Matokeo ya Uchaguzi Igunga: Radio One

Matokeo ya Uchaguzi Igunga: Radio One

Status
Not open for further replies.
Kuhusu zitto kukiri kushindwa, hili ni uharifu wa kimtandao, watu wameingilia akaunti za watu kama regia fb, zitto twita, nape jf hata mimi ni hacked lakn najaribu kupost
mie bado namwamini zitto ni mtu makini sasa hivi wanahangakia matokeo huo muda kaupata wapi? siamini kama yuko hotelini hizo ni kazi za kina nape. ccm mambo yangekuwa mazuri tungeshatangaziwa kitambo na tungeshasahau.kuhusu nani kashinda bado ni kitendawili kila mtu anavutia kwake lakini kiukweli matokeo yana utata hasa baada ya magamba kugundua jana usiku mambo yanaenda kombo.
 
Hebu tuwe serious na tuache ushabiki, Zitto amekiri CDM kushindwa kwa Kupata 45% na CCM 49% . Kama naibu katibu mkuu wa chama anakiri kushindwa nyie data hizo mnazitoa wapi?
 
Nimeshachoka kwa kila mtu anakuja na habari yake.tusubirini hyo saa 8

kweli tu mkuu nape kaja na yake hadi kapunguza users kwenye hii thread ya igunga ngoja tuone
 
Chadema inasemekana imeshinda kwa kura zaidi ya 3000 na CCM kuangukia pua na ndiyo maana hadi sasa NEC haijatoa matokeo rasmi. Dr Kafumu haamini macho yake na amekataa kusign.

Yah ni kweli CDM imeshinda ndio maana mpaka dakika hii NEC hawajatangaza matokeo wanadai bado wanahesabu kura.
 
Jamani hebu tuache tetesi tumpe nafasi Protas Magayane atupe ukweli
 
Nikamwelewa Dr Kafumu kukataa kusaini kwa point 2.
1. alisha somo Twitter ya Zitto akikiri Chadema imeshindwa
2. FFU wamewadhalilisha tena waislamu maana katika kupiga mabomu na kumwaga maji ya washa washa vijana kadhaa wa kiislamu wamepoteza baraghashia zao na wanawake wachache wa kiislamu waliokuwa wanapita karibu wamefunuliwa hijabb na hivyo kudhalilishwa kidini. Astaghafululah!!! Takbiri, Takbir!!!!

BAKWATA wawashawishi FFU kuomba radhi kama walivyoikomalia CDM,wasipofanya hvyo tutajua kuwa yale yaliyompata DC igunga na BAKWATA kuja juu,ulikuwa ni ushawishi wa serikali iliyopo madarakani.(CCM).
 
Lunch on me.
Nikamwelewa Dr Kafumu kukataa kusaini kwa point 2.
1. alisha somo Twitter ya Zitto akikiri Chadema imeshindwa
2. FFU wamewadhalilisha tena waislamu maana katika kupiga mabomu na kumwaga maji ya washa washa vijana kadhaa wa kiislamu wamepoteza baraghashia zao na wanawake wachache wa kiislamu waliokuwa wanapita karibu wamefunuliwa hijabb na hivyo kudhalilishwa kidini. Astaghafululah!!! Takbiri, Takbir!!!!
 
Ndugu zangu, tuwe wakweli tu, tumepoteza Igunga.

Tumepoteza kwa sababu moja kubwa- shahada za wapiga zimenunuliwa sana. Kata zote ambazo chadema imeshunda, turn out ilikuwa kubwa. Kata zote ambazo ccm imeshinda turn out ni ndogo sana sana. Hii tabia ya kununua shahada inayofanywa na ccm inaharibu kabisa maana ya uchaguzi. Kuna haja kufikiria kama itabidi tuwe na compulsory voting.

Toka jana usiku saa tano sisi tulishahitimisha kuwa kwa figures za matokeo toka vituoni hatuwezi kutangazwa washindi.
Ni muhimu kwenda mahakamani ili mahakama iweze kuamua masuala fulani fulani kwa mfano Mawaziri kushiriki katika kampeni na kutoa ahadi za kiserikali. Pili, tume kukataza watu ambao majina yao yamo kwenye daftari lakini hawana shahada, kupiga kura.

Suala la Kafumu kukataa kusaini, nadhani tuache masuala haya ambayo ndani ya dakika chache yatagundulika ni uwongo. Toka tunahesabu mpaka tunamaliza hatukuona 'margin' kubwa.

Kata ya Igunga mjini ndio imechangia sana matokeo mabaya.

Bitter but truth
 
Cdm wamewabinya masaburi. Mlizoea kushinda tu kirahisi....hiyo ndio indicator ya moto wa mabadiliko.
mtabakia kama Ghadafi tu, anawaita waasi panya wakati yeye ndo panya anaishi shimoni.
Endelea kujifariji hivyo hivyo!
 
Jamani tusubirini mpaka Tume wenyewe watoe matokeo,kwa maana mpaka sasa kila mtu anaamua kutoa matokeo yake,kwa heshima ya jf members tuache kuandika au kuchangia habari ambazo hatuna uhakika nazo,kwa kifupi mpaka sasa vyama vyote 8 vina nafasi ya kushinda.
Ushauri wangu jf ni chombo cha kuaminika na kuheshimika,kwa kuandika kwetu poroja za hapa na pale zitaondoa heshima hiyo na kuaminika
Nawatakieni Muwe na Muda mzuri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom