KAMA KWELI KAKANA KITU BASI HICHI KIJITOTO CHA MZEE NNAUYE HAFAI HATA KUSHIKA NAFASI YA UKATIBU KATA!!!!!!!!!!!
Ni Jana usiku tu ambapo kiongozi mmoja wa ngazi ya juu sana kwenye Chama Cha Mapinduzi alipoibuka na orodha ndefu ya takwimu alioita MATOKEO RASMI YA UCHAGUZI WA IGUNGA na kutumwagia hapa jamvini huku akitamba na maneno ya kejeli kwa watu aliowaita 'PEOPLE'S POWER sasa kwishni', leo hii akaikane kama vile anachezea akili watoto wadogo???????????
Kwa kweli inashangaza mno kusikia eti kakana ile THREAD alioanzisha na baadaye MOD wa zamu kuanza kuikimbiza hovyo kwenda kuificha uvunguni ambapo tayari tumeshaunyonya yote.
Ripoti ya Nape ilinisababishia usumbufu mkubwa, kunipunguzia sana imani kwa Tume ya uchaguzi kana kwamba ni chombo geresha tu hivyo hata chochote watakachokitangaza, mimi kama mpiga kura wa nchi hii, si imani nayo hata kidogo kwa kuwa afisa mkubwa sana ndani ya CCM alinifanya niamini vinginevyo.
Ninaamini wapo watu wengi sana wanaojikuta katika hali hii nilionayo hivi sasa kote nchini hivyo zoezi zima Igunga haina tena any legal credibility and democratic legitimacy pindi mshindani anapojigeuza refarii.
Ukigeugeu kwa kiongozi wa ngazi ya juu kiasi hicho cha Nape kwa Wana-CCM ambaye kauli yale yoyote ile, in publi or private, huchukuliwa kuwa ni OFFICIAL POSITION ya chombo anachokiwakilisha, ni jambo la hatari mno!!!
Kama kweli anadiriki kukana waka THREAD yake nzima tulishaihifadhi mbali kabisa kutokana na hiyo BLANDER YA KISHERIA aliyoifanya basi huyu kijana wa Mzee Nnauye HAFAI hata kushika nafasi ya UKATIBU KATA - ovyo kabisa hamna kitu pale.
Nape na CCM kweli mnaleta 'mzaha za akina Rage na bunduki kuwarukia viunoni bila kutambua' katika masuala nyeti kama haya ya uchaguzi.
Kama haujui maana ya kosa la KIUFUNDI ulilolitenda basi nenda ukamuulize Mzee Mukama atakuelewesha pengine kwa kukulambisha kibao cha uso maana mpaka hapa KUNA KILA DALILI uchaguzi wa Igunga kuingia DOSARI KUBWA hivyo kuhitaji tafsiri za hali ya juu kisheria.
NB: Na mpaka hapa ni vema ikaeleweka wazi kwamba KITU CHOCHOTE MATANGAZO YA MATOKEO YA UCHAGUZI kwa jina la Jimbo la Igunga KAMWE HAYAWEZI KUAMINIKA tena na mtu yeyote mwenye akili timamu na ufahamu wa sheria za uchaguzi.
Nape na CCM tayari mmeingiza taifa kwenye HASARA kubwa katika hili.