2. CUF
3. Serikali
4. Bakwata.

Kila jambo lina mwisho wake. CCM mwisho wao umefika na mfa maji haishi kutapatapa. RIP CCM
 
Hata kama CDM ikishindwa katika uchaguzi huu, (kwa uchakachuaji ama kwa haki).Lakini kwa jinsi hali ilivyo na walivyoibana CCM pale Igunga, itakaporekebisha kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza, na kuhamasisha watu, hasa vijana wajiandikishe na kujitokeza kupiga kura kwenye chaguzi zijazo, CCM imekalia kuti kavu.

The road to democracy is now clear...
 
Aishie kwa upanga, atakufa kwa upanga!

inauma eeeeh check hapo


ig3.jpg
 
Kutoka kwa Zitto Kabwe (MB)

Ndugu zangu, tuwe wakweli tu, tumepoteza Igunga. Tumepoteza kwa sababu moja kubwa- shahada za wapiga zimenunuliwa sana. Kata zote ambazo chadema imeshunda, turn out ilikuwa kubwa. Kata zote ambazo ccm imeshinda turn out ni ndogo sana sana. Hii tabia ya kununua shahada inayofanywa na ccm inaharibu kabisa maana ya uchaguzi. Kuna haja kufikiria kama itabidi tuwe na compulsory voting.
Toka jana usiku saa tano sisi tulishahitimisha kuwa kwa figures za matokeo toka vituoni hatuwezi kutangazwa washindi.
Ni muhimu kwenda mahakamani ili mahakama iweze kuamua masuala fulani fulani kwa mfano Mawaziri kushiriki katika kampeni na kutoa ahadi za kiserikali. Pili, tume kukataza watu ambao majina yao yamo kwenye daftari lakini hawana shahada, kupiga kura.
Suala la Kafumu kukataa kusaini, nadhani tuache masuala haya ambayo ndani ya dakika chache yatagundulika ni uwongo. Toka tunahesabu mpaka tunamaliza hatukuona 'margin' kubwa. Kata ya Igunga mjini ndio imechangia sana matokeo mabaya.
Bitter but truth

Vijana huwa hawapigi kura, hii nitarudia kuisema kila siku, ni wakati sasa kwa BAVICHA kuzunguka nchi nzima kushawishi vijana wenu wajiandikishe kwenye daftari la kudumu na wakat wa kupiga kura wajitokeze, siyo mikutanoni tuu....Hata uchaguzi wa mkuu october last year ilikuwa hizi hizi, otherwise mtatolewa nishai mpaka mwisho wa mchezo.
 
CCM wamekuwa na utaratibu huu kwa maeneo ambayo CDM wanaonekana kuongoza kwa asilimia kubwa ya kura kwa sasa.

Hakuna haja ya kusherehekea ushindi kwa sasa zaidi ya kuongeza Umakini kwa Timu iliyopo Igunga.

Mitandao ya Kijamii ni nyenzo kubwa kwa sasa kama sisi hapa tutaanza kujidanganya kushabikia na wananchi huko wanafungua simu zao za kihindi na kichina na kuanza sherehe huku CCM wakifanya kazi yao.

Huu ni mkakati kabisa, tangaz kwanza maeneo ambayo CDM wanaongoza ili na wao wakianza kuongoza tunabaki mdomo wazi.

maeneo kadhaa Igunga kwa sasa kuna Kimvua kinanyesha, na tunajua Ugonjwa wa Watanzania na Mvua. Wanaiogopa zaidi ya Kifo...hapo wataiacha mitaa wazi na CCM kufanya kazi yao.

Chondechonde umakini unahitajika zaidi ya kuanza kusherehekea kwa matokeao ya vituo ambavyo bado hata havijatimiza Kata 1.

CDM Igunga tia pamba masikio na hizi kelele za ushindi wa hisia za Mtu na simamieni kura, hatutaki hadithi ya Tarime. Hakuna cha Mzee wala Mwanamke ushindi ni muhimu


ADIOS

Kule tarime tunasema bhita ni bhita
 
Kutoka kwa Zitto Kabwe (MB)

Vijana huwa hawapigi kura, hii nitarudia kuisema kila siku, ni wakati sasa kwa BAVICHA kuzunguka nchi nzima kushawishi vijana wenu wajiandikishe kwenye daftari la kudumu na wakat wa kupiga kura wajitokeze, siyo mikutanoni tuu....Hata uchaguzi wa mkuu october last year ilikuwa hizi hizi, otherwise mtatolewa nishai mpaka mwisho wa mchezo.

Demography inaendelea kubadilika in favor ya opposition (hasa hasa CDM). By 2015, 20-50% ya wazee ambao wengi ni for status-quo (i.e. CCM) watakuwa no more. Sounds awkward lakini ndiyo ukweli.
 
Narudia tena na tena. Ccm wanashinda kutokana na ujinga wa watanzania.
 
Dhambi ya Wana igunga kuchagua gamba itawatafuna milele.
 
Za mwizi Arobaini, Tarime sio Igunga, kama ccm wanachakachua this tyme wananchi wamegundua mapema,Tusubiri cinema ya NEC itakuwaje,nahisi kuna mtu tayari presha ni ya kusuasua, Tume malizeni kazi mliyotumwa tujua la kufanya,muhimu Igunga sio uchaguzi wa nchi nzima,vurugi zozote zitaacha makovo Igunga wakati wenye siasa wemepaa kwa Helkopta.Chonde Tume Tangazane matokeo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom